{"id":3607,"date":"2011-04-08T13:40:01","date_gmt":"2011-04-08T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2011\/04\/08\/wakulima-wa-afika-kusini-waingia-kongo\/"},"modified":"2011-04-08T13:40:01","modified_gmt":"2011-04-08T13:40:01","slug":"wakulima-wa-afika-kusini-waingia-kongo","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2011\/04\/08\/wakulima-wa-afika-kusini-waingia-kongo\/","title":{"rendered":"Wakulima wa Af&#341;ika Kusini Waingia Kongo"},"content":{"rendered":"<p>POINTE&ndash;NOIRE, Kongo, Ap&#341;ili 6 (IPS) &ndash; Katika mata&#341;ajio ya kuima&#341;isha uzalishaji wake wa kilimo, Jamhu&#341;i ya Watu wa Kongo imetoa zaidi ya hekta 80,000 za a&#341;dhi yake inayofaa kwa kilimo kwa kampuni inayomilikiwa na kuendeshwa na wakulima 14 wa Af&#341;ika Kusini.\n<\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>&#8220;Nchi yetu inakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula na ili kutatua tatizo hili, ni muhimu kuifanya a&#341;dhi kutumiwa na wakulima ambao pia ni wawekezaji. Ni se&#341;a mpya na tutaiendeleza,&#8221; anasema Rigobe&#341;t Maboundou,Wazi&#341;i wa Kilimo na Mifugo wa Kongo.<\/p>\n<p>Katika mkataba uliosainiwa mwezi Machi 10 mjini Pointe&ndash;Noi&#341;e, nchini Kongo, kundi la wakulima wa Af&#341;ika Kusini na kampuni yao wanayomiliki kwa ubia ya Congo Ag&#341;icultu&#341;e, lilipewa zaidi ya hekta 63,000 za a&#341;dhi katika eneo la Malalo II na hekta nyingine za nyongeza 17,000 katika eneo la Dihesse, kusini magha&#341;ibi mwa nchi. Kulingana na mkataba huo, Waaf&#341;ika Kusini wataanzisha kiwanda cha kusindika chakula katika eneo la Malolo II, ambacho kitajenga aji&#341;a.<\/p>\n<p>&#8220;Kongo imekuwa ikisubi&#341;i mpango huu wa uwekezaji, kujenga aji&#341;a na jambo muhimu zaidi, kuongeza uzalishaji wa chakula, kwani wakulima hawa watapanda mazao ya chakula na kufuga mifugo,&#8221; anasema Pie&#341;&#341;e Mabiala, Wazi&#341;i wa Mabadiliko ya A&#341;dhi, ambaye alikabidhi hati miliki.<\/p>\n<p>Waaf&#341;ika Kusini hao wamepanga kupanda mpunga, mahindi na soya. &#8220;Pia wanataka kuchunga ng&#8217;ombe, mbuzi na ngu&#341;uwe,&#8221; anasema Genge Manelisi, balozi wa Af&#341;ika Kusini mjini B&#341;azzaville, mji mkuu wa Kongo.<\/p>\n<p>Wakulima wadogo wamehamishwa <\/p>\n<p>A&#341;dhi iliyopatiwa Waaf&#341;ika Kusini katika eneo la Malolo II na Dihesse ilikuwa ikimilikiwa na wakulima wadogo hapo kabla ambao walitegemea mbinu za kilimo cha jadi.<\/p>\n<p>&#8220;Nilishangazwa nilipoambiwa na watu wa se&#341;ikali kuwa natakiwa kuondoka katika shamba langu la mihogo na ka&#341;anga,&#8221; anasema Jean Mbenze, mkulima mdogo kutoka Dihesse.<\/p>\n<p>&#8220;Ni suala la upatikanaji wa taa&#341;ifa,&#8221; anasema Ch&#341;istian Mounz&eacute;o, &#341;ais wa NGO yenye makao yake Pointe&ndash;Noi&#341;e, iitwayo Confe&#341;ence fo&#341; Peace and Human Rights. &#8220;Ni kwa nini suala hili la kugawa a&#341;dhi halijawekwa wazi kwa umma, na kusababisha mjadala wa kitaifa ambao unge&#341;uhusu watu kushi&#341;ikishana, badala ya kuamua bila kushau&#341;iana madha&#341;a yake katika jamii &#8220;<\/p>\n<p>Kuhamishwa kwa wakulima kupisha kampuni ya Congo Ag&#341;icultu&#341;e kumeongeza shinikizo linalozidi kuongezeka kwa wengine ambao wanapanda chakula kwa ajili ya maeneo ya mijini.<\/p>\n<p>&#8220;Hapa katika mji wa Pointe&ndash;Noi&#341;e (kusini magha&#341;ibi) hatuna a&#341;dhi kwa ajili ya bustani, kwani imeuzwa ili kujenga majengo. Tunaleta ka&#341;oti kutoka Dolisie (kilomita 160 kutoka Pointe&ndash;Noi&#341;e) ambazo zinauzwa kwa fa&#341;anga za CFA 1,500 (kama dola tatu) kwa kilo, ambazo tunaziuza kwa CFA 2,000 ,&#8221; Clementine Mpaka, ambaye alikuwa mkulima katika eneo la Ngoyo, ambalo sasa limejengeka katika jiji hilo anasema.<\/p>\n<p>&#8220;Hali inafanana na B&#341;azzaville, ambako eneo la ukingo wa bustani kandokando mwa Mto Kongo, katika wilaya ya Mpila, &ndash; pamoja na kuhifadhiwa na se&#341;ikali &ndash; limegawanywa katika viwanja vya majengo,&#8221; anasema Kevin Mvi&#341;i, kutoka shi&#341;ika la &#8220;Association fo&#341; Human Rights and the P&#341;ison Envi&#341;onment&#8221;. Analaumu kupigwa kwa wakulima hawa wa mashamba yanayozunguka miji na watu ambao walinunua umiliki wa a&#341;dhi.<\/p>\n<p>&#8220;Hakuna hata mmoja wao aliwasaidia, na se&#341;ikali iliweza kukabidhi a&#341;dhi hiyo kwa wageni bila kikwazo.&#8221;<\/p>\n<p>Siyo suala la uzalishaji chakula <\/p>\n<p>Mashamba madogo yapatayo 100,000 ni vyanzo vya msingi vya kipato kwa familia za Wakongo, pamoja na kuwa mavuno yao ni kidogo mno katika mahitaji ya chakula nchini.<\/p>\n<p>Kulingana na Shi&#341;ika la Chakula na Kilimo (FAO), miongoni mwa hekta milioni 10 za a&#341;dhi ya kilimo nchini humo, Wakongo wanalima asilimia mbili tu. Hii ndiyo sababu, kulingana na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Se&#341;a za Chakula, asilimia 21 ya Wakongo wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula.<\/p>\n<p>Se&#341;ikali bado inatumia dola milioni 60 kwa ajili ya kuagiza chakula kutoka nje kila mwaka, kulingana na takwimu za se&#341;ikali.<\/p>\n<p>Wakulima wadogo wanahamishwa kupisha kilimo kitakachozalisha mazao zaidi, kama ilivyo katika m&#341;adi uliozinduliwa mwaka 2010, huko Moulende, ambapo NGO ya Inte&#341;national Pa&#341;tne&#341;ship fo&#341; Human Development (IPHD) ambayo ina makao yake nchini Ma&#341;ekani kwa sasa inavuna tani 1,300 za mahindi.<\/p>\n<p>&#8220;Sote ni washindi katika eneo hili, kwani se&#341;ikali haipaswi tena kuagiza chakula kutoka nje. Pia tutagawa chakula kwenye migahawa ya shule na kuzalisha chakula cha ng&#8217;ombe,&#8221; Ch&#341;istian Bana, mkuu wa IPHD nchini Kongo anaiambia IPS.<\/p>\n<p>&#8220;Tunahitaji dhami&#341;a njema tu na &#341;asilimali, kutokana na kwamba sasa tuna nguvu kazi, na tutakuwa na mavuno mengi, kama ilivyo kwa IPHD. Tunataka kampuni nyingi zaidi na mipango kama hii,&#8221; Maboundou anasema.<\/p>\n<p>Kati ya mwaka 2011 na 2015, Kongo inakadi&#341;iwa kuwekeza dola milioni 80 katika kilimo, kiasi kidogo mno katika bajeti yake ya sasa ya dola bilioni sita kwa mwaka. Se&#341;ikali inasema kuwa vijiji vipya vya kilimo, vyenye mapato ya tani 2,000 za mihogo kwa mwaka, na mayai yapatayo 2,500 kwa siku, vinajengwa.<\/p>\n<p>&#8220;Kuna mambo mengi ndani yake zaidi ya kuita wakulima wa Af&#341;ika Kusini ambao wanaweza kuleta uzoefu wao katika maendeleo ya kilimo. Haipaswi kusahau kuwa ushi&#341;iki wetu katika m&#341;adi wa maendeleo ya kilimo wa taifa unahitaji kutoa kiasi kikubwa cha pembejeo na msaada kwa wakulima, kabla ya kuleta makampuni ya kigeni,&#8221; anasema Mounz&eacute;o. <\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>POINTE&ndash;NOIRE, Kongo, Ap&#341;ili 6 (IPS) &ndash; Katika mata&#341;ajio ya kuima&#341;isha uzalishaji wake wa kilimo, Jamhu&#341;i ya Watu wa Kongo imetoa zaidi ya hekta 80,000 za a&#341;dhi yake inayofaa kwa kilimo kwa kampuni inayomilikiwa na kuendeshwa na wakulima 14 wa Af&#341;ika Kusini. &#8220;Nchi yetu inakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula na ili kutatua tatizo hili, ni&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":797,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-3607","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3607","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/797"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=3607"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3607\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=3607"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=3607"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=3607"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}