{"id":3302,"date":"2010-06-02T13:40:01","date_gmt":"2010-06-02T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2010\/06\/02\/kenya-mpango-wa-bayoanuwai-wa-umoja-wa-mataifa-unahitaji-sauti-za-wanawake\/"},"modified":"2010-06-02T13:40:01","modified_gmt":"2010-06-02T13:40:01","slug":"kenya-mpango-wa-bayoanuwai-wa-umoja-wa-mataifa-unahitaji-sauti-za-wanawake","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2010\/06\/02\/kenya-mpango-wa-bayoanuwai-wa-umoja-wa-mataifa-unahitaji-sauti-za-wanawake\/","title":{"rendered":"KENYA: Mpango wa Bayoanuwai wa Umoja wa Mataifa Unahitaji Sauti za Wanawake"},"content":{"rendered":"<p>NAIROBI, Mei 27 (IPS) &ndash; Wanawake wanachangia asilimia 90 ya uzalishaji wa chakula katika maeneo maskini vijijini na hadi asilimia 80 ya chakula katika nchi nyingi zinazoendelea, na hata hivyo wanapuuzwa moja kwa moja wakati maamuzi ya kise&#341;a yanapotolewa kuhusu kilimo na bayoanuwai.\n<\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>Hii inaka&#341;ibia kubadilika na pongezi zinapaswa kwenda kwa mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Bayoanuwai ambao utataka nchi kuhakikisha kuwa wanawake wanashi&#341;iki katika maamuzi kuhusu bayoanuwai &ndash; ikiwa ni pamoja na kilimo.<\/p>\n<p>&#8220;Hii ni kubadili mchezo na itakuwa mfano kwa mikataba ya Umoja wa Mataifa kama ile ya mabadiliko ya tabia nchi (Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi),&#8221; alisema Lo&#341;ena Aguila&#341; Revelo, mshau&#341;i mwandamizi wa jinsia katika Umoja wa Kimataifa wa Kuhifadhi Asili mjini Mo&#341;avia, Costa Rica.<\/p>\n<p>Mpango Mkakati wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa Kuhusu Bayoanuwai ya Kibaolojia (CBD) ambao uko katika majadiliano ya mwisho hapa mjini Nai&#341;obi ambao unaweka malengo na shabaha za mkataba mpya wa kimataifa juu ya jinsi ya kukabiliana na kupotea kwa bayoanuwai utaelezea wazi kuwa wanawake lazima washi&#341;iki na ufadhili utajikita katika ushi&#341;iki wao, Revelo aliiambia IPS.<\/p>\n<p>Mpango Mkakati utaweka shabaha kadhaa za bayoanuwai kwa mwaka 2020 na kuwasilishwa kwa nchi wanachama 195 kwa ajili ya kuupitisha katika mkutano wa mwisho mjini Nagoya, Japan Oktoba hii.<\/p>\n<p>&#8220;Wanawake ni walinzi wa bayoanuwai katika kilimo. Nchini Pe&#341;u, wanapanda zaidi ya aina 60 ya mihogo, nchini Rwanda zaidi ya aina 600 ya maha&#341;age,&#8221; alisema Revelo. &#8220;Ukiondoa asilimia 50 ya wakazi wakati tupo katika mgogo&#341;o wa bayoanuwai siyo suala ambalo ni zu&#341;i sana.&#8221;<\/p>\n<p>Wanawake katika mataifa yanayoendelea wana maa&#341;ifa ya mifumo ya kijamii na kiasili, ikiwa ni pamoja na kukusanya asilimia 80 ya vyakula mwitu vinavyoliwa. Wanaokoa hadi asilimia 90 ya mbegu ambazo zinatumika kwa wakulima wadogo wadogo, kulingana na Shi&#341;ika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa.<\/p>\n<p>&#8220;Wanawake wana jukumu kubwa katika asili, ma&#341;a nyingi ni wakulima na wako ka&#341;ibu na kuelewa bayoanuwai,&#8221; Ahmed Djoghlaf, katibu mtendaji mkuu wa CBD, aliiambia IPS.<\/p>\n<p>Pamoja na ukweli huu wanawake hawaonekani kuwa watekelezaji wakuu wa hifadhi, na hawaka&#341;ibishwi katika mikutano ya bayoanuwai, alisema Revelo.<\/p>\n<p>&#8220;Hata katika mijadala kuhusu upatikanaji na faida za maliasili jukumu la wanawake halijatambuliwa wazi labda katika CBD,&#8221; alisema. Tafiti zimegundua kuwa kama wanawake wanapata fedha za hifadhi, asilimia 90 zitaingia kwenye familia, wakati wanaume hutumia asilimia 15 tu kwa wastani, aliongeza.<\/p>\n<p>Wanawake wana uwezekano mkubwa wa kuathi&#341;ika na kupungua kwa bayoanuwai &ndash; neno linalotumika kuelezea aina mbalimbali ya viumbe hai ambavyo hutengeneza mfumo wa maisha duniani ambao hutoa chakula, mafuta, hewa safi na maji. Katika jumuiya nyingi wanawake ndiyo wanahamisha maa&#341;ifa kuhusu mimea, wanyama na mifumo ya kiikolojia katika kanda.<\/p>\n<p>Hata kama wanawake ni wengi kati ya wakulima wa Af&#341;ika, katika maeneo mengi kama mume akifa&#341;iki dunia, kipande cha a&#341;dhi ambacho amekuwa akipanda chakula kulisha familia katika maisha yake kitachukuliwa na ndugu wa kiume wa mume wake &ndash; na wala siyo yeye, alisema Kemi Seesink, Mnige&#341;ia katika NGO ya Wetlands Inte&#341;national, ambayo ina makao yake nchini Uholanzi.<\/p>\n<p>Mabadiliko ya kitamaduni ni ya msingi kama kuna matumaini ya kuzuia kupungua kwa bayoanuwai na kubo&#341;esha vyanzo vya vipato, Revelo alisema. &#8220;Tunataka kubo&#341;esha mwenendo usiokuwa na mwelekeo. Hii ma&#341;a nyingine ina maana kuwa kubadili utamaduni, destu&#341;i na njia za kuishi.&#8221;<\/p>\n<p>Wakati nchi wanachama wa CBD wanakamilisha mkataba wa kimataifa Oktoba, Revelo ana matumaini kuwa nchi zitawapatia wanawake jukumu kubwa katika utoaji wa maamuzi katika eneo lolote lile la bayoanuwai na viwango vya kikanda. &#8220;Wanawake wanataka kuwa wahusika wakuu na wanata&#341;ajia kuchukua nafasi zao,&#8221; alisema.<\/p>\n<p>Hata hivyo, hii itakuwa tu hatua ya kwanza, alisema Joji Ca&#341;ino wa Mfuko wa Tebtebba, akiongea kwa niaba ya makundi ya watu wazawa. &#8220;Kuna tatizo kubwa la kuhakikisha kuwa umma na mashi&#341;ika ya ki&#341;aia unashi&#341;ikishwa katika ngazi ya se&#341;ikali ya kitaifa,&#8221; Ca&#341;ino alisema.<\/p>\n<p>Uamuzi unaohusu bayoanuwai ma&#341;a nyingi yanatengenezwa na maafisa wa se&#341;ikali katika mfumo wa kutoka juu kwenda chini, alisema. Mitizamo hiyo bado ipo katika CBD ambapo mipango ya utekelezaji ya kufikia shabaha mpya za bayoanuwai &#8220;haina kumbukumbu yoyote ile ya kushi&#341;ikisha mashi&#341;ika ya ki&#341;aia hadi tutakapoziingiza&#8221; na shabaha hizi pia zimeamuliwa na wataalam, na kuacha vyama vya ki&#341;aia kupendekeza ma&#341;ekebisho kwa matumaini ya kuwa watashi&#341;ikishwa.<\/p>\n<p>Revelo anakubali kuwa bado wanawake wana hatua ndefu kwenda lakini alisema, &#8220;Ni miongoni mwa walio na usawa tu ambao tunaweza kusonga mbele.&#8221; <\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>NAIROBI, Mei 27 (IPS) &ndash; Wanawake wanachangia asilimia 90 ya uzalishaji wa chakula katika maeneo maskini vijijini na hadi asilimia 80 ya chakula katika nchi nyingi zinazoendelea, na hata hivyo wanapuuzwa moja kwa moja wakati maamuzi ya kise&#341;a yanapotolewa kuhusu kilimo na bayoanuwai. Hii inaka&#341;ibia kubadilika na pongezi zinapaswa kwenda kwa mkataba wa Umoja wa&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":232,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-3302","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3302","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/232"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=3302"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3302\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=3302"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=3302"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=3302"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}