{"id":2213,"date":"2008-07-15T13:40:01","date_gmt":"2008-07-15T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2008\/07\/15\/afya-sudan-kusini-kaibu-uangalizi-mpya-wa-huduma-za-wajawazito\/"},"modified":"2008-07-15T13:40:01","modified_gmt":"2008-07-15T13:40:01","slug":"afya-sudan-kusini-kaibu-uangalizi-mpya-wa-huduma-za-wajawazito","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2008\/07\/15\/afya-sudan-kusini-kaibu-uangalizi-mpya-wa-huduma-za-wajawazito\/","title":{"rendered":"AFYA&ndash; SUDAN KUSINI: Ka&#341;ibu Uangalizi Mpya wa Huduma za Wajawazito"},"content":{"rendered":"<p>JUBA, Julai 10 (IPS) &ndash; Mimba kubwa imemfanya mwanamke mwembamba na aliyevimba kutembea katika wodi mpya na inayovutia ya wajawazito katika Sudan Kusini huku akishikilia vipande viwili vya ka&#341;atasi vilivyofungwa pamoja. Anaonekana hana um&#341;i unaozidi miaka 16, huku akionekana akitoka kwenye mauamivu makali.\n<\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>Ateino Maclean, mmoja wa wakunga wawili tu wenye mafunzo anayefanya kazi katika Hospitali ya Kutoa Mafunzo ya Juba, anaangalia ka&#341;atasi hizo na kumwelekeza mwanamke huyo kwenda kwenye wodi nyingine. <\/p>\n<p>&#8220;Yupo taya&#341;i kujifungua kwa njia ya upasuaji,&#8221; Maclean alisema, huku akitikisa kichwa. &#8220;Alikuwa katika uchungu lakini amesubi&#341;i hadi sasa kuja hospitalini.&#8221; <\/p>\n<p>Juba, mji mkuu, sasa una wodi ya wajawazito, viti vya kujifungulia na mashine mbili za kuzalishia watoto, ambazo bado zina utepe wa siku ya kuzinduliwa &#341;asmi. Katika siku zake tano za kwanza, ilihudumia watoto 46 waliozaliwa kwa njia za kawaida na watano kwa njia ya upasuaji. Tofauti na maeneo mengine ya Kusini, kuna madawa mengi katika chumba cha kuhifadhia madawa. Maafisa wa se&#341;ikali wanakadi&#341;ia kuwa ni asilimia 25 tu ya wakazi wanatumia huduma za msingi za tiba&mdash;wodi mpya inatoa huduma bo&#341;a zilizopo Sudan Kusini kwa wanawake wa Juba na maeneo yanayozunguka mji huo. <\/p>\n<p>Mtoto mmoja kati ya hamsini wanaozaliwa anasababisha kifo cha mama <\/p>\n<p>Kulingana na Shi&#341;ika la Wakazi la Umoja wa Mataifa (UNFPA), Af&#341;ika ina kiwango kibaya zaidi cha vifo vya mama wanaojifungua duniani huku mama 820 wakifa&#341;iki dunia katika kila watoto 100,000 wanaozaliwa. Baada ya zaidi ya miaka 50 ya vita kumalizika, Sudan Kusini ina kiwango kibaya zaidi cha vifo vya mama wanaojifungua: 2,054 kwa watoto 100,000 wanaozaliwa. <\/p>\n<p>Magda A&#341;mah kutoka UNFPA anadhani idadi halisi inaweza hata kuwa kubwa zaidi. &#8220;Inatisha kwasababu wanawake wengi wanawakilisha wale wanaopata huduma, ni wangapi ambao huduma haziwafikii &#8221; <\/p>\n<p>Miaka miwili iliyopita kutembelea wodi ya wazazi ya Juba ilikuwa ni safa&#341;i ya kukatisha tamaa. Vyumba vyenye giza na vichafu, kuta ambazo zinaonekana kutaka kudondoka na ha&#341;ufu za damu. Meza za kupimia uzito zilionekana kama za kihisto&#341;ia kutoka miaka ya 1960, vifaa vya kujifungulia vilikuwa vimechakaa mno. <\/p>\n<p>Mpango wa awali ulikuwa wa kufanyia uka&#341;abati wa vyumba pamoja na hospitali nzima, kwa kutumia dola kadhaa za misaada ambazo zimetolewa baada ya mkataba wa amani wa mwaka 2005. <\/p>\n<p>Lakini UNFPA, ambayo inakuza haki ya afya na fu&#341;sa sawa kwa wote kwa kusadiai kukusanya takwimu na kubuni se&#341;a, ilitetea kuwa na wodi mpya, kubwa na yenye chumba cha upasuaji. &#8220;Ni mfano wa jinsi gani hospitali nyingine zinapaswa kufanyiwa uka&#341;abati,&#8221; Alexande&#341; Dimiti, ambaye pia anatoka UNFPA, aliiambia IPS. <\/p>\n<p>Se&#341;ikali ya Kusini mwa Sudan yenye um&#341;i wa miaka mitatu ina mpango maalum wa kazi wa kupunguza vifo vya mama wanaojifungua, pamoja na kwamba afisa mmoja alisema kuna mambo mengi ya kufanya &ndash; &#341;asilimali watu, kuhamasisha, usambazaji wa vifaa vya tiba &ndash; hivyo kushindwa kujua wapi pa kuanzia. Kiutendaji, muda wa wafanyakazi wa afya unatumiwa katika kuzima moto katika majanga ya kila mwaka ikiwa ni pamoja na kuzuka kwa kipindupindu, uti wa mgongo na su&#341;ua. <\/p>\n<p>&#8220;Afya ya uzazi inaachwa nyuma. Kuna mahitaji mengi mno yanayoshindana,&#8221; alielezea D&#341;agudi Buwa, mkuu wa UNFPA wa Sudan Kusini. <\/p>\n<p>Wakati kuna njia bo&#341;a za kushughulikia dha&#341;ula kwa kushi&#341;ikiana na mashi&#341;ika ya Umoja wa Mataifa, hakuna mifumo ya kuwa na usambazaji endelevu wa madawa na vifaa ambao Dimiti anaita &#8220;nguzo&#8221; katika mfumo wa afya ambao ungeweza kuwa na matokeo katika MMR. <\/p>\n<p>Mfumo dhaifu mno wa mawasiliano kati ya ngazi tofauti za se&#341;ikali unapaswa pia kulaumiwa, Dimiti alisema. Eneo hilo kubwa lina ba&#341;aba&#341;a chache zinazounganisha jumuiya za vijijini zilizosambaa na maeneo mengi yanakatiwa mawasiliano wakati wa msimu wa mvua. <\/p>\n<p>Ma&#341;a nyingi usafi&#341;i ni wa ghali na mgumu mno, na Dimiti alisema, wanawake wa Kusini ma&#341;a nyingi siyo watoa maamuzi kuhusu mimba na afya zao. Na hata kama wanawake wanafika hospitalini, ma&#341;a nyingi wanafanywa kusubi&#341;i na wafanyakazi wasiokuwa na mafunzo katika foleni ndefu. <\/p>\n<p>Ujuzi unahitajika mno <\/p>\n<p>Festo Juma, kiongozi mkuu wa Hospitali ya Kutoa Mafunzo ya Juba ikiwa ni pamoja na wataalam wake wa masuala ya mimba, anaoenekana amechoka anapoelezea matukio ya upasuaji ambayo yanamkabili; wanawake wanaletwa kwa malo&#341;i baada ya kusafi&#341;i mamia ya kilomita katika ba&#341;aba&#341;a mbovu huku wakiwa na maumivu makali ya kujifungua na wakiwa taya&#341;i wameshapoteza damu nyingi. <\/p>\n<p>Moja ya sehemu ya huduma ya wajawazito ya hospitali hiyo bado haijapewa mwanzo mzu&#341;i &ndash; kituo cha wakunga ambako kiasi kikubwa cha wakunga wa jadi walipewa mafunzo hakifanyi kazi. <\/p>\n<p>&#8220;Hawa (wakunga wa jadi) hawakuwa na matokeo mazu&#341;i,&#8221; Maclean anasema. &#8220;Huku wakiwa na kiasi kidogo cha elimu wanazingatia tu kile ambacho wanakijua kabla.&#8221; <\/p>\n<p>Mkunga wa jadi atabonyeza tumbo lenye mimba, kama ilivyo kwa wakunga wazee ambao wanasaidia kuzalisha katika kanda hiyo &ndash; lakini mafunzo yao hayajawapatia ujuzi wa kufikia hitimisho muhimu. Matokeo yake, Maclean anadhani, ni kupunguza heshima kwa wakunga wenye ujuzi. <\/p>\n<p>Lakini wanawake wana fu&#341;sa ndogo ya kuchagua: utafiti baada ya vita uligundua kuwa kulikuwa na wakunga nane tu wenye mafunzo&ndash; afisa wa se&#341;ikali alisema ukweli ni kwamba walikuwa sita tu &ndash; katika upande wa Kusini, ambako UNFPA inakadi&#341;ia kuwa kuna wakazi wapatao milioni 10. <\/p>\n<p>Wakunga wa jadi wa jumuiya thelathini na sita hivi ka&#341;ibuni walihitimu kutoka kwenye kozi ya miezi 18 ambayo imebuniwa maalum kwa ajili ya mahitaji ya Kusini na se&#341;ikali na UNFPA. Lakini shi&#341;ika hilo la Umoja wa Mataifa linakadi&#341;ia kuwa katika kiwango hiki itachukua miaka 60 kuweza kufikia viwango vya kimataifa vya afya ya uzazi. Utafiti wa Umoja wa Mataifa na se&#341;ikali uligundua kuwa asilimia saba ya wazazi wanaojifungua wanahudumiwa na wakunga au manesi na asilimia 13.6 tu ya wanaojifungulia katika taasisi za afya. <\/p>\n<p>&#8220;Katika maeneo ya kijijini hali ni mbaya zaidi&#8230; sababu kubwa (ya kiasi kikubwa cha vifo) ni kukosekana kabisa kwa huduma za kujifungua katika eneo la &#341;obo tatu ya Kusini,&#8221; Juma anasema. <\/p>\n<p>&#8220;Watu wetu wengi walikufa kutokana na vita. Tunataka kuwaongeza, kuendelea,&#8221; anasema nesi wa uzazi Susan Poni. Wanawake wanahamasishwa &ndash; ikiwa ni pamoja na wanasiasa wa juu &ndash; kuwa na watoto wengi, na wengi wanaanza kuzaa wakiwa vijana. Katika hali nyingine, asilimia 47 ya wasichana wanaolewa wakiwa hawajafikia um&#341;i wa miaka 15. <\/p>\n<p>Bado se&#341;ikali haijakamilisha Se&#341;a yake ya Uzazi lakini itatoa wito wa &#8220;uzazi wenye nafasi, bila kuzingatia ni watoto wangapi wanahitajika,&#8221; afisa wa wiza&#341;a ya afya Pamela Lomo&#341;o alisema. Lakini asilimia 92 ya wanawake wa Sudan Kusini hawajui kusoma na kuandika na vita vimekuwa na maana kuwa ujumbe kuhusu haki za wanawake kuchagua lini wapate mimba haujafikia wengi katika mji mkuu, ukiacha maeneo ya kijijini. <\/p>\n<p>&#8220;Kati ya kila mimba 1,000, mimba 200 ni za wasichana wa um&#341;i mdogo,&#8221; A&#341;mah anaonya. &#8220;Vijana wanakufa.&#8221; <\/p><\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>JUBA, Julai 10 (IPS) &ndash; Mimba kubwa imemfanya mwanamke mwembamba na aliyevimba kutembea katika wodi mpya na inayovutia ya wajawazito katika Sudan Kusini huku akishikilia vipande viwili vya ka&#341;atasi vilivyofungwa pamoja. Anaonekana hana um&#341;i unaozidi miaka 16, huku akionekana akitoka kwenye mauamivu makali. Ateino Maclean, mmoja wa wakunga wawili tu wenye mafunzo anayefanya kazi katika&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":492,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-2213","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/2213","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/492"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=2213"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/2213\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=2213"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=2213"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=2213"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}