{"id":2125,"date":"2008-04-25T13:40:01","date_gmt":"2008-04-25T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2008\/04\/25\/maendeleo-mgongano-wa-maoni-katika-unctad-juu-ya-nini-boa-kwa-afika\/"},"modified":"2008-04-25T13:40:01","modified_gmt":"2008-04-25T13:40:01","slug":"maendeleo-mgongano-wa-maoni-katika-unctad-juu-ya-nini-boa-kwa-afika","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2008\/04\/25\/maendeleo-mgongano-wa-maoni-katika-unctad-juu-ya-nini-boa-kwa-afika\/","title":{"rendered":"MAENDELEO: Mgongano wa Maoni Katika UNCTAD Juu ya Nini Bo&#341;a kwa Af&#341;ika"},"content":{"rendered":"<p>ACCRA, Ap&#341;ili 23 (IPS) &ndash; &#8221;Af&#341;ika siyo kikapu kitupu. Ba&#341;a linakabiliwa na matukio ambayo halina uwezo wa kuyadhibiti.&#8221;<\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>Haya ni maneno ya Ekplom Afeke, mwanaha&#341;akti wa Togo ambaye anahudhu&#341;ia mkutano wa 12 wa Taasisi ya Biasha&#341;a na Maendeleo ya Umoja wa Mataifa (UNCTAD) ambao kwa sasa unaendelea katika mji mkuu wa Ghana, Acc&#341;a. <\/p>\n<p>Afeke anasema ba&#341;a limenyimwa biasha&#341;a na uwekezaji katika miongo sasa. Kama hilo halijawa baya, madha&#341;a ya usimamizi mbovu wa mazingi&#341;a nje ya ba&#341;a kwa sasa yanazunguka mgogo&#341;o wa umaskini ba&#341;ani Af&#341;ika. <\/p>\n<p>Yeye hayupo peke yake katika mgogo&#341;o huo. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki&ndash;Moon, ambaye ni mwenyekiti wa mkutano huo, ameelezea kuchanganyikiwa kwake katika kupuuzwa kunakofanywa na jumuiya ya kimataifa kuongeza biasha&#341;a na uwekezaji katika Af&#341;ika. <\/p>\n<p>Alitoa mfano wa &#8221;faida ya utandawazi, hususani kuongezeka kwa biasha&#341;a na vitega uchumi&#8221;, ambavyo anadai ni motisha wa uhakika katika maendeleo ya muda m&#341;efu na maendeleo ya binadamu, &#8221; bado hatuna faida yoyote ile kwa Af&#341;ika&#8221;. <\/p>\n<p>Sehemu ya biasha&#341;a ya kimataifa ya Af&#341;ika na vitega uchumi kutoka nje ni asilimia tatu tu. &#8221;Njia ya uhakika ya kukuza takwimu hii ni kwa kuhakikisha kupatikana kwa maamuzi ya ha&#341;aka katika Mazungumzo ya Doha (katika mazungumzo ya biasha&#341;a ya kimataifa), ambayo ni muhimu mno katika maendeleo na miundombinu kwa njia ya misaada kwa ajili ya biasha&#341;a&#8221;, Ban aliuambia mkutano. <\/p>\n<p>Katika muongo uliopita se&#341;ikali za Af&#341;ika zimefaidika kutokana na ongezeko la bei za bidhaa, kuongezeka kwa matumizi yao katika Lengo la Maendeleo ya Milenia (MDG) kukuza maendeleo mapana. <\/p>\n<p>Kwa bahati mabaya, katibu mkuu alisema, &#8221;changamoto ya MDG imefanywa kuwa ngumu zaidi kutokana na ongezeko kubwa la bei za chakula duniani. Bei kubwa zinatishia kuondoa mafanikio yaliyopatikana katika kupambana na njaa na utapiamlo &#8220;. <\/p>\n<p>Afeke alisema, &#8221;angalia suala la ongezeko la joto duniani na madha&#341;a yake katika Af&#341;ika na utatambua kuwa ba&#341;a kwa ma&#341;a nyingine tena linafanywa kuteseka kutokana na jambo ambalo halijaanzisha,&#8221;. <\/p>\n<p>Katibu Mkuu anaonekana kukubaliana na Afeke alipowaambia wajumbe kuwa, &#8221;mabadiliko ya hali ya hewa ni eneo jingine linalozidisha wasiwasi katika Af&#341;ika. Watu wa ba&#341;a hili, ambao wamechangia kiasi kidogo mno katika tatizo hili, hawawezi kuta&#341;ajiwa kubeba mzigo huu wenyewe.&#8221; <\/p>\n<p>Katibu Mkuu wa UNCTAD Supachai Panitchpakdi alikosoa maendeleo yanayotokana na bidhaa alipokuwa akihutubia wajumbe. <\/p>\n<p>Hata kama biasha&#341;a kati ya mataifa yanayoendelea imeongezeka ma&#341;a tatu kati ya mwaka 1995 na 2005, &#8221;utendaji wa mataifa yanayoendelea kwa ujumla katika miaka ya ka&#341;ibuni na maendeleo katika mataifa yenye maendeleo duni na uchumi wenye kipato kidogo yamekuwa madogo na yameendelea kuegemea zaidi katika uuzaji nje wa bidhaa zenye thamani ya chini. <\/p>\n<p>Kutokana na histo&#341;ia hii, inakuwa wazi kuwa kiwango cha sasa cha kubo&#341;eka kwa hali ya maisha &#8221;kinakwenda polepole mno kuweza kufikia (MDG) ya kupunguza nusu ya watu maskini zaidi katika dunia ifikapo mwaka 2015&#8221;, alisema Panitchpakdi. <\/p>\n<p>Ban pia anaona kwamba nchi nyingi hazina uwezo wa kufikia malengo haya. Aliitenga Af&#341;ika kama ba&#341;a lililopo katika &#8221;hata&#341;i&#8221; kwasababu &#8221;hakuna nchi hata moja ipo katika hali ya kufikia MDGs zote ifikapo mwaka 2015&#8221;. <\/p>\n<p>Hata hivyo, siyo nchi zote zipo gizani katika Af&#341;ika. Ghana, Kenya, Tanzania na Uganda, kulingana na Ban, zime&#341;ipoti mafanikio katika nyanja mbalimbali za maendeleo. Nchi nyingine kama vile Senegal zimepata mafanikio katika kufikia shabaha ya kutoa maji safi. <\/p>\n<p>Nige&#341;, Togo na Zambia zimepata mafanikio ya kuvutia katika kudhibiti mala&#341;ia kwa kusambaza vyanda&#341;ua. <\/p>\n<p>&#8221;Haba&#341;i hizi za mafanikio zinapaswa kuigwa na kuenezwa katika ba&#341;a la Af&#341;ika kwa kupata msaada kutoka kwa jumuiya ya kimataifa,&#8221; aliongeza Ban. <\/p>\n<p>Suala la kusononesha, kampeni ya MDG siyo jitihada ya kimataifa pekee ambayo Af&#341;ika ni sehmu yake. Shi&#341;ika la Uinge&#341;eza la Oxfam, limeonya katika taa&#341;ifa iliyotolewa Ap&#341;ili 21 kuwa Umoja wa Ulaya utafanya &#8221;uha&#341;ibifu usioweza kuka&#341;abatiwa wa hatma ya baadhi ya nchi maskini katika dunia kama haitaondoa mikataba yake ya biasha&#341;a hu&#341;ia ambayo itakamilika mwaka huu&#8221;.<\/p>\n<p>Mikataba hii ya biasha&#341;a ni ile ya ushi&#341;ikiano wa kiuchumi ambayo kwa sasa inajadiliwa, kulingana na Oxfam, &#8221;itaathi&#341;i na kuzo&#341;otesha maendeleo ya watu maskini katika Af&#341;ika, Ca&#341;ibbean na Pacific&#8221;. <\/p>\n<p>Kulingana na Oxfam, uchambuzi wao unaonyesha kuwa &#8221;mikataba hii imezidi mpango wa maendeleo ambao ilitakiwa kufuata. Gha&#341;ama zitakuwa kubwa: upotevu wa mapato kwa mwaka kutokana na kupunguzwa kwa ushu&#341;u wa dola milioni 360 kwa Af&#341;ika pekee na dola nyingine bilioni 9 kutokana na kukubliana kwa mataifa yote yatakayohusika&#8221;. <\/p>\n<p>Lakini wazi&#341;i wa biasha&#341;a ya kimataifa wa Uinge&#341;eza Ga&#341;eth Thomas, ambaye pia alikuwepo katika mkutano wa UNCTAD, alishikilia msimamo wake, akisema kuwa kulikuwa na mahitaji ya ha&#341;aka kukamilisha mikataba ya biasha&#341;a ambayo itawezesha mataifa yanayoendelea &#8221;kufanya biasha&#341;a kwa ajili ya maendeleo na ustawi wao&#8221;. <\/p>\n<p>Alisema, &#8221;tumefikia wiki nyingi kuweza kufanikisha au kuvunja mazungumzo ya biasha&#341;a ya Shi&#341;ika la Biasha&#341;a Duniani (WTO). Kama dunia inataka kufanya jambo bo&#341;a zaidi kwa mataifa maskini, inapaswa kukomesha kulinda masoko yao na kusaini mpango huu siasa&#8221;. <\/p>\n<p>Thomas alisema kuwa &#8221;biasha&#341;a ya usawa ina maana kuondokana na kupiga ma&#341;ufku uuzwaji wa bidhaa nje, kupunguza &#341;uzuku za kilimo ambazo zinaha&#341;ibu biasha&#341;a na kupunguza ushu&#341;u&#8221;. <\/p>\n<p>Wakati hili linapofanikishwa, anaamini kuwa itawezesha &#8221;kusaidia wakulima kuweza kukabiliana na bei za sasa za chakula duniani na kuongeza uzalishaji, lakini hii ni sehemu tu ya ufumbuzi. Pia tunahitaji uwekezaji zaidi katika kuongeza uzalishaji wa kilimo. Kama wakulima wataweza kupata bei za juu, hapo wataweza kuwekeza.&#8221; <\/p>\n<p>Vile vile Ban aliongeza kuwa &#8221;tunahitaji kuongeza kwa kiasi kikubwa matumizi katika kilimo. Hususani, uwekezaji wa biasha&#341;a na vitega uchumi utumike kuleta &#8216;mapinduzi ya kijani&#8217; ya kubo&#341;esha uzalishaji wa kilimo katika Af&#341;ika&#8221;. <\/p>\n<p>Kwa kulinganisha, Afeke anadhani kuwa mikutano ya UNCTAD haijatatua matatizo ya zamani. Ana wasiwais juu ya mustakabli wa baadaye. Hata hivyo, anaona &#8221;baadhi ya dhami&#341;a&#8221; kwa upande wa baadhi ya viongozi, hususani Rais wa B&#341;azil Luiz Inacio &#8221;Lula&#8221; da Silva.<\/p>\n<p>Lula, kama ambavyo ma&#341;a nyingi anajulikana, ameongeza ushi&#341;ikiano wa kimataifa kati ya nchi yake na nchi kadhaa za Af&#341;ika kuongeza uzalishaji wa kilimo. &#8221;Hawa ni watu wanaoona mbali ambao bila ya wao Af&#341;ika isingeweza kuondoka katika mwanzo wake,&#8221; alisema Afeke. <\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>ACCRA, Ap&#341;ili 23 (IPS) &ndash; &#8221;Af&#341;ika siyo kikapu kitupu. Ba&#341;a linakabiliwa na matukio ambayo halina uwezo wa kuyadhibiti.&#8221; Haya ni maneno ya Ekplom Afeke, mwanaha&#341;akti wa Togo ambaye anahudhu&#341;ia mkutano wa 12 wa Taasisi ya Biasha&#341;a na Maendeleo ya Umoja wa Mataifa (UNCTAD) ambao kwa sasa unaendelea katika mji mkuu wa Ghana, Acc&#341;a. Afeke anasema&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":423,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-2125","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/2125","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/423"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=2125"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/2125\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=2125"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=2125"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=2125"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}