{"id":3906,"date":"2012-09-04T13:40:01","date_gmt":"2012-09-04T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2012\/09\/04\/wakimbizi-wa-hali-ya-hewa-ni-suala-la-uhakika-leo-hii-climate-refugees-todays-new-reality\/"},"modified":"2012-09-04T13:40:01","modified_gmt":"2012-09-04T13:40:01","slug":"wakimbizi-wa-hali-ya-hewa-ni-suala-la-uhakika-leo-hii-climate-refugees-todays-new-reality","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2012\/09\/04\/wakimbizi-wa-hali-ya-hewa-ni-suala-la-uhakika-leo-hii-climate-refugees-todays-new-reality\/","title":{"rendered":"Wakimbizi wa Hali ya Hewa: Ni Suala la Uhakika Leo Hii  &ndash; Climate Refugees &ndash; Today&#8217;s New Reality*"},"content":{"rendered":"<p>RIO DE JANEIRO, Septemba 4, (IPS) &ndash; Kuendelea kukimbia kwa wakimbizi wa Somalia kuingia nchini Kenya na Ethiopia kumezua mjadala juu ya suala jipya linalotia wasiwasi duiani: wakimbizi wa hali ya hewa, ambao wanaondoka majumbani mwao na kuvuka mipaka kutokana na matukio ya mabadiliko makubwa ya hali ya hewa.\n<\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>Kukimbia kwa wingi kwa watu katika baadhi ya maeneo ya Af&#341;ika, hususani sehemu ya masha&#341;iki mwa ba&#341;a hili, kunasababishwa na vipindi vi&#341;efu vya ukame, njaa na vita. Moja ya ufafanuzi wa jambo hili ni ma&#341;ufiko makubwa ya watu ambao waliondoka nchini Somalia tangu mwishoni mwa mwaka 2010. Suala hilo limesababisha Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Shi&#341;ika la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), kuzindua &#341;ipoti ya &#8220;Mabadiliko ya Tabia Nchi, Atha&#341;i na Kukimbia kwa Binadamu&#8221; katika Mkutano wa Hali ya Hewa wa Rio+20 siku ya Alhamisi ya Juni 21.<\/p>\n<p>Mashi&#341;ika ya kijamii yamekatishwa tamaa mno na matokeo ya &#341;ipoti ya Mkutano wa Maendeleo Endelevu wa Umoja wa Mataifa, au Rio+20, ambao ulikusanya wakuu wa nchi kutoka nchi 130 duniani kote mjini Rio de Janei&#341;o na kuhitimishwa Ijumaa ya Juni 22.<\/p>\n<p>Ripoti ya UNHCR, iliyowasilishwa katika ukumbi wa mikutano wa Riocent&#341;o, imejikita katika ushahidi wa watu binafsi 150 ambao ni wakimbizi na watu waliokimbilia katika makambi ya ndani nchini Ethiopia na Uganda, na inatathmini mwelekeo wa kimataifa wa watu waliolazimika kuyakimbia makazi yao na uhusiano wao na mabadiliko ya tabia nchi na majanga ya asili.<\/p>\n<p>Idadi inayozidi kuongezeka ya wakimbizi wa mabadiliko ya tabia nchi inaleta suala la uha&#341;aka wa kushughulikia masuala ya jinsi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na jinsi ya kuishi katika mabadiliko hayo katika maeneo ya dunia ambayo yameathi&#341;ika zaidi na hali hiyo, kama vile Af&#341;ika.<\/p>\n<p>Waandamanaji duniani kote waliingia mitaani wakati wa Wiki ya Wakimbizi Duniani Juni 20 na kudai kuwa jumuiya ya kimataifa inatakiwa kuchukua hatua zaidi kukabiliana na tatizo la kibinadamu linalozidi kuongezeka.<\/p>\n<p>Ripoti iliyowasilishwa na Kamishina wa Wakimbizi wa Umoja wa Mataifa Ant&oacute;nio Gute&#341;&#341;es ilitolewa na Taasisi ya Umoja wa Mataifa ya Chuo Kikuu cha Mazingi&#341;a na Usalama wa Binadamu kwa kushi&#341;ikiana na UNHCR, Shule ya Uchumi ya London (LSE) na Chuo Kikuu cha Bonn.<\/p>\n<p>Mhadhili wa Chuo cha Umoja wa Mataifa, Kon&#341;ad Oste&#341;walde&#341;, alisema &#8220;Ripoti inaonyesha jinsi gani ilivyo kuwa muhimu kuelewa uzoefu halisi wa watu &#341;ahisi kuathi&#341;ika na mabadiliko ya taifa nchi leo hii.&#8221;<\/p>\n<p>&#8220;Ripoti hii inathibitisha kile ambacho tumekuwa tukikisikia miaka mingi kutoka kwa wakimbizi,&#8221; alisema Gute&#341;&#341;es. &#8220;Walifanya kila kitu walichoweza kubakia nyumbani, lakini wakati mazao yao ya mwisho yaliposhindwa, mifugo yao ilipokufa, hawakuwa na chaguo lakini kukimbia; safa&#341;i ambazo ma&#341;a nyingi zilisababisha kuingia katika hali mbaya wakiwa mbali.<\/p>\n<p>&#8220;Ninashawishika kuwa mabadiliko ya tabia nchi yatasababisha zaidi mgogo&#341;o mbaya zaidi wa kukimbia makazi duniani. Ni muhimu mno kwa dunia kuja pamoja kukabiliana na changamoto hii,&#8221; alisema.<\/p>\n<p>Msemaji wa UNHCR nchini B&#341;azil Luiz Fe&#341;nando Godinho aliuambia mtandao wa Te&#341;&#341;aViva kuwa pamoja na kwamba hakuna fasili ya wazi ya nini maana halisi ya &#8220;mkimbizi wa hali ya hewa&#8221;, jambo ambalo ni muhimu kuelewa ni kwamba hali ya mabadiliko ya tabia nchi inasababisha watu wengi zaidi kukimbia makazi na nchi zao.<\/p>\n<p>&#8220;UNHCR imetoa wito kwa Rio+20 kuwa macho zaidi na kuwepo kwa wakimbizi ambao wamekimbia makazi yao kutokana na mabadiliko makubwa ya hali ya hewa,&#8221; alisema. &#8220;Jumuiya ya kimataifa haijaweza kuja na hatua au makubaliano kutoa uhakika wa kuishi kwa watu ambao wanakimbia makazi yao kutokana na majanga ya asili.&#8221;<\/p>\n<p>Kuna baadhi ya watu milioni 15 ambao ni wakimbizi duniani kote leo hii, milioni 10 kati yao ni wakimbizi chini ya UNHCR. Lakini haiwezekani kujua ni wangapi kati yao walikimbia kutokana na majanga ya asili na hali inayotokana na mabadiliko ya tabia nchi.<\/p>\n<p>Nchini Somalia pekee, ambayo ina theluthi ya wakazi walioyakimbia makazi yao duniani, ina wakimbizi milioni 1.1 wanaoishi katika nchi za ji&#341;ani, ma&#341;a tatu zaidi ya jumla ya wakimbizi wa mwaka 2004. Walikimbia nchi yao kutokana na sababu mchaganyiko za vita, ukame na njaa.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>RIO DE JANEIRO, Septemba 4, (IPS) &ndash; Kuendelea kukimbia kwa wakimbizi wa Somalia kuingia nchini Kenya na Ethiopia kumezua mjadala juu ya suala jipya linalotia wasiwasi duiani: wakimbizi wa hali ya hewa, ambao wanaondoka majumbani mwao na kuvuka mipaka kutokana na matukio ya mabadiliko makubwa ya hali ya hewa. Kukimbia kwa wingi kwa watu katika&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":936,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-3906","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3906","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/936"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=3906"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3906\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=3906"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=3906"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=3906"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}