{"id":3885,"date":"2012-07-31T13:40:01","date_gmt":"2012-07-31T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2012\/07\/31\/maswali-na-majibu-kupanda-mbegu-za-maendeleo-endelevu\/"},"modified":"2012-07-31T13:40:01","modified_gmt":"2012-07-31T13:40:01","slug":"maswali-na-majibu-kupanda-mbegu-za-maendeleo-endelevu","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2012\/07\/31\/maswali-na-majibu-kupanda-mbegu-za-maendeleo-endelevu\/","title":{"rendered":"Maswali na Majibu: Kupanda Mbegu za Maendeleo Endelevu"},"content":{"rendered":"<p>UMOJA WA MATAIFA, Julai 31 (IPS) &ndash; Rousbeh Legatis anamhoji JOS&Eacute; GRAZIANO DA SILVA, mku&#341;ugenzi mkuu wa Shi&#341;ika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO).<\/p>\n<p>Hadi sasa kuna mkanaganyiko ambao unajulikana waziwazi lakini ni vigumu kuutatua: kwani wakazi wa dunia wanaongezeka kwa kasi na &#341;asilimali zinazidi kuwa chache. Hakika, uzalishaji wa chakula unatakiwa kuongezeka kwa kiasi kikubwa cha asilimia 60 ifikapo mwaka 2050 ili kufikia mahitaji ya baadae ya chakula na mazao ya kilimo.\n<\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>Mbinu za kilimo, kwa asili ndiyo njia ya msingi ya kushughulikia tatizo hili, na kwa njia hiyo, inajenga msingi wa kutosha wa maendeleo endelevu. &#8220;Tunahitaji kuwa na akiba na kupanda,&#8221; anasema Jos&eacute; G&#341;aziano da Silva, mku&#341;ugenzi mkuu wa Shi&#341;ika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO).<\/p>\n<p>Da Silva anataka mbinu za kilimo ambazo zitaongeza uzalishaji na kupunguza atha&#341;i kwa mazingi&#341;a, kama vile &#8220;kilimo ambacho siyo cha kukatua, kilimo cha kupumzisha a&#341;dhi na usimamiaji wa pamoja wa wadudu waha&#341;ibifu ambao unaweza kuongeza uzalishaji lakini pia unapunguza madha&#341;a kwa mazingi&#341;a&#8221;.<\/p>\n<p>&#8220;Lakini hatuwezi kuwa na hali endelevu katika uzalishaji tu,&#8221; da Silva anaongeza. &#8220;Pia tunahitaji kuangalia upotevu na kuoza kwa chakula. Kati ya uzalishaji na ulaji duniani tunapoteza na kuozesha zaidi ya tani bilioni 1.3, sawa na moja ya tatu ya chakula kinachozalishwa kwa mwaka&#8221;<\/p>\n<p>Wakati upotevu wa chakula unajitokeza katika nchi zinazoendelea na unatokana na kukosekana kwa vifaa vizu&#341;i baada ya kuvuna, kuoza kwa chakula kunajitokeza zaidi katika nchi zenye viwanda vingi ambapo chakula kinachofaa kuliwa kinatupwa ovyo.<\/p>\n<p>FAO ilianzisha mbinu za kuima&#341;isha uzalishaji endelevu wa mazao (SCPI) katika mwongozo wake wa &#8220;Hifadhi na Kupanda&#8221;. Unalenga katika kuima&#341;isha uendelevu, ikiwa na maana uzalishaji wa kilimo ambao unahifadhi na kuongeza maliasili.<\/p>\n<p>Mwandishi wa haba&#341;i wa IPS Rousbeh Legatis alizungumza na da Silva kuhusu masuala yanayozunguka kilimo endelevu na maendeleo. Sehemu ya mahojiano inafuata.<\/p>\n<p>Swali: Miongo ya kuzuia mageuzi ya a&#341;dhi sasa yanaonekana yakija katika miaka ya ka&#341;ibuni, huku maslahi binafsi yakichukua udhibiti wa pengine hekta milioni 200 za a&#341;dhi kutoka kwa wakulima maskini ba&#341;ani Af&#341;ika, Ame&#341;ika Kusini na Asia. Je haki ya a&#341;dhi iwe sehemu ya ajenda za Mkutano wa Kilele wa Rio+20 <\/p>\n<p>Jibu: Ndiyo. Kuwezesha haki ya kumiliki a&#341;dhi kutambulika ni moja ya mahitaji ya msingi kabisa kwa wakulima maskini duniani kote. Ni sehemu ya msingi ya kuhamasisha mkulima kuwekeza na kutumia mali asili kwa hali endelevu.<\/p>\n<p>Hivi ka&#341;ibuni tulichukua hatua muhimu katika suala hili, kwa kupitishwa na Kamati ya Dunia ya Usalama wa Chakula miongozo ya haki ya kumiliki a&#341;dhi kwa muktadha wa usalama wa chakula. Miongozo hii inawakilisha histo&#341;ia ya msingi. Kwa ma&#341;a ya kwanza, se&#341;ikali, mashi&#341;ika ya ki&#341;aia na sekta binafsi walifikia kukubaliana kuwa na kanuni za kuhakikisha kuwa familia maskini zina haki ya kumiliki a&#341;dhi.<\/p>\n<p>Kwa kujenga kwenye msingi huu, tunahitaji sasa kukabiliana na changamoto nyingine: kanuni za uwekezaji wa kuzingatia maadili katika kilimo. Wakati miongozo inatoa picha ya jumla ya kuhakikisha kuwa kunakuwepo na utawala bo&#341;a katika haki za kumiliki a&#341;dhi, kanuni za uwekezaji wa kuzingatia maadili katika kilimo zinatakiwa kuhakikisha kuwa uwekezaji unatekelezwa kukidhi mahitaji ya wadau wote na kukuza na wala siyo kuathi&#341;i usalama wa chakula.<\/p>\n<p>Swali: Kama kilimo ni mwendeshaji mkuu wa maendeleo endelevu, ni kwa nini umuhimu huu haujaonyeshwa katika msaada wa kifedha wa moja kwa moja na ahadi za kisiasa za jumuiya ya kimataifa  Msaada kama huo na ahadi utapatikana <\/p>\n<p>Jibu: Bei za vyakula zimekuwa zikishuka tangu mapema miaka ya 1970, na hivyo kufanya kilimo kutokuwa na faida katika nchi nyingi zinazoendelea na kulazimu dunia kuzoea kununua kwa wakati mmoja tu vyakula vinavyouzwa katika masoko ya kimataifa. Mgogo&#341;o wa chakula wa mwaka 2008 ulikuwa kengele ya kuima&#341;isha dunia.<\/p>\n<p>Kwa sasa ni wazi kwa kila mtu kuwa tunahitaji kuwekeza katika maeneo ya kilimo kwenye nchi zinazoendelea, ambako zaidi ya asilimia 70 ya wakazi wenye njaa duniani wanapatikana. Miongoni mwao ni wakulima wadogo wanaozidi milioni 500 duniani kote, ambao wengi wao wanategemea kilimo kwa ajili ya sehemu ya kipato chao.<\/p>\n<p>Kilimo ni sehemu ya msingi ya mikakati ya maendeleo endelevu. Lakini kilimo kinaendeshwa na mamia kwa mamilioni ya wakulima mmoja mmoja, wafugaji, wavuvi na wanamisitu &ndash; ambao wengi wao wamejiweka mbali au wamejiondoa kabisa katika michakato ya kisiasa. Siyo lazima kuwa wana sauti sawa na wenzao wa mjini.<\/p>\n<p>Migogo&#341;o ya hivi ka&#341;ibuni ya chakula na kiuchumi imefanya watunga se&#341;a wa kitaifa na kimataifa kuangalia zaidi chanagamoto zinazokabili kilimo na wakazi wa kijijini, kwa hiyo kwa sasa tuna fu&#341;sa na wajibu wa kushughulikia changamoto hizo, siyo tu kwa kutumia misaada lakini pia kwa kukifanya kilimo na mifumo ya chakula kuwa na usawa na yenye ufanisi zaidi.<\/p>\n<p>Swali: Jitihada za Rio+20 zinatambua kuwa mabadiliko makubwa yanahitajika katika mfumo wa chakula duniani, hasa kutokana na ukweli kwamba zaidi ya watu bilioni moja wanakumbwa na njaa kila siku. Unadhani se&#341;ikali zina dhami&#341;a ya kisiasa kuangalia njia mbadala za kweli katika mfumo wa sekta ya kilimo ulioshindwa <\/p>\n<p>Jibu: Tunatakiwa kuzuia mawazo kwamba kuna mfumo mmoja tu wa uzalishaji wa kilimo duniani &ndash; ni kweli kwamba mabadiliko yanahitajika katika kuwa na kilimo mseto na mifumo mingi ya kilimo katika ngazi zote na katika nchi zote.<\/p>\n<p>Hii ni pamoja na hatua za kuongeza uzalishaji na kupunguza kupotea na kuoza kwa chakula, kwa mfano, kwa kuunda na kulinda haki ya &#341;asilimali, hasa kwa watu maskini; kuingiza motisha kwa ajili ya ulaji na uzalishaji endelevu katika mifumo ya chakula; na kukuza usawa na masoko yanayofanya vizu&#341;i ya mazao ya kilimo na chakula.<\/p>\n<p>Se&#341;ikali za kitaifa na jumuiya ya kimataifa zimeonyesha dhami&#341;a mpya ya kushughulikia changamoto hizi, na tunahitaji kuendelea kushinikiza kusonga mbele kwa dhami&#341;a hizi na utekelezaji wake.<\/p>\n<p>Swali: Ni udhaifu gani mkubwa uliopo wa utawala wa chakula na kilimo  Unaweza kutoa mifano halisi ambayo inafaa kwa matokeo ya Rio+20 ambayo yatasababisha madhaifu haya kuondoka baada ya miongo miwili ijayo <\/p>\n<p>Jibu: Kwa bahati, mafanikio ya kutokomeza njaa na kuhamia kwenye mwelekeo wa uzalishaji na ulaji endelevu yatategemea maamuzi ya mabilioni ya watu, wakiwa ni pamoja na wazalishaji na walaji.<\/p>\n<p>Mazingi&#341;a na motisha ambazo ni muhimu kwa ajili ya utoaji wa maamuzi mazu&#341;i yanahitajika, ikiwa ni pamoja na njia za kubainisha na kusimamia matatizo ya kibiasha&#341;a ambayo yanaweza kujitokeza wakati wa kutumia malengo haya mengi.<\/p>\n<p>Jambo hili, kwa upande mwingine litahitaji kujenga mifumo ya utawala ya usawa na yenye ufanisi&ndash; ambayo ni ya uwazi, shi&#341;ikishi, inayolenga katika matokeo na yanayoonekana &ndash; katika ngazi zote kutoka ngazi ya kimataifa hadi ya chini katika nchi.<\/p>\n<p>Taya&#341;i tuna teknolojia kwa ajii ya uzalishaji zaidi endelevu, lakini wakulima wadogo wanahitaji msaada kuweza kuendesha mfumo huu.<\/p>\n<p>Kuhama kutoka mfumo wetu wa sasa wa uzalishaji wa kilimo na kuingia kwenye kilimo endelevu una gha&#341;ama. Katika siku za nyuma, maskini walilipia kwa kiasi kikubwa gha&#341;ama za kuhama na kupata sehemu ndogo ya faida. Hili ni jambo ambalo halikubaliki kwa sasa. <\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>UMOJA WA MATAIFA, Julai 31 (IPS) &ndash; Rousbeh Legatis anamhoji JOS&Eacute; GRAZIANO DA SILVA, mku&#341;ugenzi mkuu wa Shi&#341;ika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO). Hadi sasa kuna mkanaganyiko ambao unajulikana waziwazi lakini ni vigumu kuutatua: kwani wakazi wa dunia wanaongezeka kwa kasi na &#341;asilimali zinazidi kuwa chache. Hakika, uzalishaji wa chakula unatakiwa&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":925,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-3885","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3885","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/925"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=3885"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3885\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=3885"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=3885"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=3885"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}