{"id":3677,"date":"2011-07-06T13:40:01","date_gmt":"2011-07-06T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2011\/07\/06\/mahakama-inayohama-yaleta-matumaini-nchini-drc\/"},"modified":"2011-07-06T13:40:01","modified_gmt":"2011-07-06T13:40:01","slug":"mahakama-inayohama-yaleta-matumaini-nchini-drc","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2011\/07\/06\/mahakama-inayohama-yaleta-matumaini-nchini-drc\/","title":{"rendered":"Mahakama Inayohama Yaleta Matumaini Nchini DRC"},"content":{"rendered":"<p>BUKAVU, DR Congo, Julai 5 (IPS) &ndash; Aska&#341;i kumi na moja waliokutwa na hatia ya kuwabaka zaidi ya wanawake 50 katika mji wa Fizi mwezi Janua&#341;i, wameanza kutumikia hukumu zao ndefu katika mji wa jimbo wa Bukavu. Kuendeshwa kwa hukumu yao kwa kasi na hatimaye kukutwa na hatia na kuhukumiwa na mahakama inayohama ni dalili nzu&#341;i ya kuka&#341;ibishwa ya kukomesha udhalilishaji wa kingono katika Jamhu&#341;i ya Kidemok&#341;asi ya Kongo.\n <\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>Katika usiku wa Janua&#341;i 1&ndash;2, kundi la aska&#341;i walifanya upo&#341;aji dhidi ya mji wa Fizi, kilomita 240 kusini magha&#341;ibi mwa Bukavu, wakilipiza kisasi kutokana na kuuawa kwa aska&#341;i mwenzao. Zaidi ya wanawake 50 walibakwa, mamia wengine walije&#341;uhiwa. <\/p>\n<p>Lakini makumi kwa maelfu ya makosa mazito ya uhalifu yanaachwa kila siku bila kushughulikiwa katika nchi ambayo mfumo wake wa she&#341;ia kwa muda m&#341;efu umekuwa ukilemewa na vita vya wenyewe kwa wenyewe, wahalifu walikamatwa kiu&#341;ahisi na uchunguzi ulikamilika kwa miezi miwili tu. <\/p>\n<p>Hii inatokana na mahakama ya jinsia inayohama, ambayo imeundwa kupitia jitihada za pamoja za Rule of Law Initiative ya Ame&#341;ican Ba&#341; Association na Open Society&#8217;s Justice Initiative. Kulingana na Dk Kelly Askin, afisa mwandamizi wa she&#341;ia za Haki ya Kimataifa katika Open Society Justice Initiative, mahakama hiyo iliendesha kesi 186 mwaka 2010 &ndash; ambapo kati ya hizo 115 zilihusu ubakaji &ndash; katika maeneo ya vijijini ya Kivu ya Kusini ambako hakuna haki kabisa. <\/p>\n<p>Kwa kesi ya Fizi, mahakama ya kijeshi ilikaa katika chumba cha mahakama cha wazi katika mji wa ka&#341;ibu wa Ba&#341;aka kwa siku kumi. Uendeshaji wa kesi ulitazamwa kila siku na mamia ya wanakijiji. Hukumu za kati ya miaka 10 na 20 zilitolewa Feb. 21 dhidi ya watuhumiwa tisa kati ya wote waliotuhumiwa. Mwanaume mmoja aliachiwa hu&#341;u, na wa kumi na moja &ndash; mtoto mdogo &ndash; alipelekwa kwenye mahakama ya watoto.   Wanaume waliokutwa na hatia watatumikia kifungo chao katika ge&#341;eza kuu la Bukavu, ambalo lilijengwa nyakati za ukoloni. &#8220;Likiwa limejengwa kubeba wafungwa 300, ge&#341;eza hili sasa linabeba zaidi ya wafungwa 1,100,&#8221; anasema De&#341;cy Muley, katibu mtendaji wa Netwo&#341;k of Human Rights Association of South Kivu. Wazi&#341;i wa she&#341;ia wa jimbo, Sadock Biganza, aliiambia IPS kuwa asilimia 40 ya wafungwa ni aska&#341;i. <\/p>\n<p>Gavana wa jimbo la Kivu ya Kusini, Ma&#341;cellin Cishambo, alikuwepo wakati wa kutolewa kwa hukumu. Akihojiwa na IPS, gavana alitoa wito wa ku&#341;ejewa kwa malengo ya kuaji&#341;iwa katika jeshi, huku akielezea ukweli kuwa DRC imekuwa na bahati ya kuingiza wanamgambo kutoka vikundi vya zamani vya waasi katika jeshi la kitaifa kwa jina la amani. <\/p>\n<p>Cishambo alithibitisha nia ya utawala wake kukomesha udhalilishaji na ubakaji. &#8220;&#8221;Siyo ma&#341;a ya kwanza se&#341;ikali ya Kongo imeandaa hukumu dhidi ya wahusika wa unyanyasaji wa Kikongo,&#8221; alisema. Mwezi Oktoba 2010, mahakama ya kijeshi ilitoa hukumu kwa wanajeshi 13 wa jeshi la Kongo la FARDC, katika eneo la Walungu. <\/p>\n<p>Luteni Kanali Vianney Kaza&#341;ama, ambaye ni msemaji wa jeshi katika Opa&#341;esheni ya Amani Leo (kampeni ya kijeshi dhidi ya vikundi vya waasi ambayo wanajeshi waliokutwa na hatia walikuwa wakitumikia) katika Kivu ya Kusini, pia aliunga mkono hukumu hiyo. &#8220;Huu ni mfano ambao utaenea. Se&#341;a ya kutokuvumilia itatumika kwa wahusika wote.&#8221; Akiandikia Mahakama ya Haki za Binadamu ya Kimataifa, Askin wa Open Society alisema hukumu hiyo inaonyesha kuwa kwa ushi&#341;ikiano kati ya se&#341;ikali na mfumo wa she&#341;ia, Umoja wa Mataifa na NGOs na wafadhili, mashitaka ya uhalifu kama huo yanawezekana hata katika ukanda uliojaa kukosekana kwa usalama. <\/p>\n<p>&#8220;Kwa ICC kwenda kwa ngazi ya juu ya watuhumiwa ambao ma&#341;a nyingi siyo &#341;ahisi kufikiwa na mahakama za ndani &ndash; na mahakama za ndani, ikiwa ni pamoja na mahakama zinazohama, zikienda kwa watuhumiwa wa ngazi ya chini &ndash; uwajibikaji utakuwa ni destu&#341;i, na unyanyasaji bila kujali utakuwa ni suala la nad&#341;a kutokea.&#8221; Anasema Askin. <\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>BUKAVU, DR Congo, Julai 5 (IPS) &ndash; Aska&#341;i kumi na moja waliokutwa na hatia ya kuwabaka zaidi ya wanawake 50 katika mji wa Fizi mwezi Janua&#341;i, wameanza kutumikia hukumu zao ndefu katika mji wa jimbo wa Bukavu. Kuendeshwa kwa hukumu yao kwa kasi na hatimaye kukutwa na hatia na kuhukumiwa na mahakama inayohama ni dalili&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":806,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-3677","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3677","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/806"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=3677"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3677\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=3677"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=3677"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=3677"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}