{"id":2176,"date":"2008-06-09T13:40:01","date_gmt":"2008-06-09T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2008\/06\/09\/somalia-kuongezeka-kwa-bei-za-vyakula-kwaongeza-matatizo\/"},"modified":"2008-06-09T13:40:01","modified_gmt":"2008-06-09T13:40:01","slug":"somalia-kuongezeka-kwa-bei-za-vyakula-kwaongeza-matatizo","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2008\/06\/09\/somalia-kuongezeka-kwa-bei-za-vyakula-kwaongeza-matatizo\/","title":{"rendered":"SOMALIA: Kuongezeka Kwa Bei za Vyakula Kwaongeza Matatizo"},"content":{"rendered":"<p>MOGADISHU, Juni 5 (IPS) &ndash; Ali Yusuf ni mbeba mizigo katika soko kuu la Mogadishu la Baka&#341;a. Anafanya kazi kwa masaa 12 kwa siku, akibeba mizigo ya watu wanaonunua vifaa kutoka kwenye soko hilo kwenda majumbani kwao na kulisha familia yake ya watoto nane. Lakini ongezeko la bei za vyakula kunamwathi&#341;i kwa kiasi kikubwa.\n <\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>&#8220;Nilikuwa naingiza chakula cha kutosha kwa watoto wangu, lakini sasa haijalishi nafanya kazi kwa bidii namna gani siwezi kupata chakula cha kutosha mezani kwa ajili ya familia yangu,&#8221; alisema Yusuf, wakati akijiandaa kupakua mkokoteni wake wenye kilo 250 za bidhaa kwa ajili ya mteja wake. &#8220;Inanipasa kubeba kiasi kikubwa cha mizigo kupeleka umbali m&#341;efu, kupitia katika mitaa hata&#341;i ya jiji hili. Lakini siwezi kupata pesa za kutosha kutumia kwa siku nzima,&#8221; Yusuf anaelezea. <\/p>\n<p>Kama ilivyo kwa Yusuf maelfu ya Wasomali wanakabiliwa na tatizo la kupanda kwa bei za vyakula. Mwezi uliopita, watu waliingia mitaani kuandamana katika sehemu kubwa ya taifa la Pembe ya Af&#341;ika lenye vita, ikiwa ni pamoja na mji mkuu wa Somalia wa Mogadishu. Maandamano hayo yaligeuka kuwa fujo wakati waandamanaji walipo&#341;usha mawe na kuchoma moto matai&#341;i ya maga&#341;i katika mitaa ya mji huo mkuu. Vikosi vya usalama vya se&#341;ikali ya Somalia vili&#341;usha &#341;isasi na kuwaua watu wawili wakati wa kuja&#341;ibu kutawanya makundi ya waandamanaji. <\/p>\n<p>Katika kukabiliana na maandamano, Nu&#341; Hassan Hussein, wazi&#341;i mkuu wa se&#341;ikali ya mpito nchini humo, alitoa am&#341;i ya kusitishwa kwa uuzaji nje wa bidhaa za vyakula kutoka nchini humo; hatua ambayo imekuwa na matokeo yanayoonekana kuwa madogo mno, kutokana na kwamba Somalia inazalisha chakula kidogo mno kwa ajili ya kuuza nje na inaingiza kiasi kikubwa cha chakula. <\/p>\n<p>Kuongezeka kwa bei za vyakula duniani kumesababisha maandamano katika Af&#341;ika, ikiwa ni pamoja na Mis&#341;i, Came&#341;oon, Senegal, na Af&#341;ika Kusini. Nchini Somalia, mambo yanakuwa mabaya zaidi kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miongo sasa. <\/p>\n<p>&#8220;Tatizo la kupanda kwa bei za vyakula kwa sasa ni la kimataifa lakini matatizo yetu ya ndani yanazidisha zaidi matatizo yetu,&#8221; anasema Mohamed Elmi, mwanauchumi wa nchini humo. &#8220;Masuala kama ya kukosekana kwa utulivu kwa muda m&#341;efu nchini humo, uchapishaji wa noti bandia kusikodhibitiwa, kuongezeka kwa kasi kwa bei za mafuta, na kuenea kwa utekaji katika maji ya Somalia ambako kunatishia meli zinazobeba vyakula kutoka nje na misaada vyote vinachangia kuongeza tatizo hapa.&#8221; <\/p>\n<p>Mfumuko wa bei wa sasa nchini Somalia umeanza na kupanda kwa kasi kwa bei za mafuta. Gha&#341;ama za usafi&#341;i zimepanda ma&#341;a dufu, na kuwepo kwa madha&#341;a katika nyanja zote za maisha. <\/p>\n<p>Kuenea kwa utekaji nya&#341;a katika pwani ya Somalia &ndash; ambayo ni ndefu zaidi katika Af&#341;ika &ndash; pia ni sababu ya tatizo. Shehena za mizigo ya kibiasha&#341;a na ya misaada ya kibinadamu zimekuwa zikitekwa ma&#341;a tu meli zinapoka&#341;ibia maji ya taifa la Somalia.Kulingana na Shi&#341;ika la Masuala ya Maji la Kimataifa, meli 25 zilitekwa katika pwani ya Somalia mwaka jana pekee. Taya&#341;i kumi zimeshatekwa au kushambuliwa mwaka huu, tukio la ka&#341;ibuni likiwa ni kushikiliwa kwa meli tatu na watekaji katika pwani ya Somalia. <\/p>\n<p>Hata&#341;i za mashambulizi hayo yanayofanywa na watekaji kumefanya meli za kuleta chakula na bidhaa nyingine kuja Somalia kuwa na bei kubwa ma&#341;a mbili zaidi, kulingana na waingizaji bidhaa wa Somalia. <\/p>\n<p>Uchapaji wa noti bandia za shilingi ya Kisomali, kumesababisha hali ya mfumuko wa bei kuwa mbaya zaidi na kuifanya shilingi kushuka thamani zaidi dhidi ya dola ya Kima&#341;ekani. Mwaka jana, dola moja ya Kima&#341;ekani ilikuwa wastani wa thamani ya shilingi 20,000 za Kisomali, lakini sasa imepanda hadi kuka&#341;ibia shilingi 33,000 kwa dola mwezi Mei mwaka huu, kufuatia kugundulika kuwa mabilioni ya noti feki za shilingi yamekuwa yakichapwa katika mashine zinazotumia teknolojia kubwa katika jimbo lenye uhu&#341;u nusu la kaskazini masha&#341;iki la Puntland. <\/p>\n<p>Noti ya shilingi 1000 ya Kisomali ni kubwa zaidi &ndash; na ambayo bado inaendelea kati ya noti za taifa la Kisomali. Noti hiyo imekuwa ikitumika kwa ka&#341;ibu miongo miwili tangu kupinduliwa kwa se&#341;ikai ya Siad Ba&#341;&#341;e mwaka 1991. Noti na sa&#341;afu nyingine za kiongozi huyo zimeshaanguka na hazitumiki tena kwani wafanyabiasha&#341;a wanazikataa kuwa zimechakaa mno kuzitumia. <\/p>\n<p>Hata hivyo, uingizaji wa vyakula kutoka nje unatozwa kodi na se&#341;ikali ya Somalia kwa kutumia dola za Kima&#341;ekani na kufanya wafanyabiasha&#341;a pia kufanya biasha&#341;a zao kwa kutumia dola ya Kima&#341;ekani. Kushuka kwa thamani ya shilingi dhidi ya dola ma&#341;a moja kumesababisha maumivu makali katika bajeti za familia. <\/p>\n<p>Katika soko kuu la Baka&#341;a mjini Mogadishu, gunia moja la kilo 50 la mchele linauzwa kwa dola 50, kutoka dola 30 za mwaka jana. Bei za mahindi na suka&#341;i pia zimepanda mno &ndash; kilo 50 za unga wa mahindi zinauzwa kwa kati ya dola 45, na lita 20 za mafuta ya kupikia zinagha&#341;imu zaidi ya dola 30. Bei hizi ni za ghali mno kwa Wasomali wengi. <\/p>\n<p>&#8220;Ninaingiza shilingi zipatazo 100,000 za Kisomali katika siku zangu mzu&#341;i zaidi, lakini hizi hazitoshi hata kununulia mlo mmoja wa familia yangu ya watoto nane,&#8221; analaumu Yusuf. &#8220;Fiki&#341;i: kilo moja ya mchele inauzwa zaidi ya shilingi 35,000 za Kisomalia, au kilo ya unga inauzwa kwa zaidi ya shilingi 30,000, sijui tunaeleeka wapi &#8220;. <\/p>\n<p>Watu katika taifa hilo lenye vita la Pembe ya Af&#341;ika la Somalia, ambapo fedha zinazotumwa na ndugu zao waliopo nje ndiyo chanzo kikuu cha mapato, kwa sasa wanaanza kuzoea mgogo&#341;o wa chakula kwa kutumia njia zao wenyewe: kwa kula mlo mmoja au miwili kwa siku badala ya milo mitatu. <\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>MOGADISHU, Juni 5 (IPS) &ndash; Ali Yusuf ni mbeba mizigo katika soko kuu la Mogadishu la Baka&#341;a. Anafanya kazi kwa masaa 12 kwa siku, akibeba mizigo ya watu wanaonunua vifaa kutoka kwenye soko hilo kwenda majumbani kwao na kulisha familia yake ya watoto nane. Lakini ongezeko la bei za vyakula kunamwathi&#341;i kwa kiasi kikubwa. &#8220;Nilikuwa&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":477,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-2176","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/2176","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/477"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=2176"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/2176\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=2176"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=2176"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=2176"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}