{"id":3663,"date":"2011-07-06T13:40:01","date_gmt":"2011-07-06T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2011\/07\/06\/tanzania-zinduka-redio-za-jamii-mkombozi-wa-elimu-ya-mtoto-wa-kike\/"},"modified":"2011-07-06T13:40:01","modified_gmt":"2011-07-06T13:40:01","slug":"tanzania-zinduka-redio-za-jamii-mkombozi-wa-elimu-ya-mtoto-wa-kike","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2011\/07\/06\/tanzania-zinduka-redio-za-jamii-mkombozi-wa-elimu-ya-mtoto-wa-kike\/","title":{"rendered":"Tanzania: Zinduka &ndash; Redio za Jamii Mkombozi wa Elimu ya Mtoto wa Kike"},"content":{"rendered":"<p>MICHEWENI, PEMBA, Julai 4 (IPS) &ndash; Kwa miaka mingi elimu kwa mtoto wa kike imeonekana kukandamizwa ikilinganishwa na wenzao wa kiume nchini Tanzania. Sababu kuu zinatofautiana &ndash; lakini mila na destu&#341;i za kupendelea mtoto wa kiume na hata imani za kidini zimekuwa moja ya sababu za kukandamiza elimu ya mtoto wa kike. Wilaya ya Micheweni kisiwa Pemba ni moja ya maeneo ambayo elimu ya mtoto wa kike haikuthaminiwa na jamii ya eneo hilo kwa miaka mingi.\n<\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>Mmoja wa waathi&#341;ika wa kukosa elimu kutokana na jinsia yake ni Bi Asha Msabaha ambaye ni m&#341;ajisi msaidizi katika Wiza&#341;a ya Elimu Zanziba&#341;, katika kisiwa cha Pemba. &#8220;Nilifukuzwa na baba yangu kutoka nyumbani kutokana na kupenda elimu,&#8221; alisema Bi Msabaha alipokuwa akitoa ushuhuda juu ya umuhimu wa elimu kwa mtoto wa kike yeye akiwa kama mfano wa kuigwa, wakati wa wa&#341;sha ya kuandaa vipindi vya &#341;edio ya jamii Micheweni kuhusu umuhimu wa elimu kwa mtoto wa kike. <\/p>\n<p>Mbali ya kufukuzwa nyumbani na kuanza kuishi katika nyumba ya msama&#341;ia mwema, Bi Msabaha ambaye anaki&#341;i kutoka katika familia maskini, anaelezea changamoto nyingi alizokumbana nazo wakati wa kutafuta elimu ikiwa ni pamoja na kuolewa katika um&#341;i mdogo na kuepuka kubakwa ma&#341;a kadhaa. Lakini hata hivyo, sasa anajivunia kuwa mtoto pekee mwenye elimu ya kiwango chake katika familia ya baba na mama yake yenye jumla ya watoto 11.<\/p>\n<p>&#8220;Nikiwa na elimu niliweza kumsaidia baba yangu kuendesha familia, kumsaidia mume wangu kulea watoto, kusaidia kusomesha mtoto na kufikia Chuo Kikuu, mtoto wa pili hadi kuwa mwalimu, mtoto mwingine yupo kidato cha sita na mtoto wa mwisho anasomea fani ya uandishi wa haba&#341;i,&#8221; alisema Bi Msabaha. &#8220;Hata nawapigia debe watoto wa ndugu zangu wasome wasikimbile kuolewa kwani si&#341;uhusu watoto wa ndugu kuolewa kabla hawajapata elimu ya kutosha.&#8221;<\/p>\n<p>Wa&#341;sha ya kuandaa vipindi maalum vya kuhamasisha elimu kwa mtoto wa kike iliyofadhiliwa na m&#341;adi wa Umoja wa Mataifa wa Joint 5 na UNESCO imekuja huku kukiwa na taa&#341;ifa mbaya za elimu hasa kwa mtoto wa kike katika Wilaya ya Micheweni. Inasemekana wilaya hiyo inaongoza kwa kuwa na watoto wengi wasioenda shule &ndash; sababu kuu ikiwa ni pamoja na wazazi hasa wa kiume kukosa hamasa ya kuwapeleka watoto wao shule kutokana na mila na destu&#341;i, viongozi wa dini kuhubi&#341;i katika nyumba za ibada kuwa watoto wa kike hawastahili kwenda shule na umaskini uliokithi&#341;i katika wilaya hiyo yenye viashi&#341;ia duni zaidi vya maendeleo Zanziba&#341;.<\/p>\n<p>Kuna sababu kadhaa ambazo wadau wa elimu waliamua kutumia vipindi vya &#341;edio kuhamasisha elimu ya mtoto wa kike. Sababu hizo alizielezea kwa ufasaha mwezeshaji wa wa&#341;sha hiyo, Bi Rose Haji.<\/p>\n<p>Redio bado inaongoza kwa kufikia wasikilizaji wengi zaidi bila kubagua ikilinganishwa na chombo chochote cha haba&#341;i &ndash; inawafikia vipofu, walemavu wa viungo, wasiojua kusoma na kuandika, na wale wasiokuwa na uwezo wa kununua gazeti na kumiliki televisheni. Lakini, aliongeza, &#341;edio za jamii ni muhimu zaidi kwani mambo mengi yanatoka katika jamii, vipindi vinataya&#341;ishwa na wanajamii, umiliki ni wa wanajamii, inatoa motisha katika jamii kuendeleza mjadala, inawafikia watu wengi wanaoishi katika mazingi&#341;a yasiyofikiwa na &#341;edio na vyombo vingine vikubwa vya haba&#341;i, haina gha&#341;ama kubwa, inahamasisha vikundi vya usikilizaji na kuibua mjadala kuhusu masuala yanayohusu maisha yao, inahamasisha upatikanaji wa huduma muhimu zinazohitajika na inasukuma jitihada mbalimbali za kampeni (kilimo kwanza, ufugaji bo&#341;a, lishe, maambukizi ya VVU n.k katika jamii husika.<\/p>\n<p>Siku tano za wa&#341;sha kuanzia Juni 12 hadi 16 zilikuja na kipindi cha mfano kilichotengenezwa na wanajamii wenyewe kuhamasisha elimu ya mtoto wa kike. &#8220;Zinduka &#8230;.Elimu kwa mtoto wa kike ni chachu ya maendeleo&#8221;.<\/p>\n<p>Kipindi hicho cha dakika 30 ambacho kilitengenezwa na walimu kutoka Micheweni, masheha, mashehe na wananchi wa kawaida kilikuwa gumzo kwa wananchi wa Micheweni kilipoanza ku&#341;ushwa siku ambayo wa&#341;sha ilimalizika.<\/p>\n<p>&#8220;Wananchi wengi wanavutiwa na kipindi na wamesema muda hautoshi hivyo unahitaji kuongezwa,&#8221; alisema meneja wa &#341;edio Micheweni, Shapandu.<\/p>\n<p>&#8220;Kipindi kinata&#341;ajiwa kubadili viashi&#341;ia vya elimu hasa kwa mtoto wa kike katika Wilaya ya Micheweni na hivyo kuchochea kasi ya maendeleo. Tutakuwa na mpango maalum wa ufuatiliaji siku zijazo kujua matokeo ya kipindi hiki katika eneo la Micheweni,&#8221; alisema Ofisa Haba&#341;i na Mawasiliano wa UNESCO, Al&ndash;Amin Yusuf. &#8220;Hata hivyo dalili zimeshaonyesha mafanikio kwani hapo zamani isingekuwa &#341;ahisi kwa viongozi wa dini kuketi pamoja na wananchi kujadili utengenezaji wa kipindi cha kuhamasisha elimu ya mtoto wa kike Micheweni.&#8221;<\/p>\n<p>Ama kweli Micheweni imezinduka kuhakikisha elimu kwa mtoto wa kike inachochea maendeleo ya kweli. Na, &#341;edio ya jamii Micheweni inafanya kazi hiyo kwa ufasha mkubwa. <\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>MICHEWENI, PEMBA, Julai 4 (IPS) &ndash; Kwa miaka mingi elimu kwa mtoto wa kike imeonekana kukandamizwa ikilinganishwa na wenzao wa kiume nchini Tanzania. Sababu kuu zinatofautiana &ndash; lakini mila na destu&#341;i za kupendelea mtoto wa kiume na hata imani za kidini zimekuwa moja ya sababu za kukandamiza elimu ya mtoto wa kike. Wilaya ya Micheweni&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":536,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-3663","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3663","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/536"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=3663"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3663\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=3663"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=3663"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=3663"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}