{"id":3427,"date":"2010-09-29T13:40:01","date_gmt":"2010-09-29T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2010\/09\/29\/kenya-walimu-wa-shule-za-msingi-wapata-matokeo-mabaya-kwenye-hisabati\/"},"modified":"2010-09-29T13:40:01","modified_gmt":"2010-09-29T13:40:01","slug":"kenya-walimu-wa-shule-za-msingi-wapata-matokeo-mabaya-kwenye-hisabati","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2010\/09\/29\/kenya-walimu-wa-shule-za-msingi-wapata-matokeo-mabaya-kwenye-hisabati\/","title":{"rendered":"KENYA: Walimu Wa Shule za Msingi Wapata Matokeo Mabaya Kwenye Hisabati"},"content":{"rendered":"<p>NAIROBI, Sep 14, 2010 (IPS) &ndash; Kama ilivyo kwa walimu wengi wa shule zote za msingi nchini Kenya, Nemwel Mokua amechanganyikiwa. Anatakiwa kufundisha kwa uchche masomo sita kwa siku, ambayo ni pamoja na mchanganyiko wa masomo ya sanaa na sayansi.\n <\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>Ana muda mchache wa kuendeleza uelewa wake wa masomo magumu ya hisabati na sayansi. Na matokeo yake, wanafunzi wake wanapata alama za chini katika masomo hayo. <\/p>\n<p>Na mwalimu wa Shule ya Misngi Le Pic huko Ri&#341;uta, Nai&#341;obi, anaishi kwa hofu ya kukaguliwa kwa shule yake na wakaguzi, ambao ma&#341;a nyingi wanamkaba koo yeye na wafanyakazi wenzake kuhusu matokeo mabaya ya shule yake katika masomo ya hisabati na sayansi. Mwaka 2008, wanafunzi wa shule anayofundisha Mokua walipata wastani wa da&#341;aja D+ katika mitihani yao. Hata hivyo, kulingana na matokeo ya Cheti ya Elimu ya Msingi Kenya 2008 huu pia ni wastani wa wanafunzi wengine katika nchi nzima. <\/p>\n<p>Kama ilivyo kwa walimu wengi wa shule za msingi nchini Kenya, Mokua anahusisha matokeo hayo mabaya ya wanafunzi wake na muda mdogo anaopata kuwekeza katika hisabati na masomo ya sayansi. <\/p>\n<p>&#8220;Pamoja na kwamba wanafunzi wangu wamebo&#341;eka zaidi katika hisabati katika miaka miwili iliyopita, lazima nikubali kuwa mfumo wa elimu nchini Kenya unaweka kazi kubwa kwa walimu. Hana muda wa kuwekezaji katika masomo ya kiufundi,&#8221; alisema Mokua. <\/p>\n<p>Lakini wiza&#341;a ya elimu inasisitiza kuwa walimu wa shule ya msingi ni lazima kufundisha kwa uchache masomo sita kwa siku. Lakini wataalam wa elimu wanasema hii inapingana na ubo&#341;a wa elimu katika shule za msingi Kenya. Na utafiti uliotolewa Agosti 25 unaunga mkono maoni ya wataalam. <\/p>\n<p>Utafiti wa &#8220;Class&#341;oom Obse&#341;vation&#8221; mjini Nai&#341;obi uliotolewa na Kituo cha Utafiti wa Wakazi wa Af&#341;ika, unaonyesha kuwa walimu wa hisabati katika shule za msingi nchini Kenya wana uelewa mdogo wa somo hilo. Na watafiti wamehoji ubo&#341;a wa mfumo wa elimu ya msingi nchini humo. <\/p>\n<p>Matokeo ya &#341;ipoti hiyo yalishtua Wakenya baada ya walimu kupata wastani wa asilimia 60.5 katika matokeo ya maja&#341;ibio ya hisabati. <\/p>\n<p>Watafiti walisema wangeta&#341;ajia walimu walioshi&#341;iki katika utafiti kupata zaidi ya asilimia 90 katika somo hilo, lakini ni kiasi cha asilimia 13 tu kiliweza kutofautisha ufaulu wa walimu na wanafunzi. <\/p>\n<p>Katika tukio moja, mwalimu mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka mitano alipata asilimia 17 katika maja&#341;ibio. Mtafiti mwandamizi wa APHRC, Dk. Moses Oketch, alielezea matokeo hayo kama &#8216;ya aibu&#8217;. <\/p>\n<p>&#8220;Matokeo yalitushtua mno,&#8221; alisema Oketch. &#8220;Tulita&#341;ajia walimu kupata maksi zaidi ya asilimia 90, lakini matokeo yao yanaka&#341;ibiana kufanana na ya wanafunzi, ambao wastani wao ni asilimia 46.89. Kuna jambo ambalo linahitaji kufanyika hapa.&#8221; <\/p>\n<p>Kulingana na watafiti, matokeo mabaya pia yanaweza kuelezea ni kwa nini wanafunzi wanafanya vibaya katika somo hilo. <\/p>\n<p>Lakini Pete&#341; Githinji, mwalimu wa hisabati katika Shule ya Msingi ya Gikandu katikati mwa Kenya alisema walimu wanatakiwa wasilaumiwe kwani se&#341;ikali imeshindwa kuwapatia vifaa vya kufundishia ambavyo vingeweza ku&#341;ahisisha masomo ya hisabati na sayansi. <\/p>\n<p>&#8220;Kuna mtizamo uliojengeka nchi nzima kuwa hisabati na sayansi ni masomo magumu,&#8221; alisema Githinji. &#8220;Nadhani se&#341;ikali haijafanya kazi ya kutosha kuhamasisha Wakenya kukubali masomo hayo.&#8221; <\/p>\n<p>Lakini &#341;ipoti imesababisha mjadala unaoendelea, huku vyama vya walimu vikilaumu se&#341;ikali kutokana na kushindwa kufundisha walimu wa kutosha waliobobea katika masomo ya hisabati na sayansi. <\/p>\n<p>Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu wa Msingi Nje&#341;u Kanyamba alisema wakati Kenya ilipozindua mpango wa elimu ya msingi kwa wote mwaka 2003, pia iliufanya bila ya kuwa na mpango sahihi wa &#341;asilimali. <\/p>\n<p>Wakati elimu ya msingi kwa wote ilipoanzishwa mwaka 2003, zaidi ya wanafunzi wapya milioni 1.3 waliandikishwa katika wiki ya kwanza. Na bado walimu walibakia kuwa wachache, Kanyamba alisema. <\/p>\n<p>&#8220;Walimu wa shule ya msingi wamezidiwa na wanafunzi waliojiandikisha katika da&#341;asa moja kutokana na uhaba wa wafanyakazi,&#8221; alisema Kanyamba. &#8220;Kutokana na wajibu mkubwa waliokuwa nao, hawawezi kupata fu&#341;sa za kuendelea na masomo yao.&#8221; <\/p>\n<p>Anakubaliana kuwa matokeo ya &#341;ipoti hiyo yataathi&#341;i maendeleo ya sayansi na teknolojia ya baadaye. <\/p>\n<p>Katibu Mkuu wa wiza&#341;a ya elimu, P&#341;ofesa James Ole Kiyiapi, alitetea mpango wa elimu kwa wote akiongeza kuwa mfumo wa elimu ya juu nchini Kenya umejikita katika mfumo wa ongezeko la thamani ambapo wanafunzi wameweza kuonyesha mafanikio katika sayansi na teknolojia katika ngazi hii. <\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>NAIROBI, Sep 14, 2010 (IPS) &ndash; Kama ilivyo kwa walimu wengi wa shule zote za msingi nchini Kenya, Nemwel Mokua amechanganyikiwa. Anatakiwa kufundisha kwa uchche masomo sita kwa siku, ambayo ni pamoja na mchanganyiko wa masomo ya sanaa na sayansi. Ana muda mchache wa kuendeleza uelewa wake wa masomo magumu ya hisabati na sayansi. Na&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":800,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-3427","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3427","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/800"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=3427"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3427\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=3427"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=3427"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=3427"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}