{"id":3598,"date":"2011-04-04T13:40:01","date_gmt":"2011-04-04T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2011\/04\/04\/afrika-macho-yote-kwa-mfuko-wa-hali-ya-hewa\/"},"modified":"2011-04-04T13:40:01","modified_gmt":"2011-04-04T13:40:01","slug":"afrika-macho-yote-kwa-mfuko-wa-hali-ya-hewa","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2011\/04\/04\/afrika-macho-yote-kwa-mfuko-wa-hali-ya-hewa\/","title":{"rendered":"AFRIKA: Macho Yote kwa Mfuko wa Hali ya Hewa"},"content":{"rendered":"<p>JOHANNESBURG, Ap&#341;ili 1 (IPS) &ndash; Benki ya Maendeleo Af&#341;ika inasema ina wasiwasi na ucheleweshwaji wa kiutawala ambao unashikilia mafanikio ya Mfuko wa Kijani wa Hali ya Hewa &ndash; moja ya mafanikio muhimu yaliyotokana na mazungumzo ya hali ya hewa ya Cancun.\n<\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>&#8220;Tumechanganyikiwa mno na mafanikio ya polepole ya kuanzisha mifumo ya kutoa maamuzi juu ya Mfuko wa Hali ya Hewa,&#8221; alisema Donald Kabe&#341;uka, Mku&#341;ugenzi Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo ya kikanda. &#8220;Lakini nina mata&#341;ajio kuwa tunaweza kwenda kwa kasi, na tunata&#341;ajia kuwa Kamati inaweza kusikiliza malalamiko ya Af&#341;ika, wasiwasi wa Af&#341;ika,&#8221; aliongeza.<\/p>\n<p>Moja ya ta&#341;ehe ya mwisho zilizowekwa na Canc&uacute;n ni kwa mkutano wa nchi 40 wa Kamati ya Mpito kubuni Mfuko wa Kijani wa Hali ya Hewa kuanza kutumika kabla ya mwishoni mwa Machi 2011. Mkutano huo umeahi&#341;ishwa hadi mwishoni mwa Ap&#341;ili, kutokana na kutokukubaliana kuhusu uwakilishi wake wa kikanda.<\/p>\n<p>Lazima makubaliano yafikiwe katika Mkutano ujao wa Pande Husika (COP), utakaofanyika mjini Du&#341;ban Desemba 2011, alisema Kabe&#341;uka.<\/p>\n<p>&#8220;Kwetu sisi Waaf&#341;ika, COP 17 lazima ije na makubaliano kamili ya Mfuko huo, utawala wake, na kuhakikisha kuwa fedha zinakuwepo,&#8221; Kabe&#341;uka alisema.<\/p>\n<p>&#8220;Nina matumaini kuwa ucheleweshaji huu ni wa muda tu na wa kiutawala, na hauhusiani na se&#341;a au vinginevyo,&#8221; aliongeza.<\/p>\n<p>Hakuna haja ya hofu <\/p>\n<p>Lakini waangalizi wengine wa mambo wanasema ucheleweshwaji huo unaeleweka, na usiangaliwe kama kushuka kwa dhami&#341;a ya kisiasa.<\/p>\n<p>Belynda Pet&#341;ie, CEO wa shi&#341;ika la hali ya hewa la OneWo&#341;ld anasema kuwa ucheleweshwaji unata&#341;ajiwa, na umesababishwa na mazungumzo juu ya aina ya uwakilishi kutoka kila kanda.<\/p>\n<p>&#8220;Mataifa mengi yanataka kusema kuwa, na kufikia makubaliano juu ya uwakilishi siyo suala la moja kwa moja, lakini nadhani tumepata mafanikio mazu&#341;i ba&#341;ani Af&#341;ika,&#8221; Pet&#341;ie alisema.<\/p>\n<p>&#8220;Wakati mikutano ikianza Ap&#341;ili, taya&#341;i kumekuwepo na mjadala kuhusu Mfuko huo,&#8221; aliiambia IPS, &#8220;na kama itaendelea kufanyika, inaweza kuleta mafanikio.&#8221;<\/p>\n<p>&#8220;Lakini uthibitisho utajichanganya,&#8221; alionya Pet&#341;ie. &#8220;Nchi zinazoendelea zinaendelea kuwa na imani kuhusu mafanikio ya kuundwa kwa mfuko, lakini juu ya kama nchi zilizoendelea zinakubaliana linabakia suala la kusubi&#341;iwa.&#8221;<\/p>\n<p>Mfumo wa mfuko huo, ikiwa ni pamoja na makubaliano ya usawa katika kusisitiza katika kuishi na mabadiliko na kukabiliana nayo bado hakujakubaliwa, alisema Pet&#341;ie.<\/p>\n<p>Mfuko wa Kijani wa Hali ya Hewa, uliobuniwa kusaidia kuunganisha, kusimamia na kuingiza fedha kusaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, ulipendekezwa mjini Copenhagen na kuingizwa &#341;asmi kwenye mfumo huko Canc&uacute;n. Unata&#341;ajiwa kusimamia hadi dola bilioni 100 kwa mwaka ifikapo mwaka 2020.<\/p>\n<p>Kufadhili kuishi katika mabadiliko ba&#341;ani Af&#341;ika <\/p>\n<p>Pamoja na Mfuko huu, Kabe&#341;uka anasema Af&#341;ika inahitaji chombo chake cha fedha.<\/p>\n<p>Mfumo unaopendekezwa, Mfuko wa Kijani wa Af&#341;ika, utasimamiwa na Benki ya Maendeleo Af&#341;ika, ili kutoa kiasi cha fedha zilizokusanywa kupitia chombo cha kimataifa kuja ba&#341;ani Af&#341;ika.<\/p>\n<p>&#8220;Mataifa ya Af&#341;ika yana matatizo maalum, na hatujafaidika kwa kiasi kikubwa na mfumo chini ya Itifaki ya Kyoto,&#8221; Kabe&#341;uka alisema, &#8220;na hivyo suala ni, je tunaweza kuwa na sehemu ndogo ya Mfuko wa Kijani, ambao unaweza kusimamiwa na Benki ya Maendeleo Af&#341;ika kushughulikia masuala maalum kwa Af&#341;ika.&#8221;<\/p>\n<p>Kabe&#341;uka alihamasisha matumaini juu ya mazungumzo yajayo ya mabadiliko ya tabia nchi ya Desemba. &#8220;Nadhani Copenhagen ilijenga mata&#341;ajio mengi mno. Katika mji wa Canc&uacute;n, matokeo yalikuwa mazu&#341;i mno, lakini yalikuwa machache. Nadhani tulikwenda Canc&uacute;n tukiwa na mata&#341;ajio machache, na tulijadiliana na kuyavuka,&#8221; alisema.<\/p>\n<p>&#8220;Kwetu sisi katika ba&#341;a la Af&#341;ika, inazidi kuwa suala la ha&#341;aka kuliko wakati mwingine wowote ule. Na nadhani tunaweza kufikia makubaliano, kwasababu masuala ambayo yalitengwa kwa ajili yetu siyo mapana kama ilivyokuwa hapo kabla,&#8221; Kabe&#341;uka alisema. <\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>JOHANNESBURG, Ap&#341;ili 1 (IPS) &ndash; Benki ya Maendeleo Af&#341;ika inasema ina wasiwasi na ucheleweshwaji wa kiutawala ambao unashikilia mafanikio ya Mfuko wa Kijani wa Hali ya Hewa &ndash; moja ya mafanikio muhimu yaliyotokana na mazungumzo ya hali ya hewa ya Cancun. &#8220;Tumechanganyikiwa mno na mafanikio ya polepole ya kuanzisha mifumo ya kutoa maamuzi juu ya&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":776,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-3598","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3598","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/776"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=3598"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3598\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=3598"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=3598"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=3598"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}