{"id":1279,"date":"2006-06-07T13:40:01","date_gmt":"2006-06-07T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2006\/06\/07\/haki-kenya-kutumia-arvs-kujaza-matumbo-wazi\/"},"modified":"2006-06-07T13:40:01","modified_gmt":"2006-06-07T13:40:01","slug":"haki-kenya-kutumia-arvs-kujaza-matumbo-wazi","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2006\/06\/07\/haki-kenya-kutumia-arvs-kujaza-matumbo-wazi\/","title":{"rendered":"HAKI &ndash; KENYA: Kutumia ARVs Kujaza Matumbo Wazi"},"content":{"rendered":"<p>NAIROBI, Juni 2 (IPS) &ndash; &#8220;ARVs zinaweza kubadili mambo, lakini hazibadili hali yangu ya kiuchumi na nijamii. Ndiyo, napata ARVs; lakini siwezi kupata chakula cha bei nafuu mezani,&#8221; anasema mtu ambaye anasisitiza kutambuliwa kama wa Kimani.\n <\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>&#8220;Hii ndiyo sababu iliyonifanya kujiandikisha katika vituo viwili vya kutoa matibabu, ili niweze kupata ARVs (madawa ya kupunguza makali ya VVU) ma&#341;a mbili: natumia seti moja kutoka kituo kimoja, halafu nauza seti nyingine kutoka kituo cha pili, ili niweze kupata kitu kidogo cha kuingiza tumboni mwangu.&#8221; <\/p>\n<p>Wa Kimani alizungumza na shi&#341;ika la haba&#341;i la IPS nje ya moja ya vituo ambavyo anapata matibabu, huku uso wake ukiwa umeungua na jua kali akiwa ameketi juu ya jiwe, akisubi&#341;i wateja wanaonunua madawa kutoka kwake. Unyanyapaa ambao unaendelea kulizunguka gonjwa la Ukimwi nchini Kenya umewafanya wateja kuogopa kupata ARVs kupitia katika mifumo &#341;asmi &ndash; kitu ambacho anahofia kinaweza kusababisha kuishi kwake na VVU kujulikana kwa umma. <\/p>\n<p>Wa Kimani, ambaye hana aji&#341;a, alianza kutumia vidonge mwaka jana. Anawatoza wateja wake chini ya dola saba kwa vidonge vinavyotosha kutumia kwa mwezi mzima. <\/p>\n<p>&#8220;Hizi siyo nyingi, lakini angalau vinanisaidia kununulia baadhi ya mahitaji ya lazima ili nisiweze kutumia madawa katika tumbo lisilokuwa na kitu. Unajua inaweza kuwa hata&#341;i,&#8221; wa Kimani anasema. <\/p>\n<p>&#8220;Nakumbuka kabla sijafiki&#341;i kuhusu biasha&#341;a hii, nilikuwa natumia madawa haya bila ya kula chakula &ndash; bali kunywa uji. Nilika&#341;ibia kufa. Nilijikuta nikiwa mdhaifu sana, nilipatwa na vidonda vya tumbo ambavyo havijapona hadi leo hii.&#8221; <\/p>\n<p>Hadi mwanzoni mwa mwezi huu, hospitali za se&#341;ikali zimekuwa zikitoza wastani wa dola 1.4 kwa kiasi kama hicho cha ARVs; hata hivyo, ada hiyo iliondolewa kuanzia mwezi Juni 1. Ka&#341;ibu watu milioni mbili wanaishi na VVU\/Ukimwi nchini Kenya &ndash; zaidi ya watu 200,000 wanahitaji kutumia ARVs. <\/p>\n<p>Suala la Wa Kimani halionekana kutokuwa la kawaida. <\/p>\n<p>Pat&#341;icia Ase&#341;o, mwanachama wa Chama cha Kupambana na Upatikanaji wa Matibabu ya VVU\/Ukimwi nchini Kenya, aliwahi kusikia haba&#341;i ya watu wengine sita wanaopatiwa ARVs kutoka zaidi ya kituo kimoja mwaka jana. <\/p>\n<p>&#8220;Nilivutiwa na nilichunguza suala hilo zaidi kwasababu watu hawa wanatoka kwenye kikundi kimoja na mimi. Nilikuta kwamba wamejiandikisha katika zaidi ya kituo kimoja ili waweze kupata madawa ya ziada kwa ajili ya kuyauza kuweza kujinunulia chakula cha kutumia sambamba na madawa,&#8221; aliiambia IPS. <\/p>\n<p>Katika baadhi ya matukio, wagonjwa ambao wana chanzo kimoja tu cha madawa hayo pia wataweza kuuza ARVs zao kujinunulia chakula, aliongeza Ase&#341;o. Hata hivyo, wanaelezea hadithi tofauti kwa wafanyakazi wa vituo vya matibabu. <\/p>\n<p>&#8220;Watakuambia kuwa madawa yao yamepotea; wengine wanadai mabegi yao yalipo&#341;wa na wezi. Lakini unapowahoji zaidi, unakuja kutambua ukweli upo wapi,&#8221; alibainisha. Ase&#341;o pia ni mshau&#341;i nasaha wa VVU\/Ukimwi katika hospitali ya se&#341;ikali. <\/p>\n<p>Wagonjwa wengine wanaoishi mbali na vituo vya kugawa ARV na ambao ni dhaifu sana kuweza kutembea hadi vituoni &ndash; ambao pia ni maskini sana kuweza kupata nauli &ndash; wanaachana tu na suala la tiba, na kutumia pesa walizonazo kununulia chakula. <\/p>\n<p>Wakati takwimu za se&#341;ikali zikionyesha kuwa asilimia 56 ya wananchi wanaishi chini ya msta&#341;i wa umaskini, maja&#341;ibu ya tiba ambayo yanayowakumba baadhi ya Wakenya wanaoishi na VVU kuuza madawa yao hayaonekani kuja kumalizika katika siku chache za baadaye. <\/p>\n<p>&#8220;Mapambanao dhidi ya VVU\/Ukimwi ni lazima yaende sambamba na mapambano dhidi ya umaskini. Kama sivyo, tunapoteza muda wetu,&#8221; anasema Omu Anzala, mhadhili mwandamizi katika Ida&#341;a ya Baolojia ya Madawa katika Shule ya Udakta&#341;i kwenye Chuo Kikuu cha Nai&#341;obi. Nai&#341;obi ni mji mkuu wa Kenya. <\/p>\n<p>Se&#341;ikali inadai kuongeza kwa kiasi kikubwa idadi ya watu wanaopata ARV katika miaka ya hivi ka&#341;ibuni: wagonjwa 39,000 walitibiwa mwaka 2005, kutoka 24,000 wa mwaka 2004. Lengo ni kuwapatia madawa watu 95,000 mwanzoni mwa mwaka 2006. <\/p>\n<p>Lakini, anasema Anzala, &#8220;se&#341;ikali iondokane na kutupatia idadi. Ni lazima itizame ubo&#341;a na uendelevu wa huduma yenyewe. Takwimu hizi zina maana ndogo wakati wagonjwa wengi wanaacha kutumia madawa au wanayauza.&#8221; <\/p>\n<p>Madai ya kuuza ARVs yanayofanywa na baadhi ya wagonjwa, na njia mbaya ambapo wengine wanasemekana kutumia madawa hayo, kumezua hofu ya kupatwa na hali ya madawa kuwa sugu dhidi ya VVU nchini Kenya. <\/p>\n<p>Wakati huu kuna aina 24 tu ya ARVs sokoni &ndash; na wakati wowote ule, mgonjwa anatakiwa kutumia aina tatu. Kama hali ya sasa itaendelea, anasema Anzala, &#8220;tunaweza tusiwe na ARVs zozote zile za kuzungumzia, kutokana na kwamba watu watakuwa sugu kwa aina zote za madawa hayo.&#8221; <\/p>\n<p>&#8220;Kuna haja ya kusimamia watu na kuona kama wanatumia madawa hayo kama inavyotakiwa, ikiwa ni pamoja na kusimamia usugu wa gonjwa hilo.&#8221; <\/p>\n<p>Wengine wanadai kuwa matatizo haya yatamalizika kama suala la lishe litazingatiwa zaidi. <\/p>\n<p>&#8220;Tunapozungumzia juu ya matibabu kamilifu ya VVU\/Ukimwi, lishe ni sehemu ya matibabu hayo. Lakini se&#341;ikali imepuuza sehemu hiyo; inatoa ushau&#341;i nasaha wa lishe imemaliza,&#8221; anabainisha Ase&#341;o. <\/p>\n<p>&#8220;Baadhi ya vituo vya kutoa tiba vinaweza kutoa tu paketi moja ya ujimix (unga wa mahindi) kwa mwezi. Hii haitoshelezi kitu.&#8221; <\/p>\n<p>Ripoti iliyotolewa mwezi uliopita na Muungano wa Kujiandaa na Utoaji wa Matibabu, kikundi cha mashi&#341;ika mbalimbali ya Ukimwi kutoka sehemu mbalimbali duniani, pia unazungumzia suala la lishe kama kikwazo kikubwa katika vita dhidi ya VVU\/Ukimwi nchini Kenya. <\/p>\n<p>&#8220;Msaada unaotolewa kwa ajili ya lishe bado ni mdogo sana labda kwa ajili ya elimu ya lishe,&#8221; unasema wa&#341;aka, wenye jina la &#8216;Missing the Ta&#341;get &ndash;&ndash; Off Ta&#341;get fo&#341; 2010: How to Avoid B&#341;eaking the P&#341;omise of Unive&#341;sal Access&#8217;. <\/p>\n<p>Ripoti hiyo iliyotolewa wiki iliyopita kabla ya Mkutano Maalum wa Ba&#341;aza Kuu la Umoja wa Mataifa juu ya VVU\/Ukimwi, ambao ulizinduliwa Mei 31 mjini New Yo&#341;k. <\/p>\n<p>Maofisa wa afya wanasema wanaja&#341;ibu kubo&#341;esha lishe miongoni mwa wagonjwa. <\/p>\n<p>&#8220;Kuna shughuli zinazoendelea kutoa huduma hii. Hospitali nyingi wanazitekeleza,&#8221; David Mwaniki, mkuu wa Ida&#341;a ya Kiufundi katika Ba&#341;aza la Taifa la Kudhibiti Ukimwi, aliiambia IPS. <\/p>\n<p>&#8220;Lakini, tunahitaji kufanya kazi zaidi kuima&#341;isha kazi hizo.&#8221;<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>NAIROBI, Juni 2 (IPS) &ndash; &#8220;ARVs zinaweza kubadili mambo, lakini hazibadili hali yangu ya kiuchumi na nijamii. Ndiyo, napata ARVs; lakini siwezi kupata chakula cha bei nafuu mezani,&#8221; anasema mtu ambaye anasisitiza kutambuliwa kama wa Kimani. &#8220;Hii ndiyo sababu iliyonifanya kujiandikisha katika vituo viwili vya kutoa matibabu, ili niweze kupata ARVs (madawa ya kupunguza makali&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":73,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-1279","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/1279","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/73"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=1279"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/1279\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=1279"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=1279"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=1279"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}