{"id":3786,"date":"2012-01-10T13:40:01","date_gmt":"2012-01-10T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2012\/01\/10\/ni-kwa-nini-afika-inapaswa-kuungana-duban\/"},"modified":"2012-01-10T13:40:01","modified_gmt":"2012-01-10T13:40:01","slug":"ni-kwa-nini-afika-inapaswa-kuungana-duban","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2012\/01\/10\/ni-kwa-nini-afika-inapaswa-kuungana-duban\/","title":{"rendered":"Ni kwa Nini Af&#341;ika Inapaswa Kuungana Du&#341;ban"},"content":{"rendered":"<p>DURBAN, Af&#341;ika Kusini, Jan 10 (IPS) &ndash; Viongozi wa Af&#341;ika wameitaka jumuiya ya kimataifa kuendesha majadiliano ya mabadiliko ya tabia nchi ya Umoja wa Mataifa, ambayo yameshaanza mjini Du&#341;ban, Af&#341;ika Kusini siku ya Jumatatu, katika ngazi tofauti, na kuwa na vipaumbele vya kukabiliana na mabadiliko hayo katika ba&#341;a.\n <\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>Rais wa Af&#341;ika Kusini Jacob Zuma alibainisha kuwa Af&#341;ika imetoka mbali tangu mazungumzo kama hayo yalipofanyika mjini Copenhagen na Cancun, katika miaka miwili iliyopita. Alisema kuwa ni lazima Du&#341;ban kuipeleka dunia mbele katika &#8220;kupata ufumbuzi ambao utaiokoa kesho leo hii.&#8221;<\/p>\n<p>Wataalam wengi wa mazingi&#341;a wamekusanyika mjini Du&#341;ban wakiwa na mata&#341;ajio mkutano huo utaamua hatma ya Itifaki ya Kyoto. Itifaki hiyo, ambayo inamaliza muda wake mwaka 2012, inaweka shabaha zinazofunga kwa mataifa 37 yenye viwanda vingi duniani na jumuiya ya Ulaya kupunguza gesi joto yanazozalisha.<\/p>\n<p>Dk. Tomaz Salom&atilde;o, katibu mkuu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Af&#341;ika (SADC), alikuwa katika Mkutano wa 17 wa Pande Zinazohusika na Mkataba wa Mabadiliko ya Tabia Nchi wa Umoja wa Mataifa (COP 17). <\/p>\n<p>Aliiambia IPS ni kwa nini COP 17 ni muhimu kufanyika ba&#341;ani Af&#341;ika, na ukanda huo unata&#341;ajia nini kutokana na jukwaa hilo la majadiliano. <\/p>\n<p>Sehemu ya mahojiano inafuata:<\/p>\n<p>Swali: Nini umuhimu wa kufanyika kwa mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi wa 17 katika kanda ya Kusini mwa Af&#341;ika  <\/p>\n<p>Jibu: Ba&#341;a zima, na hasa ukanda wa Kusini mwa Af&#341;ika, linatishiwa na madha&#341;a ya mabadiliko ya tabia nchi. Wataalam wamesema kila kitu. Wamekadi&#341;ia kuwa kuongezeka kwa mabadiliko makubwa ya hali ya hewa, na ukame kumekuwa ni suala la ma&#341;a kwa ma&#341;a zaidi kuliko ilivyokuwa hapo siku za nyuma. Kila mtu anatambua mabadiliko ya mwenendo wa mvua, ambayo yamekuwa na madha&#341;a makubwa kwa mamilioni ya watu ambao wanategemea kilimo cha mvua, hasa ba&#341;ani Af&#341;ika.<\/p>\n<p>Kwa hivyo ni mafanikio ya kupongezwa kwa Af&#341;ika, kwa ukanda wa SADC, na pia Af&#341;ika Kusini kwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa COP 17 katika kanda. Ni dalili ya wazi kuwa Waaf&#341;ika wanatambua wapi tunasimamia, ni changamoto gani tunakabiliana nazo, na jinsi gani ya kuzishughulikia. Kinachotakiwa ni kujenga uwezo wetu ili tuwe katika nafasi nzu&#341;i zaidi ya kukabiliana na changamoto zetu.<\/p>\n<p>Swali: Mata&#341;ajio ya kanda juu ya mkutano huu ni nini  <\/p>\n<p>Jibu: Mata&#341;ajio ni kuwa mapendekezo yatatolewa ili kupatiwa msaada wa kifedha ambao unahitajika ili Af&#341;ika kuwa katika nafasi nzu&#341;i zaidi ya kukabiliana na changamoto za sasa zinazoha&#341;ibu mazingi&#341;a katika ba&#341;a. Hilo ndilo tumaini langu, na ndilo tumaini letu sote. <\/p>\n<p>Swali: Je kuna mfumo wowote mpya juu ya msimamo wa kikanda wa COP 17  <\/p>\n<p>Jibu: Nadhani kuwa hatuwezi kubadili msimamo kila ma&#341;a. Tunapaswa kuwa na mwelekeo juu ya misimamo tunayokuwa nayo na ambayo tuliibuni katika mkutano wa Copenhagen, ambao ulikuwa wa COP 15. Kwa wakati huu, mataifa ya Af&#341;ika yalikuja pamoja kuwa na sauti ya pamoja na hiyo ilitengeneza msimamo wetu kama Waaf&#341;ika. Natumaini moyo kama huo utaendelezwa hata huko Du&#341;ban.<\/p>\n<p>Swali: Af&#341;ika inahitaji nini kwa sasa, ili iweze kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi  <\/p>\n<p>Jibu: Tunahitaji maendeleo. Na hatuwezi kuendelea kupewa adhabu kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, ambayo yanakuja kutokana na matatizo ambayo yamesababishwa na wengine. Hapo ndipo tunapoanzia. Na hiyo ndiyo sababu tunasema tunahitaji msaada kushughulikia changamoto hizo. Kwa kufanya hivi, hatuombi fedha nyingi.<\/p>\n<p>Swali: Kwa nini inachukua muda m&#341;efu mno kwa waendesha mazungumzo kuja na mpango endelevu  <\/p>\n<p>Jibu: Siyo jambo &#341;ahisi kwasababu suala lenyewe ni gumu. Linagusa maeneo yote muhimu kwa maisha. Maeneo hayo ni pamoja na kilimo na usalama wa chakula, masuala ya afya, aji&#341;a miongoni mwa mengine. Wakati huo huo, kuzitaka nchi kupunguza uzalishaji wa gesi joto kunagusa moja kwa moja njia zao za maendeleo. Kwa sasa kuna hoja kuwa nchi zinazoendelea hazipaswi kuzuiliwa kufuata njia zao za maendeleo kutokana na uzalishaji wa gesi joto kutoka nchi nyingine miaka kadhaa iliyopita, wakati zilipokuwa zikiendeleza nchi zao.<\/p>\n<p>Swali: Nini kitatokea kama Itifa ya Kyoto itashindwa kuwepo baada ya COP 17  <\/p>\n<p>Jibu: Hapana sidhani mkataba wa Kyoto upo katika nafasi ya kufa wakati huu. Tunachohitaji kukifanya ni kwa watu kuja pamoja kumwokoa binadamu, dunia na kuhakikisha kuwa vizazi vijavyo vinakuwa na kesho bo&#341;a. <\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>DURBAN, Af&#341;ika Kusini, Jan 10 (IPS) &ndash; Viongozi wa Af&#341;ika wameitaka jumuiya ya kimataifa kuendesha majadiliano ya mabadiliko ya tabia nchi ya Umoja wa Mataifa, ambayo yameshaanza mjini Du&#341;ban, Af&#341;ika Kusini siku ya Jumatatu, katika ngazi tofauti, na kuwa na vipaumbele vya kukabiliana na mabadiliko hayo katika ba&#341;a. Rais wa Af&#341;ika Kusini Jacob Zuma alibainisha&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":892,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-3786","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3786","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/892"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=3786"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3786\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=3786"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=3786"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=3786"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}