{"id":3497,"date":"2010-12-06T13:40:01","date_gmt":"2010-12-06T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2010\/12\/06\/mabadiliko-ya-tabia-nchi-kugeuza-kilimo-kuwa-ufumbuzi-wa-tatizo\/"},"modified":"2010-12-06T13:40:01","modified_gmt":"2010-12-06T13:40:01","slug":"mabadiliko-ya-tabia-nchi-kugeuza-kilimo-kuwa-ufumbuzi-wa-tatizo","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2010\/12\/06\/mabadiliko-ya-tabia-nchi-kugeuza-kilimo-kuwa-ufumbuzi-wa-tatizo\/","title":{"rendered":"MABADILIKO YA TABIA NCHI: Kugeuza Kilimo Kuwa Ufumbuzi wa Tatizo"},"content":{"rendered":"<p>CANC&Uacute;N, Mexico, Des 5 (IPS) &ndash; Kimataifa kilimo kinachangia uzalishaji wa hewa chafu ambazo zinasababisha mabadiliko ya hali ya hewa kwa asilimia 17, lakini kulingana na Benki ya Dunia, kilimo kinachozingatia mbinu zisizochafua hali ya hewa kinaweza kupunguza kiasi hicho cha uchafuzi na kukabiliana na changamoto za kuzalisha chakula cha kutosha kwa ajili ya idadi ya watu inayozidi kuongezeka duniani.\n<\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>&#8220;Kutokana na kilimo kuwa sehemu ya tatizo, pia ni sehemu ya ufumbuzi,&#8221; alisema Inge&#341; Ande&#341;son, makamu wa &#341;ais wa Benki ya Dunia anayeshughulika na maendeleo endelevu.<\/p>\n<p>Ande&#341;son alikuwa akizungumza na watalaam wa kilimo, usalama wa chakula na mabadiliko ya tabia nchi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kilimo na Maendeleo ya Vijijini, tukio la pembezoni mwa Mkutano wa Mabadiliko ya Tabia Nchi mjini Canc&uacute;n, Mexico Des. 4.<\/p>\n<p>Ushindi wa aina tatu <\/p>\n<p>Wataalam wa kilimo wanaweka mazingi&#341;a ambapo kilimo kinatoa &#8220;ushindi wa aina tatu&#8221;, kukusanya kaboni katika udongo, kustahimili kwa kiasi kikubwa ukame na joto kali, na kubo&#341;esha usalama wa chakula na kipato kwa wakulima.<\/p>\n<p>Ili kufikia muujiza huu itahitaji aina mbalimbali ya hatua katika maeneo tofauti, lakini taya&#341;i kuna mifano inaweza kuonekana.<\/p>\n<p>Katika eneo la milima ya Loess nchini China, maelfu ya miaka ya kilimo na ufugaji wanyama yaligeuza misitu kuwa eneo kame. Upotevu wa miti uliacha udongo wa njano kuwa &#341;ahisi kuathii&#341;ka na mmomonyoko; mmomonyoko uliingia katika mito na kujaza mchanga na kusababisha mafu&#341;iko mabaya ya kila mwaka.<\/p>\n<p>Miaka kumi na sita iliyopita, se&#341;ikali ya China na Benki ya Dunia walianza kubadili matumizi ya a&#341;dhi hiyo katika eneo hilo. M&#341;adi huo ulikusanya wakazi wa eneo hilo kujenga mabwawa ya kujaza mchanga unaotokana na mmomonyoko na makinga maji na kupanda miti ya matunda na majani katika maeneo ya milimani badala ya mazao mengine. Wakazi walilipwa kutokana na kazi yao ya kuendeleza mi&#341;adi, lakini suala muhimu zaidi lilikuwa kupatiwa vibali vya kumiliki a&#341;dhi kwa muda m&#341;efu ambayo ina&#341;ejesha hali yake ya kawaida kwa viumbe hai na kilimo.<\/p>\n<p>Katika eneo dogo la milima la Humbo nchini Ethiopia, wakulima wadogo wamefanikiwa kupanda miti na ku&#341;ejesha uzalishaji. Wakulima wa eneo hilo walitumia kanuni mpya za matumizi endelevu ya misitu &ndash; kwa kusaidiwa na majiko yanayotumia nishati ndogo ili kupunguza mahitaji ya kuni na mkaa. Pamoja na kuwezesha kukua kwa misitu iliyoha&#341;ibiwa vibaya hapo kabla, mafunzo yamewezesha wenyeji wa maeneo hayo kuanza pia kufuga mifugo na kuku ikiwa ni pamoja na shughuli zisizohusiana na kilimo.<\/p>\n<p>M&#341;adi wa Humbo ni moja ya mi&#341;adi michache ya Maendeleo Yasiyochafua Mazingi&#341;a, na kupata hundi yake ya kwanza ya dola 34,000 kutokana na kuhifadhi kaboni katika eneo la msitu wa eka&#341;i 2,700 Oktoba 2010.<\/p>\n<p>Wakulima nchini Malawi, Kenya, Bu&#341;kina Faso, Nige&#341; na Zambia pia wanashi&#341;iki katika upandaji wa miti, kuchanganya miti na mazao ya chakula na mifumo ya ugugaji mifugo.<\/p>\n<p>&#8220;Kwa kutumia njia hizi, hali ya kijani katika a&#341;dhi inakuwa endelevu kwa mwaka mzima,&#8221; alisema Ande&#341;son. &#8220;Mifumo hii inaongeza &#341;utuba ya udongo kupitia nit&#341;ojeni na kuhifadhi maji, na kuongeza uzalishaji wa moja kwa moja wa chakula, malisho ya mifugo, nishati, na mazao ya kujiongezea kipato katika upandaji huu wa miti.&#8221;<\/p>\n<p>Wakulima nchini Malawi, wameongeza mavuno ya mahindi zaidi ya ma&#341;a mbili wakati wa kupanda mazao yao chini ya miti. Dk Lindiwe Majele Sibanda, ofisa mtendaji mkuu wa shi&#341;ika la Food Ag&#341;icultu&#341;e and Natu&#341;al Resou&#341;ces Policy Analysis Netwo&#341;k, alisema nchi za Af&#341;ika zinahitaji kufanya kazi ya mikakati ambayo itazingatia vipato vya watu wa vijijini.<\/p>\n<p>Matumizi ya kilimo cha Af&#341;ika <\/p>\n<p>&#8220;Changamoto ni kwamba ba&#341;ani Af&#341;ika, tumefiki&#341;ia tu juu ya sayansi na teknolojia kama njia ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi,&#8221; alisema Sibanda.<\/p>\n<p>&#8220;Tulianza kuzungumzia kuhusu jinsi ya kuishi na mabadiliko katika ba&#341;a la Af&#341;ika kabla ya kufanya utafiti juu ya fu&#341;a ambazo zinakuja na vipato vya jamii.&#8221;<\/p>\n<p>Diana Live&#341;man, mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha A&#341;izona, alisema wakulima wadogo kwa muda m&#341;efu wameegemea zaidi katika maa&#341;ifa ya jadi kuishi katika mazingi&#341;a yao ya mabadiliko, lakini kuzidi kuenea kwa mabadiliko ya tabia nchi kunaweza kuzidi uwezo wao.<\/p>\n<p>&#8220;Matumizi ya maa&#341;ifa ya jadi wakati huu, wakati hali ya hewa imebadilika kwa kiasi kikubwa, kunaweza kuwa changamoto kwasababu kunaweza kushindwa kukabiliana na ukweli wa mambo wa hali ya sasa,&#8221; alisema Live&#341;man.<\/p>\n<p>Badala yake, alisema, sayansi ya kisasa inatakiwa kuendeleza maa&#341;ifa ya jadi kusaidia wakulima kuishi katika mabadiliko. Lakini alisisitiza kuwa wakulima wanatakiwa kuwa katikati mwa uamuzi wa kuchukua hatua.<\/p>\n<p>&#8220;Watafiti wanapaswa kuondokana na kuwachagulia wakulima wa Af&#341;ika,&#8221; alisema Live&#341;man. &#8220;Baadhi wangependa teknolojia ya kisasa wakati wengine wangependelea kuendelea na maa&#341;ifa ya jadi. Kinachotakiwa kujitokeza ni kuwepo na mfuko wa kusaidia kuishi na mabadiliko kwa ajili ya wote.&#8221;<\/p>\n<p>Wanasayansi, watafiti na watunga se&#341;a wanapaswa kuongeza kasi yao katika kutafuta hatua za kuishi na mabadiliko, alisema Sibanda, kwasababu kama hatua haitachukuliwa sasa, madha&#341;a ya mabadiliko ya tabia nchi yataangamiza jitihada za muda m&#341;efu za Af&#341;ika Kusini mwa Jangwa la Saha&#341;a katika sekta ya kilimo.<\/p>\n<p>&#8220;Hii inaweza kuondoa matumaini ambayo yamejengwa katika kufikia &#8220;Mapinduzi ya Kijani na Upinde wa Mvua&#8221; ya kipekee katika ba&#341;a la Af&#341;ika,&#8221; alisema Sibanda.<\/p>\n<p>Ba&#341;a linashinikiza mpango kabambe wa Maendeleo ya Kilimo Af&#341;ika (CAADP) ambao unalenga katika maeneo makuu manne: a&#341;dhi na usimamiaji wa maji, upatikanaji wa masoko, usambazaji wa chakula na kukabiliana na njaa na utafiti wa kilimo.<\/p>\n<p>Dk Josu&eacute; Dion&eacute;, mku&#341;ugenzi wa usalama wa chakula wa kitengo cha maendeleo endelevu katika Tume ya Umoja wa Mataifa ya Uchumi Af&#341;ika, alibainisha kuwa CAADP itaima&#341;isha sekta ya kilimo ba&#341;ani Af&#341;ika na kubo&#341;esha usalama wa chakula, lakini alionya kuwa nchi zinapaswa kuja na mipango ya kujikinga na mabadiliko ya tabia nchi ili kufanikiwa.<\/p>\n<p>&#8220;Mabadiliko ya tabia nchi ba&#341;ani Af&#341;ika ni changamoto na fu&#341;sa,&#8221; alisema Dion&eacute;. &#8220;Kwa kutumia mbinu bo&#341;a kukabiliana na madha&#341;a ya mabadiliko ya tabia nchi, tungeweza kuondokana na uagizaji wa chakula kwa watu wetu.&#8221;<\/p>\n<p>*Te&#341;na Gyuse mjini Cape Town alichangia katika &#341;ipoti hii. <\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>CANC&Uacute;N, Mexico, Des 5 (IPS) &ndash; Kimataifa kilimo kinachangia uzalishaji wa hewa chafu ambazo zinasababisha mabadiliko ya hali ya hewa kwa asilimia 17, lakini kulingana na Benki ya Dunia, kilimo kinachozingatia mbinu zisizochafua hali ya hewa kinaweza kupunguza kiasi hicho cha uchafuzi na kukabiliana na changamoto za kuzalisha chakula cha kutosha kwa ajili ya idadi&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":819,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-3497","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3497","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/819"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=3497"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3497\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=3497"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=3497"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=3497"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}