{"id":3768,"date":"2011-11-18T13:40:01","date_gmt":"2011-11-18T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2011\/11\/18\/sudan-waliokimbia-makazi-yao-washambuliwa-kwa-mabomu\/"},"modified":"2011-11-18T13:40:01","modified_gmt":"2011-11-18T13:40:01","slug":"sudan-waliokimbia-makazi-yao-washambuliwa-kwa-mabomu","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2011\/11\/18\/sudan-waliokimbia-makazi-yao-washambuliwa-kwa-mabomu\/","title":{"rendered":"SUDAN: Waliokimbia Makazi Yao Washambuliwa kwa Mabomu"},"content":{"rendered":"<p>KURMUK, Sudan, Nov 17 (IPS) &ndash; Hawa Jundi ameketi chini nje ya kibanda cha muda ambacho yeye na familia yake wanaishi sasa. Mvua kubwa ilipenya ndani na &#341;adi ilipiga a&#341;dhini huku upepo ukizidi kutikisa hema lililofungwa kwa vijiti.\n<\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>Jundi ni mmoja wa makumi kwa maelfu &ndash; na pengine mamia kwa maelfu ya watu &ndash; ambao wametawanyika katika jimbo zima la Blue Nile nchini Sudan baada ya kukimbia vijiji vyao kuepuka kupigwa mabomu ya angani. Jimbo la Blue Nile lipo kusini masha&#341;iki mwa Kha&#341;toum na mpakani mwa Ethiopia.<\/p>\n<p>Mgogo&#341;o wa kibinadamu ambao taya&#341;i upo, una uwezekano ukazidi kuwa mbaya wakati usambazaji wa chakula ukizidi kushuka. Jundi alisema familia yake inakula chakula kimoja kwa siku kwa kuchimba mizidi mwitu na kuokoteza uwele kutoka mashamba yaliyotelekezwa.<\/p>\n<p>Yeye na familia yake waliondoka kijijini mwao huko Sally, katika jimbo la Blue Nile, baada ya kushambuliwa na ndege ya kivita aina ya Antonov, ambayo ilipelekwa huko na se&#341;ikali ya Sudan. Lakini hata hapa, hajapata usalama.<\/p>\n<p>Mapema siku hiyo, alisema, alika&#341;ibia kupigwa na kipande cha bomu kilichokuwa na ncha kali kilichoanguka katika ukingo wa mto wa ka&#341;ibu, ambapo yeye na wanakijiji wenzake walikuwa wakisaka vipande vya dhahabu kwa ajili ya kuviuza ili kununua chakula.<\/p>\n<p>&#8220;Sijui ni kwa nini Antonov ilikuja kutupiga bomu, lakini tuliondoka kijijini kwetu na kuja hapa,&#8221; alisema. &#8220;Na baada ya kuja hapa, tulikuta kuwa Antonov ilitufuata pia katika eneo hili.&#8221; <\/p>\n<p>Mfuasi mmoja wa kundi la waasi la Sudan Peoples&#8217; Libe&#341;ation Movement&ndash;No&#341;th (SPLM&ndash;N) anasema Sudan inaendesha vita ya vitisho kupitia angani dhidi ya &#341;aia wasiokuwa na hatia.<\/p>\n<p>&#8220;Mkakati mkuu wa Kha&#341;toum kupiga mabomu &#341;aia ni kuvunja moyo wapiganaji,&#8221; Malik Aga&#341;, kiongozi wa SPLM&ndash;N, aliiambia IPS. &#8220;Hawa ni ndugu wa waasi &ndash; baba, mama, wake, watoto &ndash; hivyo wanadhani hii itavunja moyo wa wapiganaji.&#8221;<\/p>\n<p>Katika mahojiano kwenye kambi yake ya msituni ka&#341;ibu na ngome kuu ya waasi ya Ku&#341;muk, Aga&#341; aliiambia IPS watu wapatao 600,000 wamekimbia makazi yao.<\/p>\n<p>Idadi ya watu walioyahama makazi yao ni vigumu kuithibitisha. Mashi&#341;ika ya misaada ilijiondoa tangu mgogo&#341;o ulipoanza mapema Septemba, na makundi ya haki za binadamu hayajaweza kufika katika eneo hili tena. <\/p>\n<p>Mwezi Septemba 13, Taasisi ya Haba&#341;i ya Umoja wa Mataifa ilisema watu wapatao 100,000 wameshakimbia vijiji vyao, lakini maofisa wa Umoja wa Mataifa mjini Kha&#341;toum walikataa kutoa makadi&#341;io.<\/p>\n<p>Se&#341;ikali ya Sudan inakanusha kushambulia &#341;aia kwa makusudi. Maofisa walisema mashambulizi yana lengo la kulenga vituo vya kijeshi peke yake.<\/p>\n<p>Mashi&#341;ika ya haki za binadamu yameshutumu Kha&#341;toum kutokana na kupiga mabomu &#341;aia wa majimbo ya Da&#341;fu&#341; ikiwa ni pamoja na Kusini mwa Ko&#341;dofan, ambayo inapakana na Blue Nile na ambako waasi wa SPLM&ndash;N wanapambana na vikosi vya se&#341;ikali.<\/p>\n<p>Katika jimbo la Blue Nile, kikosi cha angani cha Sudan kinatumia ndege aina ya Antonov, ambazo ziliundwa na U&#341;usi ya zamani mwaka 1968 na zinajulikana kwa sifa yake ya kukosa shabaha. Iwe Kha&#341;toum imedhami&#341;ia ama haijadhami&#341;ia, ni wazi kuwa &#341;aia wamekuwa waathi&#341;ika.<\/p>\n<p>Katika kijiji cha Maiyes, kilomita kama 20 kutoka eneo la vita, wanakajiji walisema familia nzima ya watu sita iliuawa wakati bomu lilipodondoka katika kibanda chao na kukisamba&#341;atisha wiki moja kabla. Kilichobakia katika makazi ya familia hiyo ilikuwa ni udongo uliosamba&#341;atishwa na shimo kubwa. Pia kumeonekana vipande vya mabomu na vifaa vya nyumbani vilivyokunjwa kunjwa, ikiwa ni pamoja na kiatu kimoja cha mtoto mdogo. <\/p>\n<p>&#8220;Mmoja wa waathi&#341;ika mwenye mimba alikatwa katwa tumboni,&#8221; alisema Hede&#341; Abusita, chifu wa kijiji hicho. &#8220;Rueana Mu&#341;dis pia aliuawa hapa akiwa na mtoto wake mdogo. Pia na Busha&#341;a aliuawa hapa katika nyumba hii. Miguu yake ilikatwa katwa, na tumbo lake pia.&#8221;<\/p>\n<p>Kuna uwezekano mdogo kwa wanakijiji kupata huduma za kitabibu kama wameje&#341;uhiwa. Maiyes yupo umbali upatao masaa matatu, katika ba&#341;aba&#341;a mbovu kabla ya kufika katika hospitali ya ka&#341;ibu katika jimbo linaloshikiliwa na waasi.<\/p>\n<p>Evan Ata&#341; ni dakta&#341;i pekee katika mji unaoshikiliwa na waasi wa Ku&#341;muk, na alisema hospitali hapa imepungukiwa na vifaa. Aliongeza kuwa hospitali ina se&#341;a ya kutibu kila mtu &ndash; aska&#341;i wa se&#341;ikali, waasi, au &#341;aia.<\/p>\n<p>Katika chumba kimoja kwenye hospitali ya Ku&#341;muk, manesi walisafisha kidonda cha mpiganaji wa SPLM&ndash;N.<\/p>\n<p>Ata&#341; alisema aska&#341;i huyo aliwasili punde kutoka vitani ambako alipigwa &#341;isasi ya mguuni, na ametibiwa kwa Ketamine, dawa ambayo inasababisha kuweweseka. <\/p>\n<p>&#8220;Awali tunatoa dawa ya usingizi ambapo analala kabisa,&#8221; alisema Ata&#341;. &#8220;Lakini sasa linapokuja suala la kufunga kidonda hatuwezi kuendelea na dawa ya usingizi wakati wote, hivyo tunatoa dawa ambayo inamfanya asihisi maumivu.&#8221;<\/p>\n<p>Katika wodi nyingine, mwanaume mzee, Alton Osman, amelala kitandani akiwa na bandeji pajani mwake na mkononi. Aliokoka kidogo tu kukatwa mkono wake, Ata&#341; alisema. Osman alipigwa na kipande cha bomu, lakini alikuwa na bahati alikutwa na aska&#341;i wa SPLM&ndash;N ambao walimkimbiza hospitalini.<\/p>\n<p>Aga&#341; alitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kushinikiza Kha&#341;toum kuachana na tabia ya kupiga mabomu &#341;aia na kuwataka kujenga &#8220;ko&#341;ido la kibinadamu&#8221; ambalo lita&#341;uhusu mashi&#341;ika yasiyokuwa ya kise&#341;ikali kuleta chakula na madawa kwa watu walioyakimbia makazi yao.<\/p>\n<p>Mashambulizi yamesababisha mashi&#341;ika ya kibinadamu kuondoka katika eneo hilo. Katika safa&#341;i ya kwanza ya waandishi wa haba&#341;i katika eneo linalodhibitiwa na waasi Okt. 6 hadi 8, waandishi waliona maeneo yaliyotelekezwa ambayo hapo kabla yalikuwa yakikaliwa na NGOs na mashi&#341;ika ya Umoja wa Mataifa, ikiwa ni pamoja na Shi&#341;ika la Chakula la Umoja wa Mataifa.<\/p>\n<p>Wakati kukiwa na uhaba wa chakula cha msaada, wakimbizi wengi zaidi wanata&#341;ajiwa kukimbia kutoka Blue Nile na kuingia katika nchi ji&#341;ani. Taya&#341;i, Umoja wa Mataifa unasema, watu 30,000 wanaishi katika makambi ukivuka mpaka wa Ethiopia.<\/p>\n<p>Mgogo&#341;o wa kibinadamu katika jimbo la Blue Nile unaweza kuwa dalili ya kwanza ya kuenea kwa janga nchini kote.<\/p>\n<p>Shi&#341;ika la kukabiliana na migogo&#341;o duniani la Inte&#341;national C&#341;isis G&#341;oup (ICG), lenye makao yake mjini B&#341;ussels, mwezi Sep. 26 lilionya kuwa mgogo&#341;o kati ya waasi wa SPLM&ndash;N na se&#341;ikali unatishia kuingiza nchi nzima katika vita vya wenyewe kwa wenyewe. Katika taa&#341;ifa yake ICG ilisema kuwa viongozi wenye msimamo mkali katika chama tawala cha Rais wa Sudan Oma&#341; al&ndash;Bashi&#341; cha National Cong&#341;ess Pa&#341;ty wanatetea matumizi ya kijeshi dhidi ya vikundi vya waasi, badala ya majadiliano.<\/p>\n<p>&#8220;Jambo hili, hata hivyo, linafanya makundi ya waasi na vikosi vya upinzani nchini Sudan kuungana na hii inaweza kuchochea vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini,&#8221; lilisema shi&#341;ika hilo. <\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>KURMUK, Sudan, Nov 17 (IPS) &ndash; Hawa Jundi ameketi chini nje ya kibanda cha muda ambacho yeye na familia yake wanaishi sasa. Mvua kubwa ilipenya ndani na &#341;adi ilipiga a&#341;dhini huku upepo ukizidi kutikisa hema lililofungwa kwa vijiti. Jundi ni mmoja wa makumi kwa maelfu &ndash; na pengine mamia kwa maelfu ya watu &ndash; ambao&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":887,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-3768","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3768","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/887"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=3768"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3768\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=3768"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=3768"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=3768"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}