{"id":2137,"date":"2008-05-08T13:40:01","date_gmt":"2008-05-08T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2008\/05\/08\/haki-nchini-afika-kusini-wakimbizi-wa-zimbabwe-wanakuta-utakaso-na-makosa\/"},"modified":"2008-05-08T13:40:01","modified_gmt":"2008-05-08T13:40:01","slug":"haki-nchini-afika-kusini-wakimbizi-wa-zimbabwe-wanakuta-utakaso-na-makosa","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2008\/05\/08\/haki-nchini-afika-kusini-wakimbizi-wa-zimbabwe-wanakuta-utakaso-na-makosa\/","title":{"rendered":"HAKI: Nchini Af&#341;ika Kusini, Wakimbizi wa Zimbabwe Wanakuta Utakaso na Makosa"},"content":{"rendered":"<p>JOHANNESBURG, Mei 4 (IPS) &ndash; Wakati jua la msimu wa vuli likizama katika jiji maa&#341;ufu zaidi nchini Af&#341;ika Kusini, Kumbi ya Misheni ya Cent&#341;al Methodist jijini Johannesbu&#341;g imejaa su&#341;a zenye huzuni kubwa, wengi wakiwa mbali na nyumbani, wakitafuta fu&#341;aha katika kuta zake.\n <\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>Katika kila inchi moja ya nafasi katika sakafu za misheni hiyo &ndash; na nje ya ko&#341;ido &ndash; maskini wanatafuta makazi jinsi wanavyopenda kutoka kwenye upepo wa ba&#341;idi ambao unasafi&#341;i kati ya majengo ma&#341;efu katika jiji hili. Wanaochangamana nao katika kila usiku ni mamia ya wakimbizi kutoka ji&#341;ani wa kaskazini wa Af&#341;ika Kusini, Zimbabwe, ambao wamekimbia nchi yao kutokana na mgogo&#341;o wa kisiasa na kiuchumi. <\/p>\n<p>&#8220;Tunalala nje mitaani. Ma&#341;a nyingi tunatumia siku kadhaa bila kula kitu chochote; tunatumia wiki bila kufanya kazi,&#8221; anasema Owen Muchanyo, mwalimu wa shule ya sekonda&#341;i mwenye um&#341;i wa miaka 23 ambaye anafundisha hisabati na sayansi kutoka Chitungwiza, mji kusini mwa mji mkuu wa Zimbabwe, Ha&#341;a&#341;e. <\/p>\n<p>Amekuwa akiishi nchini Af&#341;ika Kusini kwa miezi mitatu. &#8220;Ni vema kulala mitaani, ambapo maisha yangu ni salama kwa kiasi fulani, kuliko kulala katika nyumba ambapo maisha yangu yanakuwa hata&#341;ini.&#8221; <\/p>\n<p>Idadi kubwa ya wale ambao wanajikuta mjini Johannesbu&#341;g wana maa&#341;ifa yanayohitajika kusaidia kuvuta nchi yao kutoka kwenye makapi. <\/p>\n<p>&#8220;Kuna wasomi hapa ambao wanaweza kusaidia kuendeleza nchi yao, lakini tunakuja hapa kuteseka kutokana na kwamba mtu mmoja nchini Zimbabwe na huyo ni Robe&#341;t Mugabe,&#8221; anasema Raymond Chingoma, mchambuzi wa siasa mwenye um&#341;i wa miaka 32 kutoka Ha&#341;a&#341;e ambaye aliwasili Johannesbu&#341;g Septemba 2007, akimaanisha &#341;ais wa muda m&#341;efu wa Zimbabwe. <\/p>\n<p>Zimbabwe imekuwa katika hali ya utata kwa zaidi ya mwezi sasa ikisubi&#341;i kutangazwa kwa matokeo ya u&#341;ais, ambayo yaligombaniwa zaidi na Mugabe dhidi ya kiongozi wa zamani wa vyama vya wafanyakazi Mo&#341;gan Tsvangi&#341;ai. Uchaguzi Mkuu ulifanyika Machi 29. <\/p>\n<p>Hatimaye maafisa wa uchaguzi walitangaza Ijumaa kuwa kati ya wanaume hao wawili hakuna aliyepata zaidi ya asilimia 50 ya ku&#341;a, na kumaanisha ku&#341;udiwa kwa uchaguzi katika kipindi cha wiki tatu zijazo. <\/p>\n<p>Katikati mwa kuchelewa kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa &#341;ais, kikundi kikubwa cha Movement fo&#341; Democ&#341;atic Change (MDC) &ndash; kinachoongozwa na Tsvangi&#341;ai &ndash; waliungana kunyima chama cha Mugabe cha Zimbabwe Af&#341;ican National Union&ndash;Pat&#341;iotic F&#341;ont (ZANU&ndash;PF) kuwa na wabunge wengi kwa kipindi cha miaka 28. <\/p>\n<p>Mugabe, ambaye alisemekana kwa waangalizi kuwa aliiba uchaguzi wa mwaka 2002 ambao baadhi wanaamini Tsvangi&#341;ai alishinda, sasa anasimama kutuhumiwa kutokana na kutumia se&#341;ikali na chama kuendesha mashambulizi ya kikatili dhidi ya wale ambao wanaweza kuwapinga, mbinu ambayo wakosoaji wanasema wameizoea kwa muda m&#341;efu. <\/p>\n<p>&#8220;Nimekuwa nikiunga mkono chama cha upinzani na wakati wa uchaguzi ulikuja na hivyo ikabidi niondoke kutokana na kwamba niliogopa ghasia za ZANU&ndash;PF dhidi ya wafuasi wa upinzani,&#8221; Muchanyo anaendelea. &#8220;Familia yangu ilipigwa kutokana na kwamba wengi wao ni wafuasi wa MDC. Vijana wa ZANU&ndash;PF walikuja kuvamia nyumbani kwetu, walimchukua kila mmoja nje, na kupiga kila mmoja.&#8221; <\/p>\n<p>Chitungwiza, mji ambao Muchanyo anaishi, umekuwa ngome kuu ya MDC na ni miongoni mwa maeneo ambayo yaliathi&#341;ika zaidi wakati wa Opa&#341;eseheni ya Mu&#341;ambatsvina mwaka 2005, &#8220;mu&#341;ambatsvina&#8221; inatafsi&#341;iwa kama &#8220;&#341;ejesha uta&#341;atibu&#8221; na &#8220;ondoa taka&#8221;. <\/p>\n<p>Vitendo vya polisi vilikuwa na lengo la kuondoa makazi yasiyopangwa, opa&#341;esheni hizo zilisemekana hadi Julai 2005 kuwaacha kwa uchache watu 700,000 bila makazi,kulingana na &#341;ipoti ya Umoja wa Mataifa. <\/p>\n<p>Kwa upande wake, kikundi cha haki za binadamu cha Zimbabwe cha Sokwanele kiliita uvamizi huo kama &#8220;K&#341;istallnacht ya Zimbabwe&#8221;, kwa maana ya kitendo cha kuangamiza mali za Kiyahudi mwaka 1939 kilichofanywa na wahuni wa Kinazi nchini Uje&#341;umani, wakati Taasisi ya Affo&#341;dable Housing yenye makao yake mjini Boston iliita Opa&#341;esheni Mu&#341;ambatsvina kama &#8220;mauaji ya halaiki kwa kutumia tingatinga&#8221;. <\/p>\n<p>Uzoefu wa Muchanyo siyo wa kipekee. Mwezi Machi 2007, uso uliovimba wa Tsvangi&#341;ai ulionyeshwa katika magazeti duniani kote baada ya yeye na wafuasi kadhaa walipokamatwa na kuteswa na polisi wa kuzuia ghasia. <\/p>\n<p>&#8220;Baadhi ya mambo ambayo nayasikia katika ofisi hii, usiku kwa usiku, katika kiti kile ambapo umeketi, niambie nifiki&#341;i kuwa tumepata taabu kubwa,&#8221; anasema Askofu Paul Ve&#341;&#341;yn, ambaye anaongoza Misheni ya Cent&#341;al Methodist na kuongoza huduma za kanisa na p&#341;og&#341;amu nyingine za mahubi&#341;i kwa Wazimbabwe. <\/p>\n<p>&#8220;Najiuliza ni kwa nini wameondoka katika nchi yao halafu wanaanza kwa litugia: &#8216;nilipigwa, nimeteswa, nilipigwa katika madonda ya mguuni mwangu, nina maje&#341;aha mgongoni, siwezi kulala usiku kutokana na ndoto&#8217;,&#8221;. <\/p>\n<p>Maoni ya watu ndani ya misheni hiyo yanalingana kwa ka&#341;ibu na yale ya Rais wa Af&#341;ika Kusini Thabo Mbeki ambaye, alipotembelea Ha&#341;a&#341;e mwezi Ap&#341;ili, alisisitiza kuwa kulikuwa &#8220;hakuna mgogo&#341;o&#8221; nchini Zimbabwe. <\/p>\n<p>Vivyo hivyo Wazimbabwe wanaowasili nchini Af&#341;ika Kusini ma&#341;a nyingi wanapewa mapokezi ambayo ni chini ya kuka&#341;ibishwa. <\/p>\n<p>Katika jioni ya Janua&#341;i 30 kama saa tano usiku kwa saa za Af&#341;ika Kusini, misheni hiyo ilivamiwa na maafisa kadhaa kutoka Taasisi ya Polisi ya Af&#341;ika Kusini (SAPS) ambao walidaiwa kusaka silaha, &#341;isasi na madawa ya kulevya &ndash; kutokana na wafanyabiasha&#341;a wa ndani kulalamika kuwa njia ya Byzantine imekuwa maficho ya wahuni. <\/p>\n<p>Kulingana na baadhi ya watu ambao walikuwepo usiku huo, polisi waliwapiga watu kadhaa vibaya sana, kuha&#341;ibu mali na kuiba vitu vingine; baadhi ya watu 300 walipelekwa jela. <\/p>\n<p>Elizabeth Cheza, mwenye um&#341;i wa miaka 29 ambaye alifanya kazi kama mwingizaji wa takwimu na mfanyakazi wa kujitolea wa MDC kabla ya kuondoka nchini Zimbabwe mwaka 2005, aliamshwa na afisa polisi mbele ya mtutu wa bunduki na kumkemea kwa lugha ya Kizulu akimtaka kuamka. Akielezea hadithi hiyo katika chumba kidogo katika misheni hiyo ambacho anakaa pamoja na &#341;afiki wake wa kike na binti wa miezi 11 wa mama huyo, Cheza anaelezea uzoefu wake wa usiku huo. <\/p>\n<p>&#8220;Hali ilikuwa ngumu, nilipokuwa ninalala nimekuwa nikijifunika na kanga yangu,&#8221; anasema. &#8220;Nilipoamka, yeye (afisa polisi) alinipiga kofi kama vile nimechukua muda wake mwingi. Nilificha uso wangu na kanga hiyo niliyokuwa nimeishika ilianguka, hapo nikawa uchi mbele ya mwanaume.&#8221; <\/p>\n<p>Ve&#341;&#341;yn, vete&#341;ani wa ha&#341;akati dhidi ya ubaguzi wa &#341;angi nchini Af&#341;ika Kusini, anasema pia alipigwa wakati wa uvamizi na kuona watu wakitokwa na damu baada ya kupigwa na polisi. Anaona tukio hilo kama ku&#341;udisha nyuma jamii ambayo Af&#341;ika Kusini imeanza kuijenga baada ya ubaguzi wa &#341;angi. <\/p>\n<p>&#8220;Tumekuwa na polisi hapa wakati ambapo wamekuwa wakifanya kazi vizu&#341;i jinsi wanavyokabiliana na hali, jinsi wanavyotatua migogo&#341;o: wamekuwa wakikabiliana ma&#341;a moja na kuwa na shabaha,&#8221; anasema Ve&#341;&#341;yn. &#8220;Lakini kuna upande mwingine wa polisi, na huu ni umabavu, ni kukomaa, ni wa kijinga, hausikilizi na ni wa kidikteta. Ni kila kitu ambacho usingekipenda.&#8221; <\/p>\n<p>Kwa upande wao polisi wanasema kuwa walichukua hatua kutokana na taa&#341;ifa nzu&#341;i walizopata na kwamba kuna fu&#341;sa ya kuchukua hatua za kishe&#341;ia kwa wale wanaoona hawajatendewa haki. <\/p>\n<p>&#8220;Tulikuwa na taa&#341;ifa kuwa pale palikuwa ni eneo ambalo watu wangeweza kufanya upo&#341;aji na kukimbilia katika jengo,&#8221; anasema Govindsamy Ma&#341;iemuthoo, mkuu wa mawasiliano wa SAPS katika Jimbo la Gauteng, ambapo Johannesbu&#341;g inapatikana. &#8220;Mtu yoyote yule ambaye aliona kuwa haki zake zilikiukwa (wakati wa upekuzi) angeweza kutoa taa&#341;ifa kwa kituo cha polisi cha kati, ambapo suala hilo litachunguzwa.&#8221; <\/p>\n<p>Kituo cha She&#341;ia, kliniki ya she&#341;ia kwa ajili ya umma kilichopo mjini Johannesbu&#341;g, kilichukua kesi ya watu waliowekwa kizuizini, na hatimaye kufanikiwa kuwaachia baada ya wiki za kugombana na hakimu. <\/p>\n<p>Katika uamuzi wa kutoa am&#341;i ya kuachiwa kwa waliowekwa kizuizini ambao walifananishwa na enzi za ubaguzi wa &#341;angi, Mahakama Kuu ya Af&#341;ika Kusini ilifananisha kitendo cha polisi na kuswekwa jela kwa wakimbizi kama kukumbusha zamani &#8220;za baadhi ya masuala ambayo yaliwapata baadhi ya watu wa fani yetu miaka 20 iliyopita&#8221; na kukosoa polisi na hakimu kutokana na &#8220;ukatili na kuwatendea ukatili binadamu.&#8221; <\/p>\n<p>Ujumbe wa mahakama ni kwamba wakimbizi wa Zimbabwe katika Misheni ya Cent&#341;al Methodist wanapaswa kusikilizwa zaidi. <\/p>\n<p>&#8220;Wanatuchukulia kama sisi siyo maji&#341;ani wao, lakini kama wanyama,&#8221; anasema Chingoma, wakati akijiandaa kuzunguka kwenye ko&#341;ido za misheni hiyo kutafuta mahali pa kulala usiku. &#8220;Hawatutendei vema. Unapokwenda na kuwaambia unataka aji&#341;a, wanakutendea kama vile wewe siyo Mwaf&#341;ika, na hivyo unastahili kuteseka. Lakini hatupaswi kutendewa hivyo.&#8221; <\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>JOHANNESBURG, Mei 4 (IPS) &ndash; Wakati jua la msimu wa vuli likizama katika jiji maa&#341;ufu zaidi nchini Af&#341;ika Kusini, Kumbi ya Misheni ya Cent&#341;al Methodist jijini Johannesbu&#341;g imejaa su&#341;a zenye huzuni kubwa, wengi wakiwa mbali na nyumbani, wakitafuta fu&#341;aha katika kuta zake. Katika kila inchi moja ya nafasi katika sakafu za misheni hiyo &ndash; na&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":326,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-2137","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/2137","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/326"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=2137"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/2137\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=2137"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=2137"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=2137"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}