{"id":3721,"date":"2011-09-14T13:40:01","date_gmt":"2011-09-14T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2011\/09\/14\/malawi-maji-yaendeleza-kilimo-mseto-katika-shamba-dogo\/"},"modified":"2011-09-14T13:40:01","modified_gmt":"2011-09-14T13:40:01","slug":"malawi-maji-yaendeleza-kilimo-mseto-katika-shamba-dogo","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2011\/09\/14\/malawi-maji-yaendeleza-kilimo-mseto-katika-shamba-dogo\/","title":{"rendered":"MALAWI: Maji Yaendeleza Kilimo Mseto Katika Shamba Dogo"},"content":{"rendered":"<p>BLANTYRE, Sept 13, 2011 (IPS) &ndash; Wakati mmiliki wa asili wa hekta 3.5 za a&#341;dhi alipoiuza kutokana na kujaa maji mengi, Diana Sitima na mume wake, Wilson, walikimbilia kuinunua.\n<\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>&#8220;Watu walisema tumepoteza ufahamu kununua a&#341;dhi ambayo haifai kwa kilimo. Tulianza kwa kujenga nyumba kwasababu tulitaka kuishi hapa ili kupaendeleza. Walisema nyumba itadondoka siku moja. Sasa ni miaka sita,&#8221; Diana Sitima anaiambia IPS. Kwa sasa shamba lao dogo ni mfano wa kuigwa wa kilimo mseto, ambacho huchanganya wanyama na uzalishaji wa mazao huku shughuli hizo mbili zikitegemeana kwa ajili ya ukuaji wake. Mchango mkubwa wa ukuaji huo unatokana na uwepo wa maji. Likiwa umbali upatao kilomita 15 nje ya jiji la Blanty&#341;e katika wilaya ya Chi&#341;adzulu kusini mwa Malawi, shamba hilo ni eneo la unyevu lenye migomba, miwa na kila aina ya mbogamboga. Kuna mabwawa manne ambayo yamejaa samaki, ng&#8217;ombe wawili wa maziwa, ngu&#341;uwe, mbuzi na kuku. Shamba limebuniwa ili wanyama waweze kula mazao yanayopandwa shambani humo halafu mbolea ya wanyama inatumiwa kustawisha mazao. Mabwawa yanasambaza maji ya umwagiliaji. Mafanikio ya shamba yamevutia wataalam wa kilimo, maafisa wa juu wa se&#341;ikali na hata mawazi&#341;i kutoka ba&#341;aza la mawazi&#341;i ambao hutembelea shamba kuangalia jinsi linavyozalisha. Shamba hilo linazalisha dola zipatazo 700 kwa wiki kutokana na kuuza mazao na mifugo &ndash; kipato ambacho ni kikubwa ma&#341;a 100 zaidi ya ambacho wakazi wengi wa Malawi wanaingiza, kulingana na takwimu za wiza&#341;a ya fedha. Akina Sitima pia wanaaji&#341;i wafanyakazi wa kudumu 10, na kuaji&#341;i wengine wa muda mfupi kwa kipindi cha mwaka mzima. Shamba hilo sasa ni biasha&#341;a yenye faida na timu ya mume na mke imepata mikopo benki kuwekeza zaidi. Familia inahusisha mafanikio yao na upatikanaji wa maji mengi na njia bo&#341;a za kuyasimamia katika shamba walilolinunua mwaka 1994 kwa chini ya dola 15. &#8220;Mmiliki alituuzia kama vile analitupa kwasababu lilikuwa na maji mengi na hawakujua jinsi ya kulitumia. Lakini tulijua maji ni maisha, na kwa usimamiaji mzu&#341;i tungeweza kutengeneza faida kubwa kutokana na kipande hiki cha a&#341;dhi,&#8221; anasema Wilson Sitima. Mo&#341;&#341;is Salifu, mfanyakazi wa ugani ambaye aliwapatia ushau&#341;i akina Sitima, alisaidia kubuni mfumo wa kilimo mseto ambao kwa sasa wanautumia na aliwashau&#341;i kuchimba mabwawa manne ili kupunguza kutuama kwa maji na kuifanya a&#341;dhi ifae kwa kilimo. Mabwawa hayo pia yanavuna maji inaponyesha mvua, na hivyo kuwa na maji ya kumwagilia kwa mwaka mzima. Taifa hili dogo lisilokuwa na banda&#341;i la kusini mwa Af&#341;ika lina vyanzo kadhaa vya maji ikiwa ni pamoja na maziwa matatu, zaidi ya mito yenye maji mwaka mzima 13 na maeneo kadhaa ya a&#341;dhi chepechepe. Kwa kuongeza katika hazina kubwa ya vyanzo vya maji, maeneo yenye maji nchini Malawi yanachukua zaidi ya asilimia 21 ya eneo la taifa hilo, kulingana na se&#341;a ya taifa ya maji. Hata hivyo, se&#341;a inasema kuwa vyanzo vya maji nchini humo &#8220;havijasimamiwa kiasi cha kutosha na kimkakati&#8221; kwa kutumia kilimo cha umwagiliaji ili kufikia faida za juu za kijamii na kiuchumi. Rikodi za wiza&#341;a ya kilimo zinaonyesha kuwa mwaka 2009\/2010 Malawi ilizalisha tani milioni 3.5 za mahindi, zao kuu la chakula nchini humo. Hii ilikuwa na ziada ya tani milioni moja ikilinganishwa na mahitaji ya chakula nchini humo. Kati ya mavuno ya jumla, ni tani 300,000 tu zilitokana na kilimo cha umwagiliaji. Uhaba wa a&#341;dhi pia ulio&#341;odheshwa kuwa miongoni mwa sababu kuu zinazosababisha uzalishaji duni wa kilimo nchini Malawi. Se&#341;a ya maji ya taifa inasema ukubwa wa a&#341;dhi inayomilikiwa na mtu mmoja nchini Malawi umepungua kutoka hekta 1.53 mwaka 1968 hadi hekta 0.8 mwaka 2000 na hekta 0.2 mwaka 2008 kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu. Wakitambua mapema fu&#341;sa iliyopo katika shamba, Wilson Sitima aliacha aji&#341;a inayolipa vizu&#341;i katika moja ya mabenki makubwa nchini Malawi na Diana Sitima alijiuzulu katika nafasi ya mkuu wa mauzo ili kuwekeza nguvu zao katika kilimo. M&#341;atibu wa Taifa wa Mtandao wa Mashi&#341;ika ya Ki&#341;aia ya Kilimo, Tamani Nkhono&ndash;Mvula, anasema kilimo cha mseto kina uwezekano wa kuongeza uzalishaji katika kilimo kidogo, hasa katika maeneo yenye maji mengi na ka&#341;ibu na vyanzo vya maji vya kudumu. Mfumo unajiendeleza wenyewe, anasema, kwasababu unastawi katika shughuli zinazotegemeana. Hata hivyo, Nkhono anadhani siyo wakulima wadogo wengi nchini Malawi watakuwa na shauku la kuendesha kilimo cha kibiasha&#341;a kwani wanaogopa kupata hasa&#341;a. &#8220;Wakulima wengi wadogo nchini Malawi hawataki changamoto. Afadhali wafanye shughuli kwa jinsi ya kizamani ambazo hazisaidii, hasa kutokana na a&#341;dhi ya kilimo kuzidi kupungua ukubwa wake,&#8221; anasema. Akina Sitima hawajaanza na fedha nyingi; mtaji wao ulikuwa maji yaliyokuwepo kwenye eneo husika, ushau&#341;i mzu&#341;i na kufanya kazi kwa bidii, wanasema. &#8220;Kama hakukuwa na maji, eneo hili lingekuwa limekufa. Maji yanasababisha kilimo mseto hapa na bila ya maji tusingenunua a&#341;dhi hii,&#8221; anasema Wilson Sitima. &#8195; <\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>BLANTYRE, Sept 13, 2011 (IPS) &ndash; Wakati mmiliki wa asili wa hekta 3.5 za a&#341;dhi alipoiuza kutokana na kujaa maji mengi, Diana Sitima na mume wake, Wilson, walikimbilia kuinunua. &#8220;Watu walisema tumepoteza ufahamu kununua a&#341;dhi ambayo haifai kwa kilimo. Tulianza kwa kujenga nyumba kwasababu tulitaka kuishi hapa ili kupaendeleza. Walisema nyumba itadondoka siku moja. Sasa&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":694,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-3721","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3721","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/694"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=3721"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3721\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=3721"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=3721"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=3721"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}