{"id":3911,"date":"2012-09-04T13:40:01","date_gmt":"2012-09-04T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2012\/09\/04\/mkataba-wa-kibiashaa-na-ulaya-bado-mgumu-kukubaliwa-na-kambi-ya-afika-pasifiki\/"},"modified":"2012-09-04T13:40:01","modified_gmt":"2012-09-04T13:40:01","slug":"mkataba-wa-kibiashaa-na-ulaya-bado-mgumu-kukubaliwa-na-kambi-ya-afika-pasifiki","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2012\/09\/04\/mkataba-wa-kibiashaa-na-ulaya-bado-mgumu-kukubaliwa-na-kambi-ya-afika-pasifiki\/","title":{"rendered":"Mkataba wa Kibiasha&#341;a na Ulaya Bado Mgumu Kukubaliwa na Kambi ya Af&#341;ika, Pasifiki"},"content":{"rendered":"<p>PORT VILA, Vanuatu, Septemba, 4 (IPS) &ndash; Yakiwa yamebanwa kati ya mwamba na mahali pagumu, mataifa ya Af&#341;ika na Pasifiki bado hayana uhakika kama yafuate wenzao wa Ca&#341;ibbean na kusaini Mkataba wa Ushi&#341;ikiano wa Kiuchumi na Ulaya (EPA).\n<\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>Mawazi&#341;i wa kambi ya Af&#341;ika, Ca&#341;ibbean na Pasifiki (ACP) wanakutana hapa kabla ya mkutano wa pamoja wa Ba&#341;aza la Mawazi&#341;i na Ulaya siku ya Alhamisi na Ijumaa (Juni 14 na 15). Hata hivyo, bado wako mbali mno kufikia kukamilisha mazungumzo ambayo yangewa&#341;uhusu kushi&#341;iki katika mkataba ambao Ulaya inautumia kama mbinu yake kubwa ya kibiasha&#341;a na kutoa misaada mingineyo.<\/p>\n<p>Mwaka 2008, Jukwaa la Ca&#341;ibbean (CARIFORUM), likishi&#341;ikisha wanachama 15 wa Jumuiya ya Ca&#341;ibbean (CARICOM) na Jamhu&#341;i ya Dominica, lilisaini mkataba huo. Jambo la kushangaza, Guyana, ambayo imekuwa ikisita kusaini mkataba huo hadi itakapopata baadhi ya vithibitisho, ni nchi pekee ambayo imesha&#341;idhia EPA.<\/p>\n<p>&#8220;Wakati wa kutia saini Guyana iliweza kuingiza tamko la pamoja ambalo limewekwa kama kiambatisho kwenye CARIFORUM&ndash;EPA likieleza kuwa katika kipindi cha miaka mitano kutakuwa na tathmini ya utekelezaji wa mchakato ili kujua ni kwa kiwango gani unaathi&#341;i vibaya mikakati yetu ya maendeleo na hili ni jambo &#8230; ambalo tunadhani litaingizwa katika kanda nyingine wakati wakifanya kazi ya kuhitimisha mikataba yao,&#8221; balozi wa nchi hiyo mjini B&#341;ussels Dk. P.I. Gomes aliiambia IPS.<\/p>\n<p>Katika &#341;ipoti yake kwa mkutano hapa, ukanda wa Pasifiki umeelezea mazungumzo hayo na Ulaya ambayo yalianza mwaka 2004 kama &#8220;mchakato m&#341;efu na wenye changamoto nyingi&#8221;.<\/p>\n<p>Wazi&#341;i wa Kazi, Biasha&#341;a na Viwanda wa Tonga Isieli Pulu, msemaji mkuu wa kambi ya Pasifiki, alisema kuwa wakati mataifa mawili ya Pasifiki yalisaini mikataba ya muda mfupi ya EPA &ndash; hasa kwa ajili ya kuzuia vikwazo vya masoko &ndash; ma&#341;a zote imeeleweka kuwa mikataba ya muda mfupi &#8220;ingekuwa mwanzo wa kuelelekea kwenye mikataba kamili ya EPA&#8221;.<\/p>\n<p>Mkataba wa Cotonou uliosainiwa mwaka 2000 unaingiza mpango wa ushi&#341;ikiano wenye nia ya kufanya biasha&#341;a kuwa hu&#341;ia kati ya mataifa ya ACP na EU, na pia kuelezea kuwa mpango mpya wa ukubalifu wa Shi&#341;ika la Biasha&#341;a Duniani (WTO) au EPA lazima kukubaliwa ifikapo mwishoni mwa mwaka 2007.<\/p>\n<p>Pulu alisema kuwa mataifa ya Pasifiki yamethibitisha nia yao na viongozi wao wamewapatia mamlaka &#8220;kuwa tunaendelea na mazungumzo ya mkataba kamili wa EPA kama ukanda mmoja na Umoja wa Ulaya ambao utakamilika mwaka 2012.<\/p>\n<p>Lakini alisema dhami&#341;a hii imefanywa, ila kambi ya Pasifiki inataka EPA &#8220;inayojikita kwenye kanuni a malengo yaliyopo katika Mkataba wa Cotonou&#8221; na kuwa &#8220;lazima kwenda mbali zaidi ya mipangilio ya kuingiza bidhaa katika masoko na kuingiza makubaliano ya kibiasha&#341;a na ushi&#341;ikiano wa kimaendeleo ambao utakuwa msingi wa maelezo ya ushi&#341;ikiano wa ukweli, wenye nguvu na wa kimkakati kwa muda m&#341;efu kati ya ukanda wa ACP wa Pasifiki na Umoja wa Ulaya&#8221;.<\/p>\n<p>Pulu ameituhumu Ulaya kwa &#8220;kusimamisha&#8221; mchakato, akibainisha kuwa imekuwa &#8220;ikiahi&#341;isha mikutano ya mazungumzo na ukanda wa Pasifiki tangu mwaka 2009.<\/p>\n<p>&#8220;Zaidi ya hapo hawajatoa majibu ya mapendekezo ya Pasifiki na suala zima la kutoa fu&#341;sa ya kuingiza bidhaa kwenye masoko yaliyowasilishwa Julai mwaka 2011. Hii imetishia kwa kiasi kikubwa uwezekano wa kuhitimisha mazungumzo juu ya mikataba kamili ya EPA kama ilivyotakiwa na viongozi wa ukanda wa ACP ya Pasifiki. Badala yake, Tume yaUlaya imekuwa ikishinikiza ukanda wa ACP ya Pasifiki kukubali mikataba ya muda mfupi ya EPA,&#8221; Pulu aliuambia mkutano.<\/p>\n<p>Alisema ucheleweshaji umepunguza uwezekano wa mataifa kadhaa ya Pasifiki yaliyokuwa yakitaka kuhitimisha &#8220;mikataba ya kibiasha&#341;a yenye faida kwao&#8221; na Ulaya hasa kutokana na ugumu wa mapendekezo ya tume ya kufanyia ma&#341;ekebisho she&#341;ia za masoko ya EU.<\/p>\n<p>&#8220;Katika ukanda wa Pasifiki, Fiji ingeweza kulazimishwa ku&#341;idhia mkataba wa muda mfupi wa EPA kama ukanda huo usingeweza kuhitimisha kiasi cha ku&#341;idhisha mkataba kamili wa EPA ifikapo mwaka 2014. Sekta kubwa nchini Fiji zingeathi&#341;ika vibaya na zingeweza kuanguka kwani zinategemea mpango wa upendeleo wa kuingiza bidhaa katika soko la Ulaya,&#8221; alisema.<\/p>\n<p>Kwa upande wake, mataifa ya Kiaf&#341;ika, yaliyojipanga chini ya vyombo kadhaa, pia yemeonyesha wasiwasi wao.<\/p>\n<p>Kwa mfano, Af&#341;ika ya Kati, imeelezea kuwa nchi tatu &ndash; Came&#341;oon, Guinea ya Ikweta na Gabon &ndash; wana madai maalum kuhusu ushi&#341;ikiano na Umoja wa Ulaya.<\/p>\n<p>Came&#341;oon, ambayo ilisaini mkataba wa muda mfupi mwaka 2009 kama ilivyopendekezwa na Ulaya kulinda soko la bidhaa zake katika Umoja wa Ulaya, lakini bado haija&#341;idhia mkataba huo, na imeambiwa kuwa itapewa adhabu kwa kuondolewa fu&#341;sa ya kuingiza bidhaa katika soko la Ulaya ifikapo Janua&#341;i mwaka 2014. Uamuzi wa kanuni za kuondoa fu&#341;sa ya soko unatumika kwa mataifa yote ambayo ni wasaini wa mikataba ya muda mfupi ya EPA ambayo hayaja&#341;idhia mikataba hiyo, maofisa wa ACP waliiambia IPS.<\/p>\n<p>Kwa upande wa Guinea ya Ikweta, inakabiliwa na vikwazo vya kifedha katika baadhi ya mi&#341;adi ya kikanda chini ya Mfuko wa 10 wa Umoja wa Ulaya (EDF) kutokana na kushindwa ku&#341;idhia kikamilifu wa&#341;aka wa kwanza ulio&#341;ekebishwa wa Mkataba wa Cotonou wa Juni 2005.<\/p>\n<p>Kutokana na kuongezeka kwa &#341;asilimali zake, nchi hiyo hivi ka&#341;ibuni itahitimu kutoka katika mataifa ya LDC (kambi ya nchi zenye maendeleo duni) na kuingia katika nchi yenye kipato cha kati, kwa mujibu wa mgawanyo wa Umoja wa Mataifa, mkutano wa mawazi&#341;i wa ACP uliambiwa.<\/p>\n<p>Gabon, ambayo taya&#341;i inajulikana kama taifa la kipato cha kati cha juu&#8221;, ingeweza kuona mpango wa Mfumo wa Upendeleo wa Jumla Af&#341;ika (GSP) ukiondolewa, huku taifa la Af&#341;ika ya Kati likibainisha kuwa &#8220;kwa uhakika GSP, ambao ni mpango usiokuwa na mjadala, unaendelea kutumiwa kwa maslahi ya upande wa Ulaya&#8221;.<\/p>\n<p>Jumuiya ya Af&#341;ika Masha&#341;iki, ambayo inazihusu nchi kama Kenya, Tanzania na Somalia, wanasema wamebaini &#8220;kwa wasiwasi mkubwa kuwa washi&#341;ika wetu wanaonekana kuingiza ta&#341;ehe zisizoweza kufikiwa za mwisho wa kuhitimisha mazungumzo na wamekwenda mbali kupendekeza ma&#341;ekebisho ya kanuni za kuingiza bidhaa katika soko la EC ambazo zitanyima kundi la mataifa 18 upendeleo wa kuingiza bidhaa katika soko la EU kuanzia Janua&#341;i 1, 2014 kama watakuwa hawaja&#341;idhia mikataba ya EPAs.<\/p>\n<p>&#8220;Tunaiona hatua hii kama ambayo siyo tu inaongeza shinikizo lisilokubalika katika mchakato mzima wa mazungumzo yanayoendelea ya EPA na hivyo uwezekano wa kutokufikia hitimisho la mkataba wenye uwezo wa kufikia malengo lakini pia itaathi&#341;i ushi&#341;ikiano wetu wa kikanda,&#8221; EAC iliongeza.<\/p>\n<p>Mataifa 16 ya Af&#341;ika Magha&#341;ibi na yale yanayohusu ukanda wa Masha&#341;iki mwa Kusini mwa Af&#341;ika (ESA) pia yamekuwa na wasiwasi unaofanana.<\/p>\n<p>Mataifa ya Af&#341;ika Magha&#341;ibi ambayo ni pamoja na Ghana na Nige&#341;ia, yanasema msimamo wa EU wa kutokushi&#341;ikisha mataifa ambayo yamehitimisha mikataba ya EPA, lakini hayaja&#341;idhia mikataba hiyo, unalazimu ukanda kuangalia suala hilo kama &#8220;kuna ufumbuzi mwingine&#8221;. <\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>PORT VILA, Vanuatu, Septemba, 4 (IPS) &ndash; Yakiwa yamebanwa kati ya mwamba na mahali pagumu, mataifa ya Af&#341;ika na Pasifiki bado hayana uhakika kama yafuate wenzao wa Ca&#341;ibbean na kusaini Mkataba wa Ushi&#341;ikiano wa Kiuchumi na Ulaya (EPA). Mawazi&#341;i wa kambi ya Af&#341;ika, Ca&#341;ibbean na Pasifiki (ACP) wanakutana hapa kabla ya mkutano wa pamoja wa&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":937,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-3911","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3911","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/937"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=3911"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3911\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=3911"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=3911"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=3911"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}