{"id":3664,"date":"2011-07-06T13:40:01","date_gmt":"2011-07-06T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2011\/07\/06\/biashara-mkutano-wa-istanbul-waudisha-nyuma-nchi-maskini-2\/"},"modified":"2011-07-06T13:40:01","modified_gmt":"2011-07-06T13:40:01","slug":"biashara-mkutano-wa-istanbul-waudisha-nyuma-nchi-maskini-2","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2011\/07\/06\/biashara-mkutano-wa-istanbul-waudisha-nyuma-nchi-maskini-2\/","title":{"rendered":"BIASHARA: Mkutano wa Istanbul &#8220;Wa&#341;udisha Nyuma&#8221; Nchi Maskini"},"content":{"rendered":"<p>GENEVA, Julai 4 (IPS) &ndash; Baadhi ya maamuzi yaliyochukuliwa kuhusu biasha&#341;a katika Mpango wa Utekelezaji wa Istanbul yana uwezekano wa ku&#341;ejesha nyuma nchi maskini wakati mengine ni tata mno na hayana maana yoyote, anasema Abdoulaye Sanoko, balozi katika ujumbe wa Mali katika Shi&#341;ika la Biasha&#341;a Ulimwenguni (WTO) mjini Geneva.\n<\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>Mpango wa utekelezaji ulipitishwa katika mkutano wa nne wa hivi ka&#341;ibuni wa Umoja wa Mataifa Kuhusu Nchi Zenye Maendeleo Duni (LDCs) uliofanyika mjini Istanbul, Utu&#341;uki, Mei 9&ndash;13.<\/p>\n<p>&#8220;Mataifa ya LDCs yalijadiliana, lakini hayakuwa na chaguo. Hakukuwa na matokeo, hivyo huu ni wa&#341;aka wa kukubaliana ambao siyo lazima uwe mzu&#341;i,&#8221; Sanoko aliiambia IPS alipo&#341;ejea kutoka Istanbul.<\/p>\n<p>Kituo cha Kimataifa cha Biasha&#341;a na Maendeleo Endelevu (ICTSD), shi&#341;ika la watalaam lenye makao yake mjini Geneva ambalo pia limekuwa na wawakilishi mjini Istanbul, linakubaliana kuwa &#8220;biasha&#341;a imekuwa suala tata zaidi katika majadiliano&#8221; kwa ajili ya mpango wa utekelezaji.<\/p>\n<p>Sanoko anasema, &#8220;ninapoona su&#341;a ya biasha&#341;a, ninakuwa na mawazo ya ku&#341;udi nyuma ikilinganishwa na kile ambacho WTO taya&#341;i imekiweka kuhusu upendeleo maalum wa kibiasha&#341;a.<\/p>\n<p>&#8220;Katika Mazungumzo ya Doha, imesemwa wazi kuwa mataifa ya LDCs hayatafuta ushu&#341;u wowote. Yatafanya hivyo kwa kujitolea, wakati ambapo yanahamasishwa kuima&#341;isha ushu&#341;u wao wanaoutumia.&#8221;<\/p>\n<p>ICTSD inasema kuwa toleo la mwisho la mpango wa utekelezaji linataka utekelezaji wa muda wa soko lisilokuwa na ushu&#341;u wa fo&#341;odha na lisilokuwa na mgawo wa bidhaa za kuuzwa kwa mataifa yote ya LDCs, kwa kuzingatia azimio la mawazi&#341;i la Hong Kong la mwaka 2005, na kukomesha au kupunguza vikwazo vya biasha&#341;a visivyokuwa vya halali.<\/p>\n<p>Hata hivyo, kwa Sanoko, lugha hii &#8220;imejaa utata&#8221;. &#8220;Ni mkanganyiko na ku&#341;ejesha nyuma ahadi za soko lisilokuwa la ushu&#341;u na sehemu ya bidhaa kama zilivyotolewa huko Hong Kong, kwani inahusu uwezekano wa &#8216;kupunguza&#8217; pamoja na &#8216;kukomesha&#8217; vikwazo vya biasha&#341;a visivyokuwa vya halali&#8221;, anabainisha.<\/p>\n<p>Wakati anaka&#341;ibisha wito wa kuima&#341;isha umoja wa kikanda, anasikitikia kukosekana kwa njia za kiubunifu za kufanya hivyo, hasa juu ya kufanyiwa ma&#341;ekebisho kwa kifungu cha XXIV cha Mkataba wa Jumla wa Ushu&#341;u na Biasha&#341;a (GATT), moja ya masuala ambayo yalijadiliwa mjini Geneva.<\/p>\n<p>Kifungu hiki kinasema kuwa katika ukanda unaojulikana kama wa makubaliano ya biasha&#341;a hu&#341;ia (FTAs) pande zinazohusika zinatakiwa kufanya biasha&#341;a nyingi kuwa hu&#341;ia, bila kutaja kwa kiasi gani. Mataifa ya LDCs na yale yanayoendelea yanataka makubaliano hayo yafanyiwe ma&#341;ekebisho kuingiza sehemu kubwa ya upendeleo maalum ili mataifa maskini yasitakiwe kupunguza ushu&#341;u wao kwa kiasi kikubwa.<\/p>\n<p>&#8220;Tunaelewa kuwa mkutano kama huo hauwezi kutatua matatizo yanayohusiana na she&#341;ia za biasha&#341;a, lakini tungependa ku&#341;ejea kwenye kumbukumbu ya suala hilo,&#8221; Sanoko anatoa maoni. &#8220;Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mataifa ya LDCs ni jitihada za pamoja za jumuiya ya kimataifa kuhamasisha kuendeleza nchi yetu na mtu hawezi kuzungumzia kuhusu dhana ya jumla ambayo kwa kiasi kikubwa inakubalika bila ya kuingia katika undani wake.&#8221;<\/p>\n<p>Kuhusu suala la makubaliano ya kibiasha&#341;a kama vile mikataba ya ushi&#341;ikiano wa kiuchumi (EPAs) kati ya Jumuiya ya Ulaya, Af&#341;ika, Ca&#341;ibbean na Pacific (ACP), anasema kuwa, &#8220;inapaswa kuwa ushi&#341;ikiano, lakini ni sehemu ya FTA kama ilivyo kwa mikataba mingi.<\/p>\n<p>&#8220;Unawezaje kuwa ushi&#341;ikiano kati ya nchi zenye maendeleo makubwa na nyingine ambazo zina uwezo mdogo wa kusimama kwa miguu yao wenyewe  Hii ni fu&#341;sa nyingine inayopotea ambayo inahitaji kufanyiwa ubunifu.&#8221;<\/p>\n<p>Sanya Reid Smith, mshau&#341;i wa she&#341;ia na mtafiti mwandamizi katika Mtandao wa Dunia ya Tatu (TWN) anasema kuwa katika mjadala wa mjini Istanbul ujumbe mkali umepelekwa kuwa LDCs zisishinikizwe au kushau&#341;iwa kufanya hu&#341;ia bidhaa zao zinazoingia kwani zilipofanya hivyo katika siku za nyuma zilipata atha&#341;i kubwa. TWN ni shi&#341;ika lisilokuwa la kise&#341;ikali lenye makao yake makuu nchini Malaysia.<\/p>\n<p>&#8220;Hofu pia zilielezewa kuhusu mikataba ya biasha&#341;a hu&#341;ia na mikataba ya ushi&#341;ikiano wa kiuchumi, ambayo inaweza kusababisha uha&#341;ibifu kama huo na kuzuia matumizi ya kodi ya bidhaa zinazosafi&#341;ishwa nje kutumika kwa ajili ya kujenga viwanda vya ndani kwa misingi ya bidhaa za asili,&#8221; aliiambia IPS.<\/p>\n<p>&#8220;Kutokana na msuguano katika WTO, kuna haja ya kuwa na mfuko wa mavuno ya mapema kwa LDCs ambao utahusu masuala kama soko lisilokuwa na ushu&#341;u na mgawo wa bidhaa zinazopaswa kuuzwa na kuondokana na &#341;uzuku mbaya za pamba zinazoangamiza biasha&#341;a,&#8221; Reid Smith alihitimisha.<\/p>\n<p>Suala jingine tata, kulingana na Sanoko, ni ombi la mataifa ya LDCs kupanua wigo wao wa bidhaa zinazouzwa nje ili kuwa na uwezo wa kuongeza ma&#341;a mbili sehemu yao katika biasha&#341;a ya kimataifa katika kipindi cha miaka 10. &#8220;Lakini kwa misingi ipi  Leo hii wanawakilisha asilimia moja tu ya biasha&#341;a ya dunia. Unaweza hata kuifikisha asilimia tatu lakini, kwa uhakika kwa kutumia njia ipi &#8221; anashangaa.<\/p>\n<p>Anadhani ni &#8220;shinikizo kubwa kwa LDCs&#8221; kuwataka kuzuia udhibiti wa bidhaa toka nje na kusafisha hatua zinazoha&#341;ibu biasha&#341;a wakati kilimo katika nchi za Kaskazini kinaha&#341;ibiwa.<\/p>\n<p>&#8220;Kwa mataifa ya LDCs ba&#341;ani Af&#341;ika, kilimo ni suala muhimu,&#8221; anasisitiza. &#8220;Chukua mfano wa Malawi: ilikuwa na uhaba mkubwa wa chakula, lakini katika kipindi cha miaka mitatu tu imekuwa ikijitegemea na leo hii inasafi&#341;isha nje chakula.<\/p>\n<p>&#8220;Ufumbuzi ni kuwa na se&#341;a mpya ya kilimo ambayo inatoa baadhi ya msaada kwa wazalishaji wadogo, kama vile mbegu na mbolea. Wakati huu ambapo mgogo&#341;o wa chakula unaweza ku&#341;ejea tena, kusaidia wakulima wadogo kunaweza kuleta tofauti kubwa na kusaidia wakazi kujulisha wenyewe.&#8221;<\/p>\n<p>&#8220;Katika kipindi cha miaka 30, ni nchi tatu tu za LDCs zilijinasua kutoka kundi hilo. Hii inaonyesha jinsi mafanikio yanavyokwenda polepole, hasa kutokana na idadi ya mataifa ya LDCs ba&#341;ani Af&#341;ika kuja kuongezeka kutokana na kugawanywa kwa Sudan,&#8221; Sanoko alihitimisha.<\/p>\n<p>Ma&#341;tin Kho&#341;, mku&#341;ugenzi wa South Cent&#341;e, shi&#341;ika linaloundwa na asasi za se&#341;ikali na zisizokuwa za kise&#341;ikali mjini Geneva, anasema kuwa siyo kweli kuwa LDCs hazijaunganishwa na uchumi wa dunia. Kwa hakika, nchi nyingi za LDCs zina uwiano mkubwa wa bidhaa zinazosafi&#341;ishwa nje kuliko baadhi ya nchi zilizoendelea.<\/p>\n<p>Jinsi mataifa ya LDCs yalivyounganishwa na uchumi wa dunia unazifanya kutokupata faida kwani zinabakia kuwa tegemezi mno wa kuuza nje mali ghafi na, kutokana na malighafi hizo kuendelea kushuka bei kwa mdua m&#341;efu sasa, mataifa hayo yanakabiliwa na upotevu mkubwa wa mapato, anahitimisha.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>GENEVA, Julai 4 (IPS) &ndash; Baadhi ya maamuzi yaliyochukuliwa kuhusu biasha&#341;a katika Mpango wa Utekelezaji wa Istanbul yana uwezekano wa ku&#341;ejesha nyuma nchi maskini wakati mengine ni tata mno na hayana maana yoyote, anasema Abdoulaye Sanoko, balozi katika ujumbe wa Mali katika Shi&#341;ika la Biasha&#341;a Ulimwenguni (WTO) mjini Geneva. Mpango wa utekelezaji ulipitishwa katika mkutano&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":643,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-3664","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3664","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/643"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=3664"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3664\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=3664"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=3664"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=3664"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}