{"id":3459,"date":"2010-10-26T13:40:01","date_gmt":"2010-10-26T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2010\/10\/26\/seikali-za-afika-zatakiwa-kuwekeza-kwenye-hifadhi-ya-jamii\/"},"modified":"2010-10-26T13:40:01","modified_gmt":"2010-10-26T13:40:01","slug":"seikali-za-afika-zatakiwa-kuwekeza-kwenye-hifadhi-ya-jamii","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2010\/10\/26\/seikali-za-afika-zatakiwa-kuwekeza-kwenye-hifadhi-ya-jamii\/","title":{"rendered":"Se&#341;ikali za Af&#341;ika Zatakiwa Kuwekeza Kwenye Hifadhi ya Jamii"},"content":{"rendered":"<p>WINDHOEK, Okt 23 (IPS) &ndash; Kutenga asilimia moja tu ya GDP katika hifadhi ya jamii kunaweza kuleta mabadiliko makubwa katika maisha ya watoto maskini katika ba&#341;a la Af&#341;ika.\n<\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>Kulingana na Jonathan B&#341;adshaw, p&#341;ofesa wa se&#341;a za hifadhi ya jamii katika Chuo Kikuu cha Yo&#341;k nchini Uinge&#341;eza, mataifa ya Af&#341;ika yanapaswa kuwekeza katika mifumo ya hifadhi ya jamii. Anasema kuwa hifadhi ya jamii ina faida ya muda m&#341;efu kwa watoto, ambao ma&#341;a nyingi wananyimwa fu&#341;sa za kufanikiwa wakiwa watu wazima.<\/p>\n<p>&#8220;Mataifa yote ba&#341;ani Ulaya yana mifumo ya hifadhi ya jamii kwa watoto,&#8221; B&#341;adshaw aliiambia IPS katika wa&#341;sha ya kikanda ya wabunge iliyofanyika nchini Namibia kuanzia Oktoba 20&ndash;22.<\/p>\n<p>&#8220;Wastani wa matumizi kama sehemu ya GDP katika faida za fedha kwa kutunza watoto ni asilimia 2.3. Kama nchi za Af&#341;ika zinatumia asilimia moja ya GDP katika mafao ya watoto, italeta mabadiliko makubwa katika kutokomeza umaskini. Lakini hakuna nchi inayofanya hivyo.&#8221;<\/p>\n<p>B&#341;adshaw amefanya utafiti mpana juu ya mafao kwa watoto Masha&#341;iki na Kusini mwa Af&#341;ika. Matokeo ya utafiti wake ni kwamba ka&#341;ibu mafao yote ya fedha yanayoelekezwa kwa watoto yanatumiwa na wazazi katika elimu na afya. Alitoa mfano wa Af&#341;ika Kusini ambako mafao ya jamii yamesababisha ushi&#341;iki mkubwa wa watoto kwenda shule, na kuima&#341;isha afya ya mama.<\/p>\n<p>Utafiti mwingine wa taasisi za academia na maendeleo katika Af&#341;ika zinathibitisha kuwa hifadhi ya jamii katika aina zake mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kupatia maskini fedha, mafao kwa watoto na wazee, bima ya afya ya taifa, vocha za pembejeo na kusamehe ada ya afya na elimu, inaleta tofauti kubwa chanya kwa maisha ya maskini na watu wanaoishi katika mazingi&#341;a magumu.<\/p>\n<p>Hata hivyo, kuweka kipaumbele na kutekeleza mifumo ya ulinzi wa jamii linabakia kuwa suala la pili ikilinganishwa na vipaumbele vingine vya bajeti ya taifa.<\/p>\n<p>&#8220;Ni suala la uwezo kwani se&#341;ikali inatakiwa kuchagua na nafasi ya kifedha ni ndogo. Lakini hatuombi mipango ya gha&#341;ama ya juu &ndash; inayoelekezwa vema ambayo ingegha&#341;imu asilimia moja ya GDP kufanya kazi,&#8221; B&#341;adshaw alisema.<\/p>\n<p>&#8220;Benki ya Dunia imekuwa ikisema kuwa uwekezaji wowote ule katika huduma za umma una uwezekano wa kudhoofisha ukuaji wa kiuchumi lakini tunatambua kuwa ukuaji huo haujawafikia wananchi wa kawaida. Sasa mashi&#341;ika ya kimataifa yanasema kuwa hatua ya baadaye muhimu zaidi katika maendeleo ni kuanzisha hifadhi ya jamii na hasa hifadhi ya jamii kwa watoto.&#8221;<\/p>\n<p>Namibia, ni nchi mojawapo ambayo imekuwa kiongozi katika kukuza hifadhi ya jamii tangu ilipoanza mpango wake wa kupatia watu fedha mwaka 2004. Zaidi ya watoto 100,000 kwa sasa wanafaidika na mafao ya ustawi wa jamii ambayo yamesaidia kupunguza umaskini katika kaya zinazoathi&#341;ika na VVU na UKIMWI.<\/p>\n<p>Mifumo ya hifadhi ya jamii kama huu, watafiti wanasema, inapaswa kupanuliwa katika ba&#341;a zima kwa kupata msaada wa kifedha kutoka se&#341;ikalini ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa se&#341;a &#341;afiki kwa watoto. Hata hivyo, vipaumbele vya bajeti Af&#341;ika viko mahali pengine.<\/p>\n<p>Kwa mfano, takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuwa Af&#341;ika hutumia ka&#341;ibu dola bilioni 4 katika jeshi kila mwaka. Matumizi ya jeshi mwaka 2009 yaliongezeka kwa asilimia 10.2 katika mwaka uliopita, kulingana na uchambuzi wa Taasisi ya Utafiti wa Amani ya Kimataifa ya Stockholm.<\/p>\n<p>Umoja wa Af&#341;ika unakadi&#341;ia kuwa &#341;ushwa inagha&#341;imu uchumi wa Af&#341;ika zaidi ya dola bilioni 148 kwa mwaka, ambazo ni sawa na &#341;obo ya pato la Af&#341;ika. Hatua zinazofaa kupambana na &#341;ushwa zikichukuliwa zinaweza kuleta &#341;asilimali kwa ajili ya hifadhi ya jamii.<\/p>\n<p>Kamishna wa Masuala ya Kijamii wa Umoja wa Af&#341;ika, Bience Gawanas, aliiambia IPS kuwa hifadhi ya jamii inahakikisha haki za binadamu, akisema kuwa kama mataifa ya Af&#341;ika yana se&#341;a za uchumi mkuu, yanapaswa pia kuwa na se&#341;a za hifadhi ya jamii. Alisema tume yake inaendesha ushawishi ili mataifa ya Af&#341;ika yawe na se&#341;a za kupambana na umaskini na hifadhi ya jamii ni moja ya ufumbuzi.<\/p>\n<p>&#8220;Wakati watu wanapofa&#341;iki na VVU na UKIMWI, au kufa&#341;iki kutokana na mala&#341;ia: inagha&#341;imu kiasi gani se&#341;ikali zetu &#8221; Gawana aliuliza. &#8220;Kama tunakakatua gha&#341;ama za kifo, ni hakika dola hiyo ya nyongeza wanayompatia mtu aweze kuishi ina maana kubwa mno. Hii inahusiana na vipaumbele tu. Lakini siyo hali ambayo inakatisha tamaa, kama nchi moja inaweza kuonyesha njia ni hakika nyingine zitafuata.&#8221;<\/p>\n<p>Af&#341;ika Kusini ina mafao yanayotolewa kwa watoto; Kenya inatoa fedha kwa yatima na watoto katika mazingi&#341;a magmu; Lesotho imeanzisha mafao kwa wazee. Nchini Malawi se&#341;ikali kwa kushi&#341;ikiana na Shi&#341;ika la Chakula Ulimwenguni imeanzisha mpango wa kutoa chakula mashuleni na nchini Msumbiji kuna mpango wa vocha za chakula na nchini Zambia, mpango wa maja&#341;ibio wa kutoa fedha kwa wazee wanaotunza yatima umebo&#341;esha hali ya watoto kupenda kwenda shule. <\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>WINDHOEK, Okt 23 (IPS) &ndash; Kutenga asilimia moja tu ya GDP katika hifadhi ya jamii kunaweza kuleta mabadiliko makubwa katika maisha ya watoto maskini katika ba&#341;a la Af&#341;ika. Kulingana na Jonathan B&#341;adshaw, p&#341;ofesa wa se&#341;a za hifadhi ya jamii katika Chuo Kikuu cha Yo&#341;k nchini Uinge&#341;eza, mataifa ya Af&#341;ika yanapaswa kuwekeza katika mifumo ya hifadhi&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":540,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-3459","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3459","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/540"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=3459"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3459\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=3459"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=3459"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=3459"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}