{"id":3909,"date":"2012-09-04T13:40:01","date_gmt":"2012-09-04T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2012\/09\/04\/wakimbizi-wa-sudan-wafaiki-dunia-kwa-kiu\/"},"modified":"2012-09-04T13:40:01","modified_gmt":"2012-09-04T13:40:01","slug":"wakimbizi-wa-sudan-wafaiki-dunia-kwa-kiu","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2012\/09\/04\/wakimbizi-wa-sudan-wafaiki-dunia-kwa-kiu\/","title":{"rendered":"Wakimbizi wa Sudan Wafa&#341;iki Dunia Kwa Kiu"},"content":{"rendered":"<p>JUBA, Septemba, 4 (IPS) &ndash; Wakimbizi wa Sudan wameanza kufa kutokana na kambi Kusini mwa Sudan kukosa maji kwa siku nne baada ya kuongezeka kwa watu walioingia kambini humo waliovuka mpaka kukimbia vita na njaa.\n<\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>Wakimbizi wanakimbia Jimbo la Blue Nile nchini Sudan ambapo wapiganaji wa waasi wanapambana kuipindua se&#341;ikali ya Sudan.<\/p>\n<p>Shi&#341;ika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch (HRW) lilisema mapema mwezi Ap&#341;ili kuwa &#341;aia wanateseka zaidi kutokana na kampeni ya mashambulizi ya anga yasiyochagua mahali pa kupiga.<\/p>\n<p>Voitek Asztabski, m&#341;atibu wa dha&#341;ula wa shi&#341;ika la Madakta&#341;i Wasiokuwa na Mipaka yaani Medicines Sans F&#341;ontie&#341;s (MSF), alisema baadhi ya wakimbizi walikufa wakati wakitembea kwa masaa saba hadi 10 kuelekea kwenye eneo jingine kutafuta maji baada ya kambi yao ya Kilomete&#341; 48 katika jimbo la Uppe&#341; Nile katika Sudan Kusini kukosa maji Juni 11.<\/p>\n<p>Shi&#341;ika bado linafanya utafiti wa waliokufa kujua ni watu wazima wangapi na watoto wangapi wamefa&#341;iki na sababu halisi za vifo. Hata hivyo, MSF inakadi&#341;ia kuwa wastani wa watu watano hadi 10 wamekuwa wakifa kila siku tangu maji yalipoadimika katika kambi ya Kilomete&#341; 48.<\/p>\n<p>MSF ilisema katika taa&#341;ifa yake Juni 13 kuwa &#8220;wakimbizi 15,000 waliobaki katika kambi walitembea kwa wingi kwa kilomita 25 hadi eneo la ka&#341;ibu lililokuwa na maji.&#8221;<\/p>\n<p>Mvua kubwa ilizuia mashi&#341;ika kuwasafi&#341;isha kwa maga&#341;i katika ba&#341;aba&#341;a zenye ma&#341;ufiko.<\/p>\n<p>&#8220;Tuliwaona watu wakifa kwa kiu na kukaukiwa maji mwilini,&#8221; Asztabski alisema kwa kutumia simu ya satelaiti kutoka kambi ya Kilomete&#341; 18, eneo jipya lenye kiasi kidogo cha maji. &#8220;Hilo ni tukio la kutisha ambalo tunalishuhudia hapa.&#8221;<\/p>\n<p>Baadhi ya watu walikuwa dhaifu mno kuweza kupona kutokana na kupatiwa tiba.<\/p>\n<p>&#8220;Tulikwenda mapema asubuhi siku ya Jumanne kuwapatia msaada wa kitabibu na kuwaongezea maji mwilini wakiwa njiani,&#8221; alisema Dk wa MSF E&#341;na Rijnie&#341;se katika taa&#341;ifa yake.<\/p>\n<p>&#8220;Ni mazingi&#341;a ya kutisha kwani tulishuhudia baadhi ya waliodhoofu zaidi wakifa wakiwa wanatembea &ndash; kutokana na kukaukiwa na maji mwilini kiasi ambacho huduma ya ha&#341;aka ya tiba isingeweza kuwaokoa.&#8221;<\/p>\n<p>Kwa sasa kuna wakimbizi 105,000 wa Sudan kutoka jimbo la Blue Nile katika jimbo la Uppe&#341; Nile nchini Sudan Kusini, kwa mujibu wa shi&#341;ika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR, wakati wengine 15,000 wako njiani.<\/p>\n<p>Asztabski alisema kuwa wakimbizi wanawasili wakiwa hawajapata chakula kwa muda m&#341;efu, wakiwa wana upungufu wa maji mwilini na wagonjwa kutokana na kutembea umbali m&#341;efu kutoka makazi yao ya Blue Nile. Mazingi&#341;a ya kawaida ni pamoja na ugonjwa wa mapafu wa neumonia na maambukizi mengine ya koo waliyoyapata baada ya kulala nje bila ya malazi yoyote, ikiwa ni pamoja na kuha&#341;a kutokana na kunywa maji yenye vimelea vya magonjwa.<\/p>\n<p>Alitoa wito wa kuwa na mipango ya kabla ya jinsi ya kushughulikia mgogo&#341;o huo, akisema kuwa mashi&#341;ika yamekuwa yakikabiliana na dha&#341;ula bila ya kuwa na mipango ya jinsi ya kukabiliana nayo. Kwa mfano, hakuna mpango wa nini cha kufanya baada ya kambi ya Kilomete&#341; 18 kukosa maji, jambo ambalo lina uwezekano wa kujitokeza tena katika kipindi cha wiki mbili na nusu.<\/p>\n<p>Mashi&#341;ika ya misaada yamekuwa yakitoa tahadha&#341;i kuwa wakimbizi walihitaji kuhamishwa kabla maji hayajakauka na maji&#341;a ya mvua hayajaanza na kufanya usafi&#341;i kuwa mgumu. Mwezi Machi, And&#341;ew Omale, m&#341;atibu wa dha&#341;ula wa shi&#341;ika la misaada la Oxfam Inte&#341;national, aliiambia IPS kuwa hali ya wakimbizi katika jimbo la Uppe&#341; Nile ni &#8220;dha&#341;ula iliyosahaulika&#8221; na kutoa wito wa kutolewa kwa msaada zaidi.<\/p>\n<p>Asztabski alisema mashi&#341;ika yanaendelea kukabiliwa na kukosa uwezo na &#341;asilimali. Alilinganisha ukubwa wa mgogo&#341;o huo na eneo la Ethiopia ambako alikuwa akifanya kazi mwaka jana wakati njaa nchini Somalia ilipopelekea wakimbizi kukimbilia mpakani mwa nchi hiyo ikiwa ni pamoja na Kenya. Watu wapatao milioni 10 waliathi&#341;ika na ukame katika Pembe ya Af&#341;ika. Lakini alisema kuna &#341;asilimali chache zilizopo kukabiliana na dha&#341;ula hii.<\/p>\n<p>&#8220;Kila mmoja amezidiwa na hali hii,&#8221; alisema Asztabski. &#8220;Mgogo&#341;o huu unahitaji kuangaliwa zaidi, uwekezaji zaidi.&#8221;<\/p>\n<p>Wakimbizi walianza kumiminika kutoka Blue Nile kuingia Sudan Kusini na Ethiopia mapema Septemba baada ya Sudan kumpindua gavana aliyechaguliwa katika jimbo la Blue Nile, Malik Aga&#341;, na nafasi yake kuchukuliwa na mteule wa jeshi. Aska&#341;i wa Aga&#341; wamekuwa wakipambana na se&#341;ikali tangu wakati huo, na HRW inasema &#341;aia wasiokuwa na hatia wameathi&#341;ika zaidi na ukatili wa jeshi.<\/p>\n<p>Katika taa&#341;ifa yake ya Ap&#341;ili, HRW ili&#341;ipoti ukiukwaji wa haki za binadamu kuwa ni pamoja na kuweka watu kizuizini bila makosa, mauaji, kupigwa na kuteswa. HRW ilisema vikosi vya se&#341;ikali vililenga watu walioshukiwa kuwa na uhusiano na kundi la waasi linaloongozwa na Aga&#341;, ambalo linajulikana kama Sudan Peoples Libe&#341;ation Movement&ndash;No&#341;th (SPLM&ndash;N).<\/p>\n<p>Waasi wa SPLM&ndash;N wanaendesha ope&#341;esheni zao katika jimbo la Blue Nile ikiwa ni pamoja na jimbo la ji&#341;ani la Ko&#341;dofan ya Kusini, ambako Umoja wa Mataifa unasema wakimbizi 47,000 wamevuka mpaka na kuingia jimbo la Unity katika Sudan Kusini.<\/p>\n<p>Hapo awali waasi hao walikuwa sehemu ya SPLM, ambao walipigana kwa miongo miwili katika vita vya wenyewe kwa wenyewe dhidi ya Kha&#341;toum ambavyo vilisababisha kujitenga kwa Sudan Kusini. Wakati Kusini ilijitangazia uhu&#341;u Julai mwaka jana, waasi wa SPLM katika majimbo ya Ko&#341;dofan ya Kusini na Blue Nile waliongeza &#8220;No&#341;th&#8221; katika jina lao na kujitangaza kuwa chama tofauti cha kisiasa nchini Sudan. Lakini SPLM&ndash;N ilianza kubeba silaha kupambana baada ya kuituhumu Kha&#341;toum kuwakandamiza.<\/p>\n<p>Sudan ime&#341;ejea tena na tena kukanusha kuwalenga &#341;aia katika mapigano yake dhidi ya SPLM&ndash;N. Lakini mashi&#341;ika ya haki za binadamu ikiwa ni pamoja na se&#341;ikali za Uinge&#341;eza na Ma&#341;ekani yametoa wito kwa Kha&#341;toum kusitisha mashambulizi yake dhidi ya &#341;aia.<\/p>\n<p>Asztabski alisema wakimbizi pia walielezea kukimbia mashambulizi huku wakiwa na mali chache mno na kuwafanya kutembea kwa miezi miwili kufika mpakani. &#8220;Wanatuambia haba&#341;i zinazotisha,&#8221; alisema. &#8220;Ni safa&#341;i mbaya mno na inayochosha.&#8221; <\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>JUBA, Septemba, 4 (IPS) &ndash; Wakimbizi wa Sudan wameanza kufa kutokana na kambi Kusini mwa Sudan kukosa maji kwa siku nne baada ya kuongezeka kwa watu walioingia kambini humo waliovuka mpaka kukimbia vita na njaa. Wakimbizi wanakimbia Jimbo la Blue Nile nchini Sudan ambapo wapiganaji wa waasi wanapambana kuipindua se&#341;ikali ya Sudan. Shi&#341;ika la Kutetea&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":911,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-3909","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3909","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/911"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=3909"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3909\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=3909"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=3909"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=3909"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}