{"id":3778,"date":"2011-12-08T13:40:01","date_gmt":"2011-12-08T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2011\/12\/08\/malawi-madawa-ya-kutuliza-maumivu-yatumika-kutibu-malaia\/"},"modified":"2011-12-08T13:40:01","modified_gmt":"2011-12-08T13:40:01","slug":"malawi-madawa-ya-kutuliza-maumivu-yatumika-kutibu-malaia","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2011\/12\/08\/malawi-madawa-ya-kutuliza-maumivu-yatumika-kutibu-malaia\/","title":{"rendered":"MALAWI: Madawa ya Kutuliza Maumivu Yatumika Kutibu Mala&#341;ia"},"content":{"rendered":"<p>LILONGWE, Dec 8 (IPS) &ndash; Malawi inakabiliwa na uhaba wa madawa wakati ambapo wafadhili wa kimataifa wa taifa hilo wanasita kutoa misaada ambayo ingetumika katika sekta ya afya.\n <\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>Dola zipatazo milioni 60 zimesitishwa kutolewa kutokana na madai ya matumizi mabaya na &#341;ushwa katika ununuzi wa madawa katika Boha&#341;i Kuu za se&#341;ikali. Boha&#341;i Kuu hununua madawa kwa ajili ya hospitali za se&#341;ikali. <\/p>\n<p>Kukosekana kwa misaada kumekuwa na madha&#341;a katika sekta ya afya nchini ambayo wafadhili wa kimataifa hufadhili hadi asilimia 90 ya bajeti ya afya nchini Malawi. <\/p>\n<p>Wakati baadhi ya wahisani wanatoa vifaa vya kitabibu muhimu ikiwa ni pamoja na madawa ya kuokoa maisha, haya hayatoshi kukidhi mahitaji makubwa kwani usambazaji unaishia katika hospitali kuu za &#341;ufaa tatu nchini humo zilizopo mjini Blanty&#341;e, Lilongwe na Mzuzu. <\/p>\n<p>Katika nchi nzima, wagonjwa wanaotaka huduma ya tiba kutoka hospitali za se&#341;ikali hawawezi kupata madawa kama ya kupunguza makali ya UKIMWI (ARVs), yale ya kutibu mala&#341;ia na hata ya kutuliza maumivu.<\/p>\n<p>Hospitali pia zinakabiliwa na uhaba wa vifaa vya tiba kama vile glavu na vifaa vya kupima mala&#341;ia na VVU\/UKIMWI. <\/p>\n<p>Agnes Makwasa, mgonjwa anayeishi na VVU mwenye um&#341;i wa miaka 45 kutoka mji maa&#341;ufu kibiasha&#341;a wa Blanty&#341;e, anahangaika kupata madawa ya ARVs ya bu&#341;e. Kwa miaka mitano, amepokea madawa ya bu&#341;e kwa mwezi mmoja tu kutoka katika kliniki ya se&#341;ikali ka&#341;ibu na eneo analoishi.<\/p>\n<p>&#8220;Waliniambia kuwa wasingenipatia dozi yangu nzima kutokana na kliniki kuwa na akiba ndogo ya dawa. Ilibidi ni&#341;ejee kuomba dawa nyingine baada ya wiki moja, lakini wakati huo kliniki ilikuwa haina tena madawa,&#8221; Makwasa aliiambia IPS.<\/p>\n<p>Alisema aliishia kulipa dola 50 kwa ajili ya kupata dawa katika famasi binafsi. <\/p>\n<p>&#8220;Mimi ni mjane mwenye watoto wadogo watano, na sina aji&#341;a. Naishi kwa kuuza ka&#341;anga na naingiza dola zipatazo 90 tu kwa mwezi. Hii ina maana kuwa familia yangu inaishi katika bajeti ngumu mno kutekeleza. Hii pia inatishia afya yangu sasa kwasababu siwezi kununua mlo kamili, ambao wagonjwa wa VVU wanashau&#341;iwa kutumia wanapokuwa wanatumia tiba,&#8221; alisema Makwasa. Hadi asilimia 60 ya wananchi wa Malawi wapatao milioni 13.1 wanaishi chini ya msta&#341;i wa umaskini.<\/p>\n<p>Hali hiyo pia inavikabili vituo vya afya vya Malawi katika maeneo ya vijijini kwani havina hata madawa ya kutuliza maumivu kama vile aspi&#341;in. <\/p>\n<p>Malita Nalikata kutoka Mulanje, kusini mwa Malawi, aliiambia IPS kuwa wafanyakazi wa afya katika hospitali ya eneo lake walimwambia kuwa wao na hospitali nyingine katika wilaya yake hawana madawa ya mala&#341;ia. Walimshau&#341;i kununua madawa ya kupunguza maumivu, kwani hata hayo hawanayo katika akiba yao.<\/p>\n<p>&#8220;Sina fedha, hivyo niliishia kwenda kwa mganga wa jadi ambaye alinipatia baadhi ya miti shamba ya kunywa kwa kuchanganya na uji,&#8221; alisema Nalikata. Alimlipa mganga huyo malipo ya kuku.&#8232;<\/p>\n<p>&#8220;Kuku ndiyo malipo pekee niliyoweza kuyamudu na waganga wa jadi wanakubali malipo ya aina hiyo,&#8221; Nalikata alisema. &#8232; Ni tendo la kawaida katika maeneo ya kijijini kwa watu maskini kutumia waganga wa jadi wanaposhindwa kupata huduma za tiba katika vituo vya afya vya se&#341;ikali.<\/p>\n<p>Asilimia ipatayo 80 ya Wamalawi wanatumia vituo vya afya vya se&#341;ikali, kwa mujibu wa Mtandao wa Usawa wa Huduma za Afya wa Malawi, mtandao wa mashi&#341;ika ya ki&#341;aia yanayojishughulisha na suala la afya.<\/p>\n<p>Kundi la Wahisani wa Afya nchini Malawi, mtandao wa wafadhili wa kimataifa ikiwa ni pamoja na Uinge&#341;eza, Ma&#341;ekani, Uje&#341;umani na mashi&#341;ika ya Umoja wa Mataifa, wamekataa kutoa msaada hadi se&#341;ikali itakaposafisha sekta ya afya. <\/p>\n<p>Mwenyekiti wa Kundi la Wafadhili wa Afya wa Kimataifa Athanase Nzoki&#341;ishaka aliiambia IPS kuwa wafadhili wa kimataifa wanataka se&#341;ikali kufanyia kazi mapungufu yanayokabili sekta ya afya, hasa jinsi utoaji na usambazaji wa madawa unavyoendeshwa na Boha&#341;i Kuu za Madawa. <\/p>\n<p>Wafadhili, kwa mujibu wa Nzoki&#341;ishaka, pia wana wasiwasi na &#341;ikodi mbaya ya usimamiaji wa madawa nchini humo na kuchelewesha mchakato wa ukaguzi wa ununuzi wa madawa. <\/p>\n<p>&#8220;Se&#341;ikali ina umbali m&#341;efu kufika hadi ku&#341;ejesha imani kwa jumuiya ya kimataifa, na ya Wamalawi, katika mfumo wa afya wa taifa,&#8221; alisema Nzoki&#341;ishaka. <\/p>\n<p>&#8220;Malawi itahitaji kuonyesha kuwa inaweza kutatua suala hilo kikamilifu kuondokana na kukosekana kwa ufanisi, ufujaji na &#341;ushwa katika ngazi zote za mfumo wa afya. Udhaifu katika mdua&#341;a wa usambazaji umekuwa moja ya sababu kuu za kupunguzwa au kucheleweshwa kwa baadhi ya ufadhili wa wahisani siku za nyuma,&#8221; alisema Nzoki&#341;ishaka. <\/p>\n<p>Mwaka jana, wahisani waliiacha se&#341;ikali kununua madawa kwa ajili ya sekta ya afya nchini humo, hali iliyosababisha uhaba mkubwa. <\/p>\n<p>Kwa miaka mingi, hadi asilimia 40 ya bajeti ya taifa ya Malawi inategemea wafadhili na asilimia 80 ya bajeti ya maendeleo ya taifa hilo inatolewa chini ya Mpango wa Pamoja wa Wahisani wa Kusaidia Bajeti. Mpango huo unachangiwa fedha na Uinge&#341;eza, Uje&#341;umani, Benki ya Maendeleo ya Af&#341;ika, No&#341;way, Umoja wa Ulaya na Benki ya Dunia. Hata hivyo, se&#341;ikali za Uinge&#341;eza na Uje&#341;umani zimekataa kutoa dola milioni 400 mwaka huu kutokana na kuishutumu se&#341;ikali ya Malawi kukosa utawala bo&#341;a.<\/p>\n<p>Se&#341;ikali ya Malawi imeki&#341;i kuwepo kwa uhaba huo katika mfumo wa sekta ya afya. <\/p>\n<p>Akijibu madai ya Kundi la Wafadhili wa Afya, Wazi&#341;i wa Afya Jean Kali&#341;ani aliki&#341;i kwa IPS kuwa kuendelea kuwepo kwa udhaifu katika Boha&#341;i Kuu za Madawa za taifa na mdua&#341;a wa usambazaji wa madawa kumeathi&#341;i usambazaji wa madawa katika vituo vya afya na hospitali nchini kote. <\/p>\n<p>&#8220;Se&#341;ikali inashughulikia mgogo&#341;o wa madawa kwa kuima&#341;isha uwezo wa Boha&#341;i Kuu za taifa kama ufumbuzi wa muda m&#341;efu. Katika muda mfupi, tunanunua madawa kupitia zabuni hu&#341;u wakati wa kutatua masuala ambayo yameelezwa na wahisani,&#8221; alisema Kali&#341;ani.<\/p>\n<p>Alielezea kuwa se&#341;ikali inafanya kazi ya kujenga mfumo wenye faida wa kifedha, ambao utatumiwa kufuatilia usambazaji wa madawa kwa ufanisi.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>LILONGWE, Dec 8 (IPS) &ndash; Malawi inakabiliwa na uhaba wa madawa wakati ambapo wafadhili wa kimataifa wa taifa hilo wanasita kutoa misaada ambayo ingetumika katika sekta ya afya. Dola zipatazo milioni 60 zimesitishwa kutolewa kutokana na madai ya matumizi mabaya na &#341;ushwa katika ununuzi wa madawa katika Boha&#341;i Kuu za se&#341;ikali. Boha&#341;i Kuu hununua madawa&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":667,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-3778","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3778","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/667"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=3778"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3778\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=3778"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=3778"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=3778"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}