{"id":2158,"date":"2008-05-22T13:40:01","date_gmt":"2008-05-22T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2008\/05\/22\/hukumu-ya-kifo-zambia-mahabusu-waomba-kuachiliwa\/"},"modified":"2008-05-22T13:40:01","modified_gmt":"2008-05-22T13:40:01","slug":"hukumu-ya-kifo-zambia-mahabusu-waomba-kuachiliwa","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2008\/05\/22\/hukumu-ya-kifo-zambia-mahabusu-waomba-kuachiliwa\/","title":{"rendered":"Hukumu ya Kifo&ndash;ZAMBIA: Mahabusu Waomba Kuachiliwa"},"content":{"rendered":"<p>LUSAKA, Mei 20 (IPS) &ndash; Ombi la kawaida kwa wale wanaosubi&#341;i kunyongwa katika ge&#341;eza lenye msongamano mkubwa wa wafungwa nchini Zambia ni kwa Mungu kuingilia kati kukomesha mateso yao hapa duniani na kumtaka mnyongaji anayesubi&#341;i kufanya kazi yake hiyo aje kuifanya kwa ha&#341;aka, kulingana na taa&#341;ifa ya hivi ka&#341;ibuni kutoka kwa mahabusu.\n<\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>&#8220;Inauma mno kuwa katika wasiwasi, tunaomba kunyongwa,&#8221; Chu&#341;chill Malama, 33, alielezea kwa IPS. Malama ametumikia miaka mitatu akisubi&#341;i kunyongwa katika Ge&#341;eza Lenye Ulinzi Mkali la Mukobeko, lililopo katika mji wa kati mwa nchi hiyo wa Kabwe. Hukumu yake ya kifo kutokana na kufanya mauaji ilitenguliwa na Mahakama Kuu mwezi Machi. <\/p>\n<p>&#8220;Mateso na kuugua moyoni&#8221; katika maisha yanayosubi&#341;i kunyongwa kunaweza tu kuondoka kwa maombi na kubadilishana maneno kati ya mahabusu. &#8220;Hakuna shughuli za kuweza kutuliza mawazo,&#8221; Malama alisema. <\/p>\n<p>Alielezea mazingi&#341;a ya mahabusu kama &#8220;ya mateso na ya hadhi ya duni&#8221;, na kusongamana katika vyumba vya watu 48 wanaosubi&#341;i kunyongwa: &#8220;Kila chumba &ndash; kikiwa na ukubwa wa mita mbili na nusu kwa mbili &ndash; kinapaswa kuwa na mahabusu mmoja au wawili tu, lakini kuna hadi mahabusu watano hadi sita wanaoshi&#341;ikiana magodo&#341;o mawili.&#8221; <\/p>\n<p>Hakuna vyoo wala madi&#341;isha. &#8220;Tunatumia vyoo kwa kukatiana ndoo ya plastiki yenye ukubwa wa kubeba lita mbili au mbili na nusu kwa ajili ya kinyesi cha binadamu. Ni mateso,&#8221; Malama alisema. <\/p>\n<p>Wakati wa mchana, mahabusu wanaosubi&#341;i kunyongwa &ndash; wanaofikia 306 wakati wa kuachiwa kwake &ndash; walitolewa ndani ya vyumba vyao. Lakini nafasi ambapo wangeweza kuzunguzunguka ilikuwa na ukubwa wa mita za upana tatu tu na u&#341;efu wa mita 30, alisema. <\/p>\n<p>Malama alikumbuka siku ya mateso, Feb&#341;ua&#341;i 10, 2005, alipohukumiwa kifo na Mahakama Kuu katika mji mkuu wa nchi hiyo wa Lusaka, baada ya kushikiliwa kwa miaka minne kama mahabusu. Alikuwa akituhumiwa kutokana na mauaji na wizi baada ya kuvamiwa na genge la wanyang&#8217;anyi alipokuwa akilinda kituo kidogo cha umeme cha jiji hilo yeye na wenzake sita kutoka Jeshi la Kujenga Taifa la Zambia, tawi la jeshi ambalo linafanya kazi za mi&#341;adi ya ki&#341;aia. Maafisa wawili walikufa katika shambulio hilo. <\/p>\n<p>&#8220;Nilitoa taa&#341;ifa juu ya tukio hilo kwa polisi. Lakini polisi walinigeuka. Jaji aliyenikuta na hatia aliniita mshi&#341;ika wa wahaini, lakini sikuwa na hatia. Sikuta&#341;ajia tangazo hilo, &#8216;Unahukumiwa kunyongwa hadi kufa.&#8217; Nilijihisi nimefunikwa na dunia. Nilikuwa sioni.&#8221; <\/p>\n<p>Tangu wakati huo wafanyakazi wa mage&#341;eza ambao walikuwa ma&#341;afiki walimuona kama mhalifu hata&#341;i. <\/p>\n<p>Malama aliingizwa kwenye lo&#341;i na mahabusu wengine watano siku hiyo na kukimbizwa kwa mwendo wa kasi hadi Kabwe. &#8220;Badala ya masaa mawili ya kawaida kufika Kabwe, lo&#341;i hilo lilichukua saa moja tu,&#8221; alikumbuka. <\/p>\n<p>Ma&#341;a mbili kwa mwaka baada ya hapo aliweza kuhudhu&#341;ia kesi yake katika Mahakama Kuu. Lakini kesi yake iliahi&#341;ishwa kila ma&#341;a. Katika ma&#341;a ya tatu, mwaka huu, mahakama ilimwachia hu&#341;u. <\/p>\n<p>&#8220;Sikuweza kujizuia kutoa machozi. Sikuamini nilikuwa nje ya ahela,&#8221; Malama alisema. &#8220;Nilipofika nyumbani hawakuamini. Ni kama niliyefufuka. Familia nzima, ikiwa ni pamoja na baba na mama, walitokwa na machozi.&#8221; <\/p>\n<p>Malama sasa anata&#341;ajia kujiunga na kampeni ya kupinga hukumu ya kifo. <\/p>\n<p>Wanaha&#341;akati waliohojiwa na IPS walionyesha wasiwasi wao kuwa Zambia ingeweza kukomesha adhabu hiyo hivi ka&#341;ibuni. <\/p>\n<p>Wengi wa wanaha&#341;akati waliopeleka &#341;ipoti yao kwa Kamati ya Ma&#341;ekebisho ya Katiba ya Mung&#8217;omba walikuwa wakitaka kuendeleza hukumu ya kifo katika katiba mpya nchini humo, Kelvin Hang&#8217;andu, mwanashe&#341;ia maa&#341;ufu aliiambia IPS. <\/p>\n<p>&#8220;Siwezi kwa kujiamnini kusema kuwa katiba mpya itaingiza &#341;asmi hukumu ya kifo kama hukumu ha&#341;ali kishe&#341;ia,&#8221; alisema. <\/p>\n<p>Leona&#341;d Kalinde, ambaye pia ni mwanashe&#341;ia maa&#341;ufu na mwanaha&#341;akati wa hukumu ya kifo, alisema hali hii iliakisi wale wanaopinga kukomeshwa kwa hukumu ya kifo: &#8220;Sisi kama wanaha&#341;akati, hatujafanya kazi ya kutosha kuwasilisha ujumbe. Tunapaswa kutoa elimu zaidi juu ya hukumu ya kifo. Sisi kama taifa la kistaa&#341;abu, tunapaswa kuwa tumeshakomesha hukumu ya kifo na sasa tunapaswa kuelekeza nguvu zetu kwa mageuzi ya (uta&#341;atibu wa mashitaka).&#8221; <\/p>\n<p>Askofu Enocent Silwamba, mku&#341;ugenzi mtendaji wa Huduma ya Ki&#341;oho ya Mage&#341;eza ya Zambia, kwa nguvu zake alikosoa Zambia kutokana na kushindwa kuondokana na hukumu ya kifo. &#8220;Kutokana na kuwa na mfumo wa mahakama usiokuwa kamilifu, siyo kila aliyehukumiwa kifo ametenda uhalifu,&#8221; aliiambia IPS. <\/p>\n<p>Ujumbe kutoka Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Af&#341;ika unaotembelea nchini humo hivi ka&#341;ibuni ulitoa wito kwa Zambia kukomesha hukumu ya kifo; hata hivyo, kamishina Pansy Tlakula pia alibainisha, Ap&#341;ili 18, kuwa ujumbe huo umevutiwa na ukweli kwamba nchi hiyo haijanyonga mfungwa yoyote yule katika miaka ya ka&#341;ibuni (mfungwa aliyenyongwa ka&#341;ibuni zaidi ni mwaka 1997). <\/p>\n<p>Kwa kujibu hoja, Mike Mulongoti, wazi&#341;i wa haba&#341;i na utangazaji, alisema ni Mkutano wa Katiba wa Taifa ambao hatimaye utatoa maamuzi juu ya jambo hilo. <\/p>\n<p>Tangu uhu&#341;u mwaka 1964, watu 53 wanaaminika kunyongwa hadi kufa nchini Zambia. <\/p>\n<p>Mwaka 2004, Rais Levy Mwanawasa aliahidi kutokutia saini vibali vya kunyongwa akiwa mada&#341;akani; alichaguliwa tena mwaka jana kwa kipindi cha miaka sita tena.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>LUSAKA, Mei 20 (IPS) &ndash; Ombi la kawaida kwa wale wanaosubi&#341;i kunyongwa katika ge&#341;eza lenye msongamano mkubwa wa wafungwa nchini Zambia ni kwa Mungu kuingilia kati kukomesha mateso yao hapa duniani na kumtaka mnyongaji anayesubi&#341;i kufanya kazi yake hiyo aje kuifanya kwa ha&#341;aka, kulingana na taa&#341;ifa ya hivi ka&#341;ibuni kutoka kwa mahabusu. &#8220;Inauma mno kuwa&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":340,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-2158","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/2158","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/340"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=2158"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/2158\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=2158"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=2158"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=2158"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}