{"id":3269,"date":"2010-05-17T13:40:01","date_gmt":"2010-05-17T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2010\/05\/17\/afya-muswada-wa-uganda-usizuie-madawa-yasiyotengenezwa-kwa-leseni-anakubali-wazii\/"},"modified":"2010-05-17T13:40:01","modified_gmt":"2010-05-17T13:40:01","slug":"afya-muswada-wa-uganda-usizuie-madawa-yasiyotengenezwa-kwa-leseni-anakubali-wazii","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2010\/05\/17\/afya-muswada-wa-uganda-usizuie-madawa-yasiyotengenezwa-kwa-leseni-anakubali-wazii\/","title":{"rendered":"AFYA: Muswada wa Uganda Usizuie Madawa Yasiyotengenezwa kwa Leseni, Anakubali Wazi&#341;i"},"content":{"rendered":"<p>KAMPALA, Ap&#341; 29 (IPS) &ndash; Wazi&#341;i wa Biasha&#341;a wa Uganda anakubaliana kuwa Muswada tata wa se&#341;ikali yake wa Bidhaa Bandia haupaswi kuzuia utengenezaji na uingizaji wa madawa yanayotengenezwa kwa leseni.\n<\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>Muswada huo, ulioandaliwa kutokana na fedha kutoka Umoja wa Ulaya, unataka kutoa adhabu ya makosa ya jinai kutokana na bidhaa bandia.<\/p>\n<p>Bidhaa bandia zinafasiliwa kama kutengeneza, kuzalisha, kufunga, kufunga upya, kuweka vibandiko au kutengeneza bidhaa zozote zile ambazo zimeigwa ili kuonekana zinafanana na bidhaa zinazolindwa na haki miliki bila kupata &#341;idhaa ya mmiliki wa haki miliki (IP) anayeishi nchini au mahali pengine.<\/p>\n<p>Kwa kunukuu Tamko la Doha la Shi&#341;ika la Biasha&#341;a Ulimwenguni 2001, Gagawala Wambuzi, wazi&#341;i wa biasha&#341;a wa Uganda ambaye anaongoza kutaka kupitishwa kwa muswada, alisema kuwa se&#341;ikali yake inatambua Ma&#341;ekani na Umoja wa Ulaya wamekubaliana kuwa mataifa yenye maendeleo duni (LDCs) yanapaswa kufaidi mabadiliko makubwa kuhusu IP na madawa.<\/p>\n<p>&#8220;Kimsingi suala la madawa yanayotengenezwa kwa leseni kwa ajili ya LDCs kama Uganda, Tanzania, Rwanda na Bu&#341;undi siyo haba&#341;i njema. Wanapaswa kutu&#341;uhusu kutengeneza madawa kwa leseni. Nchi za LDC lazima zi&#341;uhusiwe kufanya baadhi ya mambo ili tuweze kufika (kimaendeleo) na hivyo tuweze kutengeneza madawa kwa njia ya leseni. Hii ndiyo maana yake,&#8221; Wambuzi alikubaliana.<\/p>\n<p>Kuhusu kampeni ya mashi&#341;ika ya ki&#341;aia kuhusu madha&#341;a mabaya juu ya muswada huo kama unavyoonekana sasa, Wambuzi alisema, &#8220;hatuwezi kutengenezwa muswada unaotuumiza. Ni kwa nini tufanye hivyo; kwa faida ya nani  Muswada ni kwa ajili yetu.&#8221;<\/p>\n<p>Aliongeza kuwa maslahi ya Uganda katika she&#341;ia hiyo ni kuhakikisha ulinzi wa viwanda kutokana na bidhaa bandia ambazo alisema zinalenga bidhaa za Uganda. <\/p>\n<p>Tasisi ya Huduma za Usajili ya Uganda, ambayo ina kazi ya kusajili jina la bisha&#341;a, haki miliki na hati miliki, pia inakubali hata&#341;i zinazotokana na muswada huo katika hali yake ya sasa. <\/p>\n<p>Bise&#341;eko Kyomuhendo, kaimu msajili mkuu wa taasisi hiyo, aliiambia IPS kuwa, &#8220;tunaja&#341;ibu kuonyesha kwa wiza&#341;a inayoufadhili muswada kuwa masuala ya haki miliki hayapaswi kuchanganywa na suala la utengenezaji na upatinaji wa madawa&#8221;. <\/p>\n<p>Taasisi ina imani kuwa muswada unapaswa kuandaliwa upya kwa ajili ya kujaza mapengo katika mifumo ya she&#341;ia iliyopo kuhusu IP katika She&#341;ia ya Hati Miliki na Nembo za Biasha&#341;a.<\/p>\n<p>Kuhusu maendeleo ya kuandaa she&#341;ia hiyo, Elizabeth Tamale, afisa biasha&#341;a mkuu wa wiza&#341;a ya biasha&#341;a, aliiambia IPS: &#8220;Kwa sasa kuna baadhi ya maoni ambayo tunapaswa kuingiza katika wa&#341;aka wa mwisho.&#8221; Haya yanatakiwa kupelekwa kwa waandaaji wa muswada, alithibitisha.<\/p>\n<p>Kampuni ya Madawa yenye makao yake nchini India ya Cipla Ltd imeshi&#341;ikiana na kampuni ya Quality Chemicals ya nchini Uganda kutengeneza madawa ya ku&#341;efusha maisha kwa wagonjwa wa UKIMWI kwa leseni (ARVs) na madawa ya kupambana na mala&#341;ia. Mipango kama hiyo, chini ya mipango ya leseni ya lazima, inafanywa nchini Ghana, Af&#341;ika Kusini, na Msumbiji.<\/p>\n<p>Kupewa Leseni kwa lazima &#8220;ni pale ambapo se&#341;ikali inapo&#341;uhusu mtu mwingine kuzalisha bidhaa yenye jina lililosajiliwa au kuisindika bila &#341;idhaa ya mmiliki wa jina hilo&#8221;, kulingana na tovuti ya Shi&#341;ika la Biasha&#341;a Ulimwenguni (WTO). Maeneo yanayohusiana na biasha&#341;a ya WTO katika mikataba ya haki miliki (TRIPs) ya mwaka 1995 yana&#341;uhusu suala hili.<\/p>\n<p>Mbali ya Muswada wa Bidhaa Bandia wa Uganda na Muswada wa Kupambana na Bidhaa bandia wa Kenya 2008, Tanzania pia ilipitisha kanuni mpya mwaka 2008, zilizoambatanishwa na She&#341;ia ya Nembo za Biasha&#341;a, ambayo imetishia kuwa na madha&#341;a yanayofanana katika uzalishaji wa madawa kwa kutumia leseni kama ilivyo kwa hatua za kishe&#341;ia zilizochukuliwa na maji&#341;ani zake. <\/p>\n<p>Geo&#341;ge Baguma, afisa biasha&#341;a mkuu katika Quality Chemicals, aliiambia IPS kuwa, &#8220;miswada ya kupambana na bidhaa bandia katika Af&#341;ika Masha&#341;iki inapaswa kuwekwa kabatini. Nadhani tunafanya kazi kwa fu&#341;aha bila kuwa nayo. Bado tunahitaji makampuni ya madawa kwa wingi katika Af&#341;ika Masha&#341;iki ili tuweze kutoa madawa ya bei nafuu kwa watu wetu.<\/p>\n<p>&#8220;Madha&#341;a ya miswada hii ni kwamba viwanda vyetu vitafungwa na hatutaweza kuzalisha madawa tena. Lakini jambo muhimu zaidi siyo juu ya madawa tunayozalisha sasa. Kuna madawa machache ambayo yanazalishwa. Tunapaswa kupata teknolojia hiyo. Kimsingi, kama she&#341;ia hizo zinapitishwa tutawafanya watu wetu waendelee tu kutumia madawa ya zamani,&#8221; alionya. <\/p>\n<p>Uzalishaji wa ndani wa ARVs na kampuni ya Quality Chemicals utasaidia Uganda kutoa tiba kwa watu wanaokadi&#341;iwa kuwa 263,000 ambao watahitaji madawa hayo ifikapo mwaka 2012 na watu 342,200 ambao watahitaji tiba ifikapo mwaka 2020. <\/p>\n<p>Hakiel Mgonja, msajili msaidizi katika Wakala wa Usajili wa Biasha&#341;a na Leseni nchini Tanzania, alikubali hivi ka&#341;ibuni katika mkutano mjini A&#341;usha, Tanzania, kuwa itakuwa kosa kubwa kwa kanda kuzuia uzalishaji wa ndani wa madawa, hasa kwa kuzingatia kuwa watu wengi hawawezi kupata madawa muhimu kutokana na gha&#341;ama kubwa.<\/p>\n<p>&#8220;Nchini Tanzania tunasema kuwa tuna she&#341;ia ya biasha&#341;a na inafanya kazi, hata ya kupambana na bidhaa bandia. Huwezi kutengeneza zimwi na kulitunza nyumbani litakula watoto wako na baadaye litakula na wewe pia. Hivyo tunapaswa kujenga mifumo ya mazingi&#341;a ya sekta ya madawa kama tunataka kufikia lengo la upatikanaji wa madawa kwa wote,&#8221; alisema Mgonja. <\/p>\n<p>Ripoti ya Shi&#341;ika la Afya Ulimwenguni ya mwaka 2009 yenye jina la &#8220;Kuelekea Upatikanaji wa Madawa kwa Wote&#8221; ilionyesha kuwa asilimia 66 (au watu milioni 6,7) wanaostahili kupata madawa katika Af&#341;ika Kusini mwa Jangwa la Saha&#341;a bado hawayapati madawa ya ARV. Pia inaonyesha kuwa watu wapatao milioni tatu, ambao taya&#341;i wako katika tiba, watahitaji kuendelea kupata ARVs kwa maisha yao yote. <\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>KAMPALA, Ap&#341; 29 (IPS) &ndash; Wazi&#341;i wa Biasha&#341;a wa Uganda anakubaliana kuwa Muswada tata wa se&#341;ikali yake wa Bidhaa Bandia haupaswi kuzuia utengenezaji na uingizaji wa madawa yanayotengenezwa kwa leseni. Muswada huo, ulioandaliwa kutokana na fedha kutoka Umoja wa Ulaya, unataka kutoa adhabu ya makosa ya jinai kutokana na bidhaa bandia. Bidhaa bandia zinafasiliwa kama&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":526,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-3269","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3269","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/526"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=3269"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3269\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=3269"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=3269"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=3269"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}