{"id":2154,"date":"2008-05-20T13:40:01","date_gmt":"2008-05-20T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2008\/05\/20\/biashara-malawi-mtikisiko-kutokana-na-kushuka-kwa-bei-ya-tumbaku\/"},"modified":"2008-05-20T13:40:01","modified_gmt":"2008-05-20T13:40:01","slug":"biashara-malawi-mtikisiko-kutokana-na-kushuka-kwa-bei-ya-tumbaku","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2008\/05\/20\/biashara-malawi-mtikisiko-kutokana-na-kushuka-kwa-bei-ya-tumbaku\/","title":{"rendered":"BIASHARA&ndash;MALAWI: Mtikisiko Kutokana na Kushuka kwa bei ya Tumbaku"},"content":{"rendered":"<p>LILONGWE, Mei 15 (IPS) &ndash; Sekta ya tumbaku ya Malawi imekuwa katika mtikisiko baada ya kushuka kwa kiasi kikubwa kwa bei kulikotokana na wakulima kuendesha mgomo kushinikiza kufungwa kwa minada ya kuuzia zao hilo.\n<\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>Mauzo ya tumbaku mwaka huu yalianza kwa kishindo kikubwa kutokana na bei kufikia kiwango ambacho hakijawahi kufikiwa cha dola 11 kwa kilo. Bei ambayo, hata hivyo, haikudumu kwa muda m&#341;efu. <\/p>\n<p>Minada ya tumbaku ilifunguliwa nchini Malawi katika mji mkuu wa Lilongwe mwezi Machi huku kilo ya tumbaku ikiuzwa kati ya dola sita na kumi na moja. Hii ilileta matumaini kwa wakulima ambao walikabiliana na ugumu wa kupata faida kutokana na biasha&#341;a hiyo miaka michache iliyopita. <\/p>\n<p>Kufutwa kwa &#341;uzuku kwa wazalishaji wa tumbaku wa Malawi kwa miaka kadhaa iliyopita kumemaanisha kuwa wakulima wanapaswa kulipia gha&#341;ama zote za uzalishaji.<\/p>\n<p>Inagha&#341;imu kwa mkulima wa wastani wa tumbaku dola moja kuweza kuzalisha mazao yanayoweza kutoa kilo moja, kulingana na wiza&#341;a ya kilimo ya Malawi. Lakini kwa wengi, bei zilibadilika kati ya senti 70 na 90 kwa kilo. <\/p>\n<p>Hii ilisababisha mzigo mkubwa zaidi wa madeni kwa wakulima kutokana na kushindwa kulipia madeni kununulia pembejeo. Wakulima wengi wamepunguza uzalishaji na wengine wameamua kuchanganya shughuli tofauti za kiuchumi. <\/p>\n<p>Halafu mata&#341;ajio ya kupanda kwa bei yalijitokeza. Godwin Ludzu, mkulima kutoka wilaya ya kati ya Malawi ya Kasungu, alikuwa miongoni mwa watu waliopata bahati ambaye aliuza hadi &#341;obota 30 za tumbaku kwa dola 10 kwa kilo katika siku za kwanza za biasha&#341;a. Alijawa na fu&#341;aha kuhusu faida aliyotengeneza. <\/p>\n<p>&#8221;Bei ilikuwa nzu&#341;i mno. Nitaweza kulipia madeni yote niliyochukua wakati wa uzalishaji wa tumbaku,&#8221; alisema Ludzu. Amekuwa akipanda tumbaku kwa miaka sita. Bei za mnadani mwaka huu ni nzu&#341;i kuwahi kuzipata. <\/p>\n<p>Hata hivyo, bei ambazo siyo za kawaida hazikuwepo. Katika siku ya pili, matumaini yalimalizika. Bei zimeshuka, huku thamani ya jani ikishuka kati ya dola 2.30 na senti 60 kwa zao lenye ubo&#341;a kama huo. <\/p>\n<p>Godf&#341;ey Chapola, meneja mkuu wa Tume ya Kudhibiti Tumbaku (TCC) iliyoanzishwa kishe&#341;ia alithibitisha kuwa bei zilianza kuwa kubwa kwasababu ya uhaba wa tumbaku katika soko la dunia. Alisema kuwa baadhi ya nchi ambazo zilipanda tumbaku zimeacha kupanda zao hilo wakati nyingine zilipunguza kiwango cha uzalishaji, na kusababisha matumizi kuwa makubwa mno kuliko usambazaji. <\/p>\n<p>Kushuka kwa bei kumeathi&#341;i wakulima vibaya sana. Champhi&#341;a Gondwe, mkulima katika wilaya ya kaskazini ya Rumphi, alikwenda katika minada ya Mzuzu kaskazini mwa Malawi. Hakuweza kuuza mazao yake yoyote yale kwasababu alikuta kuwa bei za tumbaku zilikuwa ndogo mno. <\/p>\n<p>&#8221;(Bei ya Juu) imebakia katika dola 2.30. Sikuweza ku&#341;uhusu mazao yangu niliyozalisha kwa shida kununuliwa kwa bei hiyo ndogo wakati wenzetu mjini Lilongwe waliuza tumbaku kwa dola 10,&#8221; alisema Gondwe. <\/p>\n<p>Minada ya Mzuzu ilifungwa Ap&#341;ili 14 baada ya ghasia kufumuka kati ya wakulima na walinzi wa soko hilo. Wakulima walifungia wanunuzi wasiendelee na mauzo. Halafu TCC iliahi&#341;isha mauzo. <\/p>\n<p>Wakulima hawakuwa taya&#341;i kuondoka kutokana na madai yao ya kutaka bei ya juu baada ya kusikia kuna uhaba wa tumbaku duniani kote. <\/p>\n<p>Uuzaji wa tumbaku uliahi&#341;ishwa katika minada yote minne mwezi Ap&#341;ili lakini minada hiyo ilifunguliwa tena wiki iliyopita. <\/p>\n<p>Rais Bingu wa Mutha&#341;ika mwenyewe akiwa mkulima wa tumbaku, na ameshutumu wanunuzi kutokana na kuweka bei juu lakini makampuni hayo ya ununuzi &ndash; kutoka Ma&#341;ekani na Uswis &ndash; yamekanusha madai hayo. <\/p>\n<p>Taifa hilo la kusini mwa Af&#341;ika linaongoza kusafi&#341;isha nje tumbaku, kwa kusafi&#341;isha asilimia tano za jumla ya tumbaku inayosafi&#341;ishwa kwenda nje duniani na asilimia mbili ya jumla ya uzalishaji katika saya&#341;i. Kulingana na Benki ya Dunia, Malawi inazalisha baadhi ya asilimia 20 ya jumla ya tumbaku ya mi&#341;aba minne duniani. <\/p>\n<p>Nchi hiyo inapata mapato yake ya fedha za kigeni inayoka&#341;ibia asilimia 70 kutokana na kilimo, na sekta ya tumbaku inachangia asilimia 15 ya pato la taifa kwa mwaka. Watu wapatao milioni mbili kati ya wakazi milioni 13 nchini humo wanategemea tumbaku na sekta zinazohusiana nayo kwa ajili ya kuendesha maisha yao. <\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>LILONGWE, Mei 15 (IPS) &ndash; Sekta ya tumbaku ya Malawi imekuwa katika mtikisiko baada ya kushuka kwa kiasi kikubwa kwa bei kulikotokana na wakulima kuendesha mgomo kushinikiza kufungwa kwa minada ya kuuzia zao hilo. Mauzo ya tumbaku mwaka huu yalianza kwa kishindo kikubwa kutokana na bei kufikia kiwango ambacho hakijawahi kufikiwa cha dola 11 kwa&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":285,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-2154","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/2154","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/285"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=2154"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/2154\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=2154"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=2154"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=2154"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}