{"id":3862,"date":"2012-06-06T13:40:01","date_gmt":"2012-06-06T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2012\/06\/06\/wakulima-wadogo-nchini-afika-kusini-washindwa-vita-vya-usalama-wa-mbegu\/"},"modified":"2012-06-06T13:40:01","modified_gmt":"2012-06-06T13:40:01","slug":"wakulima-wadogo-nchini-afika-kusini-washindwa-vita-vya-usalama-wa-mbegu","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2012\/06\/06\/wakulima-wadogo-nchini-afika-kusini-washindwa-vita-vya-usalama-wa-mbegu\/","title":{"rendered":"Wakulima Wadogo Nchini Af&#341;ika Kusini Washindwa Vita vya Usalama wa Mbegu"},"content":{"rendered":"<p>CAPE TOWN, Af&#341;ika Kusini, Juni 5 (IPS) &ndash; Katika hali ya kufu&#341;ahia, Selinah Mncwango anafungua mfuko wake mkubwa wa plastiki na kutoa mifuko midogo midogo, kila mmoja ukiwa umejaa aina tofauti ya mbegu: uwele, maha&#341;agwe, maboga na mahindi. Mbegu hizo ndizo zinazomfanya kuonekana mwenye fu&#341;aha, ndiyo utaji&#341;i wake, ni &#8220;nguzo ya familia,&#8221; anasema mkulima huyo kutoka kijiji kilichopo kwenye jimbo la KwaZulu&ndash;Natal nchini Af&#341;ika Kusini.\n<\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>Mncwango mwenye um&#341;i wa miaka sitini na tano anatoka katika familia ya wakulima wadogo kwenye kijiji cha Ingwawuma katika pwani ya masha&#341;iki mwa jimbo hilo. Mazao anayopanda leo hii yanatokana na mbegu ambazo zimekuwa zikitolewa kutoka kizazi hadi kizazi, kwa miongo kadhaa, anasema. Mbegu nyingine zinatokana na kubadilishana na wakulima maji&#341;ani. &#8220;Mbegu zangu ni muhimu mno kwangu. Nina matumaini kuwa haitakuja kutokea siku ambapo natakiwa kununua mbegu dukani,&#8221; anasema mkulima huyo, ambaye watoto wake watano na wajukuu nane wanategemea kwa kiasi kikubwa mavuno anayopata. Anatambua kwa kina kuwa kuweka akiba ya mbegu na kubadilishana kunakuza dhana ya kupanda mazao mseto, kunaokoa fedha na kutoa usalama kwa wakulima wadogo kama mavuno yakiwa madogo. Lakini mbinu za kilimo za jadi kwa wakulima wadogo &ndash; ambazo watafiti wanasema, pia zitasaidia kupambana na uha&#341;ibifu wa udongo, zinapunguza mahitaji ya umwagiliaji na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi. Lakini kuna wasiwasi kuwa mbegu za aina hiyo zinanaweza kupotea hivi ka&#341;ibuni. Zimeanza kuondolewa katika kilimo na se&#341;ikali inalenga katika kukuza kilimo cha kibiasha&#341;a cha zao moja ambacho wanajua kitaleta mavuno mengi na ya ha&#341;aka ili kukuza uuzaji wa mazao ya kilimo katika masoko ya kimataifa. &#8220;Sekta hiyo inashikiliwa na makampuni ya mbegu na uzalishaji wa mazao ya kilimo viwandani,&#8221; anaelezea Rachel Wynbe&#341;g, mchambuzi wa se&#341;a katika Kitengo cha tathmini ya Mazingi&#341;a kwenye Chuo Kikuu cha Cape Town nchini Af&#341;ika Kusini. Wakulima wadogo wameondolewa katika sekta jinsi muda inavyosogea na wale wanaopata faida kutokana na uhaba wa chakula, anasema. &#8220;Kuna uelewa mdogo wa haki za wakulima wadogo. Mbinu za kilimo za jadi zimekuwa zikiondolewa miongo hadi miongo,&#8221; anaongeza. Nchini Af&#341;ika Kusini, na katika nchi nyingi kwenye ba&#341;a hilo, haki za wakulima wadogo zinazidi kukiukwa na se&#341;ikali na wakulima wa biasha&#341;a ambao wanataka kuendesha kilimo cha mazao yanayotumia mbegu zenye vinasaba (GM) na mbegu bo&#341;a za maaba&#341;a. Jambo hili linafanyika pamoja na kuwepo kwa Mkataba wa Rasilimali za Kijenetiki za Mimea ya Chakula na Kilimo wa Umoja wa Mataifa wa mwaka 2006 (IT&ndash; PGRFA) ambapo unalinda maa&#341;ifa ya wakulima wa jadi, kudai kupewa tuzo kutokana na mchango wao na kuendeleza mazao mseto, kuhakikisha ushi&#341;iki wao katika utoaji wa maamuzi kuhusu &#341;asilimali za kijenetiki, na kuhakikishiwa haki za kuweka akiba, kutumia na kubadilishana mbegu. Af&#341;ika Kusini na mataifa mengi ya Af&#341;ika ambayo ni wanachama wa Umoja wa Mataifa hawajasaini mkataba huo. &#8220;Mfumo wa se&#341;a wa Af&#341;ika Kusini kuhusu haki za wakulima umegawanyika na haupo wazi,&#8221; anasema Wynbe&#341;g. &#8220;P&#341;og&#341;amu za kibiasha&#341;a zinakuzwa na zinadhoofisha mbinu za kilimo cha jadi.&#8221; Kwa mujibu wa Wynbe&#341;g, msaada wa se&#341;ikali kwa wakulima wadogo siyo madhubuti na haupewi fedha za kutosha, unakosa uwezo na ma&#341;a nyingi unapuuza mahitaji ya wakulima wadogo. &#8220;Kwa bahati mbaya ma&#341;a nyingi se&#341;ikali haitekelezi mipango yake,&#8221; anaongeza. Wakulima wadogo wanakubaliana. Mncwango, ambaye ameja&#341;ibu kushi&#341;ikiana na wakulima wengi katika maeneo ya vijijini katika jamii yake kulinda njia zao za kilimo za jadi, anasema anasikitikia se&#341;ikali ya Af&#341;ika Kusini kuwatenga. &#8220;Ida&#341;a ya Kilimo inafika ma&#341;a kwa ma&#341;a kuendesha wa&#341;sha. Wanakuja na mbegu aina ya GM na nyingine za maaba&#341;a na kutueleza kuachana na mbegu zetu za jadi. Pia wanatueleza kutumia madawa ya kuulia wadudu na mbolea za chumvi,&#8221; analaumu mkulima huyo. &#8220;Kwa kutufanya kuacha mbegu zetu za jadi, wanatufanya kupoteza akiba ya mbegu zetu za jadi na kutulazimisha kuwa tegemezi.&#8221; Kwa mujibu wa Mncwango, ma&#341;a nyingi wakulima wanatambua kwa kuchelewa kuwa mbegu aina ya GM haziwezi kuhifadhiwa kwa ajili ya msimu wa kilimo unaofuata na kuwa mbegu gizo zinaangamiza mbegu za jadi. Wakulima wamejifunza kuwa mbegu zinazotengenezwa maaba&#341;a ni duni. &#8220;Haziwezi kutunzwa kiu&#341;ahisi na zinaoza kiu&#341;ahisi na zina lishe duni,&#8221; anasema. &#8220;Se&#341;ikali inazidi kutulazimisha kutumia mbegu hizo. Hata kama tunawaeleza kuwa hatuzitaki. Afadhali wangetusaidia kutujengea wigo, vifaa vya kulimia na upatikanaji wa masoko bo&#341;a,&#8221; anaelezea. &#8220;Lakini hawatusikilizi.&#8221; Watafiti kama Wynbe&#341;g anathibitisha kukosekana kwa uhusiano kati ya se&#341;a za kilimo ambazo zinaonekana ni za kimaendeleo na mahitaji ya wakulima. &#8220;Mavuno makubwa yanafaa kwa usalama wa chakula,&#8221; anasema. Law&#341;ence Mkhaliphi, meneja wa zana za kilimo katika Biowatch, shi&#341;ika lisilokuwa la kise&#341;ikali linalokuza kilimo endelevu, amekuwa akifanya kazi na wakulima wadogo katika jimbo la KwaZulu&ndash;Natal kwa miaka mingi. Anatoa maelezo zaidi. &#8220;Makampuni mengi ya pembejeo na kemikali za kilimo yanapatia se&#341;ikali motisha kuwashinikiza wakulima kutumia bidhaa zao,&#8221; Mkhaliphi anadai. &#8220;Wanataka wakulima kununua mbegu, wala siyo kuweka akiba ya mbegu hizo. Ni biasha&#341;a kubwa. Badala ya kutumikia watu, ida&#341;a za kilimo zimekuwa wakala wa makampuni ya vifaa na kemikali za kilimo.&#8221; Ida&#341;a ya Kilimo ya Af&#341;ika Kusini inakanusha madai haya. &#8220;Kushinikiza matumizi ya mbegu za biasha&#341;a badala ya mbegu za jadi siyo se&#341;a &#341;asmi ya se&#341;ikali,&#8221; anasema Julian Jaftha, mku&#341;ugenzi wa &#341;asilimali za kijenetiki wa ida&#341;a hiyo. &#8220;Se&#341;ikali haina hisa katika makampuni ya mbegu za GM.&#8221; Ida&#341;a ya Kilimo inaunga mkono mbinu zote za kibiasha&#341;a na kijadi, Jaftha anasema. Inaendesha mpango wa kitaifa wa kuingiza mbegu za jadi katika maeneo ya vijijini na ina Kituo cha Mimea ya Kijenetiki katika mji mkuu wa Af&#341;ika Kusini wa P&#341;eto&#341;ia, ili kulinda mbegu za jadi. &#8220;Mbegu za GM hazipaswi kuwa tegemeo pekee la mkulima,&#8221; anasema Jaftha. &#8220;Inatakiwa kuwepo kwa chaguo jingine kwa ajili ya wakulima ambao wanataka kutumia mbegu hizo. Tunata&#341;ajia kuwa kunakuwepo na mchakato wa kidemok&#341;asia kwa wakulima kutoa sauti zao na kuchagua wanalotaka.&#8221; Jaftha anakubali, hata hivyo, kuwa se&#341;a ya taifa haijatekelezwa ipasavyo. &#8220;Kwa bahati mbaya, inatokea katika ngazi ya jimbo kuwa wakulima hawapewi fu&#341;sa ya kuchagua,&#8221; anakubali. &#8220;Tunajua kuwa bado kuna kazi kubwa ambayo inatakiwa kufanywa.&#8221; <\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>CAPE TOWN, Af&#341;ika Kusini, Juni 5 (IPS) &ndash; Katika hali ya kufu&#341;ahia, Selinah Mncwango anafungua mfuko wake mkubwa wa plastiki na kutoa mifuko midogo midogo, kila mmoja ukiwa umejaa aina tofauti ya mbegu: uwele, maha&#341;agwe, maboga na mahindi. Mbegu hizo ndizo zinazomfanya kuonekana mwenye fu&#341;aha, ndiyo utaji&#341;i wake, ni &#8220;nguzo ya familia,&#8221; anasema mkulima huyo&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":523,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-3862","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3862","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/523"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=3862"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3862\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=3862"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=3862"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=3862"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}