{"id":3796,"date":"2012-01-26T13:40:01","date_gmt":"2012-01-26T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2012\/01\/26\/wanawake-wengi-wazee-hawana-pensheni\/"},"modified":"2012-01-26T13:40:01","modified_gmt":"2012-01-26T13:40:01","slug":"wanawake-wengi-wazee-hawana-pensheni","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2012\/01\/26\/wanawake-wengi-wazee-hawana-pensheni\/","title":{"rendered":"Wanawake Wengi Wazee Hawana Pensheni"},"content":{"rendered":"<p>ACCRA, Jan 25, 2012 (IPS) &ndash; Kando kando mwa Old Fadama, makazi duni yasiyokuwa halali maa&#341;ufu mjini Acc&#341;a, Ma&#341;iana Sayitou mwenye um&#341;i wa miaka 67 ameketi chini ya kivuli na anaendelea kujitafutia kipato kwa kuuza njugu mawe na kiasi kidogo cha maha&#341;age kwa wapita njia.\n<\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>Akiwa hajaguswa na mfumo duni wa kusaidia jamii nchini Ghana na kukosekana kwa uwezekano wa kufikiwa na mfumo wa pensheni, anawakilisha idadi kubwa ya wanawake wazee katika taifa hili la Af&#341;ika Magha&#341;ibi: ambao ni maskini, huku wakijitahidi kutafuta maisha na ma&#341;a nyingi wakiwa wamesahaulika. <\/p>\n<p>Wanaha&#341;akati wa jinsia wanasema hali hiyo ya wanawake kama Sayitou inasababishwa na sababu kadhaa, zikiwa ni pamoja na kiwango kidogo cha elimu kwa wanawake na kuongezeka kwa mifumo ya familia ndogo, ombwe la se&#341;a za huduma za jamii na ubaguzi wa kitamaduni. Katika picha hiyo kuna masoko ya aji&#341;a ya nchini Ghana, ambayo, kutokana na majukumu ya muda m&#341;efu ya jinsia, wanawake wengi wametumbukia katika sekta isiyokuwa &#341;asmi. <\/p>\n<p>&#8220;Tunahitaji kukubali kuwa wanawake wengi wanaongoza katika uchumi wetu,&#8221; anasema Elizabeth Qua&#341;co&#341; Akpalu, mku&#341;ugenzi mkuu wa shi&#341;ika la Watetezi wa Usawa wa Jinsia (Advocates fo&#341; Gende&#341; Equity). &#8220;Tunahitaji kufanya jambo kuwasaidia katika um&#341;i wao wa uzee. Wanakufa na maumivu.&#8221; <\/p>\n<p>Mume wa Sayitou alimpa talaka baada ya familia zao kuwa na ugomvi na aliweza kuwalea watoto wake watatu kati ya wanne. Anawanunulia nguo, chakula, na kulipia elimu yao kwa chini ya dola 19 anazoingiza kila siku (baadhi zinakwenda kwenye chakula chao, nguo, na bajeti ya biasha&#341;a). <\/p>\n<p>&#8220;Nataka kutunza watoto wangu,&#8221; anasema, &#8220;lakini pia anahisi maumivu ya kuishi peke yake. Naomba kuwa watoto wangu wanakuwa na afya njema, ili kesho waweze kunilea nitakaposhindwa kufanya kazi.&#8221; <\/p>\n<p>Ukiingia ndani zaidi katika makazi duni, Sanatu Seidu mwenye um&#341;i wa miaka 70 ameketi katika dawati katika eneo la wazi kwenye msingi wa zege unaoka&#341;ibia kudondoka. Amezungukwa na vyungu vinavyochemka. Huu ni mgawaha wake wa chakula wa Valne, unaouza chakula cha kaskazini. Kama ilivyo kwa Sayitou, yeye ni sehemu ya uchumi usiokuwa &#341;asmi. <\/p>\n<p>Alipoanza ka&#341;ibu miaka kumi na tano iliyopita, Seidu alipata faida kubwa ghafla, na kujenga biasha&#341;a katika jengo la kubeba watu 15, na kuingiza dola 375 kwa siku. Lakini wahamiaji wanaozidi kumiminika katika Old Fadama kutafuta aji&#341;a, na ushindani kutoka kwenye biasha&#341;a nyingine kumefanya faida yake kushuka hadi kufikia kati ya dola 60 na 90 kwa siku. <\/p>\n<p>Anatumia fedha hizo kulipia wafanyakazi sita, kufanya biasha&#341;a kuwa na bidhaa, kujilisha na kujivalisha yeye na watoto wake, ambao wawili kati ya hao wanaishi katika Mkoa wa Kaskazini, na kutunza mume wake mgonjwa, ambaye anaishi kaskazini. <\/p>\n<p>&#8220;Nakabiliwa na matatizo mengi kwasababu ya um&#341;i wangu,&#8221; anasema. &#8220;Ma&#341;a nyingine, nashindwa kujisaidia. Ma&#341;a nyingine, nalala tu kutokana na kuchoka au kuwa na maumivu mwilini.&#8221; <\/p>\n<p>Kuna mifumo ya pensheni nchini Ghana. Mkubwa zaidi ni mpango wa kishe&#341;ia unaoendeshwa na Hifadhi ya Jamii na Shi&#341;ika la Bima la Taifa (SSNIT) ambalo, ifikapo mwaka 2010, iliingiza watu 107,312 kutoka sekta binafsi na ya umma. Ni 17,229 tu kati yao walikuwa wanawake, kwasababu mpango huo ni kwa ajili ya wafanyakazi wa sekta &#341;asmi. <\/p>\n<p>&#8220;Ni kweli kuna wanaume wengi kuliko wanawake,&#8221; anasema Edwa&#341;d Ameyibo&#341;, katibu mkuu wa Chama cha Pensheni cha Taifa. &#8220;Katika mfumo wetu, ni wanaume ambao wanafanya kazi katika sekta &#341;asmi. Na wanawake wanafanya kazi katika mfumo usiokuwa &#341;asmi.&#8221; <\/p>\n<p>Kwa mujibu wa &#341;ipoti ya mwaka ya SSNIT 2010, walengwa wanapata kati ya dola 26 na 1,250 kwa mwezi. Baadhi wanafaidika na mafao madogo ya uzeeni ya miaka ya 1990, wakati mishaha&#341;a nchini Ghana ulipokuwa mdogo zaidi na michango ilikuwa midogo. <\/p>\n<p>Wale wanaopata mafao makubwa walifanya kazi katika aji&#341;a zenye kipato cha juu, wakipewa mishaha&#341;a mikubwa na kutoa michango mikubwa. Kuna wanaume 94 wanaopata pensheni ya zaidi ya dola 1,250&ndash;, ikilinganishwa na wanawake 11 tu. Zaidi ya asilimia 50 ya walengwa wanapata chini ya dola 62 kwa mwezi. <\/p>\n<p>Chama cha Pensheni cha Taifa kimekuwa kikipambana na SSNIT ili kuwa na ongezeko la chini, lakini hakujawa na mafanikio yoyote. Hadi hivi ka&#341;ibuni, SSNIT imekuwa ikitoa asilimia ya ongezeko la kila mwaka kwa kujikita katika faida ya uwekezaji wa mfuko. Mwaka jana, waliongeza dola sita kwa mwezi. Chama hicho kinatoa wito wa ongezeko la dola 62 kwa mwezi. <\/p>\n<p>Wakati huo huo, SSNIT ina mpango wa sekta isiyokuwa &#341;asmi. Ulianza kama m&#341;adi wa maja&#341;ibio mwaka 2005 na kufikia taifa zima baadaye miaka mitatu. Ni mpango unaobadilika, unao&#341;uhusu wanachama kuchangia wanachokiweza. Michango inahifadhiwa katika akaunti mbili, mmoja kwa ajili ya wastaafu na mwingine kwa maisha ya kazi. Akaunti ya maisha inaweza kutumika kila baada ya michango ya miezi mitano, mfumo ambao SSNIT anasema unavutia wafanyakazi vijana kuingia katika mpango huo. <\/p>\n<p>Lakini asilimia 32 tu ya wachangiaji katika akaunti 90,000 ni wanawake. Wakazi wa Ghana wapatao milioni 24 wamegawanyika sawa kati ya wanawake na wanaume, pamoja na kuwa wanawake wanaishi um&#341;i m&#341;efu zaidi. Na wakati kuna wanaume wengi katika sekta isiyokuwa &#341;asmi &ndash; wachuuzi, wavuvi, mafundi uashi &ndash; wanaha&#341;akati wanasema wanawake ndiyo wahusika wakuu. Hata hivyo, hakuna sababu ni kwa nini wanawake wachache wanashi&#341;iki katika mpango huo. <\/p>\n<p>&#8220;Hapo ndipo unakuta wanawake wengi, katika sekta isiyokuwa &#341;asmi,&#8221; anasema Akpalu. &#8220;Bila ya kuwa na elimu nzu&#341;i, haitawezekana kwa wengi kuwa katika sekta binafsi. Hata baadhi ambao wana elimu, kama ukiangalia walipo, ni kama pi&#341;amidi. Wako chini.&#8221; <\/p>\n<p>Pensheni nyingine, kuna mpango wa Kuwapatia Wanawake Kipato Kupambana na Umaskini (LEAP), ambao umebuniwa kwa maskini, yatima, walemavu, na wazee. Mpango huo, ambao unakua mwaka hadi mwaka, unalenga kaya 55,000, ambazo kati ya hizo asilimia 35 ni wazee. Katika asilimia hiyo, asilimia 65 ni wanawake. <\/p>\n<p>Kutegemeana na ukubwa wa kaya, faida ni kati ya dola tano na tisa kwa mwezi, zinazolipwa ma&#341;a sita kwa mwaka. <\/p>\n<p>&#8220;LEAP ni ndogo mno na zisizokuwa na maana,&#8221; anasema Akpalu. &#8220;Haishughulikii tatizo lolote lile.&#8221; <\/p>\n<p>Msaada wa nyongeza unakuja kutoka kwa mashi&#341;ika yasiyokuwa ya kise&#341;ikali, makanisa, na familia za wakazi wengi. <\/p>\n<p>Kwa sasa, katiba ya Ghana yenye um&#341;i wa miaka 20 inafanyiwa ma&#341;ekebisho. Jopo la kufanyia ma&#341;ekebisho, lililoanzishwa mwaka 2010, lilisafi&#341;i nchi nzima kukusanya maoni ya wananchi, na &#341;ipoti ya mwisho inafanyiwa kazi. Mtandao wa Haki za Wanawake Ghana unataka kupanua fasili ya ubaguzi katika katiba kuingiza ubaguzi unaosababishwa na mifumo ya kiuchumi na kitamaduni, ikiwa ni pamoja na kushughulikia masuala kadhaa ya haki za binadamu. <\/p>\n<p>&#8220;Kamati haijaingiza masuala mengi,&#8221; anasema Akpalu. <\/p>\n<p>Sayitou hapati shida ya utetezi. Anakubaliana na maisha yake na anapenda kazi anazofanya. Kila kitu ni maisha ya haki. <\/p>\n<p>&#8220;Baadhi ya watu, wamekua wameteseka tangu utotoni,&#8221; anasema. &#8220;Lakini kupitia hili, mtu anaweza kufanya kila kitu mwenyewe, kwasababu ana uwezo wa kufanikiwa. Baadhi ya watu wanazidi kuwa mataji&#341;i na wanapokuwa na um&#341;i mkubwa wanakuwa hawawezi kufanya kazi. Hawajui jinsi ya kufanya kazi.&#8221; <\/p><\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>ACCRA, Jan 25, 2012 (IPS) &ndash; Kando kando mwa Old Fadama, makazi duni yasiyokuwa halali maa&#341;ufu mjini Acc&#341;a, Ma&#341;iana Sayitou mwenye um&#341;i wa miaka 67 ameketi chini ya kivuli na anaendelea kujitafutia kipato kwa kuuza njugu mawe na kiasi kidogo cha maha&#341;age kwa wapita njia. Akiwa hajaguswa na mfumo duni wa kusaidia jamii nchini Ghana&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":896,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-3796","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3796","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/896"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=3796"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3796\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=3796"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=3796"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=3796"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}