{"id":3623,"date":"2011-05-05T13:40:01","date_gmt":"2011-05-05T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2011\/05\/05\/china-watafiti-watafuta-nishati-mbadala\/"},"modified":"2011-05-05T13:40:01","modified_gmt":"2011-05-05T13:40:01","slug":"china-watafiti-watafuta-nishati-mbadala","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2011\/05\/05\/china-watafiti-watafuta-nishati-mbadala\/","title":{"rendered":"CHINA: Watafiti Watafuta Nishati Mbadala"},"content":{"rendered":"<p>BEIJING, May 4 (IPS) &ndash; Watafiti nchini China, taifa linaloongoza kwa kuzalisha mashine za umeme wa upepo na paneli za umeme wa jua, wanafanya kazi ya kuifanya nishati mbadala kuwa ya bei nafuu, yenye ufanisi mkubwa na kuwa sehemu kubwa ya umeme katika g&#341;idi ya taifa hilo.\n <\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>Lakini pamoja na kasi kubwa ya China kuwa kiongozi katika nyanja ya nishati mbadala, uwekezaji zaidi wa se&#341;ikali unahitajika kwa ajili ya utafiti na maendeleo kama China inataka kweli kuelekea kwenye nishati mbadala katika siku zijazo, wanasema watafiti. <\/p>\n<p>Zhao Xingzhong, p&#341;ofesa katika Chuo Kikuu cha Wuhan Shule ya Fizikia na Teknolojia, anatafuta bet&#341;i za jua za bei nafuu, zenye ufanisi mkubwa. <\/p>\n<p>Matokeo ya kiutendaji yako wazi, anasema Zhao. <\/p>\n<p>&#8220;Uzalishaji wa bet&#341;i za jua hauzalishi hewa ya kaboni, na hivyo kuwa na maana kuwa hautakuwa na atha&#341;i katika mazingi&#341;a,&#8221; Zhao anaiambia IPS. &#8220;Na bet&#341;i za aina hiyo zinagha&#341;imu moja ya tano ya bet&#341;i zilizozoeleka zinazontengenezwa kwa kutumia madini aina ya silicon.&#8221; <\/p>\n<p>Pamoja na kwamba timu ya utafiti ya Zhao ni ya kipekee nyumbani na nje ya nchi, anasema msaada kutoka se&#341;ikali ya China uko mbali mno kutosheleza. Anabainisha kuwa Japan na Ko&#341;ea Kusini zimewekeza kwa pamoja kiasi cha dola bilioni 1.6 za Kima&#341;ekani katika utafiti wa kizazi cha tatu cha teknolojia ya nishati ya jua tangu mwaka 2000. Nchini China, hata hivyo, Zhao anasema kumekuwepo na mi&#341;adi ya ndani mitano tu katika nyanja ya nishati ya jua katika muongo uliopita, na kutumia dola zipatazo milioni 4.5 tu kwa kila m&#341;adi. <\/p>\n<p>&#8220;Ni vigumu kuvunja vikwazo vya maendeleo ya teknolojia kutokana na fedha ambazo hazitoshi,&#8221; Zhao anasema. <\/p>\n<p>Katika miaka ya ka&#341;ibuni, China imekuwa kiongozi wa dunia wa uzalishaji wa teknolojia ya nishati mbadala, na kuipita Ma&#341;ekani kulingana na idadi ya mashine za nishati ya upepo na paneli za jua. Kampuni ya ukaguzi wa mahesabu ya E&#341;nst &#038; Young mwezi Septemba iliitaja China kuwa eneo bo&#341;a zaidi la kuwekeza nishati mbadala. <\/p>\n<p>Makampuni ya Kichina, yakiongozwa na kampuni lenye makao yake huko Jiangsu&ndash;la Suntech, yanazalisha &#341;obo ya paneli za umeme wa jua na yanashika soko kwa kasi kutokana na kushusha bei. Fedha ya kuchagiza uchumi ya China mwaka 2009 ilitoa &#341;uzuku katika mi&#341;adi mikubwa ya kufunga nishati ya jua. <\/p>\n<p>Katika eneo la nishati ya upepo, makampuni ya ndani yamechukua soko kwa kasi kubwa katika miaka ya ka&#341;ibuni baada ya se&#341;ikali kupandisha mahitaji ya ushi&#341;ikiano wa ndani kwa makampuni ya kigeni hadi asilimia 70 kutoka asilimia 40 (hata hivyo se&#341;ikali imeshaondoa matakwa ya kushi&#341;ikiana na kampuni za ndani) na kuanzisha &#341;uzuku mpya na motisha nyingine kwa makampuni ya nishati ya upepo ya Kichina. <\/p>\n<p>Hadi mwaka 2009, kulikuwa na makampuni 67 ya Kichina ya kuzalisha mashine za nishati ya upepo na soko kwa makampuni ya kigeni likashuka hadi asilimia 37 kutoka asilimia 70 katika kipindi cha miaka mitano tu iliyopita. <\/p>\n<p>Lakini sehemu nyingi zinazozalishwa na makampuni ya Kichinia zinatokana na teknolojia ya nje, na kuwepo kwa jitihada ndogo mno katika kubuni teknolojia ya nishati mbadala ya ndani ya nchi. <\/p>\n<p>Wang Mengjie, naibu mku&#341;ugenzi wa Chama cha Nishati Mbadala cha China na makamu mwenyekiti wa zamani wa Chuo cha Uhandisi wa Kilimo China, anafanyia kazi sekta ya nishati ya taka. Anasema nishati ya taka inaweza kutumika kubo&#341;esha maisha katika maeneo ya vijijini, na kwa sasa anashi&#341;iki katika mi&#341;adi yenye lengo la kuwapatia wakulima vifaa ambavyo vinaweza kugeuza taka kuwa chanzo cha nishati isiyochafua mazingi&#341;a na mbolea. <\/p>\n<p>Kulingana na Wiza&#341;a ya Kilimo, kiasi cha taka katika maeneo ya vijijini nchini China kilifikia zadi ya milioni 35 mwishoni mwa mwaka 2009, na kuzalisha mita za ujazo bilioni 12.4 kwa mwaka. Se&#341;ikali imeongeza fedha za gesi ya taka katika miaka ya ka&#341;ibuni, na kufikia RMB bilioni 5 (sawa na dola milioni 754,547) mwaka 2009 kutoka wastani wa RMB bilioni 2.5 (dola milioni 377.2) mwaka 2006 na 2007. <\/p>\n<p>Pamoja na uwekezaji, Wang anasema China inakabiliwa na vikwazo vya teknolojia katika sekta ya nishati ya taka. <\/p>\n<p>&#8220;Katika suala la teknolojia ya dizeli ya taka, nchi za Magha&#341;ibi kama Ma&#341;ekani na Uje&#341;umani zinaongoza duniani, wakati China bado ipo katika hatua changa,&#8221; Wang anasema. &#8220;China haina she&#341;ia kamili au se&#341;a za nishati ya taka sasa. Katika mazingi&#341;a ya sasa, hakuna uwezekano kwa eneo hilo kuendelea zaidi.&#8221; <\/p>\n<p>Wakosoaji wa mambo wanasema kwa China kuvutiwa na nishati mbadala ni suala la fu&#341;sa ya kibiasha&#341;a &ndash; kiasi kikubwa inachozalisha kinauzwa nje ya nchi &ndash; na inavutiwa kidogo katika kutumia teknolojia ya gha&#341;ama kubwa nchini mwao. <\/p>\n<p>China bado haijaifikia Ma&#341;ekani katika suala zima la uzalishaji wa nishati mbadala. Nchi hiyo ni mtumiaji mkuu wa makaa ya mawe duniani na inata&#341;ajiwa kuunguza tani bilioni 4.5 za makaa ya mawe ifikapo mwaka 2020, kulingana na takwimu za shi&#341;ika la Utawala wa Nishati la Taifa. <\/p>\n<p>Wakati makaa ya mawe yatachangia mbili ya tatu ya uwezo wa nishati nchini China hadi mwaka 2020, se&#341;ikali imeahidi kuwekeza mabilioni ya dola katika kuendeleza nishati ya upepo, jua na nyuklia. Bunge la kutunga she&#341;ia nchini humo, National People&#8217;s Cong&#341;ess, sasa linahitaji makampuni yanayoingiza umeme katika g&#341;idi ya taifa kununua asilimia 100 ya umeme wake unaozalishwa kutoka jene&#341;eta za nishati mbadala. <\/p>\n<p>Takwimu za se&#341;ikali zilizotolewa Ap&#341;ili iliyopita zilisema kuwa vyanzo vya nishati isiyozalisha hewa nyingi ya kaboni vinaweza kuchangia zaidi ya &#341;obo ya umeme unaosambazwa nchini China ifikapo mwishoni mwa mwaka 2010, kulingana na shi&#341;ika la haba&#341;i la se&#341;ikali la Xinhua. Takwimu zilionyesha kuwa nishati ya maji, nyuklia na upepo zilita&#341;ajiwa kuchangia gigawati 250 ifikapo mwishoni mwa mwaka 2010, wakati makaa ya mawe yatachangia gigawati 700. <\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>BEIJING, May 4 (IPS) &ndash; Watafiti nchini China, taifa linaloongoza kwa kuzalisha mashine za umeme wa upepo na paneli za umeme wa jua, wanafanya kazi ya kuifanya nishati mbadala kuwa ya bei nafuu, yenye ufanisi mkubwa na kuwa sehemu kubwa ya umeme katika g&#341;idi ya taifa hilo. Lakini pamoja na kasi kubwa ya China kuwa&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":854,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-3623","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3623","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/854"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=3623"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3623\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=3623"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=3623"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=3623"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}