{"id":3840,"date":"2012-04-23T13:40:01","date_gmt":"2012-04-23T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2012\/04\/23\/kuishi-kwa-mlo-mmoja-kwa-siku-nchini-swaziland\/"},"modified":"2012-04-23T13:40:01","modified_gmt":"2012-04-23T13:40:01","slug":"kuishi-kwa-mlo-mmoja-kwa-siku-nchini-swaziland","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2012\/04\/23\/kuishi-kwa-mlo-mmoja-kwa-siku-nchini-swaziland\/","title":{"rendered":"Kuishi kwa Mlo Mmoja kwa Siku Nchini Swaziland"},"content":{"rendered":"<p>MBABANE, Ap&#341;ili 23 (IPS) &ndash; Ma&#341;ga&#341;et Gamedze anaendesha maisha kwa kupiga pasi katika jumuiya yake ya makazi duni ya Msunduza, ambayo yanapatikana kilomita moja nje ya mji mkuu wa Swaziland wa Mbabane. Tangu mgogo&#341;o wa kifedha nchini humo, hawezi tena kuingiza fedha ya kuweza kulipia pango katika kijumba chake cha tope cha chumba kimoja, ambacho anatumia pamoja na watoto wake watano.\n<\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>Tangu mwaka jana, kipato chake kilipungua kutoka dola zipatazo 130 hadi dola 50 tu kwa mwezi. Kutokana na kipato hicho anatakiwa kulipa kodi ya pango ya kila mwezi ya dola 35, na kiasi kidogo kinachobaki kwa ajili ya chakula na mahitaji mengine ya lazima. &#8220;Watu wengi ninaowafuata kuomba aji&#341;a wanalalamika kuwa hawana fedha kwasababu walipoteza aji&#341;a au se&#341;ikali haijawalipa wale wanaoendesha biasha&#341;a nayo,&#8221; alisema Gamedze. Mgogo&#341;o wa kifedha uliingia nchini humo mwaka 2010 baada ya mapato kutoka Umoja wa Fo&#341;odha wa Kusini mwa Af&#341;ika kupunguzwa hadi ka&#341;ibu na asilimia 60. Kipato cha Gamedze kilipungu kwa kasi kubwa na watoto wake wanne kati ya watano waliacha shule. Utafiti wa Madha&#341;a ya Mgogo&#341;o wa Kifedha wa Umoja wa Mataifa nchini Swaziland uliotolewa Machi 16 ulisema asilimia 21.9 ya kaya zilizofanyiwa utafiti zimekabiliwa na kushuka kwa kipato. Ka&#341;ibu asilimia saba ya kaya zilizofanyiwa utafiti zilikubali kuwa na mwanafamilia ambaye alipoteza aji&#341;a. Gamedze siyo mwathi&#341;ika pekee wa mgogo&#341;o wa fedha kwasababu maji&#341;ani zake wengi katika makazi duni ya Msunduza wanabaki nyumbani baada ya kupoteza aji&#341;a. &#8220;Nilipunguzwa kazi kutoka kampuni ya ujenzi baada ya se&#341;ikali kukosa fedha kuweza kuendelea na m&#341;adi wa makao makuu mwaka jana,&#8221; alisema Mancoba Gama, 32, akiwa ameketi akinywa pombe ya kienyeji katika makazi hayo duni. Aliongeza kuwa yeye na wengine wamechoka kutafuta aji&#341;a kwasabu waaji&#341;i wameshindwa kuwaaji&#341;i baada ya kuwaomba ma&#341;a kadhaa. Mgog&#341;o wa kifedha umeongeza tatizo la uhaba wa aji&#341;a nchini humo, ambao unasimamia katika asilimia 52 miongoni mwa vijana. Kwa mujibu wa mshau&#341;i wa uchumi wa Shi&#341;ika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa, Zuzana B&#341;ixiova, ka&#341;ibu nusu ya kaya zilizofanyiwa utafiti zinategemea aji&#341;a &#341;asmi kuingiza vipato vyao na wameathi&#341;ika na mgogo&#341;o wa kifedha. Watu hasa katika sekta binafsi walipunguzwa kazi au kupunguziwa mshaha&#341;a wao mwaka jana wakati baadhi ya wafanyabiasha&#341;a wadogo walifunga biasha&#341;a. Matokeo yake, changamoto kubwa ikawa asilimia 23.9 ya kaya a utafiti zililalamika kukabiliwa na tatizo la bei kubwa za vyakula. Kiwango cha mfumuko wa bei sasa kimefikia asilimia 9.43 na kimesababisha hali ngumu zaidi kwa asilimia 63 ya &#341;aia wa Swaziland wanaoishi chini ya msta&#341;i wa umaskini wa dola mbili kwa siku kuweza kumudu kununua chakula. Bei za bidhaa ikiwa ni pamoja na mafuta ya taa, na bidhaa nyingine za lazima kama vile mafuta ya kula, mahindi na mikate zimeongezeka. Na hii ina maana kuwa Gamedze anaweza tu kumudu mlo mmoja kwa siku. Clement Dlamini, mshau&#341;i mtaalam wa mafunzo, alisema utegemezi wa kaya nyingi katika aji&#341;a &#341;asmi ni dalili kuwa taifa hilo lilikuwa likitoa elimu kwa watafutaji wa aji&#341;a badala ya wajasi&#341;iamali. &#8220;Hii ni changamoto kwa taasisi zinazotoa mafunzo kuwa na mipango ya kusaidia vijana kuwa na maa&#341;ifa ya ujas&#341;iamali na usimamiaji wa biasha&#341;a,&#8221; alisema Dlamini. Dlamini pia alitoa wito kwa se&#341;ikali kushughulikia suala la upatikanaji wa a&#341;dhi. Wakazi wengi wa Swaziland hawana a&#341;dhi ambamo wanaishi na hivyo mabenki hayawezi kuwapatia mikopo kwa kuwa hawana dhamana. Hata hivyo, naibu &#341;ais wa Shi&#341;ikisho la Wafanyakazi Swaziland, Sibongile Mazibuko, aliwakosoa washi&#341;ika wa maendeleo kutokana na kusitisha msaada kwa matumizi ya kijamii ya se&#341;ikali wakati mamlaka yanaendelea kupoteza fedha. Anasema siyo haki se&#341;ikali kuendelea kupunguza mshaha&#341;a wa wafanyakazi wa umma. Hata hivyo, mshaha&#341;a wa chini nchini humo ni wa juu zaidi katika kanda kutokana na kufikia asilimia 18 ya GDP. Se&#341;ikali ya Swaziland inapendekeza kupunguzwa kwa mshaha&#341;a kwa asilimia 4.5 kwa wafanyakazi wa umma na pia kusitisha ongezeko la kila mwaka la mshaha&#341;a wa wafanyakazi hao katika jitihada za kupunguza mshaha&#341;a kwa asilimia tano. &#8220;Je kuhusu matumizi makubwa katika jeshi na matukio ya kijadi ambayo hayana faida kwetu kama vile She&#341;ehe za Ma&#341;ula &#8221; aliuliza Mazibuko. Mfalme Mswati III na Mama wa Mfalme, Ntombi Thwala, huwa hujiunga na makundi ya wanawake wanaocheza na kuimba nyimbo katika matukio mawili tofauti katika mwezi wa Feb&#341;ua&#341;i. Hii ni kwa ajili ya kushe&#341;ehekea msimu wa ma&#341;ula na se&#341;ikali inafadhili matukio hayo. Hata hivyo, gha&#341;ama za matukio hayo hazitangazwi kwa umma. Alisema haisaidii nchi wakati wa kushi&#341;ikiana na washi&#341;ika kama Umoja wa Ulaya (EU) kulipia huduma za lazima za taifa bila kulazimisha se&#341;ikali kuima&#341;isha nidhamu katika matumizi ya fedha. Mwaka huu EU itatoa gha&#341;ama za kusomesha wanafunzi waliopata da&#341;aja la kwanza katika Mpango wa Elimu ya Msingi ya Bu&#341;e hadi mwaka 2014. Mmoja wa watoto watano wa Gamedze anaendelea kuhudhu&#341;ia masomo, kwani yeye anafaidika na Mfuko wa Yatima na Watoto Wanaoishi katika Mazingi&#341;a Magumu ambao uko chini ya se&#341;ikali. Mwaka jana, se&#341;ikali ilikosa fedha na ilishindwa kulipia ada kwa wakati kwa walengwa wa mfuko huo na kwa wale wanaofaidika na Mpango wa Elimu ya Msingi Bu&#341;e. &#8220;Ma&#341;a kadhaa mtoto wangu wa kiume ali&#341;ejeshwa nyumbani kutokana na mwalimu mkuu kusema nilipaswa kulipia ada kwasababu se&#341;ikali imeshindwa kutimiza ahadi yake,&#8221; alisema Gamedze. Hatimaye se&#341;ikali ililipa ada baada ya kukopa fedha kutoka taasisi za fedha, lakini zilitosha tu kulipia mishaha&#341;a ya wafanyakazi wa umma na hifadhi ya jamii kwa wazee. Swaziland iliingia katika mgogo&#341;o wa sasa wa kiuchumi na kijamii, ikiwa ni pamoja na uhaba wa aji&#341;a wa asilimia 29 ya nguvukazi yote wakati asililimia 29 ya wakazi wanakabiliwa na uhaba wa chakula, kwa mujibu wa utafiti. Nchi hiyo pia inaongoza kwa kuwa na maambukizi makubwa zaidi ya VVU\/UKIMWI duniani, katika asilimia 26 ya wakazi wenye um&#341;i wa kuzaa watoto kwa mujibu wa Utafiti wa Afya na Idadi ya Watu wa Swaziland mwaka 2007, na hivyo kuufanya mgogo&#341;o wa kifedha kuongeza matatizo ambayo taya&#341;i yanawakabili wakazi wa taifa hilo. Wazi&#341;i wa Fedha Majozi Sithole alisema watu maskini walitelekezwa wakati madha&#341;a ya mgogo&#341;o wa fedha yalipo&#341;ipotiwa. &#8220;Kila mtu alielekeza nguvu kwenye madha&#341;a katika biasha&#341;a, benki na hata usawa kati ya sa&#341;afu ya lilangeni na &#341;and ya Af&#341;ika Kusini, na kushindwa kuangalia kaya maskini na jinsi gani zingeweza kuathi&#341;ika na mgogo&#341;o wa kiuchumi,&#8221; alisema Sithole. &#8220;Swaziland inahitaji msaada wa kimataifa ikiwa ni pamoja na kuendelea kutolewa kwa msaada na jumuiya ya kimataifa, sekta binafsi, mashi&#341;ika ya Umoja wa Mataifa na NGOs,&#8221; kaimu mwakilishi mkazi wa Umoja wa Mataifa Dk. Jamab Gulaid alisema Machi 16. <\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>MBABANE, Ap&#341;ili 23 (IPS) &ndash; Ma&#341;ga&#341;et Gamedze anaendesha maisha kwa kupiga pasi katika jumuiya yake ya makazi duni ya Msunduza, ambayo yanapatikana kilomita moja nje ya mji mkuu wa Swaziland wa Mbabane. Tangu mgogo&#341;o wa kifedha nchini humo, hawezi tena kuingiza fedha ya kuweza kulipia pango katika kijumba chake cha tope cha chumba kimoja, ambacho&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":522,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-3840","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3840","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/522"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=3840"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3840\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=3840"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=3840"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=3840"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}