{"id":3473,"date":"2010-11-19T13:40:01","date_gmt":"2010-11-19T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2010\/11\/19\/kongo-polio-yaua-100\/"},"modified":"2010-11-19T13:40:01","modified_gmt":"2010-11-19T13:40:01","slug":"kongo-polio-yaua-100","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2010\/11\/19\/kongo-polio-yaua-100\/","title":{"rendered":"KONGO: Polio Yaua 100"},"content":{"rendered":"<p>BRAZZAVILLE, Nov 12 (IPS) &ndash; Kampeni ya dha&#341;ula dhidi ya polio inaanza Nov. 12 katika Jamhu&#341;i ya Kongo, ambapo gonjwa hilo lililojikita katika jiji la kusini la Pointe&ndash;Noi&#341;e limeshaua kwa uchache watu 100 tangu mwanzoni mwa Oktoba.\n<\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>Kulingana na mamlaka ya afya ya Kongo, gonwa hilo limeshaua watu 97 huko Pointe&ndash;Noi&#341;e, mji wa kiuchumi wa nchi hiyo, watu wawili huko Dolisie na mmoja huko Nkayi, kusini magha&#341;ibi.<\/p>\n<p>Shi&#341;ika la Afya Ulimwenguni lilitoa &#341;ipoti Nov. 9 kuwa kumekuwepo na wagonjwa 184 wa kupooza na vifo 85, likisema kuwa wengi wa wagonjwa wanatoka kundi la watu wenye um&#341;i kati ya miaka 15 na kuendelea. Kwa kawaida polio huathi&#341;i watoto wa chini ya um&#341;i wa miaka mitano.<\/p>\n<p>&#8220;Hiki ni kiwango cha juu mno cha vifo, hasa kutokana na idadi ya wagonjwa na vifo. Ni janga halisi la kitaifa,&#8221; alisema Dk Jean Vivien Moumbouli, mku&#341;ugezi wa utafiti katika Maaba&#341;a za Kitaifa zilizopo B&#341;azzaville.<\/p>\n<p>Kulingana na Kituo cha Kudhibiti Magonjwa, ambacho kina makao yake huko Atlanta Ma&#341;ekani, ambako sampuli zilipelekwa kwa ajili ya kuchunguzwa, gonjwa hilo linatokana na vi&#341;usi vya polio namba 1.<\/p>\n<p>Pointe&ndash;Noi&#341;e, eneo ambako gonjwa hilo limeathi&#341;i zaidi, wakazi wameshtushwa. Se&#341;ikali haijasema kitu kuhusu maladhi hayo. &#8220;Hata hatujui nini kimetokea, tunabuni tu,&#8221; alisema Jean Bakala, mkazi wa jumuiya ya Loandjili, ambayo ili&#341;ipoti idadi kubwa ya waathi&#341;ika.<\/p>\n<p>&#8220;Baba yangu wa um&#341;i wa miaka 45 alipatwa na polio. Lakini madaktati hawakutaka kumka&#341;ibia wakihofia kuambukizwa. Hiyo ilinishtua,&#8221; He&#341;mane Bouity aliiambia IPS. Baba yake ambaye alifa&#341;iki siku kadhaa baadaye, alilazwa katika Hospitali ya Adolphe Ciss&eacute; mjini Pointe&ndash;Noi&#341;e.<\/p>\n<p>Wagonjwa wote katika mji huo wa mwambao wamepelekwa kwenye hospitali mbili kubwa katika Loandjili and Ciss&eacute;. &#8220;Sisi tumezidiwa. Sote tunaogopa,&#8221; alisema nesi wa hospitali ya Loandjili.<\/p>\n<p>Se&#341;ikali imekosolewa.<\/p>\n<p>&#8220;Hatujui ni tahadha&#341;i gani tunatakiwa kuchukua kwasababu hatujui ugonjwa huo. Wakazi wametelekezwa,&#8221; alisema B&#341;ice Mackosso, katibu mkuu waTume ya Haki na Amani, NGO iliyopo ka&#341;ibu na Kanisa la Katoliki la Pointe&ndash;Noi&#341;e.<\/p>\n<p>&#8220;Se&#341;ikali inawajibika kikamilifu kueneza ugonjwa huu, kwasababu imeshindwa kuwasiliana. Katika televisheni na &#341;edio, huoni kitu, wala husikii kitu,&#8221; alisema Roch Euloge N&#8217;zobo, kutoka NGO ya Kufuatilia Haki za Binadamu Kongo, yenye makazi yake mjini B&#341;azzaville. &#8220;Hatua za mamlaka hazijawa na ufanisi kabisa.&#8221;<\/p>\n<p>Wiki tatu baada ya wagonjwa wa kwanza kupatikana, se&#341;ikali ilikuwa bado inaja&#341;ibu kubainisha asili halisi ya gonjwa hilo. Ni katika mwanzo tu wa Novemba walianza kutoa matangazo kwa kusita juu ya tishio hilo.<\/p>\n<p>&#8220;Ni vi&#341;usi ambavyo vinashambulia mfumo wa fahamu, na kufanya mwili kupooza na kuleta mauti,&#8221; Dk Alexis Eli&#341;a Dokekias, mku&#341;ugenzi mkuu wa afya, aliviambia vyombo vya haba&#341;i. &#8220;Ni vema kuzingatia kanuni za afya ya msingi. Vi&#341;usi vinapatikana katika kinyesi na kuingia mwilini kwa njia ya mdomo. Kama hakuna ufuatiliaji mzu&#341;i wa masuala ya afya, vinaweza kujipenyeza mwilini kupitia maji mji, vinaweza kuingia mdomoni kupitia mboga mboga zisizosafishwa vizu&#341;i au matunda.&#8221;<\/p>\n<p>Kampeni ya chanjo ambayo ilianza Nov. 12 italenga kwanza wakazi wa Pointe&ndash;Noi&#341;e, halafu wakazi wengine nchini. Dozi milioni kumi na mbili za chanjo zitahitajika, kulingana na Eli&#341;a Dokekias.<\/p>\n<p>&#8220;Chanjo zimechelewa mno kufika. Wale ambao wameathi&#341;ika hawawezi tena kuokolewa, kwani unahitaji kuchuka hatua angalau wiki tatu za mwanzo, alisema Anatole Bikou, afisa tabibu wa Pointe&ndash;Noi&#341;e.<\/p>\n<p>Shi&#341;ika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF, limetangaza kutoa msaada wa dozi milioni tano zinazotoka kwenye hifadhi yake ya Denma&#341;k. UNICEF inahitaji dola zipatazo milioni 3 kununua dozi nyingine.<\/p>\n<p>Dk Edoua&#341;d Ndinga, afisa mkuu wa Mpango Kabambe wa Chanjo nchini, alikataa kusema ni dozi ngapi taya&#341;i zipo nchini Kongo.<\/p>\n<p>&#8220;Hatuna kitu. Tunasubi&#341;i jumuia ya kimataifa kuja kutupatia msaada,&#8221; alisema N&#8217;zobo.<\/p>\n<p>Takwimu kutoka EPI kwa mwaka 2009 zilionyesha kuwa wastani wa kiwango cha polio nchini Kongo kilikuwa asilimia 90. Maambukizi ya mwisho ya polio nchini humo yalikuwa mwaka 2000. Mamlaka yana wasiwasi vi&#341;usi hivyo viliingia kutoka &#8220;nchi ji&#341;ani&#8221;.<\/p>\n<p>Kulingana na Shi&#341;ika la Afya Ulimwenguni, Angola ili&#341;ipoti wagonjwa wa polio 25 mwaka 2010, na 28 wali&#341;ipotiwa katika Jamhu&#341;i ya Kidemok&#341;asia ya Kongo. Miongoni mwa wagonjwa huko Pointe&ndash;Noi&#341;e, wanne walitoka Cabinda, jimbo la Angola ka&#341;ibu na Kongo. &#8220;Tumelegeza uchunguzi wetu wa afya mipakani,&#8221; alisema Eli&#341;a Dokekias.<\/p>\n<p>Kufumuka kwa gonjwa hilo kunakuja pamoja na mafanikio ya hivi ka&#341;ibuni ya kudhibiti polio. Kulingana na WHO, idadi ya wagonjwa kimataifa mwaka huu ni 767, nusu ya idadi kama hiyo mwaka 2009. Hii inatokana na kupungua kwa kiasi kikubwa kwa ugonjwa huo nchini Nige&#341;ia na India.<\/p>\n<p>Kudhibiti gonjwa nchini Kongo kwa kutumia kampeni ya chanjo ambayo itafika nchi ji&#341;ani za DRC na Angola ni kipaumbele cha kwanza. <\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>BRAZZAVILLE, Nov 12 (IPS) &ndash; Kampeni ya dha&#341;ula dhidi ya polio inaanza Nov. 12 katika Jamhu&#341;i ya Kongo, ambapo gonjwa hilo lililojikita katika jiji la kusini la Pointe&ndash;Noi&#341;e limeshaua kwa uchache watu 100 tangu mwanzoni mwa Oktoba. Kulingana na mamlaka ya afya ya Kongo, gonwa hilo limeshaua watu 97 huko Pointe&ndash;Noi&#341;e, mji wa kiuchumi wa&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":797,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-3473","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3473","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/797"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=3473"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3473\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=3473"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=3473"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=3473"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}