{"id":3649,"date":"2011-05-31T13:40:01","date_gmt":"2011-05-31T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2011\/05\/31\/dr-congo-kupanda-mbegu-kwa-usalama-wa-chakula\/"},"modified":"2011-05-31T13:40:01","modified_gmt":"2011-05-31T13:40:01","slug":"dr-congo-kupanda-mbegu-kwa-usalama-wa-chakula","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2011\/05\/31\/dr-congo-kupanda-mbegu-kwa-usalama-wa-chakula\/","title":{"rendered":"DR CONGO: Kupanda Mbegu Kwa Usalama wa Chakula"},"content":{"rendered":"<p>KIKWIT, DR Congo, Mei 30 (IPS) &ndash; Wakulima wadogo wadogo katika Jimbo la kusini magha&#341;ibi mwa Jamhu&#341;i ya Kidemok&#341;asia ya Kongo la Bandundu wanashuhudia mavuno yao yakiwa yameongezeka ma&#341;a mbili, hii ni kutokana na msaada mkubwa kutoka se&#341;ikalini.\n <\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>Mpango wa Kunyanyua na Kusaidia Sekta ya Kilimo, unaojulikana kwa kifupi cha Kifa&#341;ansa kama PARSAR, unapatia wakulima wadogo mbegu bo&#341;a na ushau&#341;i wa mbinu za kilimo ikiwa ni pamoja na kubo&#341;esha ba&#341;aba&#341;a ili ku&#341;ahisisha kuyafikia masoko. Matokeo yake yamekuwa chanya.<\/p>\n<p>&#8220;Kabla ya mwaka 2008, chama chetu kilifanya kazi kubwa na kuzalisha kidogo: tani moja tu ya mihogo au mpunga kwa kila hekta. Lakini PARSAR ilipoanza kutusaidia, picha nzima ya azalishaji ilibadilika. Kila mwaka tangu mwaka 2008, tumezalisha tani nne au tano kwa kila hekta ya mihogo aina ya Nsansa,&#8221; anasema Guy Lase&#341;e, m&#341;atibu wa kikundi cha wakulima 44 katika wilaya iliyopo kilomita 40 kutoka mji mkuu wa jimbo, Kikwit.<\/p>\n<p>Lase&#341;e anasema kikundi cha Mulele kiko chini ya Chama cha Mbegu za Kijiji, kikundi cha wakulima 28 kilichoanzishwa na PARSAR.<\/p>\n<p>&#8220;PARSAR imeanzisha vyama vya mbegu vya aina hiyo 15, na kila kimoja kina kati ya vikundi vya wakulima wadogo 20 na 40. Vyama hivi vinabo&#341;esha aina ya mbegu na kusambaza kwa wakulima. Vina&#341;atibiwa na Mtandao wa Wakulima Wadogo wa Bandundu ambao unafanya kazi kama aina ya chama cha wakulima cha aina yake,&#8221; anaelezea Amede Mungwele, m&#341;atibu mwingine katika PARSAR.<\/p>\n<p>Katika Nsimulungu, kilomita 28 kutoka Kikwit huko Bulungu, kijiji kingine chenye vyama vya PARSAR wanalima aina ya mahindi yanayotokana na mbegu zilizobo&#341;eshwa, mpunga, ka&#341;anga na cho&#341;oko.<\/p>\n<p>&#8220;Tuna mashamba manne ya pamoja, kila moja lina ukubwa wa hekta 16. Tangu mwaka 2009, kwa kutumia ka&#341;anga aina ya j124, tumezalisha tani tatu kwa hekta, ikilinganishwa na tani moja mwaka uliopita. Suala kama hilo lilijitokeza katika mpunga aina ya i&#341;at12, ambao kwa sasa unazalisha tani nne kwa hekta, ikilinganishwa na tani moja tu au mbili mwaka uliotangulia,&#8221; anasema &#341;ais wa chama cha Nsimulungu, Nesto&#341; Nkama.<\/p>\n<p>Kufungua fu&#341;sa kwa wakulima <\/p>\n<p>Idadi ya wakazi katika jimbo la Bandundu &ndash; na DRC kwa ujumla &ndash; kwa muda m&#341;efu wamekabiliwa na uhaba wa chakula, pamoja na mazingi&#341;a ambayo kiasili yanafaa kwa kilimo. Hii ni kutokana na miaka mingi ya vita vya wenyewe kwa wenyewe ikiwa ni pamoja na kukosa mbinu bo&#341;a za kilimo.<\/p>\n<p>Mkakati wa mwaka 2008 ambao ulianzisha mpango wa se&#341;ikali wa kitaifa wa kilimo nchini Kongo wa hadi mwaka 2013 unasema kuwa ka&#341;ibu watu milioni 17 nchini DRC watakuja kukumbwa na baa la njaa. Shi&#341;ika la Chakula na Kilimo Ulimwenguni linakadi&#341;ia kuwa ka&#341;ibu asilimia 73 ya wakazi nchini Kongo wanaishi na uhaba wa chakula.<\/p>\n<p>&#8220;Taifa hilo lina hekta zipatazo milioni 135 zinazofaa kwa kilimo, ambazo ni hadi asilimia 34 ya a&#341;dhi yote ya taifa hilo, na asilimia 10 tu ya hizi zimeendelezwa,&#8221; unasema wa&#341;aka huo.<\/p>\n<p>Ni katika kukabiliana na changamoto hii kuwa se&#341;ikali ya Kongo ilianzisha m&#341;adi wa maendeleo wa PARSAR mwaka 2008.<\/p>\n<p>&#8220;M&#341;adi huu unafanya kazi katika maeneo manne: kusaidia taasisi, kujenga uwezo, kusaidia uzalishaji wa kilimo, na uka&#341;abati wa miundombinu ya msingi ya jamii na kiuchumi. Yote haya yanafanyika kwa msaada wa Benki ya Maendeleo ya Af&#341;ika ambayo ilitoa tak&#341;ibani dola milionmi 30,&#8221; anaelezea Lambe&#341;t Diango, &#341;ais wa PARSAR tawi la Bandundu.<\/p>\n<p>&#8220;Kila &#341;obo ya mwaka, tunaonyesha wakulima wadogo mbinu mpya za uzalishaji,&#8221; anasema Jean Misiwense, msimamizi wa PARSAR. &#8220;Tunawapatia mbegu bo&#341;a zinazotolewa na Mafunzo ya Kitaifa na Utafiti wa Kilimo, na kusimamiwa na Taasisi ya Mbegu ya Kitaifa (SEMASEM). Pia tunawapatia zana na vifaa, na tunafanya ufuatiliaji.&#8221;<\/p>\n<p>Kulingana na Misiwense, mbegu bo&#341;a zinakua kwa ha&#341;aka na zina kiwango cha juu cha mavuno. Pia zinastahimili magonjwa ya mimea ikilinganishwa na mbegu nyingine za jadi.<\/p>\n<p>&#8220;Kwa sasa, zaidi ya kaya 200,000 zinafaidika na kiasi kikubwa cha mazao bo&#341;a ya kilimo. Na zaidi ya kilomita 350 za ba&#341;aba&#341;a zimeka&#341;abatiwa na m&#341;adi ku&#341;uhusu wakulima wadogo kusafi&#341;isha mazao yao,&#8221; anaongeza.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>KIKWIT, DR Congo, Mei 30 (IPS) &ndash; Wakulima wadogo wadogo katika Jimbo la kusini magha&#341;ibi mwa Jamhu&#341;i ya Kidemok&#341;asia ya Kongo la Bandundu wanashuhudia mavuno yao yakiwa yameongezeka ma&#341;a mbili, hii ni kutokana na msaada mkubwa kutoka se&#341;ikalini. Mpango wa Kunyanyua na Kusaidia Sekta ya Kilimo, unaojulikana kwa kifupi cha Kifa&#341;ansa kama PARSAR, unapatia wakulima&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":856,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-3649","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3649","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/856"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=3649"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3649\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=3649"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=3649"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=3649"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}