{"id":2214,"date":"2008-07-15T13:40:01","date_gmt":"2008-07-15T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2008\/07\/15\/maswali-na-majibu-uzazi-wa-mpango-katika-uchanga-wake-sudan-kusini\/"},"modified":"2008-07-15T13:40:01","modified_gmt":"2008-07-15T13:40:01","slug":"maswali-na-majibu-uzazi-wa-mpango-katika-uchanga-wake-sudan-kusini","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2008\/07\/15\/maswali-na-majibu-uzazi-wa-mpango-katika-uchanga-wake-sudan-kusini\/","title":{"rendered":"MASWALI NA MAJIBU: Uzazi wa Mpango Katika Uchanga Wake Sudan Kusini"},"content":{"rendered":"<p>JUBA, Julai 11 (IPS) &ndash; Huku kukiwa na ba&#341;aba&#341;a chache na kukiwa hakuna miundombinu ya afya na elimu kwa watu wanaokadi&#341;iwa kufikia milioni 10 katika Sudan Kusini&mdash;sensa ya hesabu ya watu bado haijatoa matokeo &ndash; wafanyakazi wa huduma za afya wana kazi kubwa mbele yao.\n<\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>Sudan Kusini imekuwa na vita kwa miaka 50 na kuwa na kipindi kimoja tu cha miaka 10 ya amani, kabla ya Makubaliano ya Amani ya Mwaka 2005 kupatia kusini mwa Sudan kuwa na utawala wake. Se&#341;ikali ya Sudan Kusini, ambayo ni changa zaidi ba&#341;ani Af&#341;ika, pia ilishinda kudhibiti asilimia 50 ya mapato yanayotokana na mafuta katika upande wa kusini: yenye thamani ya dola zipatazo bilioni 1.5 kwa mwaka. <\/p>\n<p>Ka&#341;ibu pesa zote za se&#341;ikali zinatumika kuka&#341;abati huduma za umma zilizoha&#341;ibiwa na kulipia wanajeshi wengi wa kujitolea wa Umoja wa Mataifa ambao maafisa wa Umoja huo wamekadi&#341;ia kuwa wanafika 160,000. Mpango wa amani ni tete na kunakuwa na mazungumzo ya kila ma&#341;a na Kha&#341;toum juu ya utekelezwaji wake na hivyo kunyonya nguvu kubwa ya kisiasa. <\/p>\n<p>Kuleta dhana mpya kabisa za uzazi wa mpango &ndash; na miundo inayohitajika kufalinya suala hilo kufanya kazi &ndash; inaonekana kushindwa kabisa. <\/p>\n<p>Lakini kutokana na Sudan Kusini kukabiliwa na kiwango cha juu zaidi cha vifo vya mama wajawazito cha wanawake 2,054 kwa kila watoto 100,000 wanaozaliwa &ndash; mmoja kwa kila wanawake hamsini anafa&#341;iki dunia &ndash; shinikizo linaendelea kutafuta ufumbuzi. <\/p>\n<p>Uzazi wa mpango unapunguza mimba zisizokusudiwa, hasa zile ambazo ni hata&#341;i kwa wanawake, na hivyo unaweza kuwa na matokeo kwa idadi ya wanawake wanaofa&#341;iki dunia wakati wakijifungua, kulingana na mku&#341;ugenzi wa afya ya uzazi wa Kusini mwa Sudan, Maku&#341; Ka&#341;iom. <\/p>\n<p>Mwandishi wa IPS Skye Wheele&#341; aliongea naye kuhusu changamoto anazota&#341;ajia. <\/p>\n<p>IPS: Se&#341;ikali ya Kusini mwa Sudan iko wapi sasa kuhusu suala la uzazi wa mpango  <\/p>\n<p>Maku&#341; Ka&#341;iom: Kwa kweli hakuna se&#341;a kwa sasa. Katika &#341;asimu ya wa&#341;aka huo wa se&#341;a ya afya ya uzazi katika Sudan Kusini kunatakiwa suala la uzazi wa mpango kama moja ya masuala muhimu ambalo ni lazima se&#341;ikali kulitafutia ufumbuzi. Kwa sasa tunaja&#341;ibu kutumia fu&#341;sa yoyote ile kuzungumza na akina mama na wazazi kuhusu suala hilo. <\/p>\n<p>Lakini tunataka kuona njia za uzazi wa mpango zinaingizwa kikamilifu katika mfumo wa afya ifikapo mwishoni mwa mwaka ujao. Itakuwa na changamoto. <\/p>\n<p>IPS: Ni kiwango gani cha uelewa wa mpango wa uzazi wa mpango sasa katika Kusini  <\/p>\n<p>MK: Kiwango cha matumizi ya njia za uzazi wa mpango kipo chini ya asilimia moja kulingana na Utafiti wa Kaya wa (Umoja wa Mataifa na se&#341;ikali) ya Sudan Kusini. Kutokana na takwimu hiyo unaweza kuona wazi jinsi gani kiwango cha matumizi ni cha chini. Hii ni kutokana na kukosekana kwa ufahamu wa kutosha kuhusu umuhimu wa njia za uzazi wa mpango na upatikanaji mdogo, na kukosekana kwa wafanyakazi wenye elimu ambao wanaweza kueneza maa&#341;ifa yanayohitajika kuweza kutoa uamuzi stahili. <\/p>\n<p>Kama unakwenda katika vituo vingi vya kuwafikia watu katika vijiji, utakuta malundo ya kondomu katika hifadhi. Hakuna anayezitumia. <\/p>\n<p>Kuna masuala ya kitamaduni. Watu wanadhani kuwa njia za uzazi wa mpango ni kinyume na maadili na ni ukahaba. Watu wengine wana imani matumizi ya njia hizi ni suala lililoingizwa kutoka kwa wazungu wakija&#341;ibu kupunguza idadi ya watu wetu na wengine wanaamini kwa kutumia kondomu huwezi kufaidi tendo la ndoa. <\/p>\n<p>Lakini bila ya kutumia uzazi wa mpango hatutaweza kukabiliana na kiwango kikubwa cha vifo vya wajawazito. <\/p>\n<p>IPS: Kuna suala la kisiasa la idadi ya watu, katika Sudan Kusini, ni kweli lipo  <\/p>\n<p>MK: Watu wetu wanaamini kuwa jinsi unavyozidi kuwa na watoto wengi ndivyo unavyoweza kuwa na nguvu na heshima katika familia na jamii. Ina&#341;ejea kwenye asili ya makabila yetu, hususani yanayotokana na Nilotic, makabila (ambayo kimsingi ni ya wafugaji). Kama mnakuwa wengi katika idadi yenu, hakuna atakayeja&#341;ibu kuiba ng&#8217;ombe wako au kupigana nawe. Hivyo kitu kama hicho kipo miongoni mwa watu wetu na kimezidi kuima&#341;ishwa wakati wa vita. <\/p>\n<p>Kutokana na kupoteza zaidi ya watu milioni 2 ina maana kuwa wakazi wetu wamepungua na tunahitaji kuongezea idadi hiyo. Tishio la vita na kaskazini daima linakuwepo, hatutaweza kukabiliana na tishio hilo kama hatutakuwa na watu wengi wenye nguvu kupigana. <\/p>\n<p>Mimi binafsi nadhani kuwa tunapaswa kuzaa watoto wachache na jinsi muda unavyozidi kusogea idadi itaongezeka na utaweza kufikia kiwango cha juu cha idadi ya watu na wenye afya wakati huo. <\/p>\n<p>Siyo &#341;ahisi kuuza dhana hiyo kwa wakazi lakini jinsi muda unavyosogea wataweza kutusikiliza. Taya&#341;i watu wanaanza kuhisi mzigo wa kiucumi kwa kuwa na mtu mmoja mwenye aji&#341;a se&#341;ikalini na familia nzima yenye watu wapatao 20 wakimtegemea. <\/p>\n<p>Sisi kama se&#341;ikali hatuwaambii watoto kuwa na familia ndogo. Ni &#341;ahisi kuwaambia kama unataka wengi zaidi au watoto wachache unaochagua, lakini ja&#341;ibu kupanga na kutumia &#341;asilimali chache tulizonazo kwa njia ya uangalifu zaidi. <\/p>\n<p>IPS: Mtaanzia wapi, hasa kutokana na kwamba asilimia 92 ya wanawake wa Kusini hawajui kusoma na kuandika  <\/p>\n<p>MK: Unaanzia katika miundombinu ya afya. Hapo ndipo pa kuanzia kuzungumza na watu. Halafu tutatumia watu muhimu katika wanajumuiya kama machifu na wakunga wa jadi, watu wanaoaminiwa na watu. Tutaelimisha watu hawa halafu wanaweza kuendelea kufanya kazi. <\/p>\n<p>IPS: Ni nini haba&#341;i njema  <\/p>\n<p>Njia nyingi za uzazi wa mpango, kuanzia za kunywa vidonge hadi njia za kuzuia, zinapatikana bu&#341;e katika hospitali na baadhi ya kliniki na vituo vya afya na pia zinaweza kununuliwa kutoka sokoni. <\/p>\n<p>Hatuna takwimu lakini kulingana na watu wanaohusika na VVU kuna ongezeko la matumizi ya kondomu katika soko. <\/p>\n<p>Na uhamasishaji unaendelea vizu&#341;i sana katika jeshi. Wanalichukulia kwa uzito mkubwa mno. Wanazungumzia kuhusu hilo katika gwa&#341;ide zao. <\/p><\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>JUBA, Julai 11 (IPS) &ndash; Huku kukiwa na ba&#341;aba&#341;a chache na kukiwa hakuna miundombinu ya afya na elimu kwa watu wanaokadi&#341;iwa kufikia milioni 10 katika Sudan Kusini&mdash;sensa ya hesabu ya watu bado haijatoa matokeo &ndash; wafanyakazi wa huduma za afya wana kazi kubwa mbele yao. Sudan Kusini imekuwa na vita kwa miaka 50 na kuwa&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":0,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-2214","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/2214","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=2214"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/2214\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=2214"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=2214"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=2214"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}