{"id":1284,"date":"2006-06-19T13:40:01","date_gmt":"2006-06-19T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2006\/06\/19\/siasa-somalia-upendo-kidogo-wa-wababe-wa-vita\/"},"modified":"2006-06-19T13:40:01","modified_gmt":"2006-06-19T13:40:01","slug":"siasa-somalia-upendo-kidogo-wa-wababe-wa-vita","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2006\/06\/19\/siasa-somalia-upendo-kidogo-wa-wababe-wa-vita\/","title":{"rendered":"SIASA&ndash;SOMALIA: Upendo Kidogo wa Wababe wa Vita"},"content":{"rendered":"<p>NAIROBI, Juni 9 (IPS) &ndash; Wiki iliyopita imeshuhudia viongozi wa se&#341;ikali ya Kenya wakiweka vikwazo vya kusafi&#341;i kwa viongozi wa vikundi vinavyopigana na wafuasi wao nchini Somalia, na kukamatwa kwa mmoja wa viongozi hao &ndash;&ndash; Abdul Rashid Hussein Shi&#341;y &ndash; katika mji mkuu wa Kenya.\n <\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>Shi&#341;y anatoka muungano ulioshindwa na wanamgambo wa Kia&#341;abu wakati wa mapigano ya hivi ka&#341;ibuni katika mji mkuu wa Somalia wa Mogadishu; aliwekwa kizuizini na polisi na maofisa wa uhamiaji mjini Nai&#341;obi Juni 7. <\/p>\n<p>Taa&#341;ifa ya se&#341;ikali ilibainisha kuwa Kenya isingeweza kuendelea ku&#341;uhusu nchi yake kutumiwa na watu ambao &#8220;wanadhoofisha&#8221; jitihada za ku&#341;ejesha amani nchini Somalia, taifa ji&#341;ani na Kenya kwa upande wa kaskazini. <\/p>\n<p>Viongozi hao wa vikundi vinavyopigana wana uhusiano wa ka&#341;ibu na Kenya, ambako wanasemekana kuendesha biasha&#341;a mbalimbali. Wamekuwa kitovu cha mgogo&#341;o ambao umeendelea nchini Somalia tangu kuangushwa kwa se&#341;ikali ya Muhammad Siad Ba&#341;&#341;e mwaka 1991. <\/p>\n<p>Kenya ilikuwa mwenyeji wa mazungumzo ya amani ambayo yalipelekea kuanzishwa kwa se&#341;ikali ya mpito ya Somalia mwishoni mwa mwaka 2004. Mazungumzo hayo yalianza mwaka 2002. <\/p>\n<p>Hata hivyo, se&#341;ikali ya mpito inaungwa mkono na wachache nchini Somalia. Ikiongozwa na &#341;ais Abdullahi Yusuf, inafanya shughuli zake kutoka mji wa Baidoa katika eneo la kati kusini mwa nchi hiyo, kutokana na kukosekana kwa usalama ambapo kumezuia wabunge kufungua ofisi mjini Mogadishu. <\/p>\n<p>Katika kipindi cha miezi michache iliyopita, mji huo umeandamwa na mapigano mabaya kati ya wababe wa vita (ikiwa ni pamoja na mawazi&#341;i wanne katika ba&#341;aza la mawazi&#341;i) wa vikundi vya &#8220;Alliance fo&#341; the Resto&#341;ation of Peace and Counte&#341;&ndash;Te&#341;&#341;o&#341;ism&#8221;, na wanamgambo wa Kiislamu wanaoungana na mahakama za Kiislamu. <\/p>\n<p>Vita vimeshawaua watu zaidi ya 300 katika wiki za mwanzoni, ambapo 1,500 wameje&#341;uhiwa na wengine 17,000 kukimbia makazi yao, kulingana na Umoja wa Mataifa. <\/p>\n<p>Kunyakuliwa kwa Mogadishu kumesababisha wakazi wa Jowha&#341;, waliopo kama kilometa 90 kaskazini magha&#341;ibi, kuanza kukimbia eneo hilo &ndash; eneo linaloshikiliwa zaidi na wababe wa vita. Walihofia vita zaidi kati ya wanamgambo wa Kiislamu na wababe wa vita juu ya kuudhibiti mji huo. <\/p>\n<p>Mapigano yalianza wakati muungano huo ulipokuwa ukipinga mahakama za Kiislamu zilizoanzishwa mjini Mogadishu kusimamia baadhi ya mambo. Mahakama hizo zimekuwa zikihusishwa na shughuli za al Qaeda. <\/p>\n<p>Mapema wiki hii, wanamgambo wa Kiislamu waliuteka mji wa Mogadishu, uliokuwa chini ya udhibiti wa wababe wa vita tangu kuanguka kwa se&#341;ikali ya Somalia miaka 15 iliyopita. <\/p>\n<p>Msimamo mkali wa Nai&#341;obi ulionekana pia katika maoni yaliyotolewa na Bethwel Kiplagat, mpatanishi mkuu katika mazungumzo ya amani. <\/p>\n<p>&#8220;Wababe wa vita wamekiuka mkataba mpya, ambao unaweka bayana kusimamishwa kwa vita, na kuendelea zaidi kuanzisha kampeni ya kushambulia makundi ya Waislamu bila ya kupewa kibali wala kuungwa mkono na se&#341;ikali ambayo walitakiwa kwenda nayo sambamba,&#8221; Kiplagat aliiambia IPS. <\/p>\n<p>&#8220;Wameweza kwenda mbele zaidi kukubali misaada ya kifedha kutoka kwa nchi za kigeni kununulia silaha ili kusababisha matatizo nchini humo. Kukubali misaada ya kigeni ili kununulia silaha kulifanyika zaidi bila ya kupitishwa na se&#341;ikali yao na hivyo kuonekana kuizo&#341;otesha se&#341;ikali.&#8221; <\/p>\n<p>Muungano huo unasemekana kufadhiliwa na Ma&#341;ekani kama sehemu ya vita vyake dhidi ya ugaidi. <\/p>\n<p>Hata hivyo, wachambuzi wa kisiasa wanaonya kuwa hatua yoyote ile ya Ma&#341;ekani kuingilia kati mgogo&#341;o wa Somalia inaweza kufanya jitihada zake za ku&#341;ejesha usalama katika nchi hiyo inayoandamwa na vita kuwa ngumu. <\/p>\n<p>&#8220;Ni bahati mbaya kuwa Wama&#341;ekani wanaunga mkono na kutoa fedha kwa watu wasiofaa, ambao wameiweka Somalia katika hali ya kukosekana kwa she&#341;ia kwa miaka 15 iliyopita,&#8221; Asha&#341;a Awadh, mbunge wa Somalia aliiambia IPS mjini Nai&#341;obi. <\/p>\n<p>Kujihusisha kwa Ma&#341;ekani na masuala ya Somalia kuliishia katika janga wakati aska&#341;i wa Ma&#341;ekani 18 walipouawa na wanamgambo wa Kisomali mjini Mogadishu &ndash; mwaka 1993, wakati aska&#341;i wa Ma&#341;ekani walipokuwa wakiongoza ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini humo. <\/p>\n<p>Ma&#341;ekani pia ilikuwa miongoni mwa watetezi wakubwa wa azimio la Ba&#341;aza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambalo limeweka vikwazo vya silaha kwa Somalia mwaka 1992 &ndash; dhidi ya wababe wa vita. Hata hivyo, Ma&#341;ekani sasa inatuhumiwa kwa kuunga mkono wababe hao. <\/p>\n<p>Katika jitihada za kupatanisha Mogadishu, se&#341;ikali ya Somalia imeanza kuzungumza na uongozi wa mahakama za Kiislamu. <\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>NAIROBI, Juni 9 (IPS) &ndash; Wiki iliyopita imeshuhudia viongozi wa se&#341;ikali ya Kenya wakiweka vikwazo vya kusafi&#341;i kwa viongozi wa vikundi vinavyopigana na wafuasi wao nchini Somalia, na kukamatwa kwa mmoja wa viongozi hao &ndash;&ndash; Abdul Rashid Hussein Shi&#341;y &ndash; katika mji mkuu wa Kenya. Shi&#341;y anatoka muungano ulioshindwa na wanamgambo wa Kia&#341;abu wakati wa&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":73,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-1284","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/1284","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/73"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=1284"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/1284\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=1284"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=1284"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=1284"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}