{"id":3812,"date":"2012-03-02T13:40:01","date_gmt":"2012-03-02T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2012\/03\/02\/zimbabwe-maandamano-ya-wafanyabiashaa-wadogo-wadogo-yaweza-kuchochea-mageuzi\/"},"modified":"2012-03-02T13:40:01","modified_gmt":"2012-03-02T13:40:01","slug":"zimbabwe-maandamano-ya-wafanyabiashaa-wadogo-wadogo-yaweza-kuchochea-mageuzi","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2012\/03\/02\/zimbabwe-maandamano-ya-wafanyabiashaa-wadogo-wadogo-yaweza-kuchochea-mageuzi\/","title":{"rendered":"ZIMBABWE: Maandamano ya Wafanyabiasha&#341;a Wadogo Wadogo Yaweza Kuchochea Mageuzi"},"content":{"rendered":"<p>HARARE, Ma&#341; 1 (IPS) &ndash; Kuna jinsi ambavyo huwezi kutofautisha kati ya maisha ya Mohammed Bouazizi, muuza matunda wa Tunisia ambaye alichochea mapinduzi ya Ua&#341;abuni, na F&#341;ancis Tachi&#341;ev, muuza matunda nchini Zimbabwe.\n<\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>Maandamano ambayo aliyaanzisha yalianza baada ya Bouazizi kujichoma moto baada ya polisi kumpo&#341;a mkokoteni wake wa kuuzia matunda. Maandamano ya nchi nzima baada ya kifo cha Bouaziz yalisababisha &#341;ais wa zamani wa Tunisia Zine el Abidine Ben Ali kuikimbia nchi na kuachia mada&#341;aka. Kifo cha kushangaza cha Bouaziz kilibadili ulimwengu, na kuanza kile ambacho kinajulikana kama Zama Mpya ya Kia&#341;abu.<\/p>\n<p>Kama ambavyo Bouazizi alifanya, Ticha&#341;eva anaingiza kipato cha kawaida sana kwa kusukuma mkokoteni wake wa matunda katika eneo la kibiasha&#341;a katikati mwa jiji la Ha&#341;a&#341;e, akiuza matunda yake. Kama ilivyo kwa Bouazizi, Ticha&#341;eva anaishi kwa hofu ya polisi kupo&#341;a bidhaa zake, hasa katika kipindi hiki ambapo polisi nchini Zimbabwe na Halmashau&#341;i ya Jiji la Ha&#341;a&#341;e wameanzisha kampeni ya kuondoa wafanyabiasha&#341;a wasio&#341;uhusiwa kutoka jijini humo. <\/p>\n<p>Ticha&#341;eva alianza kufanya kazi ya kuuza matunda mwaka 2008 wakati kiwanda cha nguo alichokuwa akifanyia kazi kilipofungwa.<\/p>\n<p>&#8220;Nilichoka kutafuta aji&#341;a na njia pekee ilikuwa kuendesha maisha kwa kusukuma mkokoteni na kuanza kuuza matunda,&#8221; Ticha&#341;eva aliiambia IPS alipokuwa akiangalia polisi kama wanakuja kufanya do&#341;ia mtaani mjini Ha&#341;a&#341;e. <\/p>\n<p>Polisi na maofisa wa halmashau&#341;i wanazunguka katika jiji wakiwa kwenye maga&#341;i yao huku wakikamata wafanyabiasha&#341;a wadogo wadogo ambao wanauza bidhaa bila leseni na kuanza kuwapo&#341;a bidhaa zao. Ma&#341;a nyingi unyang&#8217;anyi huo hutumia nguvu kwani wafanyabiasha&#341;a sasa wamejipanga na wanaanza kupigana. Jan. 11 katikati mwa jiji la Ha&#341;a&#341;e kulitulia kwa muda wakati polisi na wafanyabiasha&#341;a walipoanza kupigana, huku wachuuzi wakitupia mawe polisi.<\/p>\n<p>Katika wiki za mwanzoni mwezi Janua&#341;i maofisa wa polisi waliachwa wakiwa wameje&#341;uhiwa na kituo cha polisi katikati mwa jiji kufungwa kutokana na mapigano hayo. Gazeti nchini humo la The Zimbabwean lili&#341;ipoti kuwa wafanyabiasha&#341;a wawili walikimbizwa hospitalini baada ya kuteswa na polisi. Gazeti hilo pia lilisema waandishi wa haba&#341;i wa gazeti la nchini humo la Daily News walikamatwa na kuwekwa kizuizini kutokana na kaundika haba&#341;i za tukio hilo.<\/p>\n<p>Pamoja na kuwa waandamanaji wako mbali kufikia kusababisha mapinduzi nchini Zimbabwe, nia ya wafanyabiasha&#341;a wadogo kupambana kulinda chanzo chao cha kipato ni dalili kuwa watu hawatavumilia tena kukaa kimya wakati wakiwa wanateseka.<\/p>\n<p>Mhadhi&#341;i wa siasa katika Chuo Kikuu cha Zimbabwe ambaye anafanya utafiti wa siasa na mwelekeo wa kijamii, Eld&#341;ed Masunungu&#341;e, aliliambia gazeti la Daily News kuwa pamoja na kuwa siyo suala la kawaida nchini Zimbabwe kupambana na polisi, ukweli kuwa &#341;aia wanaanza kufanya hivyo ni isha&#341;a za nyakati.<\/p>\n<p>&#8220;Watu wamechoshwa na kuteseka na hilo linaweza kuonyesha hasi&#341;a yao. Wengi wao wamekuwa wakija&#341;ibu kujiingizia kipato cha kuendeshea maisha yao kutokana na uchuuzi lakini polisi wanawachukulia hatua kali,&#8221; Masunungu&#341;e aliiambia Daily News. &#8220;Wangeamua kupambana na polisi kutokana na kuchoshwa na hali hiyo.&#8221;<\/p>\n<p>Wachuuzi wengi, kama ilivyo kwa Ticha&#341;eva, hawawezi kumudu kulipia dola 125 kwa mwezi kama ada ya leseni ili kupata kibali cha kuuza matunda katika jiji. Ticha&#341;eva aliiambia IPS kuwa kama akiingiza kiasi kikubwa, ni dola 90 tu kwa mwezi.<\/p>\n<p>Na kama ilivyo kwa Bouazizi, amechoshwa na polisi. Haba&#341;i ya Bouazizi haijaondokana na haba&#341;i ya mchuuzi huyo wa mtaani katika taifa hili la Kusini mwa Af&#341;ika. <\/p>\n<p>Ka&#341;ibu na mahali ambapo Ticha&#341;eva anauza bidhaa zake kuna wauza magazeti na ma&#341;a nyingi anachungulia vichwa vya haba&#341;i vya magazeti. Aliiimbia IPS kuwa anasoma juu ya Bouazizi lakini hataweza kufiki&#341;ia kujichoma moto hata kama anakabiliwa na changamoto kama ya Bouazizi.<\/p>\n<p>&#8220;Nasoma histo&#341;ia lakini sitajiua. Kama polisi atanivamia, nitapambana,&#8221; alisema Ticha&#341;eva akiongeza, &#8220;Tunafanya kazi kwa bidii lakini wanatupelekesha mno hatujui tufanye nini &#8220;<\/p>\n<p>Wafanyabiasha&#341;a wengine wanaungana mkono na matamshi ya Ticha&#341;eva. Wanawake kadhaa na wanaume wanaendelea kutembea katikati mwa Ha&#341;a&#341;e wakiuza kila aina ya bidhaa huku wakipuuza kukamatwa na polisi.<\/p>\n<p>&#8220;Tunapambana na polisi kwasababu ndiyo wao ambao wanaanza kutushambulia. Wanachukua bidhaa zetu kwa ajili ya kula au kuziuza majumbani mwao wakati tunataka pia kuishi,&#8221; Tafadzwa Nyamupfachitu, mama mwenye um&#341;i wa miaka 27 mwenye mapacha watatu wenye um&#341;i wa miaka sita, aliiambia IPS.<\/p>\n<p>Anatunza familia yake kwa kuuza matunda, siga&#341;a na kuuza vocha za simu. &#8220;Tunakasi&#341;ishwa na hili kwasababu pia tunataka kuishi. Tunapaswa kufaidi nchi yetu tuliyozaliwa tukiwa hu&#341;u. Kama tutashindwa kuishi kwa jinsi hiyo hakutakuwa na maisha kwetu sisi kwasababu tutageuka kuwa wahalifu au makahaba,&#8221; alisema.<\/p>\n<p>Hata hivyo, polisi wameamua kuanzisha kamata kamata hadi jiji litakapojipanga.<\/p>\n<p>Diwani wa Ha&#341;a&#341;e na mwenyekiti wa Chama cha Madiwani Waliochaguliwa nchini Zimbabwe, Wa&#341;ship Dumba, alisema kamata kamata hiyo ni muhimu kuleta utulivu katika jiji.<\/p>\n<p>&#8220;Ni lazima wafanye shughuli zao katika maeneo waliyotengewa,&#8221; alisema Dumba juu ya wafanyabiasha&#341;a wadogo. <\/p>\n<p>Matamshi ya Dumba yanakuja wakati ambapo asilimia 90 ya watu wa Zimbabwe wenye um&#341;i wa kufanya kazi hawana aji&#341;a, kwa mujibu wa Shi&#341;ikisho la Vyama vya Wafanyakazi Zimbabwe. Wengi wao ni wachuuzi ambao wamezoea kufanya kazi katika viwanda ambavyo vimeshafungwa kutokana na mgogo&#341;o wa kiuchumi wa muda m&#341;efu.<\/p>\n<p>Kamati ya Mkataba wa Wakazi (CPC), kundi la Wazimbabwe wanaopambana kupatikana kwa se&#341;a zinazowagusa watu, ilisema katika taa&#341;ifa kuwa kupambana na wachuuzi ni dalili ya halmashau&#341;i kushindwa kujua umuhimu wa wafanyabiasha&#341;a hawa wasiokuwa &#341;asmi katika uchumi.<\/p>\n<p>&#8220;Halmashau&#341;i haielewi umuhimu wa uchumi usiokuwa &#341;asmi katika maisha ya maelfu ya Wazimbabwe. Inaonyesha siyo tu kutokujua lakini kutokujali, kwa maslahi na mazingi&#341;a ambayo wakazi wanakabiliwa nayo,&#8221; CPC ilisema katika taa&#341;ifa yake.<\/p>\n<p>&#8220;CPC inatoa wito wa kumalizika kwa ha&#341;aka kwa hatua hizi zisizokuwa za kidemok&#341;asia za kuwasamba&#341;atisha maskini na kwa halmashau&#341;i kuja na mpango wa kutoa na kujenga fu&#341;sa za aji&#341;a.&#8221;<\/p>\n<p>Lakini Dumba anaendelea kusema kuwa wachuuzi wa mitaani wanahitaji leseni kuendesha shughuli zao katika jiji. <\/p>\n<p>&#8220;Hatutaki watu kusababisha ghasia katikati mwa jiji kwasababu ya kukosekana kwa aji&#341;a nchini. Hatuwezi ku&#341;uhusu watu kuuza bidhaa zao mahali popote pale. Tuna wasiwasi kuhusu masuala ya afya na usafi.&#8221;<\/p>\n<p>Bouazizi ameshafa&#341;iki muda m&#341;efu lakini mapambano yake ya kupata maisha bo&#341;a yanabakia kuwa ya kawaida kwa maskini na waliopo pembezoni ba&#341;ani Af&#341;ika.<\/p>\n<p>Joel Njagi na mtoto wake wa kiume Tinashe wanauza shoka na majembe ili kuendesha maisha yao. Ni baadhi ya wachuuzi katikati mwa Ha&#341;a&#341;e ambao wamepambana na polisi katika maandamano ya ka&#341;ibuni.<\/p>\n<p>Hawajawahi kujua aina nyingine ya aji&#341;a isipokuwa kutengeneza na kuuza majembe na shoka. Kwa wao muda ni mgumu mno na watafanya kila wawezalo kuwapatia kipato cha kuendeshea maisha yao. Njagi aliapa kutua shoka kichwani mwa &#8220;yeyote atakayeja&#341;ibu kuchukua mali zake.&#8221;<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>HARARE, Ma&#341; 1 (IPS) &ndash; Kuna jinsi ambavyo huwezi kutofautisha kati ya maisha ya Mohammed Bouazizi, muuza matunda wa Tunisia ambaye alichochea mapinduzi ya Ua&#341;abuni, na F&#341;ancis Tachi&#341;ev, muuza matunda nchini Zimbabwe. Maandamano ambayo aliyaanzisha yalianza baada ya Bouazizi kujichoma moto baada ya polisi kumpo&#341;a mkokoteni wake wa kuuzia matunda. Maandamano ya nchi nzima baada&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":303,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-3812","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3812","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/303"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=3812"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3812\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=3812"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=3812"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=3812"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}