{"id":3846,"date":"2012-05-08T13:40:01","date_gmt":"2012-05-08T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2012\/05\/08\/kuokoa-maisha-ya-akina-mama-katika-sudan-kusini\/"},"modified":"2012-05-08T13:40:01","modified_gmt":"2012-05-08T13:40:01","slug":"kuokoa-maisha-ya-akina-mama-katika-sudan-kusini","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2012\/05\/08\/kuokoa-maisha-ya-akina-mama-katika-sudan-kusini\/","title":{"rendered":"Kuokoa Maisha ya Akina Mama katika Sudan Kusini"},"content":{"rendered":"<p>JUBA, Mei 7 (IPS) &ndash; Ma&#341;tha Bo&#341;ete Angela ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika p&#341;og&#341;amu ya wakunga wa jadi katika Taasisi ya Mafunzo ya Afya ya Sudan Kusini.\n<\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>Ma&#341;tha Bo&#341;ete Angela anatazama chini ya a&#341;dhi wakati akikubali kuwa kati ya watoto wake wawili hakuna ambaye alimzaa kwa msaada wa mkunga wala dakta&#341;i. Mama wa um&#341;i wa miaka 28 katika Sudan Kusini alizungumzia ukweli huu mbele ya da&#341;asa lao katika Taasisi ya Kanisa la Katoliki ya Mafunzo ya Afya katika Sudan Kusini katika mji wa Wau, magha&#341;ibi mwa nchi. &#8220;Sikuwa najua chochote juu ya wakunga wa jadi,&#8221; alielezea. Lakini kama angekuwa na mtoto mwingine ni wazi kuwa angejifungulia kwa msaada wa mkunga wa jadi &#8220;ili kuwa mfano kwa jamii.&#8221; Sudan Kusini ina kiwango cha juu zaidi cha vifo vya uzazi duniani, kwa mujibu wa Shi&#341;ika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu. Se&#341;ikali inakadi&#341;ia kuwa zaidi ya wanawake10,000 waanafa&#341;iki dunia kila mwaka kutokana na sababu za uzazi na wengine 76,000 wanapata matatizo makubwa wakati wa kujifungua. Wanawake hapa ni asilimia 60 ya watu milioni nane nchini humu. Vifo vingi vya uzazi vinachochewa na uhaba mkubwa wa wakunga wa jadi wenye mafunzo kuwapatia ushau&#341;i wa kitaalam wanawake wakati wa ujauzito na kubainisha hata&#341;i zinazoambatana nazo. Utafiti wa taifa wa miaka mitatu iliyopita uli&#341;ipoti kuwa kuna chini ya wakunga wa jadi 150 katika mfumo wa afya wa kitaifaa. &#8220;Mama zetu, baadhi yao, wanafa&#341;iki wakati wa kujifungua,&#8221;alisema Ropani Raship, mwanafunzi mwenzake Angela mwenye um&#341;i wa miaka 20 katika Taasisi ya Katoliki ya Mafunzo ya Afya ya Sudan Kusini. &#8220;Hawan fu&#341;sa.&#8221; Badala ya kupata huduma kutoka kwa wafanyakazi wenye ujuzi, akina mama wengi wanaamua kugeukia waganga wa jadi, kama ilivyokuwa kwa Angela alipojifungua mtoto wake wa pili. Wengine hawapati msaada kabisa. Kila mtu katika se&#341;ikali ya Sudan Kusini na NGOs wanakubali kuwa kuendeleza sekta ya afya na hasa kutoa huduma bo&#341;a za afya ya uzazi kutategemeana na upatikanaji wa wafanyakazi wa afya wenye mafunzo kuingia katika mfumo wa afya ha&#341;aka iwezekanavyo. Angela, Raship na wanafunzi wenzao wanaleta uwezekano huo: Aina ya wakunga wa jadi wenye mafunzo na vijana, ambao watawekwa katika kliniki na hospitali nchini kote ma&#341;a watakapomaliza masomo yao na kupata vyeti. Lakini itachukua miaka mitatu kabla hawajaanza kuziba pengo. Na watafanya hivyo &ndash; ikiwa ni pamoja na wahitimu wengine kutoka p&#341;og&#341;amu nyingine mbili zinazotoa vyeti nchini humo watakuwa muhimu mno katika nchi ambapo wakunga wa jadi wanahitajika kwa kiasi kikubwa. Hiyo ina maana kuwa, kwa mustakabali wa baadaye, wanawake wengi wajawazito wataachwa wakitegemea wakunga wa jadi na wafanyakazi wa afya wenye ujuzi. Ma&#341;a nyingi hawa ni maji&#341;ani ambao &#8220;wana imani kuwa wana vipaji vya kuponya, au walijifunza ukunga wa jadi kupitia mafunzo ya kazini,&#8221; alisema Alaa El&ndash;Bashi&#341;, m&#341;atibu mkaazi wa Mpango wa Uzazi, Watoto Wachanga na Maisha ya Watoto au Mate&#341;nal, Newbo&#341;n &#038; Child Su&#341;vival Initiative (MNCSI) katika Hospitali Kuu ya Massachusetts. Wengi wao hawana mafunzo kuweza kubainisha au kutibu matatizo makubwa. Hali hiyo inaonyesha mjadala mkubwa katika nchi hii mpya: Ni jinsi gani unaweza kugawa &#341;asilimali chache kuokoa maisha sasa, wakati huo huo ukiwekeza vitega uchumi vya muda m&#341;efu ambavyo vitajenga mfumo wa afya endelevu  Kwa upande wake, MNCSI imeamua kufanya kile ambacho inaweza kubo&#341;esha ujuzi wa wafanyakazi wa afya. Mpango huo unawafikia kwa kutoa mafunzo na mkoba wa usambazaji wa vifaa vya afya &ndash; mikasi, glavu, nyuzi za kufungia kitovu. Katika kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja na nusu, MNCSI imetoa mafunzo kwa wanafunzi 72 kupitia mafunzo ya udhamili. Kwa upande wao, wametoa mafunzo kwa wafanyakazi wa afya zaidi ya 700 katika majimbo saba kati ya 10 nchini humo. Jimbo la nane litaingizwa katika mchakato miezi michache ijayo. Wazo hilo, kwa mujibu wa El&ndash;Bashi&#341;, ni kuwafanya wafanyakazi wa afya kupata mafunzo katika ngazi ambapo kwa uchache wanaweza kutambua matatizo na kuyapeleka kwenye vituo vya afya mapema. MNCSI inatoa vigezo vya picha kwa wafanyakazi wa afya kutoa ushau&#341;i wakati wa ujauzito ili kutambua dalili mbaya. Na kama matatizo yanaonekana wazi, wanaweza kusaidia kujifungua kwa njia salama. MNCSI pia imeanzisha kifaa &#341;ahisi kusaidia wanawake ambao wanatokwa na damu baada ya kujifungua. Kifaa hiki ni ubunifu &#341;ahisi ambacho kinaweza kusaidia kusitisha kutokwa na damu hadi mwanamke atakapofikishwa kwenye kituo cha afya. Baada ya zia&#341;a ya baadhi ya maeneo ambayo kifaa hicho kinatumika, El&ndash;Bashi&#341; alisema wafanyakazi wa afya wa majumbani wameweza kutumia kifaa hicho bila matatizo yoyote. Kati ya matukio yaliyo&#341;ikodiwa, MNCSI ili&#341;ipoti mwanamke mmoja tu ambaye alifa&#341;iki dunia. &#8220;Tunaokoa maisha,&#8221; El&ndash;Bashi&#341; alisema. Ma&#341;a zote kutajitokeza matatizo yasiyota&#341;ajiwa miongoni mwa wanawake wanaojifungua, pamoja na kuwa, alisema Susan Pu&#341;din, mku&#341;ugenzi wa mkaazi wa shi&#341;ika la Inte&#341;national Rescue Committee (IRC). Na haziwezi kuta&#341;ajiwa kwa kutambua matatizo. Njia bo&#341;a zaidi ya Sudan Kusini ni kuhakikisha kuwa wanawake wote wajawazito wanafikiwa na wafanyakazi wa afya wenye ujuzi. &#8220;Kila mtu anatakiwa kujua kuwa mwanamke yoyote yule anaweza kuwa na matatizo na anahitaji kupatiwa huduma,&#8221; Pu&#341;din alisema. Hii inahitaji kuegemea, siyo tu kwa mama, lakini kwa baba, wakunga wa jadi na made&#341;eva wa teksi. Pia inahitaji kuwafanya kutambua kuwa, kama matatizo yanajitokeza wanawake wanapokwenda kujifungua, wanapaswa kuwa na uwezo wa kuwafikisha kwenye kituo cha afya. IRC imekuwa ikifanya kazi na Sudan Kusini kwa zaidi ya miongo miwili, huku p&#341;og&#341;amu zake nyingi zikijikita katika huduma za afya. Kwa sasa inasaidia vituo vya afya 30 katika eneo la magha&#341;ibi na kaskazini mwa nchi, ambapo vitano kati ya hivyo vinatoa huduma za afya ya uzazi. Katika zia&#341;a yake ya hivi ka&#341;ibuni katika moja ya vituo hivyo, Pu&#341;din alisema alishuhudia mkunga wa jadi akiokoa maisha ya watu watano. Mama mmoja, baada ya kujifungua mapacha, alianza kutokwa na damu. Mkunga alizuia kutokwa na damu, na pia kutoka kwa mwanamke mwingine ambaye mtoto wake alitanguliza mkono. Wakati akihudumia mama wa kwanza, mkunga alimwingiza mwingine kwenye ga&#341;i la kubebea wagonjwa lililokuwa likielekea hospitalini. &#8220;Matukio kama haya yanajitokeza kila wakati,&#8221; Pu&#341;din alisema. &#8220;Siyo masuala ambayo ni ya kipekee, lakini kwa kuwa na wakunga wa jadi wenye maa&#341;ifa katika vituo vya afya ambako kuna vifaa na mfumo wa &#341;ufaa ni njia ya kuokoa maisha ya mama. Na inawezekana.&#8221; Hata hivyo haiwezekani kufanyika kwa ha&#341;aka. Inahitaji kuongeza ufahamu katika jamii halafu kufanya kazi kuhakikisha kuwa huduma zilizoahidiwa zinapatikana. Hii ina maana kujenga vituo vingi vya afya na kuwa na wakunga wengi zaidi, kama ilivyo kwa Angela na Raship, katika mfumo wa afya. Lakini katika mji wa Wau, wanafunzi katika Taasisi ya Katoliki ya Mafunzo ya Afya ya Sudan Kusini wanakubali kuwa hata kama wataaji&#341;iwa, haja ya kuwa na wakunga wa jadi haitaondoka hivi ka&#341;ibuni. Badala ya kutegemea mfumo mmoja, wengi walisema walikuwa wamejiandaa kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa afya wa majumbani na kuchukua ushau&#341;i kutoka kwao wa jinsi ya kufanya kazi na jamii. Jambo hilo, walikubaliana, ni njia bo&#341;a zaidi ya kuokoa maisha ya akina mama. *And&#341;ew G&#341;een ana&#341;ipoti kutoka Sudan Kusini kwa udhamini wa Inte&#341;national Repo&#341;ting P&#341;oject, shi&#341;ika hu&#341;u la uandishi wa haba&#341;i lenye makao yake mjini Washington, D.C. <\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>JUBA, Mei 7 (IPS) &ndash; Ma&#341;tha Bo&#341;ete Angela ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika p&#341;og&#341;amu ya wakunga wa jadi katika Taasisi ya Mafunzo ya Afya ya Sudan Kusini. Ma&#341;tha Bo&#341;ete Angela anatazama chini ya a&#341;dhi wakati akikubali kuwa kati ya watoto wake wawili hakuna ambaye alimzaa kwa msaada wa mkunga wala dakta&#341;i. Mama wa&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":912,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-3846","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3846","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/912"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=3846"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3846\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=3846"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=3846"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=3846"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}