{"id":3748,"date":"2011-10-11T13:40:01","date_gmt":"2011-10-11T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2011\/10\/11\/ghana-matatizo-ya-walemavu-yanaendelea-hata-baada-ya-miaka-mitano-ya-kuwepo-kwa-sheia\/"},"modified":"2011-10-11T13:40:01","modified_gmt":"2011-10-11T13:40:01","slug":"ghana-matatizo-ya-walemavu-yanaendelea-hata-baada-ya-miaka-mitano-ya-kuwepo-kwa-sheia","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2011\/10\/11\/ghana-matatizo-ya-walemavu-yanaendelea-hata-baada-ya-miaka-mitano-ya-kuwepo-kwa-sheia\/","title":{"rendered":"GHANA: Matatizo ya Walemavu Yanaendelea Hata Baada ya Miaka Mitano ya Kuwepo kwa She&#341;ia"},"content":{"rendered":"<p>ACCRA, Okt 11 (IPS) &ndash; Emmanuel Joseph na Geo&#341;ge Amoah, &#341;aia wa Ghana wawili ambao ni walemavu, wana maisha tofauti kabisa. Wakati wa kwanza analalia kipande cha mbao Katikati mwa Acc&#341;a,huku mwili wake nusu uchi ambao umejikunja na kwa kiasi kikubwa ukiwa umepooza, anapigwa na jua wakati akisubi&#341;i kukusanya dola tatu, wastani wa kipato chake anachokipata kwa siku kutokana na kuomba.\n <\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>Mwingine anakaa katika kiti cha kifaha&#341;i akiwa amevalia suti nadhifu, nywele zake zikiwa zimekatwa vizu&#341;i na macho yake yakiwa yako makini wakati akifanya kazi katika moja ya mabenki ya kimataifa katika kitongoji hicho hicho. <\/p>\n<p>Hao wanawakilisha walemavu wanaokadi&#341;iwa kufikia milioni mbili, ambao, kulingana na Shi&#341;ika la Afya Ulimwenguni, ni kati ya asilimia saba hadi kumi ya wakazi wote. Tak&#341;ibani baada ya miaka mitano baada ya kupitishwa, She&#341;ia ya Watu Wenye Ulemavu imeleta mafanikio madogo katika maisha yao. <\/p>\n<p>Katika ka&#341;atasi vifungu vya she&#341;ia hiyo vinaahidi fu&#341;sa nyingi za aji&#341;a, elimu ya bu&#341;e, upatikanaji wa makazi na usafi&#341;ishaji, na kukubaliwa katika jamii. Hata hivyo ukweli unabakia kuwa tofauti.<\/p>\n<p>&#8220;Ma&#341;a nyingine natukanwa,&#8221; anasema Joseph, ambaye anasema miguu yake imepooza baada ya kupigwa sindano alipokuwa mgonjwa. &#8220;Ma&#341;a nyingine watu pia wanatupiga.&#8221;<\/p>\n<p>Anaishi na kaka yake katika jamii inayojulikana kama Ofisi ya Posta. Kila asubuhi, anajisogeza ka&#341;ibu na Katikati mwa mji na kulala pembezoni mwa ba&#341;aba&#341;a. Watu wenye ulemavu kama wa kwake wamejazana katika eneo hilo, huku baadhi wakijisogeza ka&#341;ibu na maga&#341;i kwa ajili ya kuomba ili kupata mabadiliko katika maisha yao.<\/p>\n<p>&#8220;Kuna unyanyasaji wa waziwazi,&#8221; anasema Amoah. &#8220;Kwa sasa kama unakuwa na changamoto za kimaumbile, unaonekana kama mtu tofauti. Sijui kama mtu unapaswa kuendelea kuomba au kufuma au kufanya jambo jingine lolote. Kwa kiasi kikubwa, hayo ndiyo mawazo ya Ghana ya kibiasha&#341;a.&#8221;<\/p>\n<p>Kwa upande mwingine, Amoah ana bahati. Ana elimu ya chuo kikuu, na aliweza kupata nafasi katika benki baada ya shi&#341;ika lisilokuwa la kise&#341;ikali la Sight Save&#341;s lilipofanya maonesho yake ya kwanza ya kila mwaka ya aji&#341;a mwaka 2010. <\/p>\n<p>Hayuko wazi kuhusu asili ya ulemavu wake, lakini anasena aliupata alipokuwa kijana, na kusababisha kushindwa kwenda shule kwa miaka mitano. Kuwa aliweza kuendelea na masomo katika nchi ambayo ma&#341;a nyingi ulemavu unaoenekana kama uchawi au kutokuwaheshimu inaonekana kama ni ushindi. Ma&#341;afiki wake walemavu hawajawa na bahati hiyo.<\/p>\n<p>&#8220;Ni wazi kuwa hii ni changamoto kubwa na ngumu,&#8221; Amoah anasema. &#8220;Inabidi wawe tegemezi kwa familia. Wengine inabidi kutafuta aji&#341;a zisizotumia nguvu kubwa, na wachache wanaamua kuwa ombaomba. Wengi wao wanafanya aji&#341;a ambazo haziwafai kwa kiasi kikubwa, lakini inabidi wafanye hivyo ili kuweza kuendelea kuishi.&#8221;<\/p>\n<p>Hakuna hata kifungu kimoja cha She&#341;ia kimeshatekelezwa kikamilifu. Rasimu ya she&#341;ia, ambayo inapaswa kubo&#341;esha vifungu vinavyohusiana na aji&#341;a, elimu, adhabu, na kujenga mazingi&#341;a, vimeishia mahali fulani kati ya Wiza&#341;a ya Ustawi wa Jamii na Ofisi ya Mwanashe&#341;ia Mkuu wa Se&#341;ikali. <\/p>\n<p>Hili linajitokeza wakati Shi&#341;ikisho la Watu Wenye Ulemavu nchini Ghana (GFD) linaja&#341;ibu ku&#341;ejesha uhusiano wake na se&#341;ikali ili kuleta mabadiliko.<\/p>\n<p>&#8220;Kama hatutafanya hivyo, na &#341;asimu ya she&#341;ia ikipitishwa kama ilivyo, kutakuwa na mapengo mengi mno,&#8221; anasema Isaac Tuggon, wakili wa GFD. &#8220;Ni jambo ambalo lilitakiwa kuwa taya&#341;i siku nyingi zilizopita.&#8221;<\/p>\n<p>Kulingana na She&#341;ia hiyo, mazingi&#341;a yaliyojengwa &#341;afiki kwa walemavu nchini Ghana yanapaswa kupatikana ifikapo mwaka 2016. Wakati kuna majengo ambayo yamezingatia watu wenye ulemavu mjini Acc&#341;a, bado mji huo umekuwa na vikwazo vingi, ikiwa ni pamoja na majengo ya zamani ambayo yana ngazi zenye mte&#341;emko mkali na hayana lifti. Tuggon analalamika kuwa kuna kazi ndogo mno iliyofanyika kutekeleza maadili ya ujenzi, na hata majengo mapya yanakosa miundombinu bo&#341;a kwa walemavu. <\/p>\n<p>&#8220;Mikono ya se&#341;ikali imefungwa kwasababu se&#341;ikali yenyewe haifanyi kile ambacho ni sahihi,&#8221; anasema.<\/p>\n<p>Katikati mwa Acc&#341;a, ambako wiza&#341;a nyingi za se&#341;ikali ya shi&#341;ikisho zina makao yake makuu, ni Wiza&#341;a ya Ustawi wa Jamii pekee ina ngazi za kutumia kiti cha walemavu. <\/p>\n<p>&#8220;Kama naweza kwenda kila mahali, ina maana mimi siyo mlemavu,&#8221; anasema Amoah akiwa na maana kuwa ni vigumu mno kutembea katika jiji. &#8220;Ma&#341;a nyingine, ni mazingi&#341;a ambayo yanatufanya tushindwe.&#8221;<\/p>\n<p>She&#341;ia pia inataka kuundwa kwa Ba&#341;aza la Taifa la Watu Wenye Ulemavu. Ba&#341;aza limeshaanzishwa, lakini katibu wake mtendaji, Max Va&#341;don, anasema halina &#341;asilimali za kutosha. <\/p>\n<p>Moja ya kazi za ba&#341;aza hilo zimekuwa kupitisha miongozo kugawa fedha zinazotolewa kwa manisipaa, miji midogo ndani ya jiji, au Mfuko wa Wilaya. Mfuko ulianzishwa miaka ya 1990 nchini Ghana unataka kupunguza mada&#341;aka ya se&#341;ikali ya shi&#341;ikisho na kuyapeleka se&#341;ikali za mitaa. <\/p>\n<p>Mwaka 2005, kutokana na shinikizo kutoka kwa wanaha&#341;akati, asilimia mbili ya fedha hizi ziliahidiwa kugawiwa kwa watu wenye ulemavu. Fedha hizo zilikuwa zikija polepole, kama ziliweza kufika. Miongozo ilipaswa kutatua tatizo hilo.<\/p>\n<p>&#8220;Suala la msingi ni kwamba watu hawana dhami&#341;a,&#8221; anasema Va&#341;don. &#8220;Raia wa Ghana kwa ujumla hawana nia ya kusaidia walemavu. Hatutaki kabisa kujua kuhusu ulemavu. Watu ambao wanafanya kazi katika wilaya pia ni &#341;aia wa Ghana. Pia wana mitizamo kama hiyo. Hawataki kujua zaidi.&#8221;<\/p>\n<p>Mwaka 2010, Waiza&#341;a ya Se&#341;ikali za Mitaa na Maendeleo ya Vijijini ilianza kutoa maelekezo kwa manisipaa, miji midogo kuzunguka jiji, na se&#341;ikali za wilaya kusisitiza kutekeleza miongozo hiyo, ambayo, miongoni mwa mambo mengine, ilitaka kuanzishwa akaunti tofauti kubeba fedha na kamati ya kuamua jinsi ya kuingiza na kutoa fedha hizo. <\/p>\n<p>Polepole kamati zinaanzishwa na akaunti zinafunguliwa. Chama cha Acc&#341;a Met&#341;opolitan Assembly (AMA) kinasema kina zaidi ya dola 52,000 katika akaunti yake. Kulingana na ofisa wa bajeti wa AMA, kamati itaundwa katika wiki chache zijazo. <\/p>\n<p>AMA pia inakanusha madai kuwa haijatoa fedha kabla ya kutungwa kwa miongozo. Ofisa bajeti wa se&#341;ikali za mitaa ana nya&#341;aka kadhaa zinazoonyesha &#341;uzuku za mashine za kufumia na vifaa vingine vya kufanyia kazi. <\/p>\n<p>Hadi ma&#341;ekebisho ya She&#341;ia hiyo yatakapopitishwa, hakuna jinsi watu au taasisi ambao wanakiuka vifungu vyake wanaweza kuadhibiwa. Wakati huo huo, wanaha&#341;akati wengi wa masuala ya walemavu wanaona kuwa mabadiliko yanakuja polepole. Baadhi, kama ilivyo kwa Amoah, wanadhani ni mabadiliko ya polepole ya kubadili tabia ya kibiasha&#341;a ya Ghana. Wengine, kama ilivyo kwa Va&#341;don, wanadhani ni suala la jamii kujiakiasi yenyewe katika se&#341;ikali.<\/p>\n<p>&#8220;Kwa miaka mingi, anasema Va&#341;don, &#8220;sekta hii haijawahi kuwa na &#341;asilimali nyingi ikilinganishwa na nyingine, na tunaakisi uchaguzi ambao tumeufanyia kazi katika jamii. Kama watu wengi wangetoa sauti zaidi kuhusu binamu zao, shangazi, wajomba, na wengine wengi, ambao ni walemavu, watu wengi wangetoa sauti kuhusu jambno hilo, pengine se&#341;ikali ingesema, ngoja tuingize &#341;asilimali nyingi katika jambo hili.&#8221;<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>ACCRA, Okt 11 (IPS) &ndash; Emmanuel Joseph na Geo&#341;ge Amoah, &#341;aia wa Ghana wawili ambao ni walemavu, wana maisha tofauti kabisa. Wakati wa kwanza analalia kipande cha mbao Katikati mwa Acc&#341;a,huku mwili wake nusu uchi ambao umejikunja na kwa kiasi kikubwa ukiwa umepooza, anapigwa na jua wakati akisubi&#341;i kukusanya dola tatu, wastani wa kipato chake&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":879,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-3748","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3748","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/879"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=3748"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3748\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=3748"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=3748"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=3748"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}