{"id":3807,"date":"2012-02-07T13:40:01","date_gmt":"2012-02-07T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2012\/02\/07\/sierra-leone-kuwatenga-wagonjwa-wa-kifafa\/"},"modified":"2012-02-07T13:40:01","modified_gmt":"2012-02-07T13:40:01","slug":"sierra-leone-kuwatenga-wagonjwa-wa-kifafa","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2012\/02\/07\/sierra-leone-kuwatenga-wagonjwa-wa-kifafa\/","title":{"rendered":"SIERRA LEONE: Kuwatenga Wagonjwa wa Kifafa"},"content":{"rendered":"<p>FREETOWN, Feb 7, 2012 (IPS) &ndash; Alipoanguka kwa ma&#341;a ya kwanza, Elizabeth Zainab Ka&#341;gbo alikuwa mwanamke mwenye mafanikio katika um&#341;i wake wa ujana, mwenye mimba ya miezi nane na aliyefanya kazi katika sekta ya utumishi wa umma nchini Sie&#341;&#341;a Leone.\n <\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>Anakumbuka ilivyokuwa: mapigo yake ya moyo yaliongezeka kwa kasi, giza lilimjia, na baadaye alipata fahamu akiwa amelala sakafuni.<\/p>\n<p>Hakuna aliyefahamu ilikuwa ni kitu gani. Alipoteza aji&#341;a na kichanga chake, na wakati mashambulizi yalipozidi kujitokeza, ma&#341;afiki wengi, maji&#341;ani na wanafamilia walimkimbia.<\/p>\n<p>&#8220;Nilipopatwa na mshtuko na kudondoka chini, watu waliniogopa mno, walikimbia,&#8221; anasema Ka&#341;gbo.<\/p>\n<p>&#8220;Wanasema, &#8216;Usimguse, usimguse, atakuambukiza.&#8217; Hivyo kuna wakati nikianguka napata maje&#341;aha usoni mwangu.&#8221;<\/p>\n<p>Ka&#341;gbo anaugua kifafa, ugonjwa ambao unaathi&#341;i kati ya watu 60,000 hadi 100,000 katika taifa hilo la Af&#341;ika Magha&#341;ibi lenye watu wanaozidi kidogo milioni sita. Wengi bado hawajatambuliwa na ni watu wapatao 2,500 tu wanapata tiba. Wagonjwa hapa ma&#341;a nyingi wanatengwa, wanafukuzwa kutoka katika jamii zao, na hawatambui kuwa ugonjwa walionao unaweza kutibika kwa kiasi kikubwa.<\/p>\n<p>Baada ya Ka&#341;gbo kuanza kupata uzoefu wa kuanguka, mama yake alimpeleka kwa mganga wa kienyeji. Aliingizwa katika kichumba na kutakiwa kuvua nguo zake zote &ndash; na kuambiwa aahidi kutokumweleza mtu yoyote kitakachotokea.<\/p>\n<p>Alipenda kuwa mzima, hivyo aliahidi kutokutoa si&#341;i, alivua nguo zake na kuanza kuingiliwa kimwili.<\/p>\n<p>Pamoja na kuahidi kutokusema, Ka&#341;gbo alimwambia mama yake. Huo ulikuwa mwisho wa waganga wa jadi, anasema huku akitabasamu.<\/p>\n<p>Max Bangu&#341;a, m&#341;atibu na mwanzilishi wa Chama cha Kifafa Sie&#341;&#341;a Leone, ameshawahi kusikia haba&#341;i nyingi zinazofanana na ile ya Ka&#341;gbo.<\/p>\n<p>Ma&#341;a nyingi kuanguka kifafa kunahusishwa na uchawi, laana au hata kupagawa na mapepo, anasema Bangu&#341;a, ambaye chama chake kinatoa ushau&#341;i nasaha na tiba kwa wagonjwa wa kifafa na kuendesha mpango mdogo wa mafunzo ya ufundi stadi.<\/p>\n<p>Kuna imani imeenea sana kuwa ugonjwa huo unaambukiza, imani ambayo inazidisha kutengwa kwa wagonjwa wa kifafa. Bangu&#341;a anasema hata wale waliowahi kufika kwenye vituo vya afya wameshau&#341;iwa kwenda kwa waganga wa jadi kwasababu wataalam wa tiba hawakujua dalili za kifafa.<\/p>\n<p>Ma&#341;a nyingi watu wanaougua ugonjwa wa kifafa wanaondolewa kutoka shule, makazini, majumbani na kupelekwa kwa waganga wa jadi ambao, anasema, &#8220;wanawasababishia mateso&#8221; &ndash; wanachanjwa chale, wanaunguzwa moto, na kunyweshwa au kunusishwa madawa. Mmoja wa wanachama wa chama hicho aliokoka kunywa lita mbili za mafuta ya taa. Wasichana na wanawake wa um&#341;i mdogo wanatumbukia katika udhalilishwaji wa kingono kwa madai kuwa ni &#8220;tiba&#8221; ya ugonjwa huo, anasema Bangu&#341;a.<\/p>\n<p>Tiba ya kutumia vidonge vya kutibu kifafa aina ya &#8220;phenoba&#341;bital&#8221;, inagha&#341;imu Leone 10,000 (dola zipatazo mbili) kwa mwezi nchini Sie&#341;&#341;a Leone na inafanya kazi kwa asilimia 70 katika kudhibiti kifafa. Lakini watu wachache mno wanatumia dawa hiyo &ndash; wengi hawawezi kuimudu.<\/p>\n<p>&#8220;Watu hawajitokezi. Watu hawataki kujulikana kuwa wana kifafa,&#8221; anasema Bangu&#341;a. &#8220;Unyanyapaa unaoambatana na ugonjwa huo unawafanya watu kutokwenda kwenye vituo vya afya kwasababu hawataki mtu yoyote kufahamu hali yao.&#8221;<\/p>\n<p>Changamoto za kutibu kifafa nchini Sie&#341;&#341;a Leone ni kubwa. Mfumo wa afya duni nchini humo unakabiliwa na matatizo ya magonjwa ya kawaida na ambayo yanasababisha madha&#341;a makubwa kama vile mala&#341;ia,kuha&#341;a na maambukizi ya koo huku kukiwepo na miundombinu michache na watalaam wachache wa afya. Ni ugonjwa ambao unashindana na magonjwa mengi katika mfumo ambao una uhaba mkubwa wa &#341;asilimali.<\/p>\n<p>Dk. Radcliffe Du&#341;odami Lisk, mtaalam pekee wa mfumo wa fahamu katika taifa lenye watu wapatao milioni sita, anaendesha M&#341;adi wa Kifafa, ambao unafanya kazi na chama cha Bangu&#341;a kutoa huduma nchini kote.<\/p>\n<p>Ukiwa unafadhiliwa na mashi&#341;ika ya misaada ya Uinge&#341;eza, m&#341;adi huo unaendesha kliniki tatu mjini F&#341;eetown na moja mjini Bo, mji wa pili kwa ukubwa nchini humo, ambazo zinafanya kazi tofauti na hospitali za se&#341;ikali. Wafanyakazi wake wanasafi&#341;i katika maeneo mengine ya nchi kila mwezi kusambaza madawa na kutoa huduma.<\/p>\n<p>Sie&#341;&#341;a Leone ina kiasi kikubwa cha wagonjwa wa kifafa ikilinganishwa na mataifa mengi ya Magha&#341;ibi, kutokana na sababu zinazosababisha ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na ugonjwa wa uti wa mgongo, kupata maje&#341;aha wakati wa kuzaliwa na mala&#341;ia ya ubongo.<\/p>\n<p>Wagonjwa wengi hawawezi kumudu kununua madawa, hata katika gha&#341;ama ya dola mbili kwa mwezi, anasema Lisk.<\/p>\n<p>&#8220;Ingekuwa jambo jema kama tungetoa tiba ya bu&#341;e kwasababu wengi wa wagonjwa hawa hawawezi kufanya kazi &ndash; na hakuna anayeweza kuwaaji&#341;i,&#8221; anasema Lisk. &#8220;Tunaishia kuwapatia wagonjwa wachache madawa ya bu&#341;e na kuja&#341;ibu kubeba gha&#341;ama sisi wenyewe.&#8221;<\/p>\n<p>Lakini changamoto kubwa, anasema Lisk, ni kushawishi watu kujitokeza na kupata tiba.<\/p>\n<p>&#8220;Hawaamini kuwa ni ugonjwa unaoweza kutibiwa kwa madawa ya hospitalini,&#8221; anasema. &#8220;Hata hawafiki&#341;ii kwenda kumuona dakta&#341;i kwani wanadhani kuwa huu ni ugonjwa wa mashetani au uchawi.&#8221;<\/p>\n<p>Katika njia nyembamba nyuma ya msikiti masha&#341;iki mwa F&#341;eetown, kiasi cha wanafunzi wameinamia mashine za che&#341;ehani katika jengo ambalo ujenzi wake bado haujakamilika. Makao makuu ya chama cha kifafa yanatumika pia kama nyumbani kwa familia ya Bangu&#341;a, na kituo cha mafunzo ya ufundi stadi, kijulikanacho kama &#8220;Taasisi ya Upendo&#8221; kwa watu wapatao 20 wenye kifafa.<\/p>\n<p>Katika mahali hapa, watu wenye kifafa wanajifunza biasha&#341;a na wanapatiwa ushau&#341;i nasaha na msaada na tiba. Bangu&#341;a amekuwa akiendesha chama kwa miaka 11 kutokana na fedha alizopata kutokana na wahisani na michango ya wanachama.<\/p>\n<p>Che&#341;no&#341; Dumbuya alikuwa emebeba kikapu kilichojaa vyakula kwa ajili ya kupika kutoka soko la mjini F&#341;eetown, Sie&#341;&#341;a Leone, akimpelekea mama yake wakati alipoanguka kwa ma&#341;a ya kwanza. Akiwa na um&#341;i wa miaka kumi na tatu wakati huo, Dumbuya aliangusha mzigo wake huku povu likimtoka mdomoni. Kila aliyemuona alikimbia.<\/p>\n<p>Akawa anaendelea kuanguka, na hakuna aliyejua hali hiyo ilisababishwa na nini. Maji&#341;ani na ma&#341;afiki walimuogopa.<\/p>\n<p>&#8220;Wote walikimbilia mbali,&#8221; anasema Dumbuya, ambaye kwa sasa ana um&#341;i wa miaka 28. &#8220;Wote walikimbilia mbali.&#8221;<\/p>\n<p>Tangu alipoanza kutumia tiba, ni kama tu sasa haanguki tena, na alikuwa wa kwanza kuhitimu katika mpango wa mafunzo ya miaka mitatu ya chama hicho, kwa kumaliza mwaka 2007 na kuendelea kufanya kazi kama fundi che&#341;enani.<\/p>\n<p>Baada ya miaka mingi ya kuishi katika hali ya kutengwa, Ka&#341;gbo alianza kusoma hapa mwaka mmoja uliopita na chama kilimuunganisha na tiba. Anapata fedha kulipia tiba yake kutoka kanisani kwake.<\/p>\n<p>&#8220;Kama(unaelezea ma&#341;adhi yako), unapata msaada,&#8221; anasema. <\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>FREETOWN, Feb 7, 2012 (IPS) &ndash; Alipoanguka kwa ma&#341;a ya kwanza, Elizabeth Zainab Ka&#341;gbo alikuwa mwanamke mwenye mafanikio katika um&#341;i wake wa ujana, mwenye mimba ya miezi nane na aliyefanya kazi katika sekta ya utumishi wa umma nchini Sie&#341;&#341;a Leone. Anakumbuka ilivyokuwa: mapigo yake ya moyo yaliongezeka kwa kasi, giza lilimjia, na baadaye alipata fahamu&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":900,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-3807","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3807","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/900"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=3807"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3807\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=3807"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=3807"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=3807"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}