{"id":3762,"date":"2011-11-09T13:40:01","date_gmt":"2011-11-09T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2011\/11\/09\/maswali-na-majibu-sudan-na-sudan-kusini-watatatua-masuala-ya-mafuta\/"},"modified":"2011-11-09T13:40:01","modified_gmt":"2011-11-09T13:40:01","slug":"maswali-na-majibu-sudan-na-sudan-kusini-watatatua-masuala-ya-mafuta","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2011\/11\/09\/maswali-na-majibu-sudan-na-sudan-kusini-watatatua-masuala-ya-mafuta\/","title":{"rendered":"Maswali na Majibu: Sudan na Sudan Kusini Watatatua Masuala ya Mafuta"},"content":{"rendered":"<p>MIDRAND, Af&#341;ika Kusini, Nov 8 (IPS) &ndash; Sudan na Sudan Kusini watakubaliana juu ya ugawanyaji wa mafuta kati ya mataifa hayo mawili kwani kumekuwepo na dhami&#341;a ya kisiasa kutoka pande zote mbili kutafuta suluhisho.\n<\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>Hii ni kwa mujibu wa Dk. Ali Yousif Ahmed Alsha&#341;if, balozi wa Sudan nchini Af&#341;ika Kusini. <\/p>\n<p>Maoni yake yanakuja wakati Rais wa Sudan Kusini Salva Kii&#341; alimefanya zia&#341;a yake ya kwanza ya kise&#341;ikali nchini Sudan Oktoba 8. Alsha&#341;if alisema kuwa zia&#341;a ya Kii&#341; ni uthibitisho tosha kuwa kuna dhami&#341;a ya kisiasa kutoka pande zote katika kufikia makubaliano, &#8220;na haya ni mafanikio muhimu.&#8221;<\/p>\n<p>&#8220;Hatimaye watakubaliana matokeo sahihi. Ushi&#341;ikiano kati ya nchi hizo mbili ni muhimu sana; ni suala la utekelezaji wa nchi zote mbili. Wanatakiwa waweze kuchukua hatua ili waweze kuishi pamoja. Kusini haina banda&#341;i na wanahitaji kutumia banda&#341;i za Sudan,&#8221; Alsha&#341;if aliiambia IPS.<\/p>\n<p>&#8220;Wakati wa zia&#341;a hiyo walikubaliana kutokuingia tena katika vita ili kutatua matatizo yao na kwamba mazungumzo yatakuwa msingi wa ufumbuzi,&#8221; Alsha&#341;if alisema.<\/p>\n<p>Alsha&#341;if alihudhu&#341;ia Bunge la Af&#341;ika, ambalo lilihitimisha Kikao Chake cha Tatu cha Kawaida mjini Mid&#341;and, Af&#341;ika Kusini siku ya Ijumaa. <\/p>\n<p>IPS ilizungumza na Alsha&#341;if kuhusu ugumu wa kukutana kwa Sudan na Sudan Kusini baada ya kutengana mwezi Julai na uhasama unaoendelea katika mkoa wa Abyei. Abeyi inabaki kuwa sehemu ya Sudan na inaweza kuungana na Sudan Kusini kama makundi ya kikabila katika mkoa huo yatapiga ku&#341;a ya maoni kufanya hivyo.<\/p>\n<p>Alsha&#341;if alielezea kuwa mkoa wenye utaji&#341;i wa mafuta wa Abyei una wakazi wa kabila la Wadinka Ngok, kabila kubwa zaidi katika Sudan Kusini na Wamissi&#341;iya, kabila la wahamaji la kaskazini.<\/p>\n<p>Swali: Ni changaoto zipi zinaikabili Sudan na Sudan Kusini baada ya kutengana  <\/p>\n<p>Jibu: &#8220;Talaka&#8221; haikuwa &#341;ahisi. <\/p>\n<p>Kwa mujibu wa mkataba wa amani, ilikubaliwa kuwa mkoa wa Abyei uwe na ku&#341;a ya maoni kuamua mustakabali wa baadaye wa eneo hilo na kama wakazi wake wanapenda kuendelea kubakia nchini Sudan au kama wanataka kuwa sehemu ya Sudan Kusini. Katika ku&#341;a hii ya maoni ingekuwa kwa wote (Sudan Kusini) na Sudan katika kupiga ku&#341;a.<\/p>\n<p>Tatizo lilisababishwa na kukataa kwa kusini ku&#341;uhusu kabila la Wamissi&#341;iya kupiga ku&#341;a. Kusini ilisema kabila la Wadinka Ngok pekee ndiyo wapige ku&#341;a. Kaskazini walisema kinyume. <\/p>\n<p>Hadi leo hii bado uhasama unaendelea na ku&#341;a ya maoni haijafanyika. Hilo limesababisha jeshi la Sudan kuchukua eneo hilo kwasababu ya mashambulizi kutoka kwa jeshi la kusini. Sasa kuna makubaliano kwa aska&#341;i wa Ethiopia, chini ya mamlaka ya Umoja wa Mataifa, kuchukua nafasi ya Jeshi la Sudan na utawala wa pamoja utaanzishwa kati ya Sudan na Sudan Kusini na mazungumzo yataendelea.<\/p>\n<p>Swali: Ni suala lipi tata la kugawana mafuta kati ya Sudan na Sudan Kusini <\/p>\n<p>Jibu: Mkataba wa kugawana mafuta bado haujakamilika. Asilimia zipatazo 75 za mafuta yaliyogunduliwa yapo upande wa kusini na mengine upande wa kaskazini. Miundombinu yote ya mafuta, hata hivyo, ipo upande wa kaskazini.<\/p>\n<p>Kwa sasa tunajadili kugawana utaji&#341;i wa mafuta na hakuna tatizo na kugawana huko, asilimia 75 kwa asilimia 25. Suala la msingi ni upande wa bei. Pamoja na kwamba kugawana asilimia 75 kwa 25 kwa kiasi fulani siyo haki kwa kaskazini.<\/p>\n<p>Kwa mujibu wa ta&#341;atibu za kimataifa, ma&#341;a nyingi unagawa &#341;asilimali kwa asilimia 50 kwa 50 kwa miaka 10 au 15 baada ya kugawanyika kwa nchi kwani hapo awali nchi ilipokuwa moja ilichangia gha&#341;ama za kuanzisha uchimbaji n.k. Hii ndiyo sababu kaskazini inataka kutoza fedha zaidi katika usafi&#341;i, kufidia hasa&#341;a. <\/p>\n<p>Swali: Baadhi ya wachambuzi wa kisiasa wanasema kuwa China, kutokana na uwekezaji wake mkubwa katika sekta ya mafuta ya Sudan, ina nafasi kubwa ya kufanya katika diplomasia ili kupunguza mgogo&#341;o kati ya Sudan Kusini na Sudan. Unafiki&#341;i nini juu ya hili  <\/p>\n<p>Jibu: Nilikuwa balozi wa Sudan nchini China mwaka 1993 hadi 1998 na huu ni wakati ambapo tulianza kushi&#341;ikiana nao. Se&#341;ikali ya Sudan Kusini ili&#341;ithi mikataba ambayo ilisainiwa na se&#341;ikali ya Sudan wakati huo.<\/p>\n<p>Kwa hiyo China iko upande wa kusini na China pia ipo kaskazini, na ni kwa maslahi ya pande zote tatu kushi&#341;ikiana kwa njia ya kujenga zaidi.<\/p>\n<p>Kwa uzoefu wetu, China imekuwa mshi&#341;ika mzu&#341;i mno wa maendeleo na tunadhani watakuwa kichocheo kizu&#341;i mno cha utulivu na maendeleo kati ya kaskazini na kusini.<\/p>\n<p>Uwepo wa China ba&#341;ani Af&#341;ika unaibua wivu na wasiwasi kutoka mataifa ya Magha&#341;ibi, kwasababu wanaona China kama nchi yenye uchumi tulivu kabisa wakati uchumi wa Ulaya na Ma&#341;ekani unapoyumba.<\/p>\n<p>Swali: Una jibu gani juu ya madai kuwa migogo&#341;o inayoathi&#341;i jumuiya katika majimbo ya mpakani yatageuka kuwa mauaji ya kimba&#341;i  <\/p>\n<p>Jibu: Sababu kuu ya vita katika Blue Nile na Kusini mwa Ko&#341;dofan ni kwamba kuna watu wengi waliopambana na waasi wa kusini mwa Sudan wa People&#8217;s Libe&#341;ation Movement (SPLM) na jeshi lake (Sudan People&#8217;s Libe&#341;ation A&#341;my (SPLA)). Wakati kusini ilipotia saini mkataba wa amani, ilibidi iamuliwe ni jinsi gani wangeweza kusonga mbele, na jinsi gani majimbo hayo yangetawaliwa katika Sudan kaskazini iliyoungana. <\/p>\n<p>Tulianza kuwa na matatizo, yaliyosababishwa na SPLA. <\/p>\n<p>Katika Kusini mwa Ko&#341;dofan tulikuwa na uchaguzi mkuu mwaka 2009 na SPLM ilikataa hesabu ya watu, pamoja na uchaguzi kutangazwa kuwa hu&#341;u na wa haki na jumuiya ya kimataifa.<\/p>\n<p>Kutokana na sensa ya pili, walifanya uchaguzi na mgombea wa chama cha kaskazini cha National Cong&#341;ess Pa&#341;ty (NCP)alishinda na NCP ilipata viti zaidi kuliko SPLM. SPLM ilisema wakati huo kuwa ku&#341;a ziliibwa na kuanza kupigana.<\/p>\n<p>Katika Blue Nile, kuna tatizo kama hilo la SPLM katika upande wa kaskazini.<\/p>\n<p>Hivyo hakuna mauaji ya kimba&#341;i, lakini inaonekana kuwa wakati vikundi vya waasi vinaposhambulia na kuua vinaachwa tu, wakati vikundi vya se&#341;ikali vikichukua hatua kujilinda, vinaangaliwa kwa utofauti.<\/p>\n<p>Wakati wa zia&#341;a ya Kii&#341; mjini Kha&#341;toum alitakiwa kusitisha kuwasaidia waasi ambao wanapigana na kaskazini, bila kujali uhusiano wao wa awali ulikuwaje. Sudan Kusini kwa sasa ni taifa hu&#341;u na halina haki ya kuingilia masuala ya kaskazini.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>MIDRAND, Af&#341;ika Kusini, Nov 8 (IPS) &ndash; Sudan na Sudan Kusini watakubaliana juu ya ugawanyaji wa mafuta kati ya mataifa hayo mawili kwani kumekuwepo na dhami&#341;a ya kisiasa kutoka pande zote mbili kutafuta suluhisho. Hii ni kwa mujibu wa Dk. Ali Yousif Ahmed Alsha&#341;if, balozi wa Sudan nchini Af&#341;ika Kusini. Maoni yake yanakuja wakati Rais&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":0,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-3762","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3762","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=3762"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3762\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=3762"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=3762"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=3762"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}