{"id":3805,"date":"2012-01-27T13:40:01","date_gmt":"2012-01-27T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2012\/01\/27\/kuhamasisha-kilimo-cha-embe-kupunguza-madhaa-ya-mabadiliko-ya-tabia-nchi\/"},"modified":"2012-01-27T13:40:01","modified_gmt":"2012-01-27T13:40:01","slug":"kuhamasisha-kilimo-cha-embe-kupunguza-madhaa-ya-mabadiliko-ya-tabia-nchi","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2012\/01\/27\/kuhamasisha-kilimo-cha-embe-kupunguza-madhaa-ya-mabadiliko-ya-tabia-nchi\/","title":{"rendered":"Kuhamasisha Kilimo cha Embe Kupunguza Madha&#341;a ya Mabadiliko ya Tabia Nchi"},"content":{"rendered":"<p>DAR ES SALAAM, Jan 26, 2012 (IPS) &ndash; Mabadiliko ya tabia nchi yapo kila mahali, ni dhahi&#341;i na madha&#341;a yake yanajidhihi&#341;isha kwa uwazi zaidi kuliko siku za nyuma. Yanaathi&#341;i watu kutoka kila sekta na nyanja zote za maisha. Watu wanaoathi&#341;ika zaidi ni wale wanaoishi katika nchi zinazoendelea hususan katika Af&#341;ika Kusini mwa Jangwa la Saha&#341;a ambako zaidi ya asilimia 80 ya wakazi wake wanategemea kilimo cha mvua.\n<\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>Wataalam wanabashi&#341;i kuwa kilimo katika Af&#341;ika Kusini mwa Jangwa la Saha&#341;a kitaathi&#341;ika zaidi na mabadiliko ya tabia nchi. Hadi ifikapo mwaka 2050, mabadiliko katika mwenendo wa hali ya hewa utasababisha kupungua kwa wastani wa mavuno ya mpunga, ngano na mahindi kwa asilimia 14, 22 na asilimia tano kwa mpangilio huo hapo juu, hii ni kwa mujibu wa shi&#341;ika lenye makao yake mjini Washington DC lijulikanalo kama Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Se&#341;a za Chakula (Inte&#341;national Food Policy Resea&#341;ch Institute).<\/p>\n<p>&#8220;Kila mtu anatambua mabadiliko katika mwenendo wa mvua, ambayo yamekuwa na madha&#341;a makubwa kwa mamilioni ya watu ambao wanategemea kilimo cha mvua, hususan ba&#341;ani Af&#341;ika,&#8221; alisema Dk. Tomaz Salom&atilde;o, katibu mkuu wa Jumiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Af&#341;ika alipokuwa akitoa maoni yake juu ya msimamo wa Af&#341;ika katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa 17 wa Mabadiliko ya Tabia Nchi Ulimwenguni (COP 17), uliofanyika mjini Du&#341;ban, Af&#341;ika Kusini, kuanzia Novemba 28 hadi Desemba 9 2011.<\/p>\n<p>Tanzania na hasa jamii za pwani, ni miongoni mwa waathi&#341;ika wakuu wa mabadiliko haya.<\/p>\n<p>&#8220;Mabadiliko ya tabia nchi ni dhahi&#341;i &#8230; kuongezeka kwa maji ya baha&#341;i kunaathi&#341;i a&#341;dhi ya kilimo na kumeza baadhi ya visima vya maji ba&#341;idi katika mwambao wa Tanzania ba&#341;a pamoja na Zanziba&#341;, na hivyo kuongeza changamoto za kimaendeleo kwa jamii za pwani ambazo kwa kiasi kikubwa hutegemea kilimo cha kujikimu kuendesha maisha yao,&#8221; alisema Wazi&#341;i wa Nchi wa Zamani katika Ofisi ya Makamu wa Rais &ndash; Mazingi&#341;a &ndash; Dk Batilda Bu&#341;ian, alipokuwa akizindua Ripoti ya Hali ya Idadi ya Watu Duniani jijini Da&#341; es Salaam mwaka 2009. <\/p>\n<p>Kwa mujibu wa &#341;ipoti ya M&#341;adi wa Pwani wa Ushi&#341;ika wa Kusimamia Rasilimali na Mazingi&#341;a ya Pwani (TCMP Pwani) unaofadhiliwa na Shi&#341;ika la Maendeleo ya Kimataifa la Ma&#341;ekani USAID), &#8220;madha&#341;a ya mabadiliko ya tabia nchi yanaonekana wazi katika maeneo mengi ya pwani nchini Tanzania. Madha&#341;a yanata&#341;ajiwa kuongezeka zaidi katika siku zijazo na kuha&#341;ibu kabisa bayoanuwai tete katika maeneo hayo, kuathi&#341;i vibaya wakazi wa pwani, watumiaji wa &#341;asilimali za pwani, maeneo ya bu&#341;udani, miundombinu, uvuvi na utalii kama hakutachukuliwa hatua za ha&#341;aka na madhubuti.<\/p>\n<p>Jumuiya maskini za pwani ma&#341;a nyingi ndizo zinazoathi&#341;ika zaidi na zenye uwezo mdogo wa kujikwamua na madha&#341;a hayo.<\/p>\n<p>Ili kusaidia jamii za pwani kuendesha maisha katika mazingi&#341;a ya mabadiliko ya tabia nchi, m&#341;adi wa TCMP Pwani uliendesha tathmini ya kujua madha&#341;a yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi na mipango ya kuendesha maisha katika hali hiyo ya mabadiliko katika vijiji vya Mlingotini na Kitonga wilayani Bagamoyo. <\/p>\n<p>Ripoti ya tathmini iligundua kuwa vijiji hivyo viwili vinakabiliwa na tishio la kuongezeka kwa maji ya baha&#341;i, maji ya chumvi kuvamia vyanzo vya maji ba&#341;idi, uha&#341;ibifu wa miundombinu katika mwambao wa pwani, kupungua kwa uzalishaji wa zao la biasha&#341;a la mwani, kupungua kwa samaki wanaovuliwa, kuongezeka kwa mafu&#341;iko, ukame na mvua zisizokuwa za kuaminika.<\/p>\n<p>Kwa mujibu wa &#341;ipoti hiyo, hali ya mabadiliko ya tabia nchi inahitaji hatua madhubuti kuchukuliwa ili kuhakikisha kuwa jamii za pwani katika vijiji hivyo zinaendesha maisha yao hata baada ya kujitokeza mabadiliko makubwa zaidi ya hayo. Moja ya ufumbuzi ni kuwa na mipango ya shughuli mbadala kama vile upandaji wa mazao ambayo hayawezi kuathi&#341;ika kiu&#341;ahisi na mabadiliko ya hali ya hewa. <\/p>\n<p>Kilimo cha embe katika kijiji cha Kitonga katika eneo la Ruvu kwenye njia kuu ya maga&#341;i yaendayo mkoani wilayani Bagamoyo, m&#341;adi wa maja&#341;ibo ulioanzishwa na wanakijiji wa Kitonga na kupatiwa msaada na TCMP Pwani, unata&#341;ajiwa kuwa haba&#341;i njema ya mafanikio ya baadaye ya jinsi wanajamii katika maeneo ya pwani wanavyoweza kuendesha maisha yao katika hali ya mabadiliko ya tabia nchi.<\/p>\n<p>Kwa mujibu wa mwenyekiti wa kijiji cha Kitonga na mjumbe wa Kamati ya Mabadiliko ya Tabia Nchi ya Kijiji, Hamis Njagila, m&#341;adi ulianza Septemba 2010 kwa kuchagua wajumbe 12 &ndash; 6 wanaume na sita wanawake katika Mkutano Mkuu wa Kijiji ili kuunda Kamati ya Mabadiliko ya Tabia Nchi ya Kijiji kuanza utekelezaji wa m&#341;adi wa maja&#341;ibio wa kilimo cha embe. Kamati ilichagua kilimo cha embe baada ya ushau&#341;iano na Kamati ya Mazingi&#341;a ya Pwani ya Wilaya ya Bagamoyo na wataalam wa mabadiliko ya tabia nchi wa m&#341;adi wa TCMP Pwani, baada ya kufanya zia&#341;a ya kubadilishana uzoefu katika kijiji cha Mlingotini na baada ya kuhudhu&#341;ia wa&#341;sha ya kuongeza ufahamu wa mabadiliko ya tabia nchi. <\/p>\n<p>Jitihada za jamii zimewezesha kusafishwa kwa eka&#341;i 24 za a&#341;dhi, inayomilikiwa na kamati hiyo chini ya uta&#341;atibu wa umiliki wa a&#341;dhi wa kijiji. M&#341;adi una lengo la kupanda miche ya miembe ipatayo 1250 chini ya usimamizi wa ka&#341;ibu wa watalaam wa mabadiliko ya tabia nchi wa TCMP Pwani na maofisa ugani wa wilaya ya Bagamoyo.<\/p>\n<p>Upandaji wa miembe ulichaguliwa na kamati ili kuongeza faida kwa jamii na mazingi&#341;a. Miembe inaweza kuzalisha matunda kwa ajili ya chakula, kipato kutokana na kuuza matunda hayo pamoja na mbao na asali pale inapotumika kwa ufugaji wa nyuki. Miembe pia inatoa kivuli, inazuia mmomonyoko wa udongo na inaweza kupunguza ongezeko la joto duniani kutokana na uwezo wake wa kunyonya hewa ukaa. Pia inaweza kusaidia wanajamii kufaidika na kipato kutokana na mpango wa kupunguza uzalishaji wa gesi chafu za viwandani kutokana na uangamizaji wa misitu (REDD).<\/p>\n<p>&#8220;Tuliamua kuhamasisha wanajamii kupanda miti ya miembe kutokana na faida nyingi zinazotokana na miti hiyo kwa ajili ya maisha yao na mazingi&#341;a,&#8221; anasema Jai&#341;os Mahenge, mkuu wa timu ya wataalam wa mabadiliko ya tabia nchi katika TCMP Pwani.<\/p>\n<p>Hata hivyo, mipango ya kuwezesha jamii kuendesha maisha wakati wa mabadiliko ya tabia nchi katika maeneo ya pwani haiwezi kutekelezwa bila ya kuwepo kwa changamoto. &#8220;Utekelezaji wa mipango ya kuwezesha jamii kuendesha maisha katika mabadiliko ya tabia nchi kunaleta changamoto mpya na hata uwezekano wa kusababisha migogo&#341;o. Wataalam wa masuala ya pwani wanahitaji kufahamu hali hii na kuishughulikia mapema,&#8221; kinasema Kijitabu cha Mwongozo kwa Wana Mipango ya Maendeleo Kuwezesha Jamii Kuendesha Maisha katika Mabadiliko ya Tabia Nchi Kwenye Maeneo ya Pwani.<\/p>\n<p>Moja ya changamoto kubwa ni mabadiliko ya hali ya hewa yanayojitokeza kila ma&#341;a ambayo yanaweza kuathi&#341;i mipango ya kuwawezesha wananchi kuendesha maisha yao katika mabadiliko. <\/p>\n<p>Kwa upande wa TCMP Pwani, zoezi la upandaji miche ya miembe ilibidi kufanyika katika maji&#341;a ya ukame kwa kutumia umwagiliaji. Kamati ya mabadiliko ya tabia nchi katika kijiji cha Kitonga ilipendekeza maji ya kumwagilia shamba hilo katika eneo hilo lenye uhaba mkubwa wa maji yatokane na chanzo kilichopo umbali wa kilomita nne kutoka shambani. Wanakamati wanatumia madumu ya ujazo wa lita 20 ili kuhakikisha kuwa m&#341;adi huo unafanikiwa.<\/p>\n<p>Mpango wa kupanda miche hiyo ya miembe wakati wa ukame ulitokana na dhana kuwa &#8220;mabadiliko ya tabia nchi hayana maji&#341;a, tunaweza kukaa kwa miaka mitatu bila mvua, je katika hali kama hiyo ya mabadiliko makubwa ya hali ya hewa tunafanyaje &#8221; anauliza Mahenge. &#8220;Kuna jibu moja tu, kukabiliana na hali kad&#341;i inavyowezekana&#8221;.<\/p>\n<p>Mahenge anasema hii ni sababu kuu ni kwa nini m&#341;adi huo wa maja&#341;ibio ulianza kutekelezwa wakati wa ukame. Anasema madha&#341;a ya mabadiliko ya tabia nchi katika ngazi ya jamii yanahitaji hatua za kukabiliana nayo ambazo hazitegemei moja kwa moja mvua. <\/p>\n<p>&#8220;Siyo jambo &#341;ahisi kufanya kwani suala lenyewe lina mambo mengi yanayohusiana. Linagusa, miongoni mwa mambo mengine, maeneo muhimu mno ambayo ni msingi wa maisha ya watu. Mambo hayo ni pamoja na kilimo na usalama wa chakula, masuala ya afya na aji&#341;a,&#8221; alisema Dk. Salom&atilde;o.<\/p>\n<p>&#8220;Tunachotakiwa kukubaliana nacho ni kwamba watu wanatakiwa kuja pamoja kuokoa ubinadamu, dunia yetu na kuhakikisha kuwa vizazi vijavyo vinakuwa na maisha bo&#341;a,&#8221; aliongeza.<\/p>\n<p>Wanajamii katika kijiji cha Kitonga wameshasikia wito huu. M&#341;adi huo wa maja&#341;ibio una lengo la kuhamasisha wengine katika kijiji na mazingi&#341;a yanayozunguka kijiji kujifunza njia za kuendesha maisha katika mabadiliko ya tabia nchi. Taa&#341;ifa zinaelezea kuwa taya&#341;i m&#341;adi umeshaanza kuvutia wanakijiji wengine ambao wanataka kuanzisha kilimo chao cha embe cha jumuiya. Lakini, matokeo kamili bado hayajapatikana. <\/p>\n<p>&#8220;Haba&#341;i ya mafanikio inata&#341;ajiwa kusikika baada ya miaka 3 wakati wanafamilia wetu watakapoanza kufaidi matunda kwa ajili ya chakula na kubo&#341;esha maisha yao kutokana na vipato vinavyotokana na kuuza matunda hayo&#8221;, alisema Njagila.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>DAR ES SALAAM, Jan 26, 2012 (IPS) &ndash; Mabadiliko ya tabia nchi yapo kila mahali, ni dhahi&#341;i na madha&#341;a yake yanajidhihi&#341;isha kwa uwazi zaidi kuliko siku za nyuma. Yanaathi&#341;i watu kutoka kila sekta na nyanja zote za maisha. Watu wanaoathi&#341;ika zaidi ni wale wanaoishi katika nchi zinazoendelea hususan katika Af&#341;ika Kusini mwa Jangwa la Saha&#341;a&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":155,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-3805","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3805","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/155"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=3805"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3805\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=3805"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=3805"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=3805"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}