{"id":2149,"date":"2008-05-15T13:40:01","date_gmt":"2008-05-15T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2008\/05\/15\/kusini-mwa-afrika-maji-hayathaminiwi-na-hayapewi-heshima-ya-kutosha\/"},"modified":"2008-05-15T13:40:01","modified_gmt":"2008-05-15T13:40:01","slug":"kusini-mwa-afrika-maji-hayathaminiwi-na-hayapewi-heshima-ya-kutosha","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2008\/05\/15\/kusini-mwa-afrika-maji-hayathaminiwi-na-hayapewi-heshima-ya-kutosha\/","title":{"rendered":"KUSINI MWA AFRIKA: Maji &#8220;Hayathaminiwi na Hayapewi Heshima ya Kutosha&#8221;"},"content":{"rendered":"<p>MASERU, Mei 14 (IPS) &ndash; Mkutano wa siku mbili wa masuala ya maji katika Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Af&#341;ika (SADC), ambao ulifunguliwa Jumatano mjini Mase&#341;u, Lesotho, umeshuhudia wawakilishi wa se&#341;ikali, vyama vya ki&#341;aia, sekta binafsi, wafadhili na mashi&#341;ika mengine kujadili madha&#341;a yanayoweza kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa katika maendeleo ya kanda hiyo.\n<\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>Mzungumzaji mkuu To&#341;kil J&oslash;nch&ndash;Clausen alisisitiza kuwa ufumbuzi unaowezekana ulihitajika kusaidia mataifa kutekeleza haya: &#8220;&#8230;mabadiliko ya hali ya hewa ni changamoto ya nyongeza katika kufikia Malengo ya Maendeleo ya Milenia,&#8221; alisema. &#8220;Tunapaswa kukabiliana na changamoto&#8230;&#8221; <\/p>\n<p>Malengo saba, au MDGs, yalikubaliwa na viongozi wa dunia katika Mkutano wa Kilele wa Milenia mwaka 2000 katika jitihada za kuinua hali ya maisha duniani kote ifikapo mwaka 2015. Lengo la saba la MDG, juu ya mazingi&#341;a endelevu, linataka mataifa husika kupunguza nusu ya idadi ya watu ambao hawana maji safi. <\/p>\n<p>Kulingana na takwimu za ka&#341;ibuni kutoka P&#341;og&#341;amu ya Pamoja ya Kufuatilia Ugavi wa Maji na Usafi wa Mazingi&#341;a, ambayo ipo chini ya Shi&#341;ika la Afya Ulimwenguni na Shi&#341;ika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa, asilimia 40 ya watu katika Af&#341;ika Kusini mwa Jangwa la Saha&#341;a hawana maji safi na ya kutosha. Takwimu hizo, kutoka mwaka 2004, pia zinaonyesha kuwa watu wanaoishi katika maeneo ya kijijini wana maisha mabaya zaaidi kuliko wale wa mijini: ni asilimia 26 tu ya Waaf&#341;ika katika maeneo ya kijijini wana maji safi, ikilinganishwa na asilimia 55 ya wakazi wa mijini. <\/p>\n<p>Waka&#341;ti idadi hiyo kwa ujumla wake ni nzu&#341;i Kusini mwa Af&#341;ika &ndash; huku Botswana ikiwa na asilimia 95, na Af&#341;ika Kusini ikiwa na asilimia 88 &ndash;&ndash; Zambia na Angola zikiwa na asilimia 58 na 53 inaonyesha kanda hiyo bado ina umbali wa kwenda kabla ya kusambaza maji salama kwa wananchi wake wote. Msumbiji, ikiwa katika asilimia 43, ina kiwango cha chini zaidi cha watu wenye maji safi na salama katika SADC &ndash; pamoja na kwamba takwimu hii inaonyesha kubo&#341;eka kutoka asilimia 36 mwaka 1990.<\/p>\n<p>Kulingana na Umoja wa Mataifa, vikwazo vya kusambaza maji safi katika Af&#341;ika Kusini mwa Jangwa la Saha&#341;a ni pamoja na ongezeko la watu, kipaumbele cha chini kinachotolewa katika usimamiaji wa maji na usafi wa mazingi&#341;a, na kushindwa kwa ma&#341;a kwa ma&#341;a kwa mifumo ya kusambaza maji. <\/p>\n<p>J&oslash;nch&ndash;Clausen ni mhandisi wa Denma&#341;k na mtafiti ambaye anashau&#341;i mashi&#341;ika ambayo yalikutana wiki hii katika mkutano, Shi&#341;ika la Mazingi&#341;a la Umoja wa Mataifa na Ushi&#341;ikiano wa Maji wa Kimataifa: lenye makao yake mjini Stockholm ambalo linahusisha se&#341;ikali, makampuni na mashi&#341;ika ya maendeleo &ndash; miongoni mwa wengine &ndash; kusaidia kufikia mahitaji ya maji na kubo&#341;esha usimamiaji wa &#341;asilimali. <\/p>\n<p>Alisema kuna kiasi kadhaa za ufumbuzi uliopo kusaidia wanajamii kukabiliana na hali wakati upatikanaji wa maji unapopungua, na kwamba se&#341;ikali inapaswa kuangalia juu ya uwiano wa maji kuweza kufikia mahitaji ya viwandani, kilimo na matumizi ya majumbani. Bei mpya za maji, matumizi makubwa ya &#341;asilimali na kuanzishwa kwa mazao yanayostahimili ukame kunaweza kusaidia. <\/p>\n<p>Maieane Khaketla, afisa uhusiano mkuu wa Wiza&#341;a ya maliasili ya Lesotho, ambaye alifungua mkutano huo, pia alizungumzia suala la mahitaji makubwa ya maji &ndash; akisema kuwa changamoto kubwa zaidi ya kufikia malengo ya maendeleo ni kuhakikisha kuwa wananchi wanapata maji kwa ajili ya mahitai yao ya lazima, wakati huo huo kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya &#341;asilimali hiyo kutoka viwandani na katika sekta za kilimo. <\/p>\n<p>Kutokana na mataifa kadhaa katika kanda kupanga kuongeza uzalishaji wa nishati ya maji kufikia mahitaji yao ya nishati ya baadaye, Belinda Pet&#341;ie wa Shi&#341;ika la Dunia Moja ya Uwekezaji Endelevu alitaka kuchukuliwa kwa tahadha&#341;i kwa suala hilo: &#8220;Ni faida gani ya kuwekeza katika mitambo mikubwa ya nishati ya maji ambayo katika siku chache za baadaye haitakuwa na maji &#8221; Shi&#341;ika la Dunia Moja ya Uwekezaji Endelevu linatoa ushau&#341;i wa kitaalam nchini Af&#341;ika Kusini katika maendeleo endelevu. <\/p>\n<p>Alisema jibu la kuwepo kwa mvua zisizokuwa na uhakika lingekuwa ni kujenga mitambo ya nishati ya maji, na kwamba se&#341;ikali zinapaswa kuangalia njia mbadala za kupata nishati kama vile nishati ya upepo. <\/p>\n<p>Pete Ashton, mwanaikolojia ya maji kutoka Ba&#341;aza la Utafiti wa Sayansi na Viwanda la Af&#341;ika Kusini, aliuambia mkutano huo kuwa ili kuzuia mgongano na kubo&#341;esha usimamiaji wa maji, mataifa ya Kusini mwa Af&#341;ika yanapaswa kukabiliana na masuala dhaifu kama vile udhibiti wa mabonde ya maji, ma&#341;a moja. Mito ya O&#341;ange, Limpopo na Zambezi ni miongoni mwa &#341;asilimali kubwa za maji katika kanda. <\/p>\n<p>Ashton pia alisema kuwa kuna haja ya kuchukuliwa hatua za ha&#341;aka za kuanza kutumia vyanzo mbadala vya maji kama vile kuvuna maji ya mvua, na teknolojia mpya za &#341;asilimali hizi endelevu. <\/p>\n<p>&#8220;Tunapaswa kubo&#341;esha jinsi tunavyoelewa thamani ya maji,&#8221; aliona. &#8220;Hayathaminiwi na hayapewi heshima ya kutosha.&#8221;<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>MASERU, Mei 14 (IPS) &ndash; Mkutano wa siku mbili wa masuala ya maji katika Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Af&#341;ika (SADC), ambao ulifunguliwa Jumatano mjini Mase&#341;u, Lesotho, umeshuhudia wawakilishi wa se&#341;ikali, vyama vya ki&#341;aia, sekta binafsi, wafadhili na mashi&#341;ika mengine kujadili madha&#341;a yanayoweza kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa katika maendeleo ya kanda hiyo&#8230;.<\/p>\n","protected":false},"author":472,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-2149","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/2149","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/472"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=2149"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/2149\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=2149"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=2149"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=2149"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}