{"id":3524,"date":"2011-01-03T13:40:01","date_gmt":"2011-01-03T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2011\/01\/03\/dr-kongo-chanjo-tahadhai-mapema-ni-silaha-mapema-lakini-kuna-uhaba-wa-fedha\/"},"modified":"2011-01-03T13:40:01","modified_gmt":"2011-01-03T13:40:01","slug":"dr-kongo-chanjo-tahadhai-mapema-ni-silaha-mapema-lakini-kuna-uhaba-wa-fedha","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2011\/01\/03\/dr-kongo-chanjo-tahadhai-mapema-ni-silaha-mapema-lakini-kuna-uhaba-wa-fedha\/","title":{"rendered":"DR KONGO: Chanjo: Tahadha&#341;i Mapema ni Silaha Mapema Lakini Kuna Uhaba wa Fedha"},"content":{"rendered":"<p>KINSHASA, Des 8 (IPS) &ndash; Wataalam wa afya wanahofia kwamba kukosekana kwa usalama na &#341;asilimali kunaweza kusababisha kulipuka upya kwa magonjwa &#341;ahisi kuzuilika katika Jamhu&#341;i ya Kidemok&#341;asia ya Kongo (DRC). Polio &ndash; ambayo ilidhaniwa kutokomezwa nchini DRC miaka mitano iliyopita &ndash; ime&#341;ejea na kuwa tishio tena katika taifa hilo la Af&#341;ika ya kati.\n <\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>Shi&#341;ika la Afya Ulimwenguni lime&#341;ikodi wagonjwa 139 nchini kote, lakini ukusanyaji duni wa takwimu una maana kuwa wagonjwa wengi hawaja&#341;ikodiwa. Wagonjwa pia wame&#341;ikodiwa katika Jamhu&#341;i ya Kongo upande wa kaskazini, na Angola upande wa kusini &ndash; Angola inadhaniwa kuwa chanzo cha kuzuka kwa ugonjwa huo kwa sasa katika Af&#341;ika ya Kati.<\/p>\n<p>Maelfu ya watoaji chanjo wamesambazwa nchini kote katika wilaya 16 za DRC katika kampeni kabambe ya kutoa chanjo, sehemu ya jitihada pana za kufikia watoto milioni 72 katika Af&#341;ika nzima. Pie&#341;&#341;ette Vu Thi, mwakilishi wa DRC wa Shi&#341;ika la Watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF, ametoa wito kwa pande zinazopigana hususan masha&#341;iki mwa nchi hiyo kuacha kupigana ku&#341;uhusu chanjo kuendelea kwa ajili ya watoto wa chini ya um&#341;i wa miaka mitano.<\/p>\n<p>Lakini ugonjwa huo haukuzuka kwa kushtukiza.<\/p>\n<p>Mwanzoni mwa mwaka, Shi&#341;ika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa liliionya kuwa nchini DRC, &#8220;magonjwa kama yale ya kichocho, ukoma na tauni yame&#341;ejea na kwamba idadi ingeongezeka kwa kati asilimia 20 na 22 katika majimbo ya masha&#341;iki ambako bado kuna matatizo na vita kama hatua za ha&#341;aka zisingechukuliwa.&#8221;<\/p>\n<p>Kikwazo cha bajeti <\/p>\n<p>Mwezi Julai, mku&#341;uguenzi wa fedha wa Mpango wa Chanjo wa DRC (EPI) aliiambia IPS kuwa uhaba wa fedha ulikuwa na maana kwmaba chanjo kwa watoto itashindikana.<\/p>\n<p>&#8220;Kati ya zaidi ya dola milioni 130 zinazohitajika kutoa chanjo kwa watoto wote kuanzia um&#341;i wa sifu&#341;i hadi miezi 11 mwaka 2010, se&#341;ikali ya Kongo imesema haitaweza kuchangia zaidi ya asilimia moja,&#8221; alisema. &#8220;[Katika kipindi hiki,] watoto wachanga milioni tisa waliachwa tu kuambukizwa na ma&#341;adhi hayo mabaya kama vile polio ambao unaweza kuwaacha wakiwa walemavu maisha yao yote.&#8221;<\/p>\n<p>Bajeti nzima ya mwaka 2010 kwa DRC, taya&#341;i imepunguzwa kwa kiasi cha chini, na ni kama dola bilioni 5 na asilimia 50 inafadhiliwa na jumuiya ya kimataifa. Nchi inatoa asilimia 5.5 tu ya &#341;asilimali zake kwa ajili ya sekta ya afya kwa ujumla.<\/p>\n<p>&#8220;Katika Jimbo la O&#341;ientale, ambalo ni kubwa zaidi nchini humo, zaidi ya watoto wachanga 700,000 hawajapatiwa chanjo kuanzia mwanzoni mwa mwaka 2009 hadi mwishoni mwa muhula wa kwanza wa mwaka 2010; hii inawafanya kuwa &#341;ahisi kuambukizwa homa ya manjano, kifua kikuu, su&#341;ua, polio na ma&#341;adhi mengineyo, &#8221; alisema Jean Paul Makala, ofisa katika Wiza&#341;a ya Afya ya Umma na ambaye anahusika na takwimu katika EPI.<\/p>\n<p>G&eacute;nie Bulenda, nesi katika kituo binafsi cha afya cha Mt. Rita masha&#341;iki mwa jiji la Bunia, ni mama mwenye mtoto wa um&#341;i wa miaka sita.<\/p>\n<p>&#8220;EPI ilisema kwa miezi sasa haikuweza kuwa na akiba ya kutosha ya madawa na isingeweza kuwa na kiasi hicho kikubwa cha umeme kwa ajili ya majokofu ya kuhifadhia. Binti yangu ambaye alizaliwa Machi 2010 alipatiwa chanjo kwa ma&#341;a ya kwanza alipokuwa na miezi miwili, mwanzoni mwa mwezi Mei.&#8221;<\/p>\n<p>Mtaalam wa magonjwa Claude Muhiga alisema, &#8220;ni miaka tangu nchi iwe na uwezo wa kutoa chanjo kukidhi mahitaji ya watoto wachanga. Madha&#341;a yake yako wazi katika vijiji vingi: Mtu anaweza kuona idadi kubwa ya vijana wenye ulemavu wa kimwili na kiakili kutokana na kutokupatiwa chanjo katika um&#341;i wa utotoni.&#8221;<\/p>\n<p>Muhiga alielezea kuwa sababu kadhaa zinachangia kuwepo kwa pengo katika mpango wa kutoa chanjo nchini.<\/p>\n<p>&#8220;Sababu kuu ambayo inazuia watoto kutopata chanjo ni kukosekana kwa chanjo zenyewe, kukosekana kwa nishati [umeme wa jene&#341;eta na majokofu] ya kuhifadhi dawa za chanjo katika uba&#341;idi,&#8221; alisema. Kwa kuongeza maeneo mengi ya nchi hayafikiki kiu&#341;ahisi kutokana na ba&#341;aba&#341;a mbovu au kutokana na vita, na uhaba wa wafanyakazi wenye ujuzi na vituo vya afya ni kikwazo kingine.<\/p>\n<p>Changamoto inazidishwa na wazazi ambao wanakataa kupeleka watoto wao kupata chanjo kutokana na imani za kidini.<\/p>\n<p>Sophie Mokill, mama wa nyumbani ambaye ana watoto watano, aliiambia IPS. &#8220;Sijui asili au mchanganyiko wa madawa haya ambayo wanakuja kuwapatia watoto wetu na sihitaji chanjo. Unaweza kuwaona wana afya nzu&#341;i tu&#8230;<\/p>\n<p>&#8220;Ni Mungu ambaye anawalinda watoto, na wala siyo chanjo ambazo wanatuletea kutoka Ulaya.&#8221;<\/p>\n<p>Maoni yake hayaungwi mkono na Adeline Mpasi, mkazi katika eneo la pembezoni mwa mji wa Kinshasa la Kitokimosi, ambaye binti yake mwenye um&#341;i wa miaka minne hawezi kutembea, amelemaa kutokana na kuugua polio.<\/p>\n<p>&#8220;Wakati mtoto alipozaliwa, familia yangu iliishi huko Kasongolunda, katika Jimbo la Bandundu, ambako hakukuwa na kampeni ya chanjo kwa watoto. Ilikuwa tumechelewa mno wakati baba yake alipotambua kuwa amelemaa katika eneo la chini la miguu yake. Na madakta&#341;i hawakuweza kufanya chochote.&#8221; <\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>KINSHASA, Des 8 (IPS) &ndash; Wataalam wa afya wanahofia kwamba kukosekana kwa usalama na &#341;asilimali kunaweza kusababisha kulipuka upya kwa magonjwa &#341;ahisi kuzuilika katika Jamhu&#341;i ya Kidemok&#341;asia ya Kongo (DRC). Polio &ndash; ambayo ilidhaniwa kutokomezwa nchini DRC miaka mitano iliyopita &ndash; ime&#341;ejea na kuwa tishio tena katika taifa hilo la Af&#341;ika ya kati. Shi&#341;ika la&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":580,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-3524","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3524","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/580"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=3524"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3524\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=3524"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=3524"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=3524"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}