{"id":1243,"date":"2006-04-18T13:40:01","date_gmt":"2006-04-18T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2006\/04\/18\/maendeleo-kenya-ndege-ambayo-ilichukua-zaidi-ya-uhai\/"},"modified":"2006-04-18T13:40:01","modified_gmt":"2006-04-18T13:40:01","slug":"maendeleo-kenya-ndege-ambayo-ilichukua-zaidi-ya-uhai","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2006\/04\/18\/maendeleo-kenya-ndege-ambayo-ilichukua-zaidi-ya-uhai\/","title":{"rendered":"MAENDELEO &ndash; KENYA: Ndege Ambayo Ilichukua Zaidi ya Uhai"},"content":{"rendered":"<p>NAIROBI, Ap&#341;ili 13 (IPS) &ndash; Kuna mwito unaozidi kuongezeka kutaka Kenya kumaliza uadui wa kikabila katika eneo kame la kaskazini &ndash; hii ni baada ya ndege kupata ajali na kuchukua maisha ya wabunge sita na askofu ambao walikuwa katika ujumbe wa kutafuta amani katika mkoa huo.\n <\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>Wabunge na askofu huyo ni miongoni mwa watu 14 ambao walifa&#341;iki dunia baada ya ndege ya kijeshi waliyokuwa wamepanda kuanguka ka&#341;ibu na uwanja wa ndege mdogo wa Ma&#341;sabit upande wa kaskazini mapema wiki hii (Ap&#341;ili 10) &ndash; ambayo iligonga mwamba na kugawanyika vipande viwili, kabla ya kuungua kabisa. Ajali hiyo ilisemekana kusababishwa na hali ya hewa mbaya. Watu watatu waliokoka katika ajali hiyo, lakini walije&#341;uhiwa vibaya &ndash; kwa kukatika miguu na kuungua. <\/p>\n<p>Zia&#341;a hiyo ilikuwa ya kwanza ya ujumbe wa pamoja wa wabunge kwenda kutatua mgogo&#341;o wa kikabila. <\/p>\n<p>&#8220;Tunahitaji amani ya kudumu katika eneo hilo; tunahitaji watu wetu kuwa salama. Hatutaki hatua kuchukuliwa tu baada ya kupoteza maisha. Ni muhimu kwa se&#341;ikali kushughulikia mzizi wa sababu ya mapigano,&#8221; alisema Fatuma Gouyaye, ambaye amempoteza mama yake na dada zake wawili katika mashambulizi ya kijiji chao wilayani Ma&#341;sabit mwaka jana. <\/p>\n<p>&#8220;Bila ya kuwa na jambo hili, tutaendelea kuishi katika maumivu,&#8221; aliliambia shi&#341;ika la haba&#341;i la IPS katika makazi ya shangazi yake mjini Nai&#341;obi. <\/p>\n<p>Wiki iliyopita katika wilaya ya Sambu&#341;u, pia kaskazini mwa Kenya, watu wanne walikufa katika mapigano yanayoendelea ambayo pia yalilazimu idadi kadhaa ya watu kuyakimbia makazi yao. <\/p>\n<p>Kati ya wabunge watano waliofa&#341;iki, ikiwa ni pamoja na kiongozi wa upinzani Bonaya Godana, ni &#341;aia kutoka makabila yanayopigana. Mbunge wa sita, Mi&#341;ugi Ka&#341;iuki, ni &#341;aia wa wilaya ya Naku&#341;u magha&#341;ibi mwa Bonge la Ufa; alikwenda kama naibu wazi&#341;i wa usalama wa ndani. <\/p>\n<p>Mapigano ya kikabila kaskazini mwa nchi yana asili yake katika kugombea maji na malisho ya wanyama. Hata hivyo, mapigano hayo pia yameingia katika mwelekeo wa kisiasa, kulingana na Abdullahi Abdi, ofisa mtendaji mkuu wa Shi&#341;ika la Misaada Kaskazini: ambalo linafanya kazi katika eneo hilo. <\/p>\n<p>Anadai kuundwa kwa majimbo mapya katika mkoa huo kumegawanya majimbo kutokana na makabila, na kuongeza uadui kati ya wanajamii ambao walikuwa awali wakigawana &#341;asilimali kama a&#341;dhi ya malisho kabla ya mipaka ya kisiasa. <\/p>\n<p>Ukubwa wa uadui ulijionyesha wakati wa mapigano huko Ma&#341;sabit mwezi Julai ambapo watu 90 waliuawa &ndash; na ku&#341;ipotiwa kuwa mapigano mabaya zaidi ya kikabila kuwahi kutokea tangu nchi ya Kenya ilipopata uhu&#341;u wake mwaka 1963. <\/p>\n<p>Wavamizi wenye silaha ambao walisemekana kuwa wafuasi wa kabila la Bo&#341;ana walivamia vijiji vilivyokaliwa na wanajumuiya wa kabila la Gab&#341;a huko Tu&#341;bi eneo la Ma&#341;sabit, linalopakana na Ethiopia. Wastani wa watu 6,000 walikimbia makazi yao kutokana na tukio hilo. <\/p>\n<p>Uadui kaskazini mwa Kenya pia unaaminika kuchochewa na msuguano nchini Ethiopia. <\/p>\n<p>&#8220;Makabila ya Wagab&#341;a na Wabo&#341;ana kutoka jumuiya ya Wao&#341;omo nchini Ethiopia wana uhusiano wa ka&#341;ibu na Wagab&#341;a na Wabo&#341;ana wa Kenya, na uhusiano huu umeathi&#341;i hali ya hapa,&#8221; alisema Abdi. <\/p>\n<p>Kama IPS ilivyo&#341;ipoti siku za nyuma, Godana alilaumu Waasi wa Ukombozi wa Wao&#341;omo (OLF) kutoka Ethiopia kuhusika katika mauaji ya Tu&#341;bi &ndash; kwa kusema waasi wa OLF wamekasi&#341;ishwa na kabila la Wagab&#341;a nchini Kenya kuunga mkono sababu za waasi hao (angalia makala &#8216;RIGHTS&ndash;KENYA: In the Afte&#341;math of a Massac&#341;e&#8217;). <\/p>\n<p>Waasi wa OLF walianzisha mapigano dhidi ya se&#341;ikali ya Ethiopia mwaka 1993, katika jitihada za kutaka kujitenga kwa watu wa makabila ya Wao&#341;omo wanaoishi kusini mwa nchi hiyo, ikiwa ni pamoja na Wagab&#341;a na Wabo&#341;ana. <\/p>\n<p>IPS pia ilimnukuu mtaalamu wa histo&#341;ia ya jamii Paul Goldsmith, ambaye amefanya utafiti juu ya makabila ya Wakenya kwa muda m&#341;efu, aliposema kwamba kabla ya mauaji ya Tu&#341;bi, Wagab&#341;a wa Kenya wamekuwa walaumiwe kwa kuunga mkono se&#341;ikali ya Ethiopia. Hii ilisababisha mashambulizi kutoka kwa Wabo&#341;ana, na kusababisha ulipizaji wa kisasi wa jino kwa jino na kusababisha matukio ya Tu&#341;bi. <\/p>\n<p>Tafiti za Godana na Goldsmith zilipuuzwa na watu wengine katika se&#341;ikali ya Kenya, na waasi wa OLF. <\/p>\n<p>Hata hivyo, pamoja na kuwepo kwa migogo&#341;o michache katika mkoa huo, kuna silaha nyingi zinamiminika kuingia eneo hilo: mishale na vi&#341;ungu imeshachukuliwa nafasi yake na bastola nzito za aina ya &#8220;AK&ndash;47&#8221; na &#8220;bazookas&#8221;, hivyo kuyapa kibu&#341;i cha kupigana makabila yanayozozana. <\/p>\n<p>&#8220;Katika shambulizi moja katika tukio la mauaji ya Ma&#341;sabit, tuliwapoteza Wakenya 90. Katika siku za nyuma, tusingeweza kupoteza hata nusu ya watu hao,&#8221; alitoa maoni Abdi. <\/p>\n<p>Kukosekana kwa maendeleo pia kumeongeza matatizo katika mkoa huo. Hakuna zinazounganisha Ma&#341;sabit na maeneo mengine ya nchi, wakati ambapo kuna kliniki na shule chache sana na ambazo zipo mbalimbali mno. <\/p>\n<p>Mamlaka sasa zimeahidi kukabiliana na hali hii. Katika taa&#341;ifa kwa vyombo vya haba&#341;i siku ya Jumatano, makamu wa Rais Moody Awo&#341;i alisema se&#341;ikali ingeanza kuchimba visima katika eneo hilo mapema iwezekavyo, ili kupunguza kugombania &#341;asilimali. <\/p>\n<p>Muda mfupi kabla ya kifo chake, Godana alitupia lawama se&#341;ikali kutokana na kuvuta miguu yake kuhusu hali ya kaskazini. Jitihada za awali zilizochukuliwa na asasi zisizokuwa za kise&#341;ikali, viongozi wa dini na viongozi wa se&#341;ikali kuleta amani katika mkoa huo zilikuwa na mafanikio machache. <\/p>\n<p>&#8220;Hii inatokana na kwamba hatushughulikii mzizi unaosababisha tatizo. Hatupaswi kufanya kazi kama ga&#341;i la wagonjwa,&#8221; alisema Abdi, ambaye mwenyewe ni mwenyekiti wa zamani wa mpango wa amani ambao ulianzishwa baada ya mauaji ya Ma&#341;sabit. <\/p>\n<p>&#8220;Tunatakiwa kutafuta suluhisho la kudumu, ambalo ni pamoja na kuendeleza eneo hilo.&#8221; <\/p>\n<p>Ajali ya ndege ya wiki hii ili&#341;udisha nyuma kwa ma&#341;a nyingine tena jitihada za kushughulikia uadui wa kikabila. Tangu kutokea kwa ajali hiyo, bende&#341;a nchini Kenya zimekuwa zikipepea nusu mlingoti wakati ambapo vikao vya bunge vimeahi&#341;ishwa hadi wiki ijayo. <\/p>\n<p>Ka&#341;iuki atazikwa Ap&#341;ili 15. Wabunge wengine watano walizikwa mapema wiki hii (Ap&#341;ili 12) katika vijiji vyao &ndash; na kuacha hisia kwa wengi juu ya maafa makubwa ya hivi ka&#341;ibuni katika eneo lenye mgogo&#341;o la kaskazini mwa Kenya.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>NAIROBI, Ap&#341;ili 13 (IPS) &ndash; Kuna mwito unaozidi kuongezeka kutaka Kenya kumaliza uadui wa kikabila katika eneo kame la kaskazini &ndash; hii ni baada ya ndege kupata ajali na kuchukua maisha ya wabunge sita na askofu ambao walikuwa katika ujumbe wa kutafuta amani katika mkoa huo. Wabunge na askofu huyo ni miongoni mwa watu 14&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":73,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-1243","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/1243","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/73"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=1243"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/1243\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=1243"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=1243"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=1243"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}