{"id":3722,"date":"2011-09-14T13:40:01","date_gmt":"2011-09-14T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2011\/09\/14\/namibia-hakuna-njia-ila-kustahimili-mabadiliko-ya-tabia-nchi\/"},"modified":"2011-09-14T13:40:01","modified_gmt":"2011-09-14T13:40:01","slug":"namibia-hakuna-njia-ila-kustahimili-mabadiliko-ya-tabia-nchi","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2011\/09\/14\/namibia-hakuna-njia-ila-kustahimili-mabadiliko-ya-tabia-nchi\/","title":{"rendered":"NAMIBIA: Hakuna Njia Ila Kustahimili Mabadiliko ya Tabia Nchi"},"content":{"rendered":"<p>WINDHOEK, Sept 13, 2011 (IPS) &ndash; Hali mbaya ya hewa iliyotabi&#341;iwa kutokana na mabadiliko ya tabia nchi nchini Namibia ina uwezekano wa kuleta madha&#341;a makubwa katika asilimia 70 ya wakazi wa nchi hiyo wanaoishi maeneo ya vijijini na wanaotegemea kwa kiasi kikubwa katika kilimo.\n <\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>Kwa mujibu wa wataalam wa mabadiliko ya tabia nchi, Namibia haina njia nyingine ila kukubali kustahimili mabadiliko kwani mabadiliko makubwa ya hali ya hewa, kama vile vipindi vi&#341;efu vya ukame na mvua kubwa kupita kiasi, ni mambo yaliyotabi&#341;iwa katika nchi hiyo ya kusini mwa Af&#341;ika. <\/p>\n<p>Mvua kubwa taya&#341;i zimeshaanza: mafu&#341;iko mwaka huu katika Bonde la Cuvelai kaskazini mwa kati ya Namibia zilikuwa sentimita nane zaidi ikilinganishwa na msimu wa mafu&#341;iko mwaka 2009. Hii ni &#341;ikodi mpya kwa eneo ambapo ka&#341;ibu nusu ya watu milioni 2.1 nchini Namibia wanaishi. <\/p>\n<p>Kwa uchache watoto 21 wanaokwenda shule wali&#341;ipotiwa kubebwa na maji tangu kuanza kwa mafu&#341;iko mapema Feb&#341;ua&#341;i. Uha&#341;ibifu mkubwa pia uli&#341;ipotiwa katika ba&#341;aba&#341;a za Namibia, majengo na miundombinu mingine, na maelfu ya watu waliyakimbia makazi yao. <\/p>\n<p>Katika nchi ambapo baadhi ya sekta zinazochangia kwa kiasi kikubwa katika uchumi &ndash; kilimo, uvuvi na utalii wa mazingi&#341;a &ndash; zinategemea katika mali asili, ongezeko la mabadiliko litahitaji mikakati madhubuti ya kuwezesha watu kuendelea kuishi. <\/p>\n<p>Kama njia za kuwezesha kuishi na mabadiliko hazitawezekana, umaskini, kukosekana kwa kipato na kukosekana kwa fu&#341;sa za aji&#341;a kutafanya kuongeza kaya zitakazoathi&#341;ika, anasema Eph&#341;aim Nekongo, mwenyekiti wa Jukwaa la Vijana la Mkoa wa Oshana. <\/p>\n<p>Namibia taya&#341;i inakabiliwa na tatizo la uhaba wa aji&#341;a linalokadi&#341;iwa kuwa asilimia 50. <\/p>\n<p>&#8220;Madha&#341;a ya kimazingi&#341;a ya mabadiliko ya tabia nchi, kwa yale ambayo yameshaonekana na yale ambayo yanata&#341;ajiwa, kama vile kuongezeka kwa kina cha maji ya baha&#341;i, mabadiliko ya mvua yanayosababisha mafu&#341;ufiko na ukame, majanga makubwa ya kimbunga na mvua kubwa, mawimbi ya joto na kupungua kwa ubo&#341;a wa hali ya hewa, yataathi&#341;i afya ya mwanadamu moja kwa moja na isipo moja kwa moja,&#8221; alisema Nekongo, alipokuwa akizungumza katika Mkutano wa Vijana wa Namibia Juu ya Njia za Kuwezesha Kuishi katika Mabadiliko ya Tabia Nchi (NYCCC) Jul. 29 hadi 30. <\/p>\n<p>Uchumi wa nchi unategemea moja kwa moja na mazingi&#341;a hadi asilimia 30 ya pato la taifa (GDP). Hii ni kwa mujibu wa wataalam na washau&#341;i wa kiufundi wa M&#341;adi wa Kuishi katika Mabadiliko ya Tabia Nchi Af&#341;ika (AAP), mpango wa Shi&#341;ika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa unaofadhiliwa na se&#341;ikali ya Japan ambao unasaidia mataifa 20 ya Af&#341;ika kutekeleza hatua na mipango ya kuwezesha kuishi katika mabadiliko ya tabia nchi. <\/p>\n<p>Tafiti za awali zimeonyesha kuwa atha&#341;i ambazo zitasababishwa na mabadiliko ya tabia nchi katika maliasili zinaweza kupunguza GDP nchini Namibia kwa asilimia sita, ambazo ni kama dola milioni 30 katika miaka 20 ijayo. <\/p>\n<p>Wakati Namibia ni nchi inayoathi&#341;ika ambayo inachangia hewa ya kaboni (GHG) kwa kiwango cha chini kabisa, kipaumbele chake cha kwanza katika jukumu la mabadiliko ya tabia nchi ni kuhakikisha watu wanaweza kuishi katika mazingi&#341;a ya mabadiliko, anasema Wazi&#341;i wa Mazingi&#341;a na Utalii wa Namibia Netumbo Nandi&ndash;Ndaitwa. <\/p>\n<p>Kwa mujibu wa mshau&#341;i wa kiufundi wa AAP nchini Namibia, Johnson Ndokosho, Af&#341;ika inazalasha asilimia tatu tu ya GHGs katika anga. Ame&#341;ika Kaskazini na Ulaya Magha&#341;ibi huchangia asilimia 75 na idadi ya wakazi wao inaka&#341;ibiana tu na idadi ya watu katika Af&#341;ika nzima. <\/p>\n<p>&#8220;Se&#341;ikali ya Namibia inajitolea kuandaa ushahidi kuchukua hatua za muda m&#341;efu za kuwezesha kuishi na mabadiliko ya tabia nchi kwa kupunguza atha&#341;i na imeamua kufanyika kwa tafiti za kubashi&#341;i mabadiliko ya tabia nchi ili kujifunza zaidi juu ya mabadiliko hayo na madha&#341;a yake,&#8221; anasema Nandi&ndash;Ndaitwa. Anasema kuwa vijana wadogo nchini Namibia taya&#341;i wanaongoza jitihada za kujenga uchumi wa nchi na wanalenga siyo tu katika changamoto, lakini pia katika fu&#341;sa zinazotolewa na mabadiliko ya tabia nchi. <\/p>\n<p>Moja ya mi&#341;adi ambayo inafanya kazi hii ni ile ya M&#341;adi wa Kuku wa Kienyeji Mjini, unaofadhiliwa na AAP. <\/p>\n<p>Nelson Haulamba, mfanyakazi kijana ambaye ni sehemu ya m&#341;adi huo, anasema kuwa lengo la kutafuta njia mbadala za kuishi katika mabadiliko ya tabia nchi, ni kuzalisha kipato na kutoa fu&#341;sa kwa wale wanaopenda kufanya kilimo. Watu wanaoshi&#341;iki katika m&#341;adi wanafuga kuku aina ya Boschveld Chicken, ambao ni mchanganyiko wa kuku wa kienyeji sita kutoka ba&#341;ani Af&#341;ika: Venda, Matabele na Ovambo. <\/p>\n<p>&#8220;Ni kuku kutoka ba&#341;ani Af&#341;ika pekee. Ni aina ambayo inaweza kuhimili mazingi&#341;a magumu,&#8221; anasema. <\/p>\n<p>Kuku aina ya Boschveld wanaweza kuishi katika &#8220;kile ambacho asili inaweza kutoa&#8221;. Kwa hiyo wanahitaji uangalizi mdogo sana. Pia wanaweza kuhimili mazingi&#341;a tofauti ya hali ya hewa ya Af&#341;ika na wanataga mayai mengi katika mazingi&#341;a ya wazi. <\/p>\n<p>Kutokana na mvua chache, a&#341;dhi  isiyokuwa na &#341;utuba na kiwango kikubwa cha kuyeyuka kwa maji, Namibia inafaa kwa ufugaji wa mifugo kuliko kupanda mazao, anasema Haulamba. <\/p>\n<p>&#8220;Ili Namibia kufikia usalama wa chakula kwa kutumia ufugaji wa kuku, tunatakiwa kutumia aina bo&#341;a ya kuku ambao wanaweza kuishi katika mazingi&#341;a tofauti nchini Namibia.&#8221; <\/p>\n<p>Nchi inata&#341;ajiwa kukabiliwa na uhaba mkubwa wa maji, hapo ndipo maji yatakayotumika kwa mwaka yatakapopungua hadi mita za ujazo 500 kwa kila mtu kwa mwaka, miaka tisa ijayo. <\/p>\n<p>&#8220;Kupungua kwa mvua na kuongezeka kwa myeyuko wa maji kunaweza kusababisha kupungua kwa maji juu ya a&#341;dhi na kuongeza maji ya chini ya a&#341;dhi. Hali ilivyo kwa sasa, Namibia inakadi&#341;iwa kukabiliwa na uhaba mkubwa wa maji ifikapo mwaka 2020. Hii ni hali ambapo wananchi wa Namibia watahitaji maji zaidi kuliko uwezo wa nchi wa kuyasambaza,&#8221; anasema Ndokosho. <\/p>\n<p>Lakini baha&#341;i itafu&#341;ika katika baadhi ya maeneo katika kipindi cha miaka 100 ijayo. Kulingana na Ndokosho, kina cha baha&#341;i katika pwani ya Namibia kinaweza kuongezeka hadi sentimita 30 hadi 100 katika kipindi cha miaka 100 ijayo. Kuongezeka huku kunabashi&#341;iwa kusababisha mafu&#341;iko katika maeneo makubwa ya Walvis Bay na miji mingine ya mwambao wa pwani. <\/p>\n<p>Wataalam wanasema uwezo wa mataifa ya Af&#341;ika kuingiza mbinu za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi katika mipango yao ya maendeleo itakuwa sababu kubwa ya jitihada zao za kufikia na kuendeleza Malengo ya Maendeleo ya Milenia ya kupunguza umaskini, kupunguza kuenea kwa magonjwa ya kuambukiza, kufikia mazingi&#341;a endelevu na kuongeza viwango vya elimu. <\/p>\n<p>Hatua muhumi zinahitajika ili kuwezesha kuishi katika mabadiliko ya tabia nchi nchini Namibia ikiwa ni pamoja na kuhifadhi maeneo ya a&#341;dhi chepechepe na uoto wa asili ambao unaota kandokando mwa miti na vijito. <\/p>\n<p>&#8220;Maeneo chepechepe ni kama sponji,&#8221; anasema Ndokosho. &#8220;Yananyonya maji, yanatumika kama eneo la mpakani la kuzuia upepo mkali na ni vyanzo vya maji safi.&#8221; <\/p>\n<p>Anasema fukwe zinahitaji kutunzwa. Kulingana na yeye fukwe ni muhimu kwasababu zinaongeza ukubwa wa mwambao na kupunguza mafu&#341;iko katika maendeleo ya pwani. <\/p>\n<p>Hata&#341;i nyingine, anasema, zinaweza kuzuiawa kwa kuwa na mi&#341;adi ya kuzalisha vipato na kuwa na vyanzo mbalimbali vya vipato hivyo wakati huo huo ukijenga majukwaa ya kujifunzia katika kilimo na kuishi na mabadiliko ya tabia nchi. <\/p>\n<p>Uwekezaji katika vyanzo vya nishati mbadala unapaswa kufanyika ili kuhimili uwezekano wa mgogo&#341;o wa nishati. Ni muhimu kutokutegemea sana miti, Ndokosho anaongeza. <\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>WINDHOEK, Sept 13, 2011 (IPS) &ndash; Hali mbaya ya hewa iliyotabi&#341;iwa kutokana na mabadiliko ya tabia nchi nchini Namibia ina uwezekano wa kuleta madha&#341;a makubwa katika asilimia 70 ya wakazi wa nchi hiyo wanaoishi maeneo ya vijijini na wanaotegemea kwa kiasi kikubwa katika kilimo. Kwa mujibu wa wataalam wa mabadiliko ya tabia nchi, Namibia haina&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":871,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-3722","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3722","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/871"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=3722"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3722\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=3722"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=3722"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=3722"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}