{"id":1293,"date":"2006-06-23T13:40:01","date_gmt":"2006-06-23T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2006\/06\/23\/afrika-magharibi-mawazo-tofauti-juu-ya-kuhamishiwa-kwa-chales-taylo-the-hague\/"},"modified":"2006-06-23T13:40:01","modified_gmt":"2006-06-23T13:40:01","slug":"afrika-magharibi-mawazo-tofauti-juu-ya-kuhamishiwa-kwa-chales-taylo-the-hague","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2006\/06\/23\/afrika-magharibi-mawazo-tofauti-juu-ya-kuhamishiwa-kwa-chales-taylo-the-hague\/","title":{"rendered":"AFRIKA MAGHARIBI: Mawazo Tofauti juu ya Kuhamishiwa kwa Cha&#341;les Taylo&#341; The Hague"},"content":{"rendered":"<p>FREETOWN, Juni 20 (IPS) &ndash; Rais wa zamani wa Libe&#341;ia Cha&#341;les Taylo&#341; alipelekwa The Hague, siku ya Jumanne, kukabiliana na hukumu ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu wakati wa vita vya Sie&#341;&#341;a Leone katika miaka ya 1990.\n <\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>Rais wa zamani huyo awali alikuwa akishikiliwa katika mji mkuu wa nchi hiyo wa F&#341;eetown, ambako mahakama ya uhalifu wa kivita inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa imemhukumu kutokana na makosa 11. Mahakama Maalum ya Sie&#341;&#341;a Leone bado inahusika na kumfungulia mashitaka Taylo&#341;, hata kama kuanzia sasa atakuwa kizuizini katika Mahakama ya Wahalifu ya Kimataifa huko Scheveningen, ka&#341;ibu na The Hague. <\/p>\n<p>Taylo&#341; alihamishwa kwa mamlaka ya Ba&#341;aza la Usalama la Umoja wa Mataifa, katika jitihada ya kuima&#341;isha utulivu katika kikanda hiyo. <\/p>\n<p>&#8220;Ni wazi kwamba Cha&#341;les Taylo&#341; bado anaungwa mkono katika ukanda huo. Tunatakiwa kuijenga amani iliyopatikana kuliko kuisamba&#341;atisha,&#8221; mwanadiplomasia wa Uinge&#341;eza mjini F&#341;eetown aliiambia IPS, siku ya Jumanne. <\/p>\n<p>Kiongozi huyo wa zamani alishitakiwa alipokuwa bado yupo mada&#341;akani kwa madai ambayo ni pamoja na kuendesha mauaji, kuaji&#341;i aska&#341;i watoto, udhalilishaji kingono na kushambulia wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa nchini Sie&#341;&#341;a Leone. <\/p>\n<p>Akikabiliwa na shinikizo la kimataifa na vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo ambapo waasi walika&#341;ibia kuingia mji mkuu wa Libe&#341;ia wa Mon&#341;ovia, alikubali kwenda uhamishoni nchini Nige&#341;ia mwezi Agosti 2003 &ndash; lakini alikabidhiwa kwa mahakama ya Sie&#341;&#341;a Leone mwezi Machi mwaka huu. <\/p>\n<p>Taylo&#341; anatuhumiwa kushi&#341;iki kwa kiasi kikubwa katika mauaji ambayo yalitokea nchini Sie&#341;&#341;a Leone mwishoni mwa ka&#341;ne iliyopita. <\/p>\n<p>Mahakama ya kivita inaangalia zaidi kipindi cha kuanzia mwanzoni mwa Novemba 30, 1996. <\/p>\n<p>Hii ni siku ambayo mkataba wa amani ulioshindwa ulisainiwa baina ya se&#341;ikali na waasi wa &#8220;Revolutiona&#341;y United F&#341;ont (RUF)&#8221; ambao walianzisha mapambano Machi 1991, na kufanya mauaji, ubakaji na kukata viungo vya miili ya mamia ya &#341;aia katika vita vilivyodumu kwa miaka 11. Wapiganaji wa RUF walikuwa wakatili sana kutokana na tabia yao ya kukata miguu ya waathi&#341;ika wa vita. <\/p>\n<p>Waasi hao waliingia Sie&#341;&#341;a Leone wakitokea Libe&#341;ia kwa madai ya kuungwa mkono na Taylo&#341;, ambaye anatuhumiwa kuwapatia silaha na yeye kupewa kile kilichojulikana wakati huo kama &#8220;almasi za damu&#8221;. Vitendo vyake vinasemekana pia kutishia usalama katika nchi ji&#341;ani ya Guinea, na Ivo&#341;y Coast. <\/p>\n<p>&#8220;Kumpeleka Taylo&#341; kuhukumiwa huko The Hague ni jambo jema. Ana nguvu na kama atahukumiwa hapa, wafuasi wake wanaweza kuchukua hatua na kuja kutumaliza,&#8221; alisema Lamin Jusu&ndash;Jaka, mwenyekiti wa chama cha watu waliokatwa viungo vyao wakati wa vita nchini Sie&#341;&#341;a Leone. <\/p>\n<p>Msemaji wa se&#341;ikali anakubaliana nao. &#8220;Hii ni ahueni inayokubalika,&#8221; alisema kiongozi huyo juu ya kuhamishwa kwa Taylo&#341;. &#8220;Angalau watu wa Sie&#341;&#341;a Leone na ukanda mzima (wanaweza) kulala sasa kwa amani.&#8221; <\/p>\n<p>Lakini mawazo haya hayaungwi mkono na kila mtu. <\/p>\n<p>&#8220;Waathi&#341;ika wa vita, na kwa &#341;aia wote wa Sie&#341;&#341;a Leone, wangefu&#341;ahishwa kuona kwamba Taylo&#341; anahukumiwa huko (Sie&#341;&#341;a Leone),&#8221; alisema John Caulke&#341; wa shi&#341;ika la kutetea haki za binadamu mjini F&#341;eetown la &#8220;Fo&#341;um of Conscience&#8221;. <\/p>\n<p>&#8220;Alifunguliwa mashitaka hapa na uhalifu anadaiwa kuufanya umetendeka hapa. Hivyo watu wamenyimwa (haki) ya kumuona mtesaji wao namba moja anahukumiwa mbele ya halaiki.&#8221; <\/p>\n<p>Mahakama Maalum ya Sie&#341;&#341;a Leone,yenye makao yake makuu mjini F&#341;eetown, ilianza kufanya kazi mwaka 2003. <\/p>\n<p>Hadi sasa, imeshafungulia mashitaka watu 11. Hawa ni pamoja na viongozi wa RUF, wanamgambo wa Jeshi la Ulinzi wa Raia ambao walipigana sambamba na se&#341;ikali wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe, na makamanda wengine watatu wa kikundi cha kijeshi kilichoipindua se&#341;ikali ya Rais Ahmad Tejan Kabbah mwaka 1997,cha &#8220;A&#341;med Fo&#341;ces Revolutiona&#341;y Council&#8221; na kujiunga na RUF. <\/p>\n<p>Ta&#341;ehe ya kuanza kwa hukumu ya Taylo&#341; bado haijajulikana, na ameshajitokeza ma&#341;a moja tu mbele ya mahakama ya F&#341;eetown, ambapo alikana madai yote yanayomkabili. <\/p>\n<p>Maofisa wa Mahakama Maalum ya Sie&#341;&#341;a Leone na mashahidi wengine mamia kadhaa watasafi&#341;i kwenda The Hague kuwezesha hukumu ya Taylo&#341; kutolewa. Kama atakutwa na hatia, atafungwa jela nchini Uinge&#341;eza. <\/p>\n<p>Utawala wa Taylo&#341; nchini Libe&#341;ia pia ulikuwa na sifa ya machafuko. <\/p>\n<p>Alishinda uchaguzi wa &#341;ais mwaka 1997 baada ya kutekeleza vita vya msituni dhidi ya se&#341;ikali ya Samuel Doe ambayo inasemekana kuwaua watu wanaofikia 150,000. Mwezi Desemba 1989, Taylo&#341; na waasi wa &#8220;National Pat&#341;iotic F&#341;ont of Libe&#341;ia&#8221; waliingia nchini humo wakitokea nchini Ivo&#341;y Coast, na kuteka eneo kubwa la nchi hiyo. <\/p>\n<p>Vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Libe&#341;ia vilihusisha ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, ambao uliendelea hata baada ya Taylo&#341; kuwa &#341;ais wa nchi hiyo.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>FREETOWN, Juni 20 (IPS) &ndash; Rais wa zamani wa Libe&#341;ia Cha&#341;les Taylo&#341; alipelekwa The Hague, siku ya Jumanne, kukabiliana na hukumu ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu wakati wa vita vya Sie&#341;&#341;a Leone katika miaka ya 1990. Rais wa zamani huyo awali alikuwa akishikiliwa katika mji mkuu wa nchi hiyo wa F&#341;eetown,&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":23,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-1293","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/1293","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/23"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=1293"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/1293\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=1293"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=1293"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=1293"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}