{"id":3902,"date":"2012-08-23T13:40:01","date_gmt":"2012-08-23T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2012\/08\/23\/vifo-vya-watoto-wanaozaliwa-vyaonyesha-jinsi-bajeti-ya-india-ilivyokuwa-ndogo-2\/"},"modified":"2012-08-23T13:40:01","modified_gmt":"2012-08-23T13:40:01","slug":"vifo-vya-watoto-wanaozaliwa-vyaonyesha-jinsi-bajeti-ya-india-ilivyokuwa-ndogo-2","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2012\/08\/23\/vifo-vya-watoto-wanaozaliwa-vyaonyesha-jinsi-bajeti-ya-india-ilivyokuwa-ndogo-2\/","title":{"rendered":"Vifo vya Watoto Wanaozaliwa Vyaonyesha Jinsi Bajeti ya India Ilivyokuwa Ndogo"},"content":{"rendered":"<p>SRINAGAR, India, Agosti 23 (IPS) &ndash; Mwaka baada ya se&#341;ikali ya India kuanza kuwalipa wanawake wajawazito ili kujifungulia watoto wao katika hospitali za se&#341;ikali, shinikizo la wingi wa watu linaonekana katika hospitali za nchini humo ambazo hazina wafanyakazi wa kutosha na vifaa.\n<\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>Kati ya Feb&#341;ua&#341;i na Mei, watoto wachanga 397 walifa&#341;iki dunia katika hospitali ya G.B. Pant jijini humo, mji wa mapumziko wakati wa maji&#341;a ya joto wa kaskazini mwa Jammu na jimbo la Kashmi&#341;, na hivyo kuonyesha mapungufu ya hospitali za se&#341;ikali nchini humo.<\/p>\n<p>&#8220;Mtoto wangu aligeuka &#341;angi na kuwa wa kahawia ma&#341;a tu baada ya muuguzi kumpiga sindano na kufa&#341;iki hapo hapo,&#8221; Haleema Akhta&#341;, mama aliyekuwa na uchungu aliiambia IPS.<\/p>\n<p>&#8220;Niliona idadi kadhaa ya watoto wakifa&#341;iki mbele ya macho yangu kwa muda wa masaa machache tu. Mazingi&#341;a ya hospitali siyo ya utu. Tungekuwa na uwezo tungeenda hospitali za binafsi,&#8221; Akhta&#341; aliyetokwa na machozi aliiambia IPS.<\/p>\n<p>Uchunguzi wa se&#341;ikali wa vifo hivyo uliofanywa na Dk. Showkat Za&#341;ga&#341;, dakta&#341;i maa&#341;ufu na katibu mkuu wa zamani wa se&#341;ikali ya jimbo, ulisema vilisababishwa na uhaba wa wafanyakazi na vifaa.<\/p>\n<p>&#8220;Kuna usimamiaji mbovu wa utawala wa hospitali,&#8221; Za&#341;ga&#341; alisema katika &#341;ipoti yake.<\/p>\n<p>&#8220;Ni mwanafunzi mmoja wa shahada ya uzamili na muugizi mwenye mafunzo walikuwa wakiangalia watoto wagonjwa kwa uka&#341;ibu. Nilihesabu watoto wachanga 27 ambao hawakuwa na madakta&#341;i wa kuwashughulikia katika kitengo cha uangalizi wa ka&#341;ibu wa watoto wachanga,&#8221; Za&#341;ga&#341; ali&#341;ipoti.<\/p>\n<p>Ikitoa mfano wa &#341;ikodi za hospitali, &#341;ipoti ilisema kuwa hospitali zimeshuhudia vifo 981 vya watoto wachanga mwaka 2010 na 985 mwaka 2011, wastani wa asilimia 20 ya vifo &ndash; ma&#341;a mbili ya kiwango kinachokubalika katika hospitali za se&#341;ikali nchini India.<\/p>\n<p>Kamati nyingine ya wabunge kutoka Jammu na Kashmi&#341; ilikusanyika kuthibitisha matokeo ya Za&#341;ga&#341;. Mustafa Kamal, mjumbe wa kamati ya bunge ya jimbo, aliiambia IPS &#8220;vifo vilijitokeza kutokana na kukosekana kwa vifaa, uhaba wa wafanyakazi na mfumo mbaya katika hospitali.&#8221;<\/p>\n<p>Kiwango cha vifo vya watoto wachanga katika hospitali ya G.B. Pant kilionyesha hali kama hiyo katika hospitali ya wilaya ya Malda, katika jimbo la Bengal Magha&#341;ibi, mwezi Novemba 2011. Zaidi ya watoto 26 walifa&#341;iki katika kipindi cha wiki mbili kutokana na maambukizi.<\/p>\n<p>Mwezi Machi 20, wazi&#341;i wa afya wa India Ghulam Nabi Azad, aliitwa kutoa &#341;ipoti mbele ya Bunge, na kukubali kuwa kiwango cha vifo vya watoto wachanga wa India (chini ya mwaka mmoja) ni asilimia 47 kwa kila watoto 1,000 wanaozaliwa wakiwa hai na hali hiyo kuwa mbaya zaidi ya mataifa ji&#341;ani ya Nepal, S&#341;i Lanka na Bangladesh.<\/p>\n<p>&#8220;Nchini India, vjfo vya watoto wachanga ni asilimia 47 kwa kila watoto 1,000 wanaozaliwa wakiwa hai, ambao ni sawa na vifo vya watoto wachanga milioni 1.25 kwa mwaka,&#8221; Azad alisema. Ni taifa la Pakistan ambalo lina kiwango kibaya zaidi cha vifo vya watoto wachanga katika ukanda wa Kusini mwa Asia, alisema.<\/p>\n<p>Ripoti iliyotolewa Juni 13 na Shi&#341;ika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) kama sehemu ya kuelekea kwenye &#8216;Miaka ya Kutimiza Malengo ya Milenia mwaka 2015&#8217; iliiweka India katika kiwango cha juu zaidi cha vifo vya watoto wachanga katika watoto 48 kwa kila watoto 1,000 wanaozaliwa wakiwa hai. Mpango huo unafuatilia maendeleo ya nchi kwa kuangalia mafanikio katika kupunguza vifo vya uzazi, vifo vya watoto wachanga na watoto wadogo na unahusisha washi&#341;ika mbalimbali.<\/p>\n<p>Kwa mujibu wa &#341;ipoti ya UNICEF, Pakistan ina kiwango cha juu zaidi cha vifo vya watoto wachanga katika watoto 70 kwa kila watoto 1,000 wanaozaliwa wakiwa hai, ikifuatiwa na India yenye watoto 47, Nepal watoto 41, Bangladesh watoto 38 na S&#341;i Lanka watoto 26.<\/p>\n<p>Ripoti ya UNICEF ilisema kuwa vifo hivi vingi vinazuilika kwa kupata huduma za afya kabla, wakati wa kuzaliwa na ma&#341;a tu baada ya kuzaliwa kwa mtoto.<\/p>\n<p>Kwa upande wa Jammu na Kashmi&#341;, kwa mujibu wa takwimu za se&#341;ikali zilizopatikana kwa IPS, kuna madakta&#341;i wa watoto 24 tu wanaohudumia zaidi ya watoto milioni wenye um&#341;i wa chini ya miaka sita.<\/p>\n<p>Chama cha Madakta&#341;i cha Kashmi&#341; (DAK) kinasema kuwa hospitali nyingi siyo tu kwamba zinakosa wataalam wa magonjwa ya watoto lakini pia vifaa vya msingi vya kuokoa maisha kama vile vifaa vya kuingiza hewa. &#8220;Hakuna dakta&#341;i anayeweza kufanya kazi bila ya kuwa na miundombinu ya msingi ya afya,&#8221; &#341;ais wa DAK Nissa&#341;&ndash;ul&ndash;Hassan aliiambia IPS.<\/p>\n<p>Katika jitihada za kupunguza kiwango cha vifo vya watoto wachanga, se&#341;ikali ilizindua mpango wa Janani&ndash;Shishu Su&#341;aksha Ka&#341;yak&#341;am (JSSK) Juni 2011, ambao una lengo la kulinda maisha ya mama na watoto wachanga wanaozaliwa, kwa kutoa huduma kadhaa bu&#341;e kwa mama wajawazito katika hospitali za se&#341;ikali nchini kote.<\/p>\n<p>Huduma za bu&#341;e katika mpango wa JSSK ni pamoja na kujifungua kwa kawaida au kwa upasuaji, huduma za matunzo na kupatiwa mlo mzu&#341;i kwa akina mama hadi siku 30 baada ya kujifungua pamoja na usafi&#341;i wa bu&#341;e kutoka majumbani kwao kwenda hospitali na ku&#341;udi.<\/p>\n<p>Sampuli ya mfumo wa usajili (SRS) uliofanywa mwaka 2010 na Msajili Mkuu wa India ulionyesha kuwa mipango ya kuwafanya wanawake wajawazito kupata huduma za wataalam taya&#341;i unafanyika katika mazingi&#341;a ya kitaasisi.<\/p>\n<p>Lakini kuna tofauti kubwa jinsi mipango yenye nia ya kupunguza vifa vya watoto wachanga inavyotekelezwa katika nchi yenye wakazi bilioni 1.2 wanaoishi katika majimbo 27 katika mazingi&#341;a yanayotofautiana.<\/p>\n<p>Wakati majimbo kama ya Ke&#341;ala, Tamil Nadu na Andh&#341;a P&#341;adesh yali&#341;ikodi chini ya asilimia moja ya uzazi uliofanywa na wakunga wasiokuwa na ujuzi, jimbo la Jha&#341;khand katikati mwa India bado lina asilimia 46.5 ya uzazi unaoendeshwa na wakunga wa jadi wasiokuwa na maa&#341;ifa.<\/p>\n<p>Wanaha&#341;akati maa&#341;ufu wa afya wanakubali mipango kama ya JSSK lakini wanasema se&#341;ikali inahitaji kutumia mipango mingi kama hiyo kufikia Lengo la Maendeleo la Milenia (MDG) la kupunguza kiwango cha vifo vya watoto wachanga kwa theluthi mbili, kati ya mwaka 1990 na 2015.<\/p>\n<p>Dk. Mi&#341;a Shiva, m&#341;atibu wa shi&#341;ika lisilokuwa la kise&#341;ikali la &#8220;Health, Equity and Society&#8221;, anaelezea ukweli kwamba matumizi ya India katika afya yalikuwa ni asilimia sita ya GDP mwaka 1991, na kwa sasa yamepunguzwa hadi kufikia juu kidogo ya asilimia moja ya GDP mwaka 2011.<\/p>\n<p>&#8220;Kwa asili, kupungua kwa kiasi hicho kwa GDP kumesababisha atha&#341;i katika mfumo wa utoaji wa huduma za afya &ndash; hivyo siyo &#341;ahisi kuwapeleka wanawake wajawazito hospitali,&#8221; alisema Shiva ambaye yupo katika kamati kadhaa za afya.<\/p>\n<p>Mwezi Feb&#341;ua&#341;i, se&#341;ikali ilitangaza kuwa ifikapo mwishoni mwa mpango wa 12 wa India wa miaka mitano mitano, ambao utaweza kuanza kufanya kazi mwaka huu, matumizi katika afya yataongezeka hadi asilimia 2.5 ya GDP &ndash; na kufika dola t&#341;ilioni 1.67 mwaka 2011.<\/p>\n<p>Lakini Shiva alisema bado India inatakiwa kufanya kazi hadi kufikia chini ya nusu ya kile ambacho mataifa mengi yenye hali ya uchumi kama ya kwao India, kama vile B&#341;azil, yanatumia katika sekta ya afya.<\/p>\n<p>Kwa mujibu wa &#341;ipoti ya Benki ya Dunia ya mwaka 2010, matumizi ya afya ya umma nchini B&#341;azil yalikuwa asilimia 3.72 ya GDP mwaka 2008 lakini yaliongezeka hadi asilimia 4.13 ya GDP mwaka 2009. <\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>SRINAGAR, India, Agosti 23 (IPS) &ndash; Mwaka baada ya se&#341;ikali ya India kuanza kuwalipa wanawake wajawazito ili kujifungulia watoto wao katika hospitali za se&#341;ikali, shinikizo la wingi wa watu linaonekana katika hospitali za nchini humo ambazo hazina wafanyakazi wa kutosha na vifaa. Kati ya Feb&#341;ua&#341;i na Mei, watoto wachanga 397 walifa&#341;iki dunia katika hospitali ya&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":934,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-3902","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3902","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/934"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=3902"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3902\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=3902"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=3902"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=3902"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}